Mkurugenzi wa Mauzo,Huduma za kabla na Usambazaji wa Vodacom Tanzania,Exaud Kiwali(kulia) akielezea njia mbadala za kuweza kuchangia kutuma fedha kwa kutumia huduma ya M-Pesa kwenda 300100 kwa ajili ya Mamlaka ya Elimu Tanzania na fedha hizo kuweza kuendeleza elimu nchini hususani kwa wanafunzi wasiojiweza.(katikati)Mkurugenzi wa Uhamasishaji na Ukuzaji Rasilimali wa Mamlaka ya Elimu Tanzania,(kushoto)Meneja Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Nector P.Foya
Mkurugenzi wa Mauzo,Huduma za kabla na Usambazaji wa Vodacom Tanzania,Exaud Kiwali(kulia) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari wakati wa kuzindua kampeni ya kuchangia fedha kwa Mamlaka ya Elimu Tanzania kupitia huduma ya M-Pesa kwa kutuma mchango wake kwenda 300100 kwa ajili ya kuweza kuwasaidia watoto wasiojiweza,(kushoto)Mkurugenzi wa Uhamasishaji na Ukuzaji Rasilimali wa Mamlaka ya Elimu Tanzania.
KAMPUNI ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania imeingia makubaliano na Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) ambapo wananchi sasa wataweza kuchangia maendeleo ya elimu nchini kupitia huduma ya Vodafone M-Pesa.

Mkurugenzi wa Mauzo, Huduma za Kabla na Usambazaji wa Vodacom, Exaud Kiwali alisema jana kuwa mpango huo umefikiwa baada ya Vodacom Tanzania kuingia mkataba wa ushirikiano kati yake na TEA.

Vodafone M-Pesa ni huduma ya kutuma na kupokea pesa kwa kutumia simu za mkononi ambayo hutolewa na Vodacom Tanzania kwa wateja wake kwenda mtandao mwengine wowote Tanzania.

Kiwali alisema kwamba mteja wa Vodacom aliyejisajili na huduma ya Vodafone M-Pesa sasa anaweza kuchangia fedha kwa kutuma mchango wake kwenda namba 300100.
Alisema mpango huo ni sehemu ya mkakati wa Vodacom Tanzania wa kusaidia jamii katika sekta ya maendeleo ya elimu.

“Ikumbukwe kwamba hivi sasa Vodacom Tanzania kupitia Mfuko wake wa kusaidia jamii (Vodacom Foundation) ina programu maalum ya kukuza elimu na kupitia mfuko huo inatoa kompyuta na madawati pamoja na kujenga madarasa ya shule mbalimbali za sekondari hapa nchini”, alisema.

Vodacom Tanzania ina mkakati wa kuendelea kushirikiana na wadau mbalimbali wa elimu hapa nchini ili kukuza na kuboresha kiwango cha elimu.

Kwa kutumia huduma ya Vodafone M-Pesa, uchangiaji wa maendeleo ya elimu hivi sasa utakua umefanywa rahisi na Kiwali alitoa wito kwa Watanzania kutumia ipasavyo mpango huu.

Naye Mkurugenzi wa Uhamasishaji na Ukuzaji Rasilimali wa Mamlaka ya elimu Tanzania Seif Mohamed aliishukuru Vodacom Tanzania kwa ushirikiano huo ambao alisema una lenga kukuza kiwango cha elimu hapa Tanzania.

“Kupitia huduma ya M- PESA, wachangiaji wa maendeleo ya elimu wataweza kuchangia moja kwa moja bila makato yeyote kwa mchangiaji au mpokeaji”, alisema.

Alisema kwa kuanzia michango yote itakwenda katika kampeni maalum ya kuchangia wanafunzi wenye ulemavu inayoendeshwa na mamlaka hiyo.

Mpango huu utawezesha watanzania wengi kushiriki kuchangia maendeleo ya elimu nchini popote walipo kupitia M-PESA.

