
Watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu wanaotoka Kikundi cha New Hope Family Street Children jijini Dar es Salaam, wakiandamana huku wakiwa na mabango yenye ujumbe unaoitaka Jamii na Serikali kuwajali kwa kuwapatia haki yao ya kupata elimu na maisha mazuri. Watoto hao ambao asilimia kubwa wanaishi mitaani katikati ya Jiji walifanya maandamano hayo kivyao baada ya kutoalikwa kwenye shughuli mbalimbali za maadhimisho ya Siku ya Mtoto Afrika leo.

Mkurugenzi wa Maendeleo ya Jamii wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Leoni Msimbe (kulia) akiangalia michoro ilichorwa kwenye kuta za jengo la Watoto Muhimbili kwa msaada wa OTIS. Kushoto ni Esther Micahael ambaye ni Mhandisi Mauzo wa OTIS

Mkurugenzi wa Maendeleo ya Jamii wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Leoni Msimbe (kulia), akiwalisha keki watoto wanaopata matibabu kwenye Hospitali ya Muhimbili jijini Dar leo.

Watoto wanaopata matibabu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Dar es Salaam, wakipuliza kuzima mishumaa kwenye keki iliyoandaliwa wakati wa uzinduzi wa michoro iliyochorwa kwa msaada wa Kampuni inayotengeneza lifti ya Otis kwenye Jengo la Watoto la MNH, ikiwa ni moja ya shamrashamra ya maashimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika jijini leo

Mkurugenzi wa Kampuni ya OTIS, Justine Lyatuu
(kushoto) akigawa zawadi kwa watoto wakati wa hafla hiyo.
AIBU NA TUNASIKITISHA TANZANIA....DUH!
ReplyDeleteWATOTO WAKIBONGO HUYO 'WINNIE THE POOH' KATUNI WANAMJUA? ANAHUSU NINI KWA MAADILI YAO?.... TUMESHINDWA KUWA NA KATUNI ZINAZOFANANA NA UTAMADUNI WA KWETU WENYEWE JAMANI?? AIBU TUPU.