Asalaam aleykhum,
Kaka Issa nimerudi tena kwa ajili ya mtoto Abdulkarim ,ni mtoto wangu wa kwanza wa kiume ambae ana miaka 13, Amekua na tabia mbaya sana ya kuondoka nyumbani mara kwa mara na kwenda kuishi mtaani ,Mwanzo Alianza kutoroka nyumbani akiwa na Miaka 7 alikua anaondoka tunapoihi anaenda kwa bibi yake mfano kama aliondoka asubuhi basi jioni utajulishwa kafika huko kwa bibi yake, Aliendelea na hiyo tabia nikawa namchapa kwasababu ya hiyo tabia hapo akawa anakaa hata miezi 4 au 5 kisha anarudia tena .
Kaka Issa nimerudi tena kwa ajili ya mtoto Abdulkarim ,ni mtoto wangu wa kwanza wa kiume ambae ana miaka 13, Amekua na tabia mbaya sana ya kuondoka nyumbani mara kwa mara na kwenda kuishi mtaani ,Mwanzo Alianza kutoroka nyumbani akiwa na Miaka 7 alikua anaondoka tunapoihi anaenda kwa bibi yake mfano kama aliondoka asubuhi basi jioni utajulishwa kafika huko kwa bibi yake, Aliendelea na hiyo tabia nikawa namchapa kwasababu ya hiyo tabia hapo akawa anakaa hata miezi 4 au 5 kisha anarudia tena .
Hata maudhurio yake shule yakawa mabaya ikafikia hatua akawa anarudishwa darasa nikaona ni bora nimtafutie boarding huko nako alisoma mwaka wa kwanza vizuri tu ila mwaka uliofuata akaanza tena tabia ya kutoroka shule na kwenda kuzurula mtaani hata mara ya mwisho alitoweka shuleni kwa siku 5 akiwa darasa la 4 (2007) walimu wakanifahamisha tukashirikiana kumtafuta alipopatikana wakanishauri nimrudishe nikaenae nyumbani ili aweze kusoma katika mazingira ya karibu na nyumbani,Hivyo ikabidi nirudi nae nyumbani.
Nikampeleka tena shule ya day huko akawa anaenda shule vizuri nikamuwekea utaratibu kwa kumfuatilia nilipoona anamuelekeo mzuri nikampa uhuru wa mtoto ili ajione hafuatiliwi sana haukupita muda mrefu akarudia tabia ya kutoroka tena na safari hii akawa anapanda mabasi anaenda hadi mikoani !Nakuna kipindi nilimtangaza hadi kwenye blog ya jamii, ilisaidia kidogo lakini bado hajaacha.
Kwa kweli tabia hii kwa sasa imekua sugu kwani anaweza anatoweka nyumbani kwa mwezi mzima nahangaika kumtafuta baada ya muda anaenda kwa ndugu yeyote. Ukimuuliza kwanini unatoroka nyumbani anasema kuna kitu kinamwambia aondoke ila badae anaogopa kurudi anajua nitamchapa!
Wadau naomba msaada wa ushauri wa mawazo. Nimfanyeje mwanangu huyu???
Regards
Mzazi.
Regards
Mzazi.
pole mzazi. Je anaishi na mama yake au mama wa kambo? Jaribu kuwa karibu naye. punguza ukali, mpe upendo mkubwa kwake, mtimizie mahitaji yake muhimu, muulize kwa kina na kwa upole nini hasa tatizo. Na mfuilie kwa karibu mienendo yake.
ReplyDeletemdau wa kwanza hapo juu amenena kwanza kaa nae kwa upendo muulize nini chanzo cha tatizo,then jaribu maombi najua hilo utaliona la kipuuzi hasa kama tunatoka katika dini tofauti ila hapa siongelei dini so uchukue ushauri wangu maana ni njia ya kumsaidia mtoto,kwa maelezo yako hapo juu unasema kuna kitu kinamwambia aondoke nyumbani kama kweli basi mtoto wako kavamiwa na roho chafu sisi wakristo tunaoita mapepo na anahitaji msaada wa maombi,najua ushauri kama huu utaonekana wa kipuuzi ila unaweza kuwa ndio ushauri wa busara na wakumsaidia,mpeleke mtoto akaombewe sio lazima wewe ubadili dini au yeye abadili dini la hasha bali kupata ufumbuzi wa tatizo.
