Global Publishers, wachapishaji wa magazeti pendwa nchini, leo Alhamis
wametembelea wodi ya watoto wadogo wenye matatizo ya kuvimba vichwa
(Hydrocephalus), na kutoa misaada ya kibianadamu kama vile sabuni,
mafuta ya kujipaka, pampers, Dettol, nk. Wodi hiyo iko ndani ya
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na ina takriban watoto 30 wenye
matatizo hayo, na wengi wao wanatoka nje ya Dar es salaam.
Jambo la kusikitisha kuhusu watoto hawa, wengi wao baada ya kuzaliwa
wamesuswa na akina baba hivyo mzigo wote kuachiwa akina mama. Kutokana
na kutokuwa na ndugu katika jiji la Dar es salaam, akina mama hao
hukosa mahitaji muhimu hata ya sabuni kwa ajili ya kufua nguo za
watoto wao ambao hujisaidia haja ndogo na kubwa kila wakati wakiwa
kitandani.
Ingawa serikali inatoa huduma ya chakula na matibabu kwa watoto hao
bure na chakula kwa wazazi wao, ambao hulazimika nao kukaa wodini na
watoto wao, lakini wanahitaji misaada ya kibanadamu kwa wingi, kwani
hali ni mbaya, na wakati mwinginehukosa hata kipande cha sababu cha
kufua mikojo ya watoto wao. Wito unataolewa kwa wadau wengine
kuwakumbuka akina mama hawa.
Aiddha, Global Publishers imetoa misaada ya chakula na bidhaa zingine
za usafi kwa wanafunzi walemavu wa shule ya Sekondari ya Jangwani
jijini Dar es salaam, ambao nao hupata huduma mbalimbali za matibabu
katika Hospitali hiyo ya Taifa.

Wanafunzi hao, ambao wako kidato cha kwanza hadi cha nne, wote ni
walemavu na wanatembelea viti vya magurudumu. Nao wanahitaji sana
misaada ya kibinadamu.
walemavu na wanatembelea viti vya magurudumu. Nao wanahitaji sana
misaada ya kibinadamu.
.jpg)
Global Publishers kwa mgonjwa mmoja wa wagonjwa
.jpg)
Bw. Abdallah Mrisho akimsukuma mmoja
wa wagonjwa kuelekea kwenye hafla
nani kama mama? jamani machozi yamenitoka nilivyomwangalia huyo mama kashika mwanae na utamwona kama anamawazo ya mbali vile......Kweli usipompenda na kumweshimu mama yako utalaaniwa sana...
ReplyDeleteNawapongeza sana GPL Mungu awazidishie sana, kuna baadhi ya wadau tungependa kuchangia hata Tsh.50 ingesaidia japo kwa sabuni na sukari ya kuweka kwenye uji wa mtoto, Tatizo ni kwamba zitafikaje hizo pesa/msaada kwa walengwa? naomba kaka mithupu futilia kwa hilo au jaribu kuwasiliana na GPL
ReplyDeleteGlobal Publishers mfano wa kuigwa. Lakini halahala isiwe ni katika kuelekea oktoba..kwani kuna kautamaduni hako ka watu wenye nia za kisiasa kuanzia kwa jamii ili wavute imani za wapiga kura
ReplyDeletepoleni sana akina mama mnaouguza hao watoto wenye matatizo ya vichwa,na pia nawapa hongera sana kampuni ya global publisher kwa kuonyesha kujali hao watoto,Mungu atawarudishia pale mlipopunguza,je na sisi wananchi wa kawaida tukitaka kuchangia walau kidogo tulichonacho utaratibu ukoje?ancle michuzi naomba jibu
ReplyDeleteBig up global publisher. kwa kweli huo ni mfano wa kuigwa. Je mna namna yeyeto ya watu kuweza kuchangia ili wawa-support kwa hilo?
ReplyDeletenoma zaidi ni pale issue hii ilivyowekwa sanjari na hoja za bajeti ya serikali¬!!!
ReplyDelete