Rais wa Hope 2 Others Karen Klemp na Rick Klemp wakisoma risala yao wakati wa makabidhiano ya ufunguo wa hii ambulance. Hope 2 Others ni shirika lisilo la kiserikali lenye mako makuu yake Winscosin na linafanya kazi katika nchi za Tanzania na Guatemala.
Kabla ya kuzungumza na wageni waliohudhuria makabidhiano ya gari hili la wagonjwa Joel Mburu anaonekana akionesha ufunguo wa gari alioupokea kutoka wa Meya wa Sun Prairie Bwana Joe Chase, akiwepo pia Kep Anderson mkuu wa kitengo cha EMS. Hii gari itakatumwa Tanzania katika kipindi cha kati ya wiki mbili hadi tatu na itakuwa katika mji wa Arusha.
Joel Mburu, akiwa mbele ya gari ya kubebea wagojwa iliyotolewa kwa shirika la Hope 2 Other kutoka mji wa Sun Prairie Jimbo la Winscosin kwa ajili ya New Life Band. Watu wengine kwenye picha ni pamoja na Meya wa Sun Prairie, Joe Chase, Rais wa Hope 2 Others, Karen Klemp pamoja na Makamu wa Rais Rick Klemp.Wengine ni walimu na wanfunzi wa Sun Prairie na shule zingine zavitongoji vya Sun Prairie
Joel Mburu, akiwa mbele ya gari ya kubebea wagojwa iliyotolewa kwa shirika la Hope 2 Other kutoka mji wa Sun Prairie Jimbo la Winscosin kwa ajili ya New Life Band. Watu wengine kwenye picha ni pamoja na Meya wa Sun Prairie, Joe Chase, Rais wa Hope 2 Others, Karen Klemp pamoja na Makamu wa Rais Rick Klemp.






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 08, 2010

    JAMANI BENDERA YETU KILA SIKKU INAPINDULIWA KWA NINI HAWASIKII?

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 08, 2010

    Mzee za kazi! nakushukuru sana kwa hii blog yako, kwa kweli blog nyingine zote wanafunga tera kwa hii ya kwako.

    Mimi naomba kujua kupitia kwako na kwa wanajamii nzima amabao wanatembelea blog hii.

    Ni kwa nini hapa nchini misaada mingi ya wafadhili huelekezwa baadhi ya mikoa tu ni si mikoa yote kwa ujumla?

    Je? Ni michakato gani hufanyika ili msaada uende mkoa au woilaya husika?

    manake inauma sana, mikoa mingine iko nyuma, kwa kila kitu hata hinyo vimisaada havifiki. jamani naomba tusaidieni tanzania ni yetu sote,

    nawasilisha,

    Mdau.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 08, 2010

    litumike kweli tu hilo gari,wasije kulifanya dala dala tu au kuwatoza nauli wagonjwa kwani hata polisi nao si wana magari?,we wapigie simu kama unatatizo ,watakwambia hawana mafuta.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 08, 2010

    Siku nyingine wakumbuke kutoweka bendera upside down.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 08, 2010

    Well done kaka Joel, kazi nzuri ni mfano wa kuigwa

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 08, 2010

    Garfi? ama kweli sasa!!

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 09, 2010

    Sawa tunashukuru kwa msaada na sisi pia tuchangie kuhifadhi gari hili ili liweze ksaidia watu wengi kwa muda mrefu sana.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 09, 2010

    mnaopiga kelele juu ya bendera kupinduliwa hebu tuelimisheni hapa. mnataka rangi gani iwe juu? mnataka mistari ya njano ielekee upande gani? ni wapi inaposema kuwa ni kosa mtu kuweka bendera namna walivyoiweka hawa hapa?

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 09, 2010

    Gari poa ila nafikiri wese linamwagika vilivyo. Juu ya bendera: Wao wamatuzawadia gari, bendera ni sie wenyewe tumepindua.
    Blackmpingo

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 09, 2010

    Litabeba cement za bosi na kuzipeleka site ya nyumba yake. Litakuwa linaonekana nje ya bar jioni. Watanzania nawajua sana.

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 09, 2010

    Kaka Michuzi,
    Nasisitiza tena ujumbe kwa wanaoshika bendera ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kupiga nayo picha wazingatie inavyotakiwa kushikwa. hii ni pamoja na wanaotaka kuichora au kutumia rangi zake.
    Umeibana komenti yangu naomba na hii usiibane. I am serious about how pipo handle our national flag...Thank You
    "Mzee wa Serious Issue"

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 09, 2010

    unyeuliza suala la misaada kwenda sehemu moja umesahau ile methali inasema muamba ngozi huvutia kwake? Ni kuwa hao wanaokwenda kutafuta hiyo misaada wanatokea sehemu hizo na huwezi jua hawajawahi kufika huko unakotaka misaada ifiki hawajui kuna shida huko pia ua hata kama kuna watu wanaishi hizo sehebu. Unajua kuna watoto waishi oyesterbay hawajawahi kuingia na kuona nyumba ya makuti ikoje zaidi ya hizo za makumbusho? Akitoka nje ya nchi akienda kuomba misaada ataombea sehemu aliyoishi tu....

    Jitahidini huku kijijini kwenu mpeleke kijana wenu akasome akifika huko ataweza kuwatafutia misaada.

    Ila mimi sifagilii hii misaada basi tu...Hilo gari tungeweza kulinunua peke yetu kama tungeamua...Tumezoea kusubiri watu watuletee tu na kuzania kuwa wao wanazo nyingi kuliko sisi. Yaani wao wakienda kwa bank ni kuchota tu hela ndio tunavyofikiri..Unazania hao hapo kwenye picha tunaowaona wanamaisha ya juu sana kuliko raia wa kawaida wa bongo? Wala ni watu wakaida tu lakini wamejichangisha na wengine hata kuuza vitu vyao ambavyo hawavitumii tena kuraise fund. Na watoto wengine huwa hata wanauza lemmon juice ...tuanzage moyo wa kujichangisha na kujituma.Halfu vyakupewa havidumu na hatuvitunzi kwa vile hatujatoa hela na hatuna uchungu nao. hilo gari utaliona linavyobondwa tu . kama tungepay wenyewe tungejua kulitunza vizuri..

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...