Na Woinde Shizza
wa Globu ya Jamii, Arusha
Kundi la majambazi watatu wakiwa na silaha nzito limeua watu wawili akiwemo mfanyabiashara mwenye asili kiasia na kupora mamilioni ya fedha mijni hapa.
Tukio hilo ambalo limethibitishwa na polisi mkoani hapa limetokea jana majira ya saa kumi na nusu jioni katika mtaa wenye shughuli nyingi za kibiashara wa Sonali Soko Kuu mjini Arusha.
Watu walioshuhudia tukio hilo wamesema kuwa kabla ya mauaji hayo majambazi, ambayo idadi yake yake kamili haijaweza kufahamika, yaliteka mtaa huo na kupiga risasi hovyo hewani na kusababisha taharuki katika eneo hilo na maeneo ya jirani.
Katika tukio hilo mfanyabiashara Swaleh Hussein Alli (35) aliuawa kwa kupigwa riasi kadhaa kichwani na kufariki dunia papo hapo, huku mfanyabiashara ndogo ndogo mwanamama Paschalina Antony (32) mkazi wa Unga Limited aliuawa kwa kupigwa risasi kifuani wakati akipiga mayowe bada ya kushuhudia majambazi hayo yakammiminia risasi Alli.
Mashuhuda hao walisema kuwa kabla ya tukio hilo walifika watu kadhaa na kuingia katika duka la mfanyabiashara huyo wakijifanya wanataka kufanya manunuzi. Ghafla tu watu hao kila mmoja akiwa na silaha walimnyooshea bunduki mfanyabaishara huyo na kuwaamuru wafanyakazi wa duka hilo kulala chini na kuanza kumiminia risasi mfanyabaishara huyo.
“Tukio lenyewe lilikuwa kama filamu hivi watu hao waliingia dukani kama wateja wakauliza bei ya nguo na vitu vingine wakati tunajaribu kuwaonyesha ghafla wakageuka na kukaa kila upande na silaha wakatuamuru kulala,tulichiosikia ni milio ya risasi na harufu ya damu tulipoamka tukamkuta tajiri yetu amekufa”alisema mmoja wa watumishi wa duka hilo ambaye hakutaka kutajwa jina gazetini.
Naye John Kumbau mfanyabiashara wa soko kuu alisema kuwa majambazi hayo yalikuwa mengi na yalipofika katika eneo hilo yalijigawa katika makundi matatu na kuhakikisha kuwa hayana mtu wa kuwazuia baada ya tukio.
“Unajua mimi niliona kila kitu kwa hofu ya kuuawa nikanyamaza kimya,yule mama aliyeawa alipiga kelele nikaona akipigwa nikakaa kimya lilikuwa tukio la kutisha”alisema Kumbau
Akizungumzia tukio hilo kamanda wa jeshi la polisi mkoani hapa Basilo Matei alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuongeza kuwa majambazi hayo yalikuwa na gari aina Toyota Corrola Premio lenye rangi ya kijivu ambapo mapaka sasa namba zake za usajili hazijaweza kufahamika.
Kamanda Matei alibainisha kuwa uchunguzi wa awali unaoonyesha gari hilo liliporwa kutoka mjini Moshi siku tatu kabala ya tukio hilo .
“Baada ya tukio hilo tulifanya mawasilianio ya haraka na majirani zetu ,tukajulishwa kuwa gari hilo lililotumika liliporwa kutoka Kilimanjaro”alisema Matei.
Aidha aliwataka wananchi mkoani hapa kutoa taarifa zozote zitakazoasaidia kukamatwa kwa wahusika wa tukio hilo baya kuwahi kutokea katika siku za hivi karibuni.
“Wahusika wa tukio hili lazima watakamatwa hawataweza kuuushinda mkono mrefu wa dola kila mahali tumejizatiti ni lazima watiwe nguvuni.
Tukio hilo kubwa la mauaji na uporaji ndilo tukio kubwa kuwahi kutokea mwaka huu baada ya watu wanaoasadikiwa majambazi kumwua mwanamke mmoja aliyetajwa kwa jina Jackline Deo mkazi wa Lemara mwishoni mwa mawezi januari mwaka huu ambapo hata hivyo katika tukio hilo majambazi hayo hayakuchukua kitu chochote na baada ya siku tatu nao waliuawa na polisi.
TUNALAANI MAUAJI HAYO! Damu zisizo na hatia zimemwagika bure. Hivi majambazi, kwani mkipora mali tu bila kutoa uhai wa watu huwa hamjisikii vizuri? Ni mpaka muue ndio uporaji ukamilike? Nadhani hao majambazi wangeweza tu kupora mali pekee (japo nayo ni kinyume cha sheria - ila ni bora kuliko kufanya vyote, yaani kupora mali na kuua wanaoporwa) bila ya kusababisha hivyo vifo.
