Diwani wa kata ya Kiusa ,manispaa ya Moshi Athuman Ramole (CCM) akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani akitangaza nia ya kugombea jimbo moshi mjini. Picha na habari na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii kanda ya Kaskazini

DIWANI wa kata ya Kiusa,katika manispaa ya Moshi, Athuman Ramole (CCM) maarufu kwa jina la ‘Buni’,ametangaza kumng’oa mbunge wa jimbo la Moshi mjini Philemoni Ndesamburo katika kinyang’anyiro cha kugombea ubunge wa jimbo hilo.

Hatua hiyo ya Ramole kutangaza nia yake hiyo imekuja miezi michache baada ya wanachama na makada wa chama hicho tawala wengine wanne kutangaza nia yao hiyo ya kutaka kumuondoa Ndesamburo ambaye anaongoza kwa miaka 10 sasa.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Moshi Ramole ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya maadili katika baraza la madiwani wa manispaa ya Moshi na mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM mkoa wa Kilimanjaro alieleza dhamira yake kuu ni kutetea maslahi ya wananchi.
Ramole ambaye pia ni mfanyabiashara mashuhuri mjini hapa alisema mbali na kutetea maslahi ya wananchi pia ameahidi kusimamia na kudhibiti mikataba isiyokuwa na maslahi kwa umma inayoingiwa baina ya serikali ,halmashauri na wawekezaji.

“Kitu cha kwanza ambacho nategemea kufanya pindi nitakapo pewa ridhaa na chama changu na wananchi wakaamua kunichagua nitahahakikisha hakuna mikataba yoyote itakayoingiwa na halmashauri yetu, ambayo haitakuwa na maslahi ya umma”, alisema Ramole.
Akionyesha kuguswa na sula la wafanyabiashara ndogondogo maarufu kama wamamchinga Ramole alisema tatizo la ajira kwa vijana ni sehemu ya mambo ambayo angependa kuyashughulikia pindi atakapo pata nafasi.

“Katika hili nategemea kufanya mapinduzi makubwa ya kimaendeleo katika nyanja za viwanda, ajira, utalii na biashara kwa kufufua viwanda ambavyo vitasaidia kupungu8za tatizo la ajira kwa wakazi wa Moshi”alisema Ramole.
Wengine walikwisha tangaza nia ya kuwania ubunge katika jimbo la Moshi mjini ni mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi mkoa wa Kilimanjaro Thomas Ngawaiya, aliyekuwa mhasibu mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Gipson Lyamuya na mwenyekiti wa chama cha walemavu mkoa wa Kilimanjaro Batista Mwindivita.
Jimbo la Moshi mjini linatizamwa kwa mapana kisiasa, baada ya kushikiliwa na upinzani tangu kuitishwa kwa uchaguzi mkuu uliofanyika katika wa vyama vingi mwaka 1995.
Miongoni mwa wabunge wa upinzani waliowahi kuliongoza jimbo hilo ni pamoja na Joseph Mtui, aliyechaguliwa kwa tiketi ya NCCR-Mageuzi kati ya mwaka 1995 hadi 2000 na badaye Philemon Ndesamburo, kati ya mwaka 2000 hadi sasa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 22, 2010

    Tout le Monde Makida Makida, anacheza Makida Makida.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 23, 2010

    nina kutakia kila la kheri buni. ulionyesha upendo wako kwa mji wa moshi ulipo kaa pembeni wakati mafisadi walipotaka kuwacha uwanja wa mapumziko wa moshi utumiwe kama security ya kupata mkopo kutoka bank.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...