Mzee wangu ameomba nimsaidie kumtafuta kijana wake anaitwa Masanja aliyezaliwa mwaka 1970 , Mama yake ni Bibi Emiliana Mayowa Kisabago aliyewahi kuwa Katibu Muhtasi ofisi ya RDD -MWANZA kuanzia mwaka 1973 kuendelea .Mama huyu ni mwenyeji wa kijiji cha Katoma mkoa wa Kagera .

Mwenye taarifa ya kijana huyu au mama huyu naomba
tuwasiliae kwa namba 0655 297783
au email: osicstz@yahoo.com
Natanguliza shukrani
Mdau Dar

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 21, 2010

    Hi, jaribu weka details kamili sio nusu nusu, kwani "Masanja ni wengi tu weka jina lake kamili, alisomea shule gani na mwaka gani, au chuo gani, mara ya mwisho alikuwa anafanya nini na anaishi wapi, ikiwezekana basi weka hata picha yake!!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 21, 2010

    Wewe anony huoni kwamba huyu baba anamtafuta mwanaye ambaye anakumbuka mwaka tu aliozaliwa kwa kuwa alimuacha huyo bibi na ujauzito? sasa atajuaje details zake wakati alimkataa? au alimkimbia au mazingira yalisababisha chochote?

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 21, 2010

    Kabla ya ku-post kitu cha muhimu, kisome na kukihakiki makosa kwanza. Haiwezekani yeye azaliwe 1970 halafu miaka 3 baadae (1973) awe Katibu ofisi ya RDD!

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 21, 2010

    anony wa tatu kutoa maoni, nadhani una frustrations fulani, hauko sawa kabisa. jaribu kujipumzisha au punguza mawazo. dah umenisikitisha sana!! hebu soma tena hiyo post!!!
    Martin

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 21, 2010

    Wewe hapo juu unayekosoa ndio unatakiwa usome vizuri....Mmeambiwa mtoto alizaliwa mwaka 70 na mama wa huyo mtoto ndio alikua anafanya kazi rtd mwanza mwaka 73....

    Mimi kwa huyo baba swali langu ni hili ilikuaje upoteane na mama watoto wako na mtoto wako muda wote huo? Au ndio wale wazee wa zamani deadbeat dads wenye fikira potofu za kukimbia majukumu na kutegemea watoto watawatafuta wakiwa wakubwa?

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 22, 2010

    ile nyimbo ya q chif " si ulinzaa wewe ukanikataa sasa iweje unaona ninafaa" miaka 40 jamani hapana this is three much!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...