
Mwanaidi Hassan, mcheza netiboli nguli wa Jeshi stars, akilia kilio cha furaha baada ya
kutangazwa mwanamichezo bora wa mwaka 2009.

Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Idd Kipingu akimkabidhi tuzo na zawadi ya sh. milioni moja, mwanamichezo Bora wa TASWA, Mcheza Netiboli wa timu ya Taifa na JKT Mbweni, Mwanaid Hassan katika hafla iliyofanyika punde kwenye Hoteli ya New Afrika, Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Mshindi wa tatu, mnyenyua vitu vizito, David Nyombo na Golikipa wa Simba, Juma Kaseaja. Anmayeshuhudia ni Mwenyekiti wa TASWA, Boniface Wambura

Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Serengeti, Mark Bomani akimkabidhi Juma Kaseja tuzo ya mwanamichezo bora wa mwezi Januari 2009.

Mwanamichezo Bora wa mwezi Decemba 2009, David Nyombo ambaye ni bingwa wa kunyanyua vitu vizito, akikabidhiwa tuzo ns zawadi ya sh. 300,000.
OT:: Nilikua naangalia post za zamani za blog yako ...yeah niko bored Nikaona hii picha...what happened ankal wangu..within four years span ume baloon hivyo? Please watch out hizo lunch offers na party unazozipata kila siku...chukua rain check kama unaona aibu kukataaa wasije wakatuulia bure na macholesterol bado tunakuhitaji. Hebu jinagalie tu mwenyewe duh utamu wa sindimba"
ReplyDeleteyani mwana michezo bora wa mwezi anapewa zawadi ya shilingi laki 3 tu????!!!! jitihada zoteeeeeee unapewa lakin 3???? tutaendelea kweli kimicheza kama mambo yenyewe ndio haya?? laki 3 si inaishia kwenye vocha ya simu tu!!!!
ReplyDeleteMAXIMO alikuwa anambania tu JUMA KASEJA, heri mkataba wake umeisha aende kwao BRAZIL akauze njugu hakuna Nchi wala Club itakayomchukua, kwa ukocha gani? miaka yake 4 ya ukocha bongo hakuna taji lolote.
ReplyDeleteHongera Juma Kaseja
ReplyDeleteUmependeza na umetoka kiproffessional zaidi ndani ya suti yako.Hongera