Gari zikiwa zimepandana mara baada ya lori la mchanga kufeli breki na kugonga gari lililokuwa mbele yake na kupelekea gari hilo kugonga la mbele yake na kuendelea.ajali hii imetokea leo majira ya saa nane mchana maeneo ya magomeni mikumi.hakuna aliepoteza maisha katika ajali hii.wananchi waliofika katika ajali hiyo wakiangalia jinsi magari yalivyoharibika vibaya mara baada ya kutokea kwa mzinga huo.lori lililosababisha ajali ya magari yapatayo 6 likifanyiwa matengenezo mara baada kuzimika katika mzinga huo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 16, 2010

    Nomba kuuliza ajali kama hii nashikiliwa dereva au muwajiri?? i mean nani analifa hasara dereva au mwajiri wake?

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 16, 2010

    Kwa miaka mingi sana tumekuwa tukiona na kusikia "Lori la mchanga lilikosa brake na kuzoa wapita njia" au "kusababisha ajali" n.k. na maisha ya watu wengi hupotea.

    Kumbukumbu yangu inaniambia haya malori huwa yanaendeshwa mwendo wa mashindano. Mfano yale yanayoenda njia ya Chalambe kule Mbagala mpaka kimanzichana?... Haya huwa yanaendeshwa mwendo wa hatari kabisa. Nina maswali mawili tu: Kwanza, Haya malori huwa yanakaguliwa ubora wake wa kuwa barabarani? Je, madereva wana-leseni halali na wanazo-sifa zinazotosha kuendesha haya malori?

    Maswali haya pia ninayaelekeza kwa madereva wa mabasi ya abiria.

    Mdau,
    Ughaibuni

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 16, 2010

    Poleni mliohusika. Inasemekana Dereva wa lori alishikwa na ugonjwa wa kifafa.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 16, 2010

    Ajali hizi zitatokea hata kwenye ma flyover yanayopigiwa kelele. Tutafute ufumbuzi wa kweli wa matatizo ya foleni. Tutafute ufumbuzi wa kweli wa matatizo ya ajali barabarani.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...