ReplyDeletePole Ndugu yangu, hali hiyo inaweza kumsononesha sana mzazi, lakini muombe Mungu akupe uwezo wa kukabiliana na hali hiyo, unapokuwa na mtoto wakati wote unafikria kumjengea maisha yake ya baadae lakini hali inapokuwa hivyo inakuwa inakatisha tamaa..mimi ningekuomba uweze kumchunguza vizuri huyo mtoto kwanini ankaimbia ,usiwe mkali.mpende jaribu kuwa karibu naye nakama labda mazingira ya nyumbani ndiyo yanayosababisha basi jaribu kutatatua..pia kama ni mtu wa dini jaribu aweze kumbewa
ReplyDeleteAmeni
Kuna uwezekano wa kuwa na mambo mawili:
ReplyDelete# kuna nguvu za giza
# nyumbani kuna 'vitu' vinavyomfanya huyo mtoto asipende kukaa humo nyumbani - yaani vinamsukuma kwenda kutafuta faraja sehemu nyingine. (Ila hii haingii akilini kwani mbona hata akienda 'boarding' bado anatoroka shule?).
Suluhisho:
# Jaribu kukaa na mwanao uongee nae kwa upole na utaratibu (au tafuta mtu ambae huyo mtoto hupendelea kwenda kwake sana / mtu ambae huyo mtoto yuko nae 'comfortable', aongee nae - Kulikoni?)
# Jitafakarini na hapo nyumbani kwa ujumla, je mnachangia kwa hiyo tabia ya mtoto? Labda ni wakali sana, ama hamumsikilizi, ama hamumjali, hivyo kupelekea mtoto kujihisi kuwa hahitajiki au labda hathaminiki na familia yake? (Hayo masuala ya mama wa kambo kama yapo, ndio yanaweza yakachangia, lakini believe you me, kuna mama wa kambo wana roho nzuri, na hawabagui watoto, ni mpaka mtu uulize ndio utajulishwa kuwa ni mama wa kambo - wengine huwapa watoto wa kambo mapenzi ya mzazi kuliko hata pengine mama zao wazazi).
# Tafuteni watu wa maombezi (wachungaji etc) wamuombee, pengine ana mapepo mawili matatu.
Poleni sana, Mungu amnusuru mwanenu, na apokee muujiza wake katika Jina la Yesu Kristo wa Nazareth. Amen. Amekwisha kupona.
Muone Dr. waakili. huyo kama bi polar vile.
ReplyDeletendugu yangu nakupa pole sana kwa matatizo ya mwanao kweli inaumiza roho sana km mzazi hakunakitu kinauma km mtotowako unayempenda anaanza kuwa natamia ambayo ukubaliani nayo hata mimi yamesha nipata najua unaumia kiasi gani sasa cha kufanya kabla yayote mtangulize mungu sijui ww nidini gani lkn wote tunamwabudu muumba mmoja kama nimkiristo funga na kusali sana halafu uwe mpole sana kwa huyu mtt unajua ukali ukizi mtt naye mtukutu km ukali inatoka kwako upunguze kama sio kuacha kbs halafu mchunguze mkeo km ni yeye ndio chazo cha mtt kukimbia kwasababu ya ukali wake sijui mtoto anaishi na mama wakambo au hiyo ujaeleza ukifuata haya ninayokushauri hakika mtoto wako atakuwa mzuri nautarudi hapa kutoa ushughuda
ReplyDeleteMpeleke hospital kama alianza toka mdogo hivyo kuna matatizo ya akili hapo au Certain vitamin deficiencies ....Anaweza kupewa dawa zikawa zinamsaidia kujudge...
