Kipa wa Taifa Stars Mwarami Mohamed akidaka nyasi wakati ndinga linaelekea nyavu ndogo baada ya mkwaju wa kuchinja uliopigwa na Robinho baada ya kupata pande saaaafi toka kwa Kaka
Kipa wa Stars Mwarami Mohamed na mabeki wake
wakijiuliuza wakati Robinho na wenzie walkifurahia bao

Nani wa kumlaumu?
Taifa Stars wanajibu mapigo kwa mashambulizi ya mara kwa mara langoni pa Brazil ambao timu yote iko ndani ya 18

NDINGA LIMEANZA KIASI CHA DAKIKA KUMI ZILIZOPITA NA BRAZIL INAONGOZA KWA BAO 1-0 LILILOFUNGWA NA ROBINHO MNAMO DAKIKA YA 7 KATIKA UWANJA WA NESHNO MPYA.


UWANJA HAUJASHONA KIHIIIIVYO KAMA ILIVYOTARAJIWA NA HUENDA HII INATOKANA NA FOLENI ZA MAGARI TOKA KILE PEMBE, HIVI TUNAVYOONGEA NI SAA 12.25 NA BADO WADAU WANAMIMINIKA UWANJANI...

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 24 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 07, 2010

    weka picha sio maneno au hadi picha mmeambiwa hadi match iishe

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 07, 2010

    Munaweza wadau tamaza match at;

    http://www.firstrow.net/watch/20502/3/watch-tanzania-vs-brazil.html

    Enoy!

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 07, 2010

    Ahsante sana Michuzi,
    Endelea kutuhabarisha matukio na maendeleo huko uwanjani.
    Kampuni,
    Norway

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 07, 2010

    Kamau unaona uwanja huo sie tunaona uwanja wetu tukiwa ulaya anyway tunafungwa magoli ya kutosha but at least tuna uwanja mzuri unavutia kuangalia mpira

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 07, 2010

    brazil 2 Tanzania 0, mpira unaendelea kipindi cha kwanza. magoli Robinho amefunga mabao yote mpira unaendelea dakika ya 38 kipindi cha kwanza.
    Mpira upo live ktk hii linki:
    live http://atdhe.net/20083/watch- tanzania-vs- brazil
    Mdau
    Jijini London

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 07, 2010

    Ankal tupostie na videos tafadhali.

    Mdau wa Canada.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 07, 2010

    Wabongo poleni. Tunaenjoy mechi laivu ughaibuni.... bureee!! La Pili lishaingia. I'm sure by the time the evening is over labda 7-0 hivi???

    I feel so sad for the millions spent for this to happen.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 07, 2010

    Thats called bad business investment, this is very much reflecting the intelligence and technical skills of this country, which are very much reflecting back to the personals involved.

    Such an excellent team, the pit mark of football team, with such skills and attractiveness, the envy of any football nation,still we couldn't fill the stadium, for few Million US dollars invested towards the game?

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 07, 2010

    Ngassa na Mgosi wanaonekana kuwa mwiba kwa ngome ya Brazil ktk lala salama ya kipindi hiki cha kwanza cha mechi. Ngassa anaonekana kukubalika hapa jijini London na watazamaji wa gemu hii live.

    Sasa ni half-time timu ziko mapumzikoni.

    live on http: atdhe.net/20083/watch-tanzania-vs-brazil

    Mdau
    Jijini London

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 07, 2010

    Tanzania wanacheza vizuri. Link nyingine..

    www.ilemi.com

    cheers

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 07, 2010

    Sasa ndo nini hapo nchi inatangazajwe half time ukicheki kwenye soapcast ni matangazo ya brazili mwanzo hadi mwisho yani hata tanapa wameshindwa lipia kutangaza national park zetu watu kibao wanacheki online hii game na hakuna matangazo ya Tanzania yoyote kwahiyo mtu mpaka aka google ndo aijua faida ya hii mechi bado sijaiona ni ujinga mtu wacha tutukanwe na wakenya

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 07, 2010

    you can watch the game at
    http://www.ustream.tv/channel/copa-mundial

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 07, 2010

    Naona uwanja umejaa kabisa! ha mlifikiria nini kwa bei kama hizo kwa mechi ya kirafiki? tusubiri tujuwe kilichopatikana mlangoni.

