MO akiwa na Viongozi wa Chuo cha Uhasibu akiongozwa na Mkuu wa Chuo Bw.Emmanuel Kingu(wa pili kulia) wakati wa kukagua Majengo ya Chuo hicho(Kushoto) Rais wa Chuo Bw.Evans Crispin(Kulia) Waziri Mkuu wa Chuo Bw.Mbaraka Ismail.
MO akizindua Viti Maalum kwa ajili ya kukalia wanafunzi wakati wa Kujisomea”VIMBWETA”.
MO akiwa na Uongozi wa Chuo hicho pamoja na Wanafunzi wakiwa wanaonekana wamekalia viti hivyo(VIMBWETA).
Baadhi ya Wanafunzi wa Chuo cha Uhasibu TIASO wakimsikiliza Mh.Mohammed Dewji Mbunge wa Singida Mjini(hayupo pichani) alipokuwa akiongea na Wanafunzi wa Chuo hicho kuwahimiza kusoma kwa bidii na pia aliwaahidi wanafunzi hao kuwapa Jezi za Michezo seti 5 pamoja na Mipira 20.
MO akimkabidhi cheti mmoja wa viongozi wa wanafunzi
MO akimkabidhi cheti Waziri wa Wanawake na Maendeleo ya Jamii(TIASO) Mh.Fatuma Hamisi akipokea cheti cha Uongozi bora.
MO akimkabidhi cheti cha Uongozi Bora Rais wa TIASO,Mh.Evans Crispin.
Mo akila konozzzzz na baadhi ya wanafunzi wanaoonekana kufurahia ujio wake
MO Katika Picha ya Pamoja na Uongozi wa Chuo cha TIASO.










Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 19, 2010

    Jamani huyu Mbunge wa Singida inaelekea anajituma, kwani namuona mara kwa mara kwenye shughuli na anajichangaya vizuri na wananchi wake. Wabunge wengine hawafanyi lolote zaidi ya kushibisha matumbo yao, hata kama na yeye anakula japo pia anafanya na vitendo. Im so proud of you MO keep it up a good job, Singida needs so much from you.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 20, 2010

    this guy looks very sincere, caring and honest... i saw his pictures before here, i think he was talking to a disabled sister (he sat down, on the floor with her). I think it all comes down to liking what you do, and its not always about the money. Too bad he cant run for presidency because if he does i will be the first one to vote for him.

    Thank you MD keep up the good work, you are a true MP, please continue to make changes.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 20, 2010

    kwa kweli kaka mo anajitahidi mno, sote tunaona, ingetakiwa na wengine wafanye hivi tuone.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 20, 2010

    jamaa ana upendo sana huyu. nimefurahishwa sana.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 20, 2010

    sio siri MO anajituma sana na anafanya kazi zake kwa moyo mmoja. wengine matumbo yatapasuka bungeni, maana huyu kama mnakumbuka hata mpira huwa anajichanganya sana, nakumbuka huwa anacheza na wachezaji mpaka anavua shati kwa furaha. ni mfano wa kuigwa.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 20, 2010

    Du ! hivi viti vinaitwa "Vimbwete" au "Vimbweta" wanaojua historia ya hili jina watufafanulie mie kumbukumbu yangu inaniambia ni vimbwete hivi ....

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 20, 2010

    i have seen him once in mwanza and he really loook stylish

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 21, 2010

    Prof Mbwette ( yule aliepewa jukumu la kurundika wanafunzi bila nyezo muhimu pale mlimani) alitumwa aende nje ya nchi akaangalie vyuo vingine vinawezaje kukidhi mahitaji ya wanafunzi. Alirudi akawaambia UDSM wajenge hayo mabenchi ili wanafunzi wakiwa wanasubiri vyumba kule wapumzike na wajisomee. Kama kawaida wajukuu wa mzee wakalinasa hilo na kulibatiza VIMBWETE.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 21, 2010

    Jina sahihi ni vimbwette. Jina hilo limetokana na jina la Prof. Tolly Mbwete (ambaye ni Engineer by profession) aliyebuni wazo la kujenga madawati ya aina hiyo wakati yuko University of Dar es Salaam.

    Prof. Tolly Mbwete hivi sasa ni Vice Chancellor wa Open University of Tanzania.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 21, 2010

    ni "vimbwete" wale waliowahi kukuaa kwenye mdigrii, nje ya Nkruma, TBS na kwingineko mlimani wanaelewa vizuri sana kuhusu hili.

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 21, 2010

    Nice to hear that Prof is now at Open University as VC. Hiyo habari nilikuwa sina .Thanks. Praise.

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 21, 2010

    Jina sahihi ni VIMWETE! Nakikumbuka kile cha pale karibia na iliyokuwa Faculty of Engineering wakati huo (nje ya geti la Engineering kwa mbele kidogo kama unaelekea DARUSO ama mabwenini), pale kwenye majani yale ambayo pia ni njia, kwa mbele yake kuna kamfereji hivi kadogo; pembezoni mwa Theater Rooms zile. So ni VIMBETE na sio VIMBWETA.

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 21, 2010

    Mo utukumbuke katika ufalme wako mheshimiwa. Tunashukuru kwa misaada ila tunakuomba ile timu inayoitwa African Lyon, iwe ni timu ya Singida ili nasi tuone ligi kuu.
    Jingine Mheshimiwa mbunge ni yale maombi yangu binafsi kwako ambayo tayari yako mikononi mwa msaidizi wa Mr. Hassan, yaani dada Sabrina. Nitakushukuru kama tu maombi yangu yatafanikiwa ili mke wangu naye awe mjenzi wa taifa kupitia rasilmali zako. namba ya mawasiliano ni 071 524 3201

    ReplyDelete
  14. yaliyomo yamoJune 21, 2010

    hahaha
    siku hizi jina la vimbwete halijulikani, linalojulikana ni VIMBWETA. LAKINI VINGI VIMEBOMOKA-BOMOKA.
    nimemisi sana hayo majina
    vimbweta,
    mdigrii,
    atb,
    thieta,
    yombo
    holl wani
    holl siksi
    revo skwea
    fass
    daruso
    hil pak
    caro wa hil pak
    tembo kadi wa hil pak
    na zaidi KUNJI.
    DUH.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...