‘Vodacom na Mamlaka ya Elimu Tanzania inawaomba watumiaji wa mtandao huo, kushiriki katika kampeni hii kwa kuchangia kupitia M-PESA”, alisistiza

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 17, 2010

    Jamani wanababa wabongo angalieni diet zenu.kila nikiangali picha nyingi vijana wadogo wanono wanono sana. Not healthy kwa kweli. Halafu mtu akianguka ghafla oh kaupiwa jini... sababu tulikuwa nae jana alikuwa mzima wa afya. Kumbe high cholestrol, duabetic..anatembea navyo hajui. Mambo ya kunenepa ni ishara ya pesa yamepita na wakati. Physical fit ndio in thing. kha!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 17, 2010

    Ni asilimia ngapi za mchango zitaenda direct kwa walengwa na ngapi sitaenda kwenye administration...Nadhani mngeweka hii ili kila mtu ajue akichangia hapo.

    Michango hii huku tuliko haifanywi na kampuni za kibiashara kabisa...Hizi zinatakiwa kufanywa na non profit organizations tu. Watu watachanga michango yao but at the end of the day kila kitakachopelekwa kitakua na label ya Vodacom..Hapo ukumbuke hii ni kampuni ya kibiashara hivyo wakilabel hiyo misaada ni wanajitangaza (advertising)na pia hamna atakayejua kuwa kuna watu wengine walichangia hiyo msaada na hata kwenye vitabu vyao vya kodi itakua ngumu kutofautisha donation na mapato. Na kama kampuni la kibiashara sielewi kuwa linaruhusiwa kukusanya donation. Na wafanyakazi watakao shughulikia hii mishango watalipwaje? ...Oh well kwa vile Tanzania hakuna sheria na wala Kodi haieleweki kwa hiyo kila mtu anajifanyia analotaka.......

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 17, 2010

    I second you mtoa maoni wa kwanza..Watu waelimishwe hili. Wakimwona MO namahela yake lakini mwembamba labda wanazania ubishoo...kwetu ile mentality ya unene ni afya sijui itaisha lini...Kila siku heart attacks tu halafu wababa wadogo wadogo...

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 17, 2010

    Hata mimi nimefikiri hii ingekua ni major disaster imetokea ningewaunga mkono kufungua hii number. Hili tatizo nila muda mrefu hivyo kulichangia kwa simu ni kwa muda mfupi tu au...

    ReplyDelete
  5. pilipili shambaniJune 18, 2010

    unene wetu unakuhusu nini? kwanza umesikia sisi ni modal? hoja ya hapa ni uchangiaji wa elimu. kama unataka mambo ya umodo nenda ukakutane na vidosho wenzako kina remtula na hasanali.

    kwanza hati ataki zetu wewe zina hu???

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 18, 2010

    tunashukuru sana vodacom kwa michango yenu mimi na wakubali TEA la Walemavu sasa hivi ni zaidi ya madaftari ni zaid ya kalamu na vitamu mimi sina ulemavu lakin ninafanya kazi katika mashirika ya watu wenye ulemavu kwa hiyo nayaelewa sana maswala yao hata kama ukiwanunulia madaftari kama miundo mbinu ya kuwafikisha shuleni bado ni duni huyo mtoto atakipataje hicho ktabu? hata kama mkimpa wheel chair lakin shule anayosoma imejaa ngazi mserereko wheelchair hiyo haitamfaa itabidi atambae aende darasani na je akiwa shule choo cha shule kimejengwa kukidhi mahitaji ya mlemavu wa viungo? najua mtasema special school sasa hivi hawazitaki tena kwani zinaongeza ubaguzi na wazazi wengine wakiwapeleka watoto huku wanawatelekeza shule zikifungwa hawaendi kuwachukua kuna viziwi walimu wao wa lagha ya alama hawatoshi machapisho au vitabu vya nukta tundu kwa ajili ya wasioona havitoshi pia kwa hiyo katika mgao zingatieni hilo

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...