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 07, 2010

    Watu wengine bwana mfungage tu midomo kwa vile hamjui kitu...hiyo soapcast uwakutangazie nchi yako umenunua tangazo huko? Acheni nyie...wanatangaza matangazo kwa vile wanajua wabrazil wngi ndio wanastream an anyewalipa who knowsni kutoka brazil...Nyie mnapenda vya bure tu hamjui chochote basi kuongea tu ujinga...We ulisikia wapi watu wakutangazie nchi yako kwenye site yako...Fungua yako na utangazze hiyo game live ucharge wmatangazo unayoyataka

    Kutangaza jina lishatangazika kwa njia kubwa kila mtu leo kaona Tanzinia inacheza na Brazil...Matangazo yapi direct na indirect hivyo kaa kimya...hao wasouth america wanavyojua kwetu ni jungle tu sasa leo wamekanyaga mpaka Tanzania kwanza wakirudi kwao watasema tulifika Tanzania na wana uwanja mzuri sana. na utalii utazidi.....

    na huyo anayesema tumelipa hela kwa hii...umetoa hata senti tano wewe au unagoogle siku nzima kuona free streaming...Hela hajatoa hata sent...Govt haikutoa hata sent sasa nyi nini kina wauma?


    Fanyeni uchunguzi kamla ya kulala mika...Kuna mengi ya kukosoa lakini wenye hela wakiamua kutumia watakavyo kaeni kimya kama hana hela nyamazeni

    Mdau USA...mseme mnavyotaka lakini game limechezwa...

    ReplyDelete
  15. AnonymousJune 07, 2010

    Tanzania v Brazil. All highlights and goals available at www.bongoline.com

    ReplyDelete
  16. AnonymousJune 07, 2010

    uwanja mweupeee utadhani lipuli ndo inacheza ndo faida ya viingilio vikubwa imekula kwenu na hela haijarudi hata robo viti vingi kuliko watazamaji next time msiwe na tamaa kiasi hiki mmewanyima walalahoi uhondo kwa ajili ya tamaa zenu TFF ovyo sana

    ReplyDelete
  17. AnonymousJune 07, 2010

    Mdau US nakuunga mguu, watanzania wa ajabu sana ninawashangaa kulalamika pesa si zao wala si za kodi ya serikali yao. Wenye pesa zao wamekaa kimya wao ooh zimepotea bure wamewaomba muwafanyie analysis? Watu wanainvest kwenye stock market na inaliwa yote, watu wanacheza kwenye makasino kila siku na wanaliwa na kesho wanacheza tena. Haya mechi imechezwa leo mmekosa kunywa uji wenu? Pesa si zenu zwauma nini? Na mnajuaje kama mwenye pesa kapata hasara? UDAKU TU KAMA KAMAU MAU

    ReplyDelete
  18. AnonymousJune 07, 2010

    MBONA KIWANJA KIMEKAA KAMA WEMBE WA TOPAZ HAYO MAJANI VP YAMEWEKWA KAMA TOPAZ HEHEHE KIINGILIO KIKUBWA UWANJA UMEKAA TUPU

    ReplyDelete
  19. AnonymousJune 08, 2010

    Anonymous jun 07, 09:54...wewe ni kamau nini? mana unaonekana unachuki binafsi na kiwanja chetu au sijui watanzania wote...si mtuache kama kiwanja kimakaa kama kiwembe au topaz weh kinakuuma nini?? nyie mnacho? hata robo hamfikii...shut up!! and write sense!! kiswahili cha kenya ulichoandika, sasa napata wasiwasi na nyie wakenya..
    mdau,
    USA

    ReplyDelete
  20. AnonymousJune 08, 2010

    TANAPA walipie muanze kuchonga ngenga,maana mwajifanya mwajua sana kuhusu matumizi sahii ya pesa ya serikali na taasisi zake.Pia issue sio uwanja kujaa,kwanza maeneo mengi ambayo hayakuwa na watu ni yale ambayo mtazamaji akikaa hatoweza kuona mpira vizuri.Acheni ukuda hasa nyie mlio nje ya Tanzania,mwajifanya mnauchungu na nchi,si mrudi basi tuwaone makelele tuuu!
    Kwa heriiii

