Kaka Michuzi,
Ni matumaini umzima pamoja na crew yako yote.
Ni matumaini umzima pamoja na crew yako yote.
Naomba nitoe dukuduku langu juu ya kituo hiki.
Kituo hiki kinaonekana kuwa na walakini hususan kwa wenye kununua umeme wa pesa nyingi. Utafika pale na uhakika wa pesa uliotoa kulingana na umeme unaouhitaji, ukirogwa kutupa jicho pembeni tu umeliwa. Pale zitapunguzwa pesa zako na utaambiwa umetoa hela pungufu pale utakapoanza kuuliza kwa nini umepewa umeme kidogo na ulioutaka.
Nimefikia kusema haya kwani hii leo alfajiri tukio hili limemtokea tena mume wangu kwa mara ya pili. Mara ya kwanza alifika pale kweupe akitaka umeme wa laki mbili na akatoa laki mbili, umeme ukatoka wa laki na nusu. Kuuliza vipi mbona umenipa pungufu akaambiwa kwa kujiwa juu tena kuwa umetoa laki na nusu na si laki mbili! Kwa vile si mpenda kuzozana akamwambia tu mimi najua nimetoa laki mbili lakini kama wewe unasema nimetoa laki na nusu na iwe wewe ndio mkweli na yeshe. Akaondoka zake.
Leo asubuhi, mimi mwenyewe nilimhesabia pesa na kumpa laki moja, kufika pale akatoa pesa then akaangalia upande kuja kurudisha macho anamuona jamaa katoa mkono kwenye droo la pesa au chini ya meza huku kashika pesa akiwa anaiangalia angalia, mume wangu akamuuliza vipi? Hiyo hela ina mashaka??? Akajibiwa ndio ni feki! Mume wangu akamuuliza kwa hiyo ulikuwa ushaingiza umeme wa laki tayari? Akajibiwa hukutoa laki umetoa elfu tisini.

Hapa ni kwamba keshapigwa elfu ishirini, kumi aliyoipunguza katika hesabu ya laki na kumi ambayo alisema feki aliyoitoa kwenye droo au chini ya meza. Kama kawaida hakubishana ila akamwomba basi kaa na kadi mi nipeleke umeme nyumbani nikiwa naenda kazini nitakupitishia elfu kumi, jamaa akagoma, ikabidi atoe simu yake aiwache.
Kufika nyumbani akaniambia ulinipa kiasi gani,
Kufika nyumbani akaniambia ulinipa kiasi gani,
nikajibu akaniambia basi kile kituo kina matatizo.
Tulipokuwa tunaenda kazini tulipita pale kituoni akaacha ile hela na kuchukua simu yake akarudi akaniambia that guy is guilty! He could not look at me straight into my eyes!
Je ulishawahi kupata malalamiko kama haya kutoka kwa mtu mwengine juu ya kituo hiki?

Dada next time nenda na mume wako alafu mumewe aangalie pembeni wakati wewe unakodoa macho kama chura kabanwa na mlango uone kama jamaa atajaribu hako kamchezo kake kachafu. Akithubutu tu, weka physical description zake hapa watu tumshughulikie. Hapa kwetu justice inapatikana mtaani tu na sio mahakamani.
ReplyDeletetanzania inasikitisha sana.wizi kila angle,kila level.hawa watu wa aina hii wako karibu kila ofisi nchi hii.wote ni mafisadi kama wale wa EPA tofauti ni nafasi tu hawana ila ni wale wale...
ReplyDeletenext time andika number za pesa kwenye karatasi au toa photocopy hizo pesa ili mkimwitia polisi kuwepo na ushaidi otherwise anaweza wakatalia kwamba mmempa pungufu au feki na hamtakuwa na ushaidi wowote ule inawezekana ndio mchezo wake huo au la kabda hamjampa pesa mwelezeni mnajua tabia yake chafu ili asiwalalie tena
ReplyDeleteHao jamaa mimi nawafahamu. Ni lile kabila la wapenda pesa!!!!
ReplyDeleteNi matapeli wazoefu
simple.next purchase dont dare go there!
ReplyDeletenext time mkienda kununua msimpe cash hapo ndo usanii unapoanza huyo nyumbu mumpe hela mojamoja na awe anaangalia kama ni feki au la mumpe kumi moja baada ya nyingine na namba muwe mmeandika ili asije akabadili na hela feki inaelekea ana noti feki na huwa ukizubaa anabadilisha na hela yako halali ni mpuuzi sana mkamstaki makao makuu ya tanesco wamuwekee mtego ili akose ajira akawe kibaka achomwe moto malipo ni hapa hapa za mwizi arobaini, poleni sana ina hii ikera sana
ReplyDeleteTunashukuru kwa taafifa, sisi ndiyo kazi yetu kuwakomesha watu kama hao. Tutampelekea moto very soon. kaka pole kwa kilichokukuta. Dawa ya motot ni moto.
ReplyDeleteMdau mwenye machungu na vifisadi na mafisadi papa.
Mimi nilishakwenda pale kununua umeme wa laki moja nikaambiwa kuna not ya elfu kumi ni fake, ikarudishwa baada ya kuhesabiwa...kule ndani ni giza kidogo na kwa kile kidirisha sikuona alichofanya kama ni kubadilisha ile noti au sijui alifanya nini...niliambulia kununua umeme wa elfu tisini lakini hadi leo naaamini ule ulikuwa mchanga wa macho yaani nilifanyiwa ujanja...kwa habari hii naamini kwamba niliibiwa na wewe uliyeleta habari hii hapa na mimi si watu pekee kutupiwa changa...wengiwameshaumia na hatua zichukuliwe au kama hazitachukuliwa tuepuke kununua umeme wa hela nyingi pale!!
ReplyDelete