Ankal naomba urushe hii ili wadau
waweze kunisaidia kwa maelezo yao.
Wadau jana nilipata bahati ya kwenda kushuhudia mechi kati ya Taifa Stars na Brazil. Ninalo dukuduku langu ambalo ningependa wana blog hii ya Jamii wanisikie.Na naomba nieleweke haya ni mawazo yangu binafsi.Katika ile mechi mabango ya matangazo yaliyokuwa yamezunguka kiwanja kizima ni mabango ambayo kiukweli yalikuwa si matangazo yaliyozoeleka hapa nchini: Brahma; Embratel; Germed; Fazum 21, Extra extra; Seara, Lupo Lupo na mengine mengi tu ambayo nilikuwa sijawahi kuyasikia hapa nchini kwetu.
Matangazo yetu kama NMB na Serengeti yalikuwa nyuma ya hayo Matangazo ya kigeni, kwa hiyo hayakuwa yakionekana kiurahisi kwa sisi ambao tulikuwa tumekaa mbali kidogo.
Dukuduku langu ilikuwaje matangazo ya Kibrazil yakapewa kipaumbile sana. Ningependa kujua ni kipi kilipelekea ile hali na ikumbukwe kuwa tumetumia gharama ambayo haijawahi tokea nchini kuleta timu yenye hadhi kubwa kama Brazil?
Mimi kitaaluma ni Mwana Uchumi na sikujiingiza kwenye malambuno ya Kina Kamau kwa sababu nilitaka kuona kwanza mechi yenyewe, na isitoshe nakuabaliana na watangulizi walioelezea kuwa tusiangalie sana hela iliyoleta timu bali tuangalie matunda yatakayopatikana baada ya ile mechi.
Wakati mechi ikiendelea nilitumia mda mwingi kuyaangalia yale Matangazo na Maswali mengi yakawa yanakuja kichwani mwangu, Hivi ni kweli tunajitangaza hapa au wale tuliowaleta ndio wanajitangaza. Mechi ya jana iliweza kuonekana nchi nyingi sana ikiwemo Tanzania, je haikuwa muda muafaka kwa sisi kuweka bidhaa zetu ili watu wajue Tanzania kunapatikana nini. Kiukweli mimi nilikerwa sana na ile hali, iwaje watu tuliowalipa hela wao ndio wawe vinara kutangaza bidhaa zao.Sasa ilikuwa na maana gani kuwalipa?
Hapa kweli tutaacha kukubaliana na Kamau kuwa tuna misuse resources? Yani zile Dakika 90 zilikuwa zina maana sana kwetu kujitangaza. Ila kilichofanyika jana ni kukuza uchumi wa comredi Luiz Inacio Lula da Silva na watu wake katika nchi ambayo tunasema tunatamani uchumi wetu ukue kwa kuanzia na nyanja ya matangazo.
Jana mimi nilichotaka nacho kiwanjani ukiacha maumivu ya kufungwa vibaya ni majina ya bidhaa ambazo sijui kichwa wala miguu yake sema nikutano nayo kwenye moja ya Maduka yetu hapa nchini nitamwambia Muuzaji anipatie nikatest Kwa sababu jina nalijua ila kilichomo sikijui. Hapo nitakuwa nimekuza Uchumi wa nani? Jibu litakuwa moja tu,Brazil.
Watanzania tuamke haya ni mambo madogo madogo tu ila tusipoyachukulia kwa Uzito wake yanakuja kutagharimu mbele ya safari. Inaelekea wengine wanaweza kusema kuwa wabrazil walikuwa na rights zote kufanya hivyo kwa mfano Tv channel yao ilinunua haki.
Hapo ndipo yatapotokea maswali mengi, Bilioni tatu walizosema zimetumikaje? au kuna wajanja wameweka hela Mfukoni. Inabidi tuelezane ukweli.
Upande wa pili wa dukuduku, nafikiri TFF wamejionea wenyewe hali ya kiwanja.Kiwanja hakikujaa, huku kukiwa na tetesi kwamba tiketi nyingi zilinunuliwa.Inawezekana kweli mtu akanunua tiketi ya bei ya juu kiasi kile hasiende kiwanjani? Sipendi kuingia kwa undani suala hilo ila nategemea kupata majibu mengi baada ya TFF kutoa report ya mechi.
Nachotaka kuongelea hasa nikuwakumbusha TFF kwamba wapenzi wa mpira hapa nchini ni wale ambao wana kipato cha kawaida kabisa.Liwe basi ni fundisho kwa mechi zitakazokuja, TFF wafanya liwezalo kundi hili nalo lijumishwe.Jana hatukapata kabisa radha ya ushangiliaji. Inaingia akilini kweli mtu kalipa 200,000 pale VIP aanze tu kumshangilia Ngasa alivyojitahidi kupenya ngome ya Brazil!