    ReplyDelete
  21. AnonymousJune 08, 2010

    We mdau wa Us huna lolote pamoja na wanao kusapot wakati kamau anatutukana kila mtu alikuwa akitetea kwamba hili gemu ni ktk kuitangaza nchi, kwa taarifa yako walio wengi na walengwa wamecheki gemu hii kwa kupitia site mbalimbali hivyo basi ilitakiwa nchi ijitangaze ktk site hizo hata kama ni moja au mbili walau matangazo yetu yangerushwa hewani mwisho wa siku ni brazili tu wamejitangaza na sie kutoka patupu,na kama uwezo wa kununua matangazo hatuna tumewaita wa nini kama sio ujinga , naamini this time Kamau ataandika article nzuri kabisa kuonyesha jinsi gani sisi ni vichwa maji kazi kukurupuka, wenzetu wamejiandaa kuweka matangazo online ktk site zilizoonyesha hili gemu sie tunafikiri kuweka bango uwanjani lililoandika serengeti nd kazi imekwisha, wapi tanapa na mashirika mengine makubwa nao wangeshindwa ku buy air time, Tafakari wabongo sio kusifia tu kila kitu, hakukuwa na plan yoyote, wengi wameishia kuona brazil inacheza na tanzania na brazili kujitangaza kwasana maana hata burger za brazili tumezijua ila tanzania hakuna ajuaye kuna nini,afu bado watu inasifia. Nonsense

    ReplyDelete
  22. AnonymousJune 08, 2010

    tff jifunzeni kuweka viingilio vikubwa mumevuna mulichopanda

    ReplyDelete
  23. AnonymousJune 08, 2010

    JAMANI, KUMBE HIVI NDIVYO TULIVYO!!! WE ARE NOT CREATIVE!!! HIVI NI KWELI TANZANIA TUNA UWANJA HUU TU NDIYO WA KUJIVUNIA KUVUTIA UTALII??? TUNA NMB NA SERENGETI TU? NAUMIA SANA.
    TUNA VIVUTIO KIBAO, NA HUU NDO ULIKUWA WAKATI WA KUTANGAZA VIVUTIO VYA UTALII. TUNGEWEKA BANGO LIMEBANDIKWA PICHA YA MLIMA KILIMANJARO, HUU NDIYO UNGEKUWA WAKATI MWAFAKA KUUJUZA ULIMWENGU KUWA KWELI MLIMA KILIMANJARO UPO TANZANIA, TOFAUTI NA WANAVYOTANGAZA WALE WEZI, JIRANI WETU WAKENYA. TUNA MBUGA NZURI ZA WANYAMA, TUNA NGORONGORO, SELOUS, YAANI MAMBO KIBAO; LAKINI HATA TANGAZO MOJA LETU UKIACHIA NMB NA SERENGETI TUUU, AAH AAH AAH AAAH!!
    TUMEONA MATANGAZO YA WABRAZILI TU UTAFIKIRI MPIRA UMECHEZWA KWAO!! YAANI GEMU ILIJULIKANA KWA KIPINDI CHOTE HICHO LAKINI TUMESHINDWA KUJIANDAA!!!! UTALII GANI TULIOTANGAZA SAAAASAAAAA??????????

    TUKO MBELE SANA KATIKA KULOLOMA, KUJISIFU NA KUFISADI TU, LAKINI NAMNA YA KUINGIZA PESA HATUJUI. TUNATEGEMEA KUWAVUNA WAFANYAKAZI TOKANA NA KODI ZAO MAANA HAO TUNAWAWEZA, TUNAKATA TU VYOVYOTE TUTAKAVYO. NA NDIYO MAANA HATUTAKI KUWASHUSHIA MAKATO YA KODI TUNAJUA HATUNA KWA KUPATIA. KWA SABABU HATA HUKO KWA WAFANYABIASHARA HATUWEZI KUWATOZA IPASAVYO; NA TUMESHUHUDIA TUKIWAPUNGUZIA KODI; LAKINI BADO TUKIZIDI KUWAKABA KOO WAFANYAKAZI WETU.

    TUNASEMA BWANA, TUACHIE NINI HUKU TUNAYAONA???? WANASEAMA MFICHA UCHI HAZAI. TUKIACHA KUSEMA HAWATAJUWA KUWA TUNAUMIA.

    MNUNE MSINUNE, UJUMBE NDIYO HUO.

    ReplyDelete
  24. AnonymousJune 08, 2010

    nyie TFF mmelala doroooo mlitegemea uwanja utatapika ili mzikombe vizuri Mungu amewakomesha kisicho rizki hakiliki kuna watu wengi saaana walitamani kuona hiyo mechi ila mmewadhulumu haki yao na nyie mmekosa mapato aliyekuja na wazo la hivyo viingilio arudi school fasta kwani hamuoni hali ya uchumi ilivyo tete????? TAMAA ILIMPONZA FISI

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...