Mkurugenzi Mtendaji wa Global Publishers & General Enterprises Ltd na mjasiriamali, Bw. Eric Shigongo, anatarajiwa kuhutubia nchini Marekani katika Mkutano maalum ulioandaliwa na Watanzania waishio nchini humo (Diaspora Council of Tanzanians in America - DICOTA).
Katika mkutano huo unaotarajiwa kufanyika kwa muda wa siku nne kuanzia Julai 1, mwaka huu katika jiji la Minneapolis, Marriott Hotel, Minnesota, Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mh. Aman Abeid Karume, amealikwa kuwa mgeni rasmi. Viongozi wengine watakaohudhuria mkutano huo ni pamoja na maofisa waandamizi na wafanyabishara wakubwa kutoka Serikali ya Tanzania na Marekani.
Aidha, Mwenyekiti Mtendaji wa makampuni ya IPP, Bw. Reginald Abraham Mengi, naye ni miongoni mwa wageni waalikwa wa mkutano huo ambao unafanyika kwa mara ya pili nchini humo ukiwakutanisha Watanzania waishio ughaibuni. Mada mbalimbali zitatolewa na Watanzania waishio ndani na nje ya Marekani.
Mwenyekiti Mtendaji wa Globu ya Jamii, Ankal, naye anategemewa kuwepo kwenye mkutano huu ambao ripoti zinasema watu kibao wamejianddikisha kuhudhuria na wengine wanaendelea kumiminika.
Katika mkutano huo, Bw. Shigongo anatarajiwa kutoa mada itakayoelezea jinsi ya kufanikiwa kiuchumi katika mazingira ya Tanzania na anatarajiwa kuwahamasisha Watanzania waishio ughaibuni kuwekeza nyumbani Tanzania.
Katika siku za hivi karibuni, Bw. Shigongo amejipatia umaarufu kwa kutoa elimu, ushauri kwa vijana na wanafunzi wa shule za msingi, sekondari na vyuo vikuu nchini kupitia mikutano na hafla mbalimbali anazoandaa au kualikwa kwa lengo la kutoa elimu ya ujasiriamali kwa vijana wa kitanzania.
Jamani mnyonge mnyongeni ila haki yake mpeni jamani....HILI JIANAMUME NI BONGE LA HANDSOME!!!
ReplyDeleteJamani mie kwa ziada tu hebu Marry Raphael muandalie huyo baba nguo za maana asije akatuaibisha huko kwa watu. Siunajua hawa ndio walokole waliobaki
ReplyDeleteEbwana Shigongo mbona mtandao wako wa Global publisher haupatikani hewani umeubadilisha au umeamua kuufunga.
ReplyDeleteKwa yeyote anayejua jamani kwani namiss hadith zake.
mdau UK.
haya bwana shigongo hongera sana.mallesa hapa.
ReplyDeleteMdau hapo juu uko wapi usiupate mtandao wa Global wakati uko hewani 24/7?...hebu cheki hapa:http://www.globalpublishers.info au hapa http://www.globalpublisherstz.com vyovyote unaupata tu tena kwa sana...
ReplyDeleteKongamano la watanzania waliopo Marekani. Habari njema hizi.Rais, Mawaziri huwa na mikutano kama hii, wanapokuja. Na huwachagua idadi na watu waliopangwa kuuliza maswali. Cha kusikitisha, Wengi wenye hoja za haja hutupwa.Hii, inanukuia harufu ya vacation fulani hivi. Swali la kizushi: Kwa nini mkutano usifanyike Kenya si kuna Diaspora ya Watanzania?
ReplyDeleteHaya tunaomba agenda mapema na ripoti ya:
1. Mikakati ya kutokomeza rushwa, ujanja ujanja na ufisadi.
2. Uwajibikaji ktk ofisi za umma.
3. Nishati:Uhakika na upatikanaji muafaka wa maji,umeme,mafuta ya magari na yale ya kuendeshea mitambo, pamoja na gesi asilia.
4. Kwa nini Tanzania inabaki kuwa maskini, hali huduma duni: afya, ustawi wa jamii, elimu na upatikanaji wa fursa mbalimbali.
Mdau
US