Hayati Profesa Haroub Othman

Wiki hii tunatimiza mwaka (kwa tarehe za kiarabu) tangu mzee wetu Haroub Othman atangulie mbele za haki. Wanafamilia, ndugu, jamaa na marafiki tutakua na kisomo (hitma) katika Msikiti Ngazija siku ya Alkhamis kuanzia saa 11 alasiri. Kwa kupitia blogu yako naomba kuwakaribisha wote watakaoweza kuhudhuria.

Kwa wale walio mbali nasi basi nawaomba msimsahau mzee wetu katika Du'a zenu. Kwa walioko Zanzibar hitma itasomwa tarehe 26 mwezi huu, taarifa za muda na msikiti zitatolewa baadae.


Natanguliza shukurani
zangu na nakutakieni wiki njema.
Tahir H. Othman

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 17 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 14, 2010

    Ni Mwaka mmoja tangu ututoke majonzi na uchungu bado tunayo utadhani msiba ulikuwa jana tu.Inshaallah Mwenyezi Mungu atakupa maghfira na atajalia kaburi lako liwe bustani katika bustani za peponi.Amin.
    I REALLY MISS U UNCLE!!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 14, 2010

    Unajua mimi sikufahamu kama Prof Haroub alikuwa Mwarabu kwa muda wa miaka minne yote niliyosoma pale UD. Nimejua leo pale mwanae alposema kuwa ni mwaka mmoja wa kiarabu tangu afariki ili tusome hitma. Mwenyezi Mungu aendelee kuipumzisha roho ya Prof pahala pema.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 14, 2010

    mdau acha fitna kwenye mambo ya kuwa serius,wapi imeandikwa alikuwa muarabu,umeambiwa kwa mwaka wackiarabu,ambao waislam ndo wanafata,kama ilivyo kwa wakiristu kufata mwaka wa kizungu,na wachina wana mwaka wao,thailand na nchi nyingi pamoja na dini tofauti zinatofautiana mwaka.sasa unaposema hivyo tukuelewaje,think before u talk,rest in peace profesa.ammen

    ReplyDelete
  4. Hadj Drogba "mwana chelsea"June 14, 2010

    Ni mwaka mmoja tangu TANZANIA Impoteze mwanazuoni wa hali ya juu kabisa.Tutakukumbuka daima profesa,mbele yetu nyuma yako profesa HAROUB OTHMAN,Wewe ulikua kisima cha elimu ambapo wengi wamechota,umetuachia urithi wa hekima na busara.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 14, 2010

    kufuata tarehe ya kiarabu sio maana kwamba Prof alikuwa Mwarabu. Maana yake wanafuata kalenda ya kiislam.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 14, 2010

    Kusema mwaka wa kiarabu haimainishi moja kwa moja kuwa Prof. Othman H. alikuwa mwarabu. Alivyoitoa ni reference tu ya kuhesabia na si lazima iwe kama unavyofikiria.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 14, 2010

    Angetumia tarehe ya kalenda ya kiislamu. Hivi Tanzania inamkakati gani wa kupika kizazi hiki ili tuweze kuwapata watu kama Marehemu Prof Haroub?
    Tunamuombea na inshallah Mwenyezi Mungu ampumzishe pema.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 14, 2010

    mtoa comments wapili, kusema tarehe za kiarabu hakumaanisaha ni muarabu , kawaida waislam tunatarehe zetu za kiislam sio hizi zinazotumika kawaida nasio kuitwa kwa kiarabu ni maandishi tu na kwa ilivyozoeleaka lakni ni kwaida huitwa ni tarehe ya kiislam. ndio maana kufunga kwa ramadhani na sikukuu za kiislam always zinachange kutoka na hizo tarehe.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 14, 2010

    Ni kwa majonzi makubwa sana tunamkumbuka Prof wetu na kwa sisi tuliomjua kidogo alikuwa binadamu mwema sana, na kichwa cha kweli.

    Tahir hebu tusaidie hapa kwani Prof alikuwa Mwarabu...? Mi sidhani maana sikuwahi ona maumbile yoyote ya Kiarabu katika mwonekano wake. Au wewe Tahir ndio umependelea kuitoa hiyo kalenda kiarabu..?

    Mungu amuweka pema peponi Mwanamapinduzi msomi wetu.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 14, 2010

    Mtume wa mwisho Muhammad S.A.W anasema anayeongea Kiarabu ni Mwarabu..uwe mweusi mweupe, na menginyo wewe ni Mwarabu.Ama kuhusu tarehe hizo zinazoitwa za Kiarabu ni Tarehe za Kiisilamu au Hijiria yaani mwaka kuanzia Mtume Muhammad(S.A.W) Alipohama Makkah kuelekea Madiinah ndio karne ya Kiisilamu ilipoanziana mwaka huu wa Kiisilamu huenda kwa mwendo wa Mwezi(mwezi mwandamo)kutofautisha na ule mwaka wa Kikiristo(Gregorian) ambao huendana na mwenendo wa Jua.
    Masuala mengi ya Kiisilamu huendana na tarehe hizi za Kiisilamu, kama ilivyo Marehemu Prof.Haroub Othman alikuwa Muisilamu na Uisilamu hutangulia kwanza kabla ya weusi/Uafrika kwa mtu mwenye kuzingatia.
    Khamis Hassan Batanyaga

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 14, 2010

    We anonymous wa Mon Jun 14, 12:53:00 PM.

