akikata utepe kufungua rasmi hoteli ya Lake Tanganyika mjini Kigoma leo mchana.Kushoto ni Mmiliki wa hoteli hiyo Bwana George Nzunda na kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Kanali Simbakalia. akisalimiana na Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe muda mfupi baada ya kuwasili mjini Kigoma leo mchana tayari kwa ziara ya kikazi ya siku mbili.Kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Kigoma Kanali Simbakalia.
akisalimiana na baadhi ya wafanyakazi wa Hoteli ya Lake Tanganyika mjini Kigoma muda mfupi baada ya kuifungua leo mchana.
akikagua mandhari ya Hoteli ya Lake Tanganyika muda mfupi baada ya kuifungua mjini Kigoma leo mchana.Kulia ni Mmiliki wa Hoteli hiyo Bwana George Nzunda na katikati ni Mkuu wa Mkoa wa kigoma Kanali Simbakalia.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 15, 2010

    Finally muheshimiwa rais amefika Kigoma kuwaona wakina brozer K. Kweli uchaguzi nuksi! Harudi tena hapo mpaka atakapomaliza urasi wake 2015, labda.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 15, 2010

    Jk ni bonge la president,unajua kitu kikubwa kwa binadamu ni kujichanganya,zitoo 2days ago aliwasha moto bungeni na kumsakama JK kwa kujenga chuo kikuu dodoma kuwa ameiba sera ya chadema,lakini leo kikwete wanacheka na kufurahi,huo ndo uongozi,sio marais wengine wa africa ukiwalogelea tu utazushiwa kila kesi,nadhani polisi wetu waige mfano wa rais kipindi cha uchaguzi,sio waanze kupiga upinzani ovyo

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 16, 2010

    Rais apenda raha kupita kiasi. Ashughulikie mambo ya maana kufungua hoteli sio kazi yake, mambo gani hii!!!!

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 16, 2010

    Mambo hayo wana Kigoma. Lake tanganyika hotel hiyo sasa msilalelale. Hamasisheni utalii wa ndani isiwe ni hoteli ya wanaokuja kigoma tu. Halafu raha iliyoje bwana mdogo anacheka na JK nanyi mko pembeni mnashangilia. hamuoni kuwa anapeta Oktoba? migebuka oyee

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 16, 2010

    Hizi ni kampeni tu hamna lolote!! Hiyo hotel inasaidia watanzania wa kawaida wangapi mpka presida akafungue ???
    Mawazili husika si wapo!!!

    Huyu presida sio na safari zake za ajabua ajabu, mara kwenye msiba shemejie na mengi (4 what ??), mara kufungua hotel arusha,mara nje... safari kibao zisizo na faida kwa Taifa zaidi kuongeza mzigo kwa taifa.

    Wadau, Hivi mnajua rais akisafiri anasafiri na watu wangapi?? wanakula posho kiasi gani?? Ghalama za safari ni kiasi gani ??
    Ghlama za maandalizi anapokwenda ni kiasi gani ???
    Hizi zote ni pesa za kodi za walalahoi wanaozidi kuminywa na bajeti za kifisadi fisadi tuu.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 16, 2010

    Kakaa Ramos,ni wewe??Dar mpaka Kigoma!!!!(Alpha na Omega za reli hizo)Big up man.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 16, 2010

    Bwana George Nzundahongera kwa kufungua hotel ya nguvu. Lakini sasa jaribu kuonekana kwamba wewe ndiye mwenye hiyo hoteli. Nasema hivi kwa sababu viwalo vyako haviendani kaisa, hata kidogo na uwezo wako mkubwa wa kiuchumi. Nakutakia kila la kheri kwenye biashara yako. Mdau wa DSM.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 16, 2010

    Yule sio Bw Ramos alisoma kibaha? ee bana vp ww..from Dar mpaka Kigoma..kamugisha K anakutafuta babu..acha e mail yako hapa..

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 16, 2010

    Wewe Anony wa Wed Jun 16, 08:16:00 AM una lako jambo. JK ni ni binadamu kama wewe. Ni mtu wa watu. Kumbuka kabla hajawa Rais alikuwa akiishi maisha ya kawaida tu kabla ya kubanwa na maswala ya ulinzi na usalama wake. Anastahili kujichanganya na watu. Ndo maana anatajwa kuwa ni mtu wa watu. Wewe hujawahi kwenda msibani? Acha longolongo zako. JK yuko Juu sana katika masuala ya Kijamii na kujichanganya. Huyo ndo Rais wa watu tuache kusemasema tu. Je una uhakika kama safari zake ulaya hazina maslahi kwa nchi? "waswahili wanasema NO research, No right to open your mouth (to speak). Lazima katika masuala mengine tuwe Fair, sio kukosoa kila jambo. BIG UP JK, ENDELEA HIVO HIVO KUWA MTU WA WATU. JICHANGANYE MPAKA KIELEWEKE. HIYO NI CREDIT KUBWA KWAKO AMBAYO HAKUNA KIONGOZI ALIYEPITA ALIWAHI KUWA NAYO, LABDA BABA WA TAIFA, hayati JK NYERERE. aliyekuwa kipenzi cha watu. NAWE UNA KIFUPISHO CHAKE JK. Kumbuka msemo usemao- KELELE ZA MLANGO HAZIMFANYI MWENYE NYUMBA KUKOSA USINGIZI.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 16, 2010

    Nyie mnaouliza kama watanzania wanaenda Lake Tanganyika Hotel, mko Kigoma au? waulizeni wana Kigoma wenyewe wanavyofaidi huduma pale hotelini: kigoma pesa iko, na inatumika kwa kujivinjari pia ikiwemo hapo hotelini. Kama unabisha..... njoo Kigoma uone. Mnafikiri kigoma ya leo ni ile ya kusubiri treni? kuna usafiri kibao kwenda Dar.

    George Nzunda wasikusakame: wanaosema kuhusu viwalo vyako ni limbukeni, wale wanaovaa suti popote bila kujali mazingira...wasikusakama kila mtu na interest zake! Kigoma juu!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...