ReplyDeleteKwanza huyo mfanyabiashara mwenyewe alikuwa anauza duka la nguo na viatu! Sasa kweli jamani huyo ni mtu wa kuvamiwa na silaha? Mmepora shing ngapi kwani? Usikute ni laki 3 mpaka milioni 1! Kweli ndio utoe uhai wa mtu? Je watu tukianzisha bishara zetu za ma-diamond, ma-tanzanite na ma-gold, ndio hali itakuwaje? Bishara itafanyika kweli? Ndio maana Bongo watu hawaji-engage na Biashara za magari ya kifahari sana, sasa nimeelewa kwa nini!
Sasa jamani hata huyo mama aliyekuwa anapiga mayowe nae mumemuua? Hivi kweli nyie ni watu au majuluni? Mi nadhani kuna haja ya ku-limit hizi sinema za ajina James Bond na wengineo kama hao, kwani nafikiri people have been watching too much television ama movies! Jamani wabongo wenzangu, wale huwa wanaigiza tu! Sio kweli! Sasa nyinyi mnaiga kila kitu!
NINALAANI MAUAJI HAYO! Vyombo vya dola tunaimani kuwa HAKI itatendeka, na wauaji watakamatwa na kuchukuliwa hatua stahili. Ila tafadhali, MSIBAMBIKIE WATU KESI, ILI TU KUURIDHISHA UMA KUWA HATUA ZILICHUKULIWA! Mjitahidi kuwatafuta hao waliofanya hayo mauaji, ndio wakamatwe na kufikishwa mbele ya sheria.
Yaani mtu kujitafutia riziki yake kihalali ndio iwe tabu? Mnataka tujifungie ndani kwa hofu ya kuuwawa nanyi? Hivi huwa mnafikiria uchumi wa Tanzania kweli wakati mnaenda kufanya mauaji na uporaji? Sasa tukijifungia wote ndani ndio huo uchumi utakuwaje? Si ndio utazidi kudorora?
Kwa Majambazi wote, YOU CAN RUN, YOU CAN HIDE BUT YOU CAN'T ESCAPE THE LONG ARM OF THE LAW! TIME IS ALL YOU HAVE! (You Can't run From the LONG Arm of the Law for Long!).
May the Deceased Rest in Peace. Amen.
Majambazi imetosha sasa. Kuacha watoto wachanga bila baba zao na mama zao ni ukatili uliopitiliza. Hivi ni kosa mtu akifanya kazi halali na kujipatia riziki? Chukueni basi hicho mnachotaka tuachieni roho zetu tutafute tena.... jamani, inauma sana.
ReplyDeletewewe anoni namba 1 isije ikamwa wewe unahusika na huo mchongo!!!
ReplyDelete""Wahusika wa tukio hili lazima watakamatwa hawataweza kuuushinda mkono mrefu wa dola kila mahali tumejizatiti ni lazima watiwe nguvuni"".
nimeipenda hiyo Kamanda Matei.
Majambazi wanajua fika kuwa maisha yao ni mafupi, huwa siwaelewi kuwa wanafurahiaje maisha huku wakijua fika kuwa kuna siku tu watakamatwa na kufa kifo kibaya kwa kupigwa risasi au kuchomwa moto au kupondwa mawe! Ni maisha ya ajabu sana. Ni watu ambao walishachanganyikiwa. Mioyo yao haitatulia mpaka siku ya mwisho. Mbaya zaidi utawakuta wameoa wasichana warembo na waliojituliza bila ya wao kujua kuwa waume zao ni majambazi halafu hujipachika majina ya wafanyabiashara! Ukweli ni kuwa tunaishi nao humo mitaani na watu wanawajua. Poleni sana wafiwa. Marehemu mpumzike kwa amani kaburini mpaka kiama.
ReplyDeleteHaya msimu wa uchaguzi umeshaanza ni kawaida ujambazi kuongezeka.
ReplyDeleteNi tukio baya na la kuhuzunisha sana. Mtu kajinyima, kaanzisha biashara yake, leo from no where, mtu anakatisha uhai wake utadhani yeye au wao ndo watarithi hilo duka. Siku za majambazi hao zinahesabika. LAKINI BADO NAJIULIZA, HIVI HAWA ASKARI WETU, AU HAWA WANAOJIITA USALAMA WA TAIFA, TUNAOWALIPA MISHAHARA WATULINDE NA WANAZAGAA HOVYO MITAANI WANAKUWA WAPI KUZUIA MATUKIO KAMA HAYA. BAHATI MBAYA MWANDIHI HAJATUAMBIA TUKIO HILO LIMEDUMU KWA MUDA GANI, KWELI WATU WAFYATUE RISASI, WAJIPANGE, WAUE, WAPORE, WAINGIE KWENYE GARI, WATOWEKE KWENYE MITAA YA ARUSHA YENYE FOLENI, KWELI ASKARI HAWAKUSIKIA MILIO YA RISASI HIZO? Kwa kweli mi nashauri wanajeshi ndo wawe polisi, na polisi wawe wanajeshi labda tutakuwa na imani kwamba tunalindwa. Aibu!!!
ReplyDelete