    Kwani wanatumia mwaka wa kizungu(kalenda ya kizungu)kama wewe, ni wazungu? kwa habari yako kuna kalenda nyingi sana duniani, inategenea umechagua ipi. Kila mtu ana uhuru wa kutumia kalenda anayotaka.

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 14, 2010

    Nadhani mtoto wa Marehemu alikosea hapo juu kuandika, aliandika imefikia mwaka mmoja kwa tarehe za Kiarabu. ilipaswa kuandika kwa tarehe za Kiislamu, kama sijakosea huo ni mtizamo wangu. RIP Comrade.
    mdau Pakacha UK.

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 14, 2010

    Brother Michuzi,
    nashukuru sana kwa kuniwekea hili tangazo. Kwa kuwa mimi ni mdau wa blogu yako nilitaraji huu mjadala ungetokea kwa kuwa ni kawaida ya mabandiko yote. Ifahamike kuwa mimi si mtaalamu wa lugha na dhumuni langu ni kuwatangazia marafiki kuhusu hitma ya mzee kwa njia nyepesi na ya haraka. Mjadala wa kama tarehe ni ya kiarabu au kiislamu (ingawa sina uhakika kama waarabu wakristo wanatumia tarehe tofauti) nitawaachia TUKI, Bakita na wadau.

    tahir

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 15, 2010

    Oh my God, hata sikujua kama Prof. Othman amefariki!!! Kila ninapokumbuka enzi zangu pale mlimani namuwaza pia, kumbe hata hayupo nasi tena maskini! Poleni sana kwa msiba wanafamilia, ndugu, marafiki na Watanzania wote kwa ujumla, huyu alikuwa msomi muhimu sana nchini na nje ya nchi! Mungu ailaze pema peponi roho yake, na awatie nguvu wote mlioumizwa na kifo chake moja kwa moja!

    ReplyDelete
  15. AnonymousJune 15, 2010

    Allahuma firlahu, waarhamahu waaskanahul filjanna.

    (US Blogger)

    ReplyDelete
  16. AnonymousJune 15, 2010

    Mchangiaji wa pili, Hapa duniani kuna KALENDA TANO KUU zinazoashiria MIEZI NA MIAKA: (1) Gregorian Calendar, yaani kalenda ya kizungu, ambayo inatumika zaidi na mwaka mmoja ni mzunguko wa sayari yetu (planet earth) kuizunguka jua (wastani wa siku 365 na robo). (2) Kalenda ya pili ni kalenda ya HIJRA ambayo ndiyo ya Kiislamu. Hii inafuata mzunguko wa mwezi kuuzunguka dunia. Ina miezi 12 na, kwa wastani, ina siku 12 chache zaidi ya mwaka wa kizungu. Waislamu hutumia kalenda hii katika funga ya Ramadhani, n.k. (3) Kalenda ya Kichina (4) Kalenda ya Bani Israil ambayo ilikuwa ni kama kalenda ya hijra hadi hapo walipoamua waufanye mwaka wao uwe na siku 365 hivyo wakaongeza siku 12 katika mwezi mmoja wa mwisho wa mwaka. Wahabeshi wa Ethiopia pia waliamua kuunda mwezi wa 13 ili mwaka wao uwe na siku 365. (5) Mwaka wa kiajemi (Persian) (siku hizi Iran) ambao unaanza na sherehe za Nauroz. Unguja na Pemba Washirazi wa pwani na vijijini bado huadhimisha siku hii kwa KUKOGA MWAKA. Baada ya maelezo haya, nachukua fursa hii kuwapa pole Auntie Saida, Tahir na familia yote ya Prof. Haroub na kumwomba Muumba amlaze mahali pema peponi. Amin.

    ReplyDelete
  17. AnonymousJune 15, 2010

    Mchangiaji wa pili. Wahenga wamesema, kuuliza si ujinga. Kama hujui kitu bora uulize uelimishwe. Nadhani hapa si forum ya wewe kuonyesha chuki na prejudices zako. Kama una principles zozote au heshima cha kufanya ni wewe kuomba msamaha (hii si zeutamu)kwa comments zako zisizokuwa na kichwa wala miguu. Profesa H Othman we will never forget you. Asante kwa kutuelimisha, uzalendo wako na utetezi wako wa wanyonge kupitia legal aid programme yako. You made a difference. RIP!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...