Mheshimiwa Waziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Dk. Diodorus Kamala (akihutubia) Ijumaa 18 Juni 2010 amekutana na Watanzania waishio Uingereza kwa lengo la kuwafahamisha wananchi hao masuala mbalimbali ya Utangamano wa Jumuiya hiyo.

Ziara ya Mheshimiwa Dk. Kamala inatokana na ombi la wananchi hao kwa Waziri Mkuu Mheshimiwa Mizengo Pinda alipotembelea London mwezi Mei mwaka huu. Mheshimmiwa Pinda aliwaahidi wananchi hao kumtuma Dk. Kamala kuja kutoa ufafanuzi kuhusiana na maendeleo na mapatano yaliyofikiwa katika Jumuiya hiyo.

Mmkutano huo ulifanyika katika Ofisi ya Ubalozi wa Tanzania, London. Mikutano mengine miwili ya Waziri huyo na Watanzania itafanyika katika miji ya Reading leo Jumamosi, 19 Juni 2010 na Manchester ni kesho Jumapili, 20 Juni 2010, yote kuanzia saa kumi jioni.

Hotuba kamili ya Mheshimiwa Waziri itatangazwa kwenye tovuti ya Ubalozi baadae.


Mheshimiwa Waziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Dk. Diodorus Kamala, (pili kushoto), Mheshimiwa Balozi wa Tanzania hapa nchini Uingereza, Mama Mwanaidi S. Maajar, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania hapa Uingereza, Bwana John Lusingu na Mwakilishi kutoka Jumuiya ya nchi za Afrika Mashariki.

wadau wakifuatilia hotuba ya waziri
wengi walijitokeza kumsikiliza Dk. Kamala




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 19, 2010

    jamani siasa kazi.

    ReplyDelete
  2. Ndibalema Junior (Finland)June 19, 2010

    Ze wadauzzz! jamani Dr shayo yuko wapi? manake hasikiki. Hata hapa kwenye hii shughuli haonekani. Aliahidi kuwa atarudi Nyumbani Tanzania kuja kujiunga na vijana wenzake kujenga taifa la Tanzania? where is he? I have been following him seriously kwa vile mtizamo wake wa kutoa solution ya changamoto yanayoikumba taifa letu la Tanzania

    Au alikuwa hayuko serious?

    Ningefurahi sana kusikia kama alitimiza hiyo ahadi yake aliyeitoa mbele ya wanajamii kupitia blog hii

    Ila huko aliko, ombi langu kwake asijiingize kwenye SIASA.

    Nawakilisha

    ReplyDelete
  3. Akulina Alphan (Tripol Libya)June 19, 2010

    Mdau wa Finland, Dr Shayo yuko Tanzania, na yuko katika chuo kikuu Huria, Ila sinauhakika yuko hapo kama nani, ila mara ya mwisho nilikutana naye akitokea Zanzibar alikokuwa amekwenda kutoa mafunzo.

    Ninakubaliana na wewe kabisa kuwa vijana kama akina Dr shayo, John Mashaka, na wengineo Taifa likitaka kuwafaidi kwa uelewa wao wa mambo, wasijichanganye na "POLITICS" Huko nadhani watamezwa na misukosuko ambayo itawafanya mchango wao katika taifa uwe politicised

    Ombi, tushitikiane nao katika kujenga Taifa la Kitanzania hasa kwa ajili ya vizazi vijavyo. Hawa ndiyo wanaoweza kuwa na vision, mission and kutupatia core values ambazo zikijadiliwa zitaweza kutoa sura na mwelekeo wa kule tunakotaka kufika.

    Wanablog ya jamii, msinielewe vibaya, siyo hawa akina Dr shayo, na Akina John Mashaka tu. kama wewe ni kijana unajiamini na unajua unamchango wako ambao unafikiria utasaidia kujenga hili taifa letu, usisite kujitokeza.

    we need you
    we need your thinking
    we need your inputs
    we need your critical mind and criticism
    Where we can differ it should not be taken kuwa mko upande wa "pili wa shiling"
    ila ionekane kama chachu ya kumsaidia yeyote atakayekuwa CEO wa Taifa la Tanzania ifikapo 2010

    Nawasilisha

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 19, 2010

    Shayo ok, Mashaka ni no kwa sababu ya majigambo!

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 19, 2010

    Uncle Nimetoa maoni yangu kuhusu hii mada lakini umeyaficha. Nauliza tena what is the rationale eti waziri kuzunguka nchi za nje kutafuta maoni. By the way kuna taratibu za kiserikali za ukusanyaji maoni hayo. Yeye anatakiwa kuwa sehemu ya Baraza la mawaziri na si kuzurura kwa kutumia fedha zetu walipa kodi kwa kisingizio cha maoni sijui nini. This is the wastage of taxpayers fund. Kama kuna ulazima saaaaana wa Kamala kwenda nchi za Nje kuleezea mchakato wa Afrika Mashariki kwa nini asianzie hapo rwanda, burundi, kenya nk. Kwanza watanzania wapo zaidi ya milioni 42 ndani ya nchi na si wote wamesaekezwa kuhusu huo mchakato,Sasa this Dr. is wasting our money...this is wahat I call tourism.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...