Bwana Michuzi:
Kwa niaba ya New England Umoja, tunapenda kuwaalika jamaa na marafiki wote kwamba kutakuwa na shughuli za Soka Fest 2010 kuanzia Julai 2 hadi Julai 4, 2010 hapa Massachusetts.

Huu ni mwaka wa tisa toka 'New England Umoja' uanze shughuli hizi hivyo tunaomba watu wajitokeze kwa wingi.
Kwa maelezo zaidi angalia
www.newenglandumoja.net

Au wasiliana na Katibu wetu Bwana Salum Salum (617) 308.2971
Tunatanguliza shukran!
Isaac A. Kibodya,

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 22, 2010

    Vizuri sana bwana Michuzi kupata habari ya hii wikiendi..! Nimefanikiwa kuudhuria Tamasha hili miaka miwili sasa kwa kweli nilifurahi kuona Watanzania wengi wanafurahi. Michezo ilikuwa ni mizuri, chakula safi (ng'ombe mzima) walimuangusha...!

    Tutaonana Tena,
    Mtanzania,
    Dallas, TX

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 23, 2010

    Ahaaa mbona dj richmaka yuko bongo acheni uongo, but party yao inakuwaga bomba kishenzi

    Mdau

    new york

    ReplyDelete
  3. abdulla kh hassanOctober 15, 2012

    Kwa masikitiko makubwa nimepokea msiba wa aliyekuwa mhadhiri muandamizi na Mhariri Mtendaji wa Research News Later katika Chuo Kikuu Cha Taifa Cha Zanziba. Profesa Mohammed A. Mohammed.
    Daima nitamkumbuka sana kwa wema, ukarimu na ukakamavu wake katika kulisukuma mbele gurudumu la elimu nchini.
    hadi anaaga dunia alikuwa natumikia kitengo cha utafiti na ushauri, suza.
    profesa ingawa hatunawe kiwiliwili lakini mawazo yako mema na mazuri tutayaendeleza daimaa.
    inshallah allah akulipe kheri nyingi na malipo mema.
    INNA LILLAHI WAINNA ILAIHI RAJIIUN...

    MWANAFUNZI ,SUZA. 2003-2006
    ABDULLA KH HASSAN

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...