Rais wa RBP OIL& Industrial Technology Ltd,Mama Rahma Al Kharoos akiongea leo na waandishi wa Habari waliofika katika hotel ya South Beach,Kigamboni.Mama Rahma leo ameweza kuwakutanisha watoto wanaoishi katika mazingira magumu toka katika vituo 6 vinavyolea watoto hao pamoja na timu ya Taifa ya wanawake (TWIGA STARS) kwa kuweza kula nao pamoja chakula cha mchana na watoto hao ikiwa ni katika kuadhimisha siku ya Mtoto wa Afrika,vituo hivyo ni NEW LIFE,HANANASIFU,UMRA,TANZANIA MITINDO HOUSE,MOTHER TERESA pamoja na CHACHUMA.Nahodha wa timu ya Twiga Stars,Sophia Mwasikile akitoa shukrani zake za dhati kwa niaba ya Timu hiyo kwa Rais wa RBP OIL& Industrial Technology Ltd,Mama Rahma Al Kharoos kwa kuwaandalia hafla hiyo siku ya leo.
Meneja uhusiano wa kampuni ya RBP OIL& Industrial Technology Ltd,Ibrahim Khatrush akiwa pamoja na Afisa kutika Ustawi wa Jamii,Bi. Sophia Ally wakipanga namna watakavyogawa tisheti kwa watoto ikiwa ni katika kuadhimisha siku ya Mtoto wa Afrika inayoadhimishwa tarehe kama ya leo kwa kila mwaka katika hotel ya South Beach leo.
watoto wakipata chakula cha mchana katika hotel ya South Beach,Kigamboni leo.
baadhi ya wachezaji wa timu ya Taifa ya wanawake (Twiga Stars) wakiwachukulia chakula watoto waishio katika mazingira magumu.
watoto wakiogelea kwa furaha
Rais RBP OIL& Industrial Technology Ltdakiwa katika picha ya pamoja na watoto waishio katika mazingira magumu toka vituo mbali mbali pamoja na timu ya Taifa ya wanawake Twiga Stars.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 17, 2010

    Mungu akubariki mama Rahma kwa kuwakumbuka watoto hawa wanaohitaji malezi na upendo kutoka kwa jamii nzima.Hakika nao wanatamani kuishi kama watoto wengine wanaoishi na kulelewa katika mazingira mazuri na kupata mahitaji yao ya msingi.Ni changamoto kwetu wote katika jamii na hasa wale ambao MUNGU AMEWABARIKI kwa kuwa na kipato kizuri kuwasaidia watoto hawa.MUNGU akuongezee zaidi ya kile unachotoa dada.

    (Mwanajamii kweli ukiwatembelea na kuwaona watoto wanaoishi katika mazingira magumu machozi yatakutoka hebu fikiria wewe au mtoto wako angekuwa kama hawa utapata picha halisi)

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...