MAREHEMU ELISAELI PETER SWAI

Familia ya Mzee Elisaeli Peter swai (aliyefariki 11/05/2010 ) wa Kinondoni, Dar Es Salaam inapenda kutoa shurkani zao za dhati kwa ndugu jamaa na marafiki walioshiriki kwa njia moja ama nyingine kwa hali na mali katika kufanikisha kumsindikiza Baba yetu mpendwa Mr Elisaeli Peter Swai katika safari yake ya mwisho hapa Duniani na kuupumzisha mwili wake tarehe 15/05/2010 hapo shambani kwake Kimara. Raha ya Milele umpe ebwana na mwanga wa milele umuangazie apumzike kwa amani – Amen

Mungu awabariki sana ndugu jamaa na marafiki wa Arizona na watanzania wote waishio Marekani ambao waliweza kuwafariji kwa hali na mali Peter Kilaba Swai (Mtoto wa Marehemu) Laura Swai (Mkwe wa Marehemu) na Stella Elisaeli Swai (Mdogo wa Marehemu) katika kipindi chote hiki kigumu.

Mungu awabariki sana watanzania waishio
Uholanzi kwa faraja zenu zilizomfariji dada yetu
Happy Eliseli Swai (Mtoto wa Marehemu).

Mungu awabariki sana ndugu , jamaa na marafiki na watanzania wote waishio Uingereza kwa upendo wao hekima na faraja walizowapatia Hellen Mammy Elisaeli Swai (Mtoto wa Marehemu) na Richard Shem Sekuba (Mkwe wa Marehemu) katika wakati huu mgumu
Mungu awabiriki ndugu , jamaa , marafiki na majirani wote wa mzee Swai pale Kimara, ndugu , jamaa , marafiki na majirani zetu pale Kinondoni , Mastaff wa Shirika la BIMA (NIC) Tanzania, Wachungaji na Waumini wote wa kanisa la Lutheran Kinondoni , Madaktari na Wauguzi wa Hospitali ya Dr. Mvungi Kinondoni.

Mungu awabiriki sana watu wote walisafiri toka moshi na pande zote za nchi na Dunia kuja kuhudhuria mazishi ya Baba yetu mpendwa Mzee Elisaeli Peter swai.

NI VIGUMU KUMSHUKURU KILA MTU ALIYESHIRIKI KWA HALI NA MALI KWA KUTAJA MAJINA ,BALI TUNAOMBA MZIPOKEE SHURKANI ZETU ZA DHATI KWA PAMOJA , SISI FAMILIA YA MAREHEMU TUNASEMA ASANTENI SANA HATUNA CHA KUWALIPA NA MUNGU AWABARIKI MUENDELEZE MOYO WENU HUU MLIOTUONYESHA KWA YOYOTE YULE
ASANTENI SANA NA
MUNGU AWABARIKI SANA

BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA JINA LAKE LITUKUZWE AMEN
KWA MAWASILIANO ZAIDI WASILIANA NA
Ludovick Kileo ------- +255787554554, +255652509316
Mzee Ruben Swai --- +255784614050
Gerald Swai ---------- +255755548707



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...