ReplyDeleteusimchape jamani mtoto huyo sio utundu ...ni Cognitive impairment tafuta Dr mwenye kujua magonjwa haya na atakusaidia ...
Ndugu yangu mpendwa.
ReplyDeleteMtoto wako anahitaji maombi. Kuna pepo au jini linamsumbua. Wasiliana na watuy wanaomjua Mungu watamwombea ili kukata roho ya pepo au jini inayomuhangaisha. Hapenmdi kufanya hivyo. Lakini pia, onyesha upendo mkubwa kwake. Usimpige. Hajui atendalo.
Kama utahitaji ushauri wa kumuombea, basi eleza kupitia forum hii ya michuzi na nitakuandikia email kupitia kwa michuzi. Nasoma blog ya michuzi kila siku kwa hiyo nitapata maelezo yako.
Mungu akubariki.
kaka yangu pole sana,inavyoonekan huyo mtoto ana tatizo ambalo linahitaji maombi,naomba umpeleke kwenye maombi atafunguka tu kwa jina la Yesu.kwa sababu tatizo siyo hapo nyumbani tu mbona na shule ya boarding alitoroka?
ReplyDeletePole mzazi.
ReplyDeleteMimi nafikiri huyo mtoto anahitaji malazi ya ukaribu.Tafadhali acha fimbo kabisa,jaribu kuongea naye upatejua sababu hasa inayomfanya afanye hivyo.
1. Kwa sasa hivi nafikiri pia umri unamsukuma kufanya baadhi ya mambo,tafuta mtu wa kumpa councel(ushauri nasaa.nafikiri hapo Dar kuna mashiriki kama EMAU, COUNCENUTH.
2.Sio vibaya pia ukatafuta watu wa MUNGU wakamuumbea ila nashauri yote hayo yaende sambamba na malezi ya ukaribu na upendo badala ya fimbo.
mpeleke kwa watalamu!! waswahili wamesha mchezea huyo mtoto!!bangala kuna mganga anaitwa DR. beat mpeleke uko !!utamuona mbaya wako kwenye kioo!!
ReplyDeletemtoto ana allegic na home hapo kama vipi hama hapo amia kwengine,hakikisha unamlipa mwenye nyumba kodi yake yote kabla hujaama.
ReplyDeleteACHA TABIA YA KUPIGA MTOTO.MWEKE KARIBU AWE RAFIKI YAKO MKUBWA,NA UKIRUDI JIONI USIKOSE KUMLETEA ZAIDI.
katika kusoma koote, kweli nimeamini kuna wadau wana imani finyu sana.
ReplyDeletemmbora kati ya wote ni huyo aliyekupa ushauri wa kumuona daktari, au saikolojist mmoja akusaidie.
mtoto atakuwa na tatizo fulani katika ubongo wake, kitu kinachomsukuma kukimbia. hili pia linaweza kuwa ni malezi ya hapo home.
ikishindikana zaidi, basi mtoto kama huyo mpeleke kwa bibi au shangazi yake, kijijini ambako sehemu ya kuchezea au kujiachia hakuna.
mpeleke kijijini huyo akalime kwanza na shule ya huko itamkaa vizuri tu.
..Huyu mtoto anakipaji flani hivi.. nahisi kama cha Vasco Da Gama.. mchunguze vizuri.
ReplyDeleteHuyo mtoto hana tatizo lolote. Ni mtoto wa kiume huyo, kwa hiyo ana msukumo mkubwa wa kuondoka kwa baba.
ReplyDeleteMi mwenyewe ni kidume na home niliondoka toka niko 16, (yeah yeah najua mtasema huyu ana 13 lakini si manjua watoto wa siku hizi wanakua haraka) na mpaka sasa napeta. Mwanzoni walidai eti nina mapepo nikaombewe.
Matokeo yake wakati naombewa wale walionileta ndio wakaanguka chini kumbe wenyewe ndio wana mapepo.
Kwa huyo mzee tuliza boli mpe ushirikiano kamanda wako, muda si mrefu ataacha kula kwa dingi.