Kwa leo nimeona nizungumzie hayo ila nikipata nafasi tena nitazungumzia hii kero ya wandishi wetu wa Habari kukosa ushirikiano kabisa kutoka kwa wadau. Hali ilikuwa inatisha wakati Brazil ilipowasili nchini juzi usiku, Waandishi wa kimataifa walipewa mwongozo mzuri na kupata picha ambazo walizitegemea. Ila wa kwetu sasa ambao binafsi mimi niliona ndio wapewe nafasi zaidi,kupata picha ilikuwa kutumia ujanja ujanja tu na uzoefu wao wa siku nyingi. Hii hali imekuwa ikijuridia rudia kila mara wakati timu za kimaifa zinapowasili nchini. Inahitaji ijadiliwe kwa kina ili siku za usoni tuone mabadiliko.
Wako Mdau Hans.
mdau hao ni mabingwa mara 5 wa dunia hivyo hao sio wa kawaida kama unavyofikiri wewe au unaona wamekubali kucheza tanzania hivyo wako sawa na misri au cameroon ,please kisoka jamaa wanaheshika dunia nzima shukuru Mungu wako umefanikiwa kuwaona live hao jamaa timu nzima gharama yao ni bajeti yetu ya nchi kama miaka 5 hivi,pia wanapokea maombi dunia nzima wakacheze mpira
ReplyDeleteMdau Hans. Naamini kama watanzania wengi tungekuwa na uwezo wa kufikiria na kujiuliza maswali kama ulivyojiuliza pamoja na kuchangia au kutaka ushauri au kutoa ushauri basi tungeweza kufika mbali zaidi. Kwa upande mmoja au mwengine watanzania wengi ambao wapo katika nafasi muhimu (nyeti) mbalimbali wamekuwa wakipelekwa pelekwa na wageni ikiwa ndio njia pekee yao ya kujipatia manufaa au SIFA. Ukiachilia mbali swala la waandishi wa habari kupewa nafasi, sasa hivi nenda uwanja wa ndege wa JKN Airport wewe mtanzania utasachiwa hadi nguo za ndani na mgeni anapita (naomba ieleweke kusachiwa ni kitu cha kawaida ila pale mgeni anapoaminika). Inabidi watanzania tuamke na tuanze kujali na kupenda vyetu. USIPOJIPENDA AU MSIOPOJIPENDA AU USIPOJIWEKA JUU NANI ATAKAE KUWEKA JUU?
ReplyDeleteNi mawazo tu..
Mdau Ubatani
Yaani watu walimshikia bango nyang'au Kamau mpaka nikaogopa kana kwamba manyang'au wote waliopo bongo wanaweza kufanyiziwa! Mie ni mmoja wa watu waliopinga hii ziara, sababu nawajua hawa wenzetu, ni matajiri kushinda sisi, nchi yao inongozwa na weupe, kuna kaubaguzi sana nchini mwao, hasa kwenye swala la madaraka na uongozi, maana weusi wanaonekana bado nyani!
ReplyDeleteAnyway, swala la matangazo mie nalo nililiona, angalau mie nilitazama kwenye mtandao, hii ina maana wakati wa kuandika mkataba baina ya TFF na Wabrazil, sie hatukuangalia na kusoma mkataba vizuri, tulikurupuka kuwataka wabrazil waje kucheza kwa kila hali, tukasahau walalhoi, watoto wa shule za msingi, yatima na wasiojiweza, sidhani hata vijana wetu kwenye soccer academies walialikwa na kupewa nafasi ya kuangalia mchezo wajifunze, wao TFF walitolea macho maswala ya viingilio na kuanza kuyapigia maesabu huku wakisahau "clauses" za kwenye mkataba, ila sidhani ndugu yangu kama hilo ni geni kwetu, sie huwa hatuwezi kusoma mikataba kabisa, hasa tunapojua kuna kaulaji ketu apo, mifano iko mingi na bado inatutesa leo bongo.
Wenzetu huwa wanaweka vipengele kibao na vya kuwasaidia wao, hasa "the ones in small print"!
Sio swala hilo tu ndugu yangu, ila hawa wabrazil kama tungewatumia vyema kweli tungefaidika, hasa kwenye hilo swala la matangazo ya bidhaa zetu nchini, maswala ya kijamii achilia mbali swala la mbu tu! Kama vile watoto yatima, elimu na michezo mashuleni.
