akisalimiana na baadhi ya wauguzi na wafanyakazi wa hospitali ya Maweni wakati wa uzinduzi wa Maabara ya uhifadhi Damu Salama jana mchana.
Mwakilishi kutoka wizara ya Afya Dr.Pamela Sawa akimpa Rais Jakaya mrisho Kikwete maelezo ya uhifadhi wa damu Salama katika mabara ya kisasa katika hospitali ya Maweni mjini Kigoma muda mfupi baada ya Rais kuifungua maabara hiyo jana mchana
(picha na Freddy Maro)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 16, 2010

    Duh Muheshimiwaaaaaaaaaa, hatimae umeenda kigoma, Kati ya mikoa ambayo iko nyuma kimaendeleo Tz ni Kigoma, mpaka leo barabara moja ya lami, Maji na umeme wanasoma magazetini ingawa kuna chanzo kizuri cha umeme kutoka lake Tanganyika , hata sijui tatizo nini??
    Mi nadhani Mhashimiwa amepita kule kwakuwa ule wakati unakaribi!!!

    ReplyDelete
  2. Tunashukuru kwamba Raisi amefungua maabara hiyo ya kisasa lakini kwa jinsi mkoa wetu wa Kigoma ulivyoachwa nyuma bila huduma muhimu za kijamii ikiwemo umeme mi naona ni kazi bure maana itafika wakati hiyo maabara itashindwa kufanya kazi kwa vile umeme hautakuwepo. maana hata hicho chanzo tulichokitegemea kutoka mto Malagarasi jamaa wa Millenium challenge wametoa nje.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 16, 2010

    SERIKALI YA JK INAYAJUA VIZURI MATATIZO YA MKOA WA KIGOMA ILA INAFANYA KIBURI TU KUYATEKELEZA NA SI KIGOMA TU TZZ IMEJAA MATATIZO LUKUKI,IPO SIKU WANANCHI WATAFANYA MAAMUZI YA TOFAUTI,KWANI SI MSAFARA WAKE USHAWAHI KURUSHIWA MAWE??????? PIPO WAMECHOKA

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 16, 2010

    Kweli kombe la dunia liko juu. jamaa hata maoni hawatoi siku hizi. Jamani, kwa yule anaesema kigoma maji na umeme wanavisoma magazetini nafikiri haijui kigoma. Hali sio mbaya kiasi hicho siku hizi, Kigoma iko nyuma lakini inasogea kidogo kidogo: sio kweli kuwa barabara yenye lami Kigoma ni moja: anaesema hivyo haijui Kigoma. Wawekezaji wa ndani na nje msikatishwe tamaa: karibuni. Kigoma ya miaka mitano iliyopita sio kigoma ya sasa.. kumbukeni pia msafara uliorushiwa mawe sio wa Kikwete, ni wa Mkapa. Nawashukuru na kuwapongeza vijana wa "urusi" kigoma kwa mchango wao wa masuala yahusuyo maendeleo: mko juu na mko creative: ikiwezekana wana kigoma waweke record ya maoni ya "urusi" na yasambazwe kwa wengi watu waone jinsi ndugu wa Kigoma walivyo ... kigoma haiko nyuma kiasi wengi wanavyofikiria.. tembea ujionee

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...