Eti "mpeleke kwa maombi ana mapepo sijui nini". Kwani yeye mwenyewe hamjui Mungu na hawezi kumuomba akamtatulia shida yake mpaka atafute watu wa kumuombea???
ReplyDeleteKama ni kuomba huo niwajibu wa mwanadamu, ndugu yangu funga na kuomba Mungu akutatulie hilo tatizo lako wewe mwenyewe pamoja na kutafuta msaada wa madaktari wa saikolojia.
Pili huyo mtoto inawezekana yuko very bright na shuleni michosho tu anaona anapoteza muda, na nyumbani hakuna vitu vya kuchallenge ubongo wake hivyo anapokuwa yuko bored anatafuta extiment nje ya nyumba, hebu mtafutie hizi games uone kama hujakuja kulalamika hapa mtoto wangu hatoki nje kawa addicted. Tafuta WII au Xbox au playstation3 kisha mpe yeye iwe yake uone!
ANAKAA NA MAMA WA KAMBO AU MAMA MZAZI? tafadhali jibu hilo swali nikusaidie.
ReplyDeleteMimi kwanza ningekushauri uweke fimbo chini, pili ukampeleke kwa mganga wa akili tatu ujaribu kutumia wakati mwingi nae kwani huenda ikawa ni mtoto anaehitajia attention ya wazazi wake sana, na vilevile wakati unamfanyia yote hayo mpatie dawa ya kiroho(yaani jaribu kumsomea qurani na huku unamuomba mwenyezimungu akusaidie na akuvue kwa mtihani huu amin)
ReplyDeletePOLE MZAZI.
ReplyDeletekwanza angalia vizuri lazima hapo kuna tatizo.jenga urafiki wa karibu na mtoto wako ili awe wazi kukueleza yanayomsibu.kwa mfano anvyotoroka nyummbani halafu anaogopa kurudi kwa sababu ya kuogopa kuchapwa guo ni uhusiano mbaya kati yako na mtoto.KUMBUKA huyoo ni mtoto na anafikiria kitoto...lazima kama mzazi uone kwamba anapita vizuri stage zote hadi kufikia utu uzima.ZINGATIA huyu mtotoo sasa hivi ni miaka 13 na yuko katika umri wa adolesence na sasa hivi anastruggle kutafuta identity ,usipoangalia vizuri ndio kwanza atapotea kabis a wakati huu.muweke mtoto huru kimawazo ,namaanisha mjengee dhana ya kwamba wewe ndie rafiki yake wa karibu na akueleze kitu chochote anachowaza au taka...hata kama akikwambia kitu ambacho unaona ni cha kijinga then mfafanulie na umwambie hiki kitu hakifai na umpe sababu za kumconvice kweli hiki kitu sivyo NA SIO KIMCHAPA KILA MARA KWA SABAA ATAONA FIMBO NI KITU CHA KAWAIDA TU.jE? Mwanao ana marafiki? ni wa aina gani? vipi uhusiano wako,mtoto,mzazi mwenzio na ndugu zenu?
ACHA KUKIMBILIA KUSEMA MTOTO ANA TABIA MBAYA BILA KUANGALIA KWA KINA KILA UPANDE...
SAVE CHILDREN
maombi ni silaha
ReplyDeleteANGALIA UHUSINAO WENU NA MTOTO
JE! ANAISHI NA WAZAZI WOTE?
KILA JAMBO AU TATIZO LINA SULUHISHO...KAMA UTAWEZA KUMPELEKA KWA WANASAIKOLOJIA MPELEKE.
KUNA WATOTO WENGI WALIOKUWA NA MATATIZO KAMA HILI LAKINI WALIPATIWA UFUMBUZI...