Hebu wazee siku moja angalieni hawa jamaa wakicheza mechi ya kirafiki na sema England, kila kitu pale uwanjani kitakua kinawahusu FA ya England, Brazil wanachukua mshono wao BASI!
Jamani tuwe waangalifu na mikataba, tusahau 10% na ujanja ujanja, TUSOME HAYO MAANDISHI KWA MAKINI SANA, HASA YALE MAANDISHI MADOGO MADOGO!
HATA MIE NDIO HILO NILIKUWA NA LALAMIKA MATANGAZO YETU BIA SERENGETI WANYWAJI HATA WAKIZIDI SIO SANA NJE BANK YA HAPAHAPA SIJAONA ZA WEBSITE KUHUSU UTALII BONGO AU MAJI SAFI AU MAJI UHAI AU SIJUI SIAGI ZA SIMBA UTUMBO MTUPU SIJUI LINI TUTAENDELEA, NA NCHI IMEONESHA HAIJALI.
ReplyDeleteJENGINE NCHI IMEONESHA HAIJALI MASIKINI HATA KUSHUSHA TICKET TZSH ELFU 5 na 500 TUMESHINDWA MPAKA Tzsh 10,000 ? AIBUUUUUUUUU NAU ONEVU WAWATU WAHALI ZA CHINI BAHATI HIZO HAZITOKEI.. Juma
Mdau Hans,tupo pamoja
ReplyDeleteHongera kwa kuweza kuuzulia mchezo wengine tuliambulia highlights tu kwenye internet.
Mimi nakubaliana na wewe katika concerns zako lakini nachosema ni kwamba kama ulivyotumia busara yako ya kwanza ya kutolumbana na hoja ya bwana Kamau kutona na kusubiri mazao ya investment, nafikiri utumie busara hiyo hiyo kujua hawa jamaa waliotangaza walilipa kiasi gani. Kumbuka matangazo anapewa the highest bidder.Na watangazaji wanaangalia kama ni worth kutumia hiyo hela kutangaza(Return on Investment).Kwa hiyo nafikiri ni muhimu TFF wajibu haya maswali kwa wananchi kabla hatuja washutumu.Tayari tunajua wamechemsha kwenye viingilio ndio maana wamekosa watu.
Mchangiaji
Wenye akili zao Kama kamau walishawaambia Tanzanians you are party animals and the most funniest creatures in the world!! Wasio na akili zao waliamua kumshambulia genious kamau who foresaw all that shit. Anyway Mdau Hans kwa kukusaidia tu mi hapo nimeambua bidhaa moja tu, hiyo BRAHMA. Hiyo ni Bia aka Bierre aka Matingasi aka maji ya uzima, ni bia ya kibrazi, zipo hapa UK hasa zinapatikana kwenye supermarket za Somerfields Cooperatives na zinauzwa kwa bei ya promotion two quids per 4pack! ni bia imported fro brazil! Hiyo smbratel nadhani ni mtandao wa simu wa brazil!! nikirudi kwenye mshangao hata mi kwakweli nilipoona picha hapa michuzi nilishangaa kuona hiyo brahma beer nikajua hiyo bia labda kuna kampuni linaimport bongo from brazil. lakini hiyo mechi Ina mazingaombwe meng. Kwanza ujue Coordinator wa mechi hiyo ni Mbrazil nadhani ulimwona wakati akitambuliswha na tenga kwa waandishi. nilishangaa mechi inapigwa kwetu hela tumelipia sisi lakini coordinator katolka kwao, na walimuelezea kabisa kwa waandishi kwamba yeye ndo kafanikisha ujio!!!! Anyway hapo kuna kiini macho manake nadhani hayo makampuni ya brazil NAyo yalikamuliwa hela za ufadhili. Cha ajabu tuliambiwa mechi itatuuza badala yake mechi imeishia kutangaza bidhaa za makampuni ya brazil! hiyo brahma ni bia hara wazingu wanaopenda sana hapa iko poa sana!!! cha ajabu Tena tynaambiwa eti serikalo haikulipia hata senti moja wakati tunafahamu serikali ilitenga shs billioni Sita na kuteua kamati chini ya waziri ili kuhakikisha timu moja kubwa iataletwa Tanzania wakati ikielekea Africa kusini!! Any Tanzania ukiifikilia sana waweza pasuka kichwa. tunafanyana sana wajinga!!! tumekalia maneno meeeeeeengi wakati hamna kitu!! Mimi naamini sana kuwa kamau yuko sahihi sana!! Tanzanians are the funniest creatures I have ever come across!!!! kaeni na nchi yenuna ujinga wenu usiotibika
ReplyDeleteMichu, wapostie waTanzania wanaoishi Uingereza waangalie kipindi leo saa 4 usiku (za Uingereza) kinaitwa Albino United.
