JK na kombe la dunia lilipotua Tanzania
1. Amini usiamini, mwaka huu wetu afrika,
raha afrika kusini, ni kweli pamefurika,
raha isiyo kifani, furaha kwa kila rika,
KOMBE kubwa duniani, na mashindano afrika;

2. Tanzania nasi tuende, kweli raha imefika,
tamu zaidi ya tende, FIFA wametualika,
tusiliache liende, lazma libaki afrika,
KOMBE kubwa duniani, na mashindano afrika;

3. Tusiache wajisifu, japo wametajirika,
maendeleo hafifu, sio sifa ya afrika,
tuiache hiyo hofu, tuungane kila rika,
KOMBE kubwa duniani, na mashindano afrika;

4. Kameruni nigeria, wote hawa waafrika,
wamo pia algeria, ivori kosti afrika,
yabidi kushangilia, kweli tumetajirika,
KOMBE kubwa duniani, na mashindano afrika;

5. Hii ndio hadhi yetu, nasi tumetajirika,
afrika nyumbani kwetu, mashindanoni afrika,
kweli kombe hili letu, sio bora kung´atuka,
KOMBE kubwa duniani, na mashindano afrika;

6. Mlimani tusiache, onyesha kuelimika,
tuonyeshe kila cheche, pia tuache dhihaka,
tuache kuwa wachache, ishangilie afrika,
KOMBE kubwa duniani, na mashindano afrika.

Kwa maoni tuma:
kade030@gmail.com.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 13, 2010

    kidogo niko nje ya mada lakini sio mbaya mimi ni mwanamke niko nje ya nchi maisha yangu nimetafuta mwenyewe bila msaada ya wazazi na mungu akanisaidia nikafanikiwa kimaisha sasa shida moja nina ndugu zangu nawapenda sana naninataka nawao wafanikiwe km mimi lakini shida moja nihivi mimi najitahidi sana kutumahela nyumbani lakini wao wanaona mimi napata hela nyingi sana pasipo jasho kama vile nachota na beleshibila jasho wakisikia ulaya WANAFIKIRI HELA unapata kirahisi ukituma hela wanasema hela gani hii mtu anatuma amekaa ulaya miaka yotehii hawajuii huku nitofauti na africa hakuna cha ndugu huku useme ukihishiwa utakimbilia kwa ndugu au jirani au utakopa kwa mtu kodi ya nyumba ikifika tarehe 1 inatakiwa umesha lipa kinyume na hapo vitu vitatupwa nje bila ya hidhini yako maisha ya nje nimagumu sana kwa vile hawajui tu nakibaya zaidi ukijitahidi kutuma hela haitafanya mambo ya maendeleo nikwamba wakishapata wanalewea kwa kwenda mbele nawewe huku umefunga mkanda husubutu hata kunywa soda nifanyeje naombeni ushauri wapendwa

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 13, 2010

    mdau wa kwanza, pole ndugu yangu, hiyo ndio mentality ya kila mwafrika ambaye yuko afrika, sio watanzania ni waafrika wote mentality ni moja, nayo ni kuwa ukiwa ulaya basi una pesa.

    Siwalaumu sana kwani kosa kubwa ni waliopo nje wanapokuja nyumbani na majisifu kuwa kazi ni rahisi na unalipwa £ au $ nzuri kwa saa, hawasemi kama kuna mabils tele toka health insurance mpaka bili ya maji.

    Matokeo yake nyumbani tuliopo nyumbani tunaconvert £ au $ muipatayo kwa saa na kuona kuwa mnapata pesa za kutosha sana.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 13, 2010

    1. Umesema la uhakika,
    huu mwaka wa Afrika,
    tumeonyesha linafikika,
    lengo tukiliweka,
    tukitaka kwa uhakika,
    kuendelea tutafika,
    tufanye kazi bila kuchoka,
    ni sharti lisiloepukika.
    Mungu ibariki Afrika.
    2. Kuhusu comments za kwanza hapa juu, hilo tatizo ulilolisema nalielewa pia kwa sababu lilinifika mimi. Watu ambao una ulazima wa kuwasaidia ni wazazi na watoto wadogo tu, si watu wenye nguvu zao ambao wamekuwa tegemezi. Wewe waeleze ukweli wa ugumu wa maisha ya ulaya. Nakushauri kuwa, kama unaweza, wanzishie miradi midogo ya kiuchmi, japo iwe ni kuwanunulia gari dogo (saloon au pick-up) la biashara au duka dogo la vifaa vya kila siku. Baada ya hapo, kwa vile umekwishawawezesha, nawa mikono yako. Huu utamaduni wa tabia tegemezi naona unaenea sana siku hizi. Vijana wanachagua kazi, wanaamka saa wanazotaka, wanataka vitu vya gharama, wanaishi 'beyond their means', n.k. wengi wao wakiwa tayari kufanya utapeli au hasa hasa kwa kujua kuwa mjomba, kaka, etc. atanipa tu. Shime tufanye kazi za halali, including kilimo. Kuna nchi nyingi watu wanauana kwa ardhi wakati sisi tumezikalia mamilioni ya hecta tunangojea tufanyiwe kila kitu. Uvivu ni kufuru. Kwa kifupi mdau, kama walivyosema watu wa busara, ukimfundisha mtu kuvua/kulima umemsaidia maisha yake yote, ukiimpa chakula leo tu umemsaidia leo tu. Kwa hivyo,wawezeshe kisha waache wajitegemee (endelea kuwasaidia wazazi, hiyo ni amri ya Muumba).