PIA WAZAZI MSIWE SANA WAKALI KWA WATOTO KWA SABABU KUMBUKA VICHWA VYAO VINAWEKA KUMBUKUMBUU SANA KWA SABABU HAVINA VITU VINGI KAMA VYA WATU WAZIMA.kumbuka ni nini ambacho huyu mtoto labda aliwahi kufanyiwa ambacho kilipelekea kuondoka nyumbani kwa mara ya kwanza kabisa.
sa nyingine ugomvi wa wazazi mara kwa mara unaweza kusababisha watoto kukimbia nyumbani hatimaye kupotea
Je huyo mtoto ana ndugu zake,kaka,dada au mdogo?
wao wakweje kama wapo?
suluhisho linapaswa litafutwe.
pia nenda kwa walimu wa shule zote alizopitia na ujaribu kupata profile yake na ni marafiki wa aina gani alikuwa nao
pia watoto wengine wanatumiwa kufanya shughuli za kichawi kama mtotto fulani (nchi inahifadhiwa)
yule mtoto alifanya mambo ya ajabu na hakuchangamana na watoto wenzie lakini sio kupenda kwake.kwa sababu wazazi walikuwa wakalisana hakuthubutu kuwaambia kazi anzozifanya usiki mpaka jirani mmoja alivyoamua kumwita mtot na kuzungumza nae kirafiki...mtoto aliogopa kwa mara ya kwanza lakini baada ya uda alimwamia kila kitu///
jaribu kila njia uone kama hujapata ufumbuzi
lol kipaji cha vasco da gama kweli umenichekesha , sio lazima awe kichaa lakini jaribu kumpeleka pale muhimbili kwenye kile kitengo cha hawa watu pale kuna wataalam wa aina nyingi pale wanaweza kutambua kinachomsibu watakuwa wanamfanyia therapy kama mara tatu kwa wiki ni wazuri sana kwenye ushauri nenda kwanza pale, sijasema mwanao ni kichaa hapana ila pale huwa wanadili na ishu kama hizi
ReplyDeleteHamia Mtaa wa Saba kutoka hapo unapoishi sasa hivi! Matatizo yote hayo (watoto kuumwa-umwa n.k) yataisha.
ReplyDeleteAsalaam Aleikum
ReplyDeletePole kaka kwa masumbufu uyapatayo.Kama waliotangulia wengine kusema.
Huenda mtoto amekosa upendo wa mama ndio maana anakimbia hapo nyumbani, au kama mama yake yupo basi huenda ikawa nguvu za Giza, yaani uchawi au mapepo(majini)au mtoto ana dalili za Schizophrenia ambayo hudhani anasikia sauti au kuona vitu!
Kuna tiba za Kisunnah toka ndani ya Quraan ya kudeal na masuala haya iwe ya Ki-Psycholojia au mambo ya nguvu za Giza.Jaribu kuepuka ushauri wa watu wanaotumia mizimu au vitabu vya elimu za uchawi!Tiba halisi ni Tiba ya Quraan na Sunnah...Yesu wa Nazaret kweli alikuwa akiponya watu lakini sio hawa wanaomnadi Yesu, kwani Yesu hakuja isipokuwa kwa Taifa la Israeli tu!
Waisilamu tuna Tiba zetu tulizofundishwa na Mtume wetu kipenzi na wema waliotangulia.Hizi tiba ni Tibb Ruqyah(Exorcism)..Kam utaweza kumsomea msomee Surat Baqarah yote na nyumbani kwako isomwe Baqarah, Ayat Kursiyu, Surat Swafa, Surat Jinn, na Ayah za kuangamiza na kuchoma uchawi(Ibtwaru Sihr) fanya zoezi hili kila siku na simamisha visimamo vya usiku na ufunge kwa ajili ya Allah na jaribu kujiepusha na kumlaumu mtoto.
Kuna Masheikhe maarufu hapo Dar na mikoa mingine wanatoa tiba hizi za Ruqyah ungejaribu kumpeleka
Wasiliana na Sheikhe Wa Maduga Morogoro kwa msaada wa hili tatizo
Nambari zake za simu ni 0716 288098 au 0754 804257 Huyu anatibu kwa Quraan na Sunnah ukimuandalia nauli yako atakuja mpaka kwako kukufanyia Tiba na kuondosha majini wabaya ndani ya nyumba yako kwa kuwachoma moto wa Quraan na hawatarudi tena.