ReplyDeleteHicho kipindi kinazungumzia ushirikina na mauji ya albino yaliyotokea Tanzania.
Kipindi: Albino United
Channel: More 4 (kwenye Freeview iko namba 14)
Muda: 10PM BST
Waangalie wachambue.
Cheers
Mdau Hans, kila tangazo location ya kuweka tangazo lina bei yake. Kumbuka mchezo ulikuwa ukionywesho kwenye tv za Brazil na kwingine duniani. Tangazo la uwanjani sio lazima kuwaonyesha waliopo uwanjani tu bali pia wengi ambao wanaangalia tv. Kw mfano wadau tuliopo kiwanja wengi tuliona kwenye mtandaoo live!
ReplyDeleteKwa kifupi hayo matangazo yalikuwepo kwenye bei za VIP ambapo uwenda product zatu awakuweza kulipia VIP price.
-Mdau Kiwanjani
we mwana uchumi bure kabisa utakuwa ulikuwa unakariri kupass mitihani rudi shule usome kwa uelewa..
ReplyDeleteyani hujui kwanini bango moja linawekwa mbele lingine nyumba
unataka waweke bango la NMB mbele hata kama hawajalipa hela yakutosha kuwekwa mbele? jinga kabisa
Mie nashangaa mnamshambulia Hans sijui kwanini? Yeye kauliza kwanini matangazo ya bidhaa zetu hayakuwepo, sasa hilo lilikua swala la TFF kutafuta orders za adverts toka TBL, Voda, Zantel, AZAM etc etc. Swala kwanini TFF hawakuangaika kupata hayo matangazo ndo tungependa kujua, sidhani kama makampuni yetu yangeshindwa kulipia haya mabaongo wazee!
ReplyDeleteTukumbuke hizi ni nchi sio club, Mchezo umeonyeshwa nchi zingine na Brazil sababu TFF hawakusoma ama walikubali kijinga kusaini mkataba wakijua ivyo, na tunajiuliza inakuaje? Timu ya taifa ya nchi ikicheza nyumbani tunategema mcheza kwao hutunzwa bila kujali unacheza na Brazil au timu toka Mars! Ikimaanisha kila kipengele na ushee lazima kilalie nyumbani, wazee mkinieleza TFF hawakujiandaa ntawaelewa lakini sio swala la VIP au nini sijui!
Hapa TFF walichemsha. hawakusoma mkataba vizuri, walikurupuka tu na tena imekua habari ile ile kuhusu Tanzania na mikataba!
Mdau Hans labda nikwambie tu, ungefanya utafiti wako kwa kina zaidi. Ni kwamba, TFF wapo kibiashara zaidi. Yale matangazo yamelipiwa ushuru kwa TFF. Zile ndio pesa zinazowawezesha kurudisha gharama ya kuwaleta Brazil. Sasa kwa mfano ukiweka tangazo la NMB mbele ili ijitangaze kimataifa wakati kuna tangazo la nje ambalo lingeweza kulipia mara 20 ya pesa ambayo NMB ingetoa, huoni kwamba ni busara kuweka matangazo ya nje mengi zaidi ili TFF kuweza kupata pesa nyingi zaidi?
ReplyDeleteNawasilisha.
Thank you Mr. Hans for mentioning all these problems not including the fact that few people came to watch the game contrary to what mentioned early that the stadium is going to be packed with thousands of spectators, I said once and i say now Tanzanians are pure low minded people they like to show off, and most of them like short cut we kenyans even though we share same problems as many developing countries but we can not make this kind of dummy deal only few countries in the continent can do that like Zimbabwe. Tanzanians are corrupt and like to talk fast to taperi you. It doesn`t matter how many facts you people are going to bring in this blog Tanzania will NEVER be like KENYA you will always kiss our ass you are down and will continue to be down before you talk shit about Kenya you should blame your decision to go to socialism I know you are starting to wake up but I tell you what, you are still behind in the darkness. Yes in Kenya we killed each other because of controvesial Election and that is what we are but you Tanazians are changing corrupt leaders one from the other you are so scared of your government even if it doesn`t represent you and your children you still kiss CCM ass day and night NOT in Kenya my Friends you need to be tough to be Kenyan leader. Brazil game was another scame you don`t see it now but the impact of it will start showing, few days ago your president refused to increase you more Salary but he can sneaky and find money to pay Brazil to come to play in his stadium. I guess he did for himself and his family. You were told the 200,000 Shs tickets were sold out but I saw many empty chairs on the same podium so how are you going to tell your folks about that? Scared of CCM? Wake up Tanzanians This is not the time of Stone Ages. Don`t continue to be Dummies as you are, learn from Kenya be like Kenyans. I have told you the trueth and you are going to live with it, Kenya is better than Tanzania and it will always be.