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 13, 2010

    loo kwa kweli hawa ndugu zetu sio siri wanakera na kuchosha hata uwatumie hela kila wiki wao wanataka tuu uendelee kutuma na kazi hawataki kufanya yani ni vibomu kila siku kuwa tuu muwazi kama mie jamani eeh hali ya uchumi ngumu iko kila mahali na watu hawana ajira na wengine masaa ya kufanya kazi yamepunguzwa kwa huyo mkiona kavu mjue na mie mambo yako tight otherwise hutaezeka nyumba nawajua sana mimi hawa watu ulaya hela hazichumwi kwenye matawi ya miti na bado bills lol hapana ukipiga tuu simu kusalimia loo utajuta kila mtu ana lake utadhani tunafanya kazi imf!!

    ReplyDelete
  5. Baba UbayaJune 13, 2010

    Afrika 2taendelea kula kwa macho 2.kwa nchi za Afrika kuchukua kombe hilo inabidi 2ckilizie vizazi vya sasa ambavyo vita2wakilisha 2018 na 2022.at the moment,robo fainali still itaendelea kuwa our most achievement.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 13, 2010

    Michuzi tunakuomba hala hala kwa hisani yako ya kusaidia jamii kwenye blogu hii ya jamii, comment ya kwanza kabisa iweke iwe habari peke yake tusaidiane mawazo maana hii ishu ni very sensitive na inamgusa kila mtu. Maana haya ya mjomba mjomba kwa kweli yanaumiza na wengine wakishajua tu ndugu zao wako nje basi hawataki kufanya kazi, na ukimnyima pesa utaluona maneno debe, anaringa ye tajiri, yuko ulaya kaukata basi ilimradi mtu unakosa amani. Weka hii mada iwe mtundiko peke yake, tufanyeje jamaniii! Ukisema usaidie wazazi peke yake watu ndio watakwenda kuhamia hapo hapo hata kama wana wajukuu tayari na wao watarudi kuwa watoto wadogo wategemee hao wazazi kwa kuwa wanajua mtoto aliye nje ya nchi atatuma pesa ya kula!!

    Aliyedata

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 14, 2010

    Ni kweli kabisa kuwa watu wengi sana katika bara letu Afrika wakijua tu mjomba, kaka, binamu, n.k. yuko nje au ana kipato fulani wanakuwa tegemezi sana, Wengine hata wanapanga bajeti kutokana na kipato cha ndugu na jamaa wakijua kuwa bomba la pesa liko wazi. Kama alivyosema mchangiaji wa tatu, waanzishie kamradi kutokana na uwezo wako halafu waachie wajitegemee, vinginvyo utawalemaza. Wakishindwa kuelewa hilo ni shauri lao si tatizo lako wewe.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 14, 2010

    sijui tufanyeje wadau???

    acha nyie mlioko ng'ambo, hata alieko dar naye yanamkuta hayo.

    unaweza ukaamka asubuhi saa kumi na mbili, pika cha dogo kalala, majirani wamelala, unajeandaa unaenda kazini. ukirudi jioni unapitia kwenye mishe-mishe (maana mshahara wenyewe hautoshi), saa nne usiku ukirudi home hata vyombo vilivyonywea chai havijasafishwa!

    jumamosi au jumapili unajifulia nguo mwenyewe, piga pasi safisha nyumba, watu wanakuona kama kinyago. ukitoka utasikia bro. nitoe kidogo basi, ukipita mtaani utasikia kamanda fegi basi, au mani niachie hata jero mtu wangu! kina dada nao utasikia, naomba elfu moja, naomba soda!

    ukimtafutia mtu kazi siku mbili kaacha. kisa? ohh pale kazini wananyanyasa sana wafanyakazi.

    kuvuta bangi mtindo mmoja. ukiona anaharibika ukimrudisha kijijini maneno ni balaa - oh fulani mbinafsi, kashindwa hata kumsaidia ndugu yake!!

    inakera!!!!!

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 14, 2010

    Nimpongeze aliyeleta mada hii na pia nakubaliana na aliyeshauri mada hii kwamba itungikwe peke yake ili ipate mjadala ulioshiba. Suala la tabia ya kuomba inayoambatana na uvivu, kwa sasa hapa Bongo ni tatizo la kitaifa, na sio tu kwa watu wanaoishi nje ya nchi. Kuanzia ndugu, majirani hata yeyote anayekufahamu, kuomba ni tabia sugu kwa sasa. Na hii kuwa imeanzia ngazi ya mtu binafsi, imesababisha kwenda ngazi ya juu katika jamii hadi kitaifa. Tumefika mahali watu wanapanga mikakati ya kuomba, yaani kuomba imekuwa utamaduni mpya wa watanzania. Imekuwa kawaida kwa sasa jirani, rafiki, ndugu kukuomba chochote, (Nauli, hela ya chai, mtaji, hela ya vocha n, k) Ndio maana hata viongozi wetu wamefikia mahali badala ya kubuni miradi ya kuiongezea nchi kipato, wanachokijua sana ni KUOMBA WA WAFADHILI - kwasababu huko ndiko walikotokea hiyo ndio tabia wanayoifahamu - yaani - kuomba.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...