Fuata ushauri wa Kidaktari kuhusu matatizo ya mtoto wako huenda akawa na Schizophrenia.
Nduguyo
Khamis Hassan Batanyaga
Huyo ndio wale wanaitwa NUNDA.. Hakuna cha kulogwa mapepo wala nini. Kuwa karimu na mwanao achana na mambo ya fimbo. From 7yrs to 13yrs ni miaka 6 hiyo, anatoroka akiwa bording na akiwa home pia. Hivyo huyo ni SUGU NUNDA am sorry to say that. Usikate tamaa hicho ndicho cha muhimu jaribu kuwa mwenye subira na mpole.
ReplyDeletehuyo mtoto atakuwa na depression ebu jaribu kuwa naye karibu na kama mdau mmoja alivysema hapo juu mnunulie nintendo games zitamtuliza msongo wa mawazo ila pia anahitaji ushauri nasaha kutoka kwa wataalam wana mbinu za kuongea na watoto wa jinsi hiyo hadi mtoto anasema nini kinamkwaza ila huyo atakuwa hana raha tu kuna kitu ana miss
ReplyDeletekingine pia ebu jaribu kumchunguza usije ukakuta wenzake wanamfanyizia mambo ya ajabu, manake kizazi hiki kimekata kamba. mtoto wa ndugu yangu kavulana nako tangu kana miaka sita, anaaga kwenda shule kumbe kutwa anashinda mtoni wenzake wanamchezea, akaamishwa shule akawa nanaendeleza libeneke mamake kachapa wee kamuombeaa mtoto akapoa akamuamisha shule nyingine.sasa ana miaka kumi na karudia tena darasani ataenda wiki tuu hala anaenda tena kushinda mtoni sasa hii sijui ni nini kwa kweli saa nyingine unawapa kila kitu na mapenzi mema lakini ndo hivyo tena. pole ndugu
ReplyDeleteMimi nakuambia tena mimi ni mkisto na nakubali sala zinasaidia lakini mpeleke kwa dr mtoto toka miaka 7 awe anaondoka tu . na kama alifanya akiwa boarding skull the same?
ReplyDeleteWewe ni mzazi siju ni baba au mama lakini kuna swali je ulikua unatumia BC before na ni ipi? na kama ni pills je uliacha hizo kwa muda gani kabla huja TTC. Na kama ni hukuwa hata na prep pia kuna worry hapo...TZ wanawake wanatakiwa kufundishwa sana juu ya hizo BC sana tu. Zina side effect nyingI sana na zingine zikitumiwa bila kujua after conception...apart from birth defects ambazo ni physical pia kuna uwezekano wa kuwamental challenged...
huyo mtoto anahitaji kumwona dr msaidie kwa future yake
Mzazi, nakupa pole sana, mimi ni mzazi pia ninajua ni uchungu kiasi gani ulio nao kama mzazi juu ya mtoto wako huyo. Ushauri wangu ni huu: Msimpige mtoto wala msiwe wakali, mwonyesheni upendo na kumjali. Tatizo la mtoto wako ni kubwa na si la tiba ya kibinadamu bali tiba ya maombi kupitia Jina la Yesu. Sifahamu dini yako lakini maombi hayana mipaka ili mradi uwe na imani. Kama uko Dsm unaweza wasiliana na Mtumishi wa Mungu anaitwa Israel namba yake ya Simu 0784 353213 au kwa watumishi wengine waliookoka, ukihitaji kuwasiliana nami namba yangu ni 0732 688608 kwa msaada zaidi, au kama uko mkoa mwingine basi nenda Kanisa lolote la watu waliookoka utapata msaada wa maombi. Chukua hatua haraka kabla mambo hayajawa mabaya zaidi. Nakutia moyo ukiamini tatizo lako litakwisha kwani hakuna lisilowezekana kwa Mungu, wako watu waliokuwa wana matatizo makubwa kuzidi hayo ya mwanao na wamepona kupitia Jina la Yesu. Amini tu. Mungu akusaidie!
ReplyDelete