Henry Galinoma (njano kichwani) na kundi lake
Mwanamziki machachari Henry Galinoma aka ButiJiwe mwenye maskani yake nchini Uholanzi anatarajiwa kutingisha jukwaa la onyesho kubwa la Midzomerhout Festival mjini Emmen, huko Holand.
Mwanamziki huyo wa mziki wa dansi wa afrika mashariki amechaguliwa kuwa ndiye mwanamziki pekee wa kiafrika nchini Uholanzi kuwakilisha katika onesho hilo,ambapo
pia atawaongoza jukwaani wanamziki watakao kwenda na mwavuli wa jina la "Africa Breezze".
Mwanamziki Buti Jiwe ameachia hewani album iliyobeba jina la "Samahani" ambayo inatamba katika vituo vingi vya redio ndani na nje ya Tanzania.hata hivyo Buti Jiwe ameahidi kuachia Remix ya album hiyo kabla ya kumalizika mwaka 2010 kuhakikisha kwamba washabiki na wadau wa mziki wanapata mdundo wenye kuleta "Raha" katika burudani ya mziki.

Buti Jiwe amewaomba wadau na washabiki wa mziki walio ndani na nje ya Bongo kukaa mkao wa kula!!

Wakati huo huo CD za Buti Jiwe zinahitaji pia
msambazaji mzalendo,atakaye sambaza CDs katika nchi za afrika mashariki.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...