Kaka Michuzi habari za kazi,
Sisi wakazi wa Ukonga kuanzia Mombasa, Mazizini, Masika, Moshi Bar, kwa diwani, Mkolemba, mpaka Kivule tuataabika sana na barabara yetu, hasa kipindi hiki cha mvua. Tunaomba msaada. tunajua katapila lipo ila naona TANRODS na Manispaa ya Ilala hawana mafuta basi watuambie ni kiasi gain ili tuweze kuchanga na tuchongewe barabara. Nakumbuka mara ya mwisho kupitisha greda ni 2008 mpaka leo na ukiiona barabara kama haikai watu.
Mdau Ukonga Sitakishari
hamieni huku mtaa wa usino, mikocheni.
ReplyDeletekaka uliyetoa maombi hayo ni sahihi kabisa madiwani wa pande zote wamelala si jaluo wala Jerry barabara uchaguzi mpaka uchaguzi, Makongoro anakwambia sina muda na wala sitagombea uko tena jimbo limegawanywa hatuna mtu wa kutufikiria jamani km tatu dakika 45 jamani tuonee huruma.
ReplyDeleteMpigie simu Diwani Slaa 0714 902 655. Kwa kuwa anao uwezo atawasaidieni.
ReplyDeleteJama sijaona seemu ina matatizo ya maji kama ukonga gongolamboto yani maji ya bombo kwa mara ya mwisho kutoka sijuwi ni miaka mingapi nyuma alafu uchaguzi ukifika ni watu walewale wana rudi madarakani . sijuwi sisi wa tz tuna rooho gani nzuri ya kumuonea uruma mtu kumtoa madakani au sijuwi tuna penda kuwaona kina mama wanavyo teseka na kutafuta maji . yani hawa madiwani wanatakiwa watoke akuna sehemu iko nyuma dar kama ukonga .
ReplyDeleteMmh jamani, huyo diwani Slaa apigiwe simu kwani yeye haoni? Au umeshakuwa uongozi wa kubembelezana? Kwani barabara tajwa iko chini ya TANROADS? Manake kuna barabara maeneo ya Morogoro store/Karibu hotel ambazo hazikuwahi kufikiriwa kutengenezwa zimepigwa lami mwezi wa jana (May) na TANROADS, ina maana wanachagua barabara za kutengeneza?
ReplyDeleteKwa kifupi maeneo ya ukonga hiyo hayana uongozi, ili kujikwamua ifanyike harambee ya wakazi kutoka Mombasa mpaka Kivule, barabara ikarabatiwe kwa nguvu zao wenyewe. Kwa sababu mkisubiri barabara za uchaguzi kwa uchaguzi, mtazeeka....