ReplyDeleteHANS KWELI UMEONYESHA KUWA SHULE YAKO YA UCHUMI NI YA KUDESA PALE CHINI KWENYE MDIGRII UDSM!
ReplyDeleteWewe mchumi gani usiyejua kanuni za kutangaza matangazo? Kwa kuwa uwanja uko kwenu basi watu wawekewe matangazo bure tu bila kutoa pesa au wakatae kuweka matangazo ya nje yaliyolipiwa pesa kwa kuwa hatujui maana yake?
Kama hao wengine kina Lager Serengeti na wengineo wameshindwa kulipa fees za matangazo basi matangazo yao yawekwe tu? Uchumi gani wewe umesomea usiyejua kanuni za biashara hata kama ungesoma enzi za Ujamaa bado ungejua kuwa kwenye uchumi huria ni survival for the fittest? Kwa usomi wa aina hii ndio maana watu kama Kamau wanatutukana matusi ya nguoni. Na hao kina UTALII Kama wanaongozwa na watu wa aina yako sichangai kuwa hawakutumia fursa hii kulipia matangazo na kujitangaza walijibweteka wakisubiri dezo, na pengine wengi wao ndio waliokuwa wakipinga sasa mmejua kuwa hiyo pesa haikuwa yenu ya Ujamaa bali ni ubepari na biashara mnaanza kupiga kelele!
Hao walidhamini pambano hilo na haki ya kurusha live pambano hilo lililenga zaidi huko wanakorushiwa game hilo
ReplyDeleteMdau Hans, you have said it all. I feel sorry for your being at the stadium and enduring the humiliation. But you know what, we Tanzanians deserve it. First, didn't it cross our minds why a 1st team would like to pay a 108th? And if the match was financed through TV rights and adverts, then why did we have to cough billions? Wajinga ndio wali wao!
ReplyDeleteUnless TFF gives an account of the income, I believe our tax money has been used to subsidize fanatism. No offense here as I am myself a soccer fan but I believe the decision was purely fanatical.
And I am really bothered by those who say that money is not a problem. They are probably the reason why our country is in such a mess!
WATANZANIA MTABAKI MBUMBUMBU HATA KAMA MMENDA SCHOOL.SASA WEWE NI MCHUMI AND THEN HUELEWI KWA NINI MATANGAZO YALE YALIKUWA SIO YA KI-TZ?MPIRA UMEONYESHWA DUNIA NZIMA NA TV ZA KIMATAIFA HIVYO KUNA MASHIRIKA YA MATAIFA MBALIMBALI AMBAYO YALILIPIA HAYO MATANGAZO FOR THEM TO BE POSTED ON,AND EVERY POSTING SITE HAS VARYING PRICES,THOSE SITES WHICH WILL BE ON A FREQUENT VIEW NORMALLY ARE HIGHLY PRICED.HUU USOMI WA BONGO NI BURE KABISA AND FOR THIS REASON NDO MAANA VIHIYO KIBAO
ReplyDeleteKama 5-1 ni nyingi vipi hapo juzi juzi tu Brazili walipowapa kichapo Portugal 6-2... tazama linki hii
ReplyDeletehttp://www.youtube.com/watch?v=5Iw3X4r4XOM&feature=related
Mchumi,
ReplyDeletemakampuni, mabenki ya Tanzania mtaji mdogo sana wakishindana na makampuni ya Marekani ya Kusni, Asia, Afrika Kusini bila kutaja Ulaya na Marekani ya Kaskazini.
Hivyo mabango ya NMB kufichwa ni dalili ya kuwa na pesa ndogo.
Mdau
Shimoni Kariakoo.
Niliasa kwa kamau tuwe werevu, tusishangirie tu kama mazoba.
ReplyDeleteTumeishia kurambwa pande zote...Ashakum si matusi, kufungwa tumetolewa na Rwanda, tumefungwa na brazili, na si dhani kama tumepata faida yoyote.
Nahisi kwenye hili gemu TFF (Tanzania) Haikua na sauti yoyote zaidi ya ukarimu wetu wa YES Sir, Will do!
Mdau sijasoma barua yako yote ambayo ni refu sana. Lakini kwa ufupi tu ni kuwa je umeshaiona hiyo contract waliyosaign. Unajuaje matangazo yao ilikua party of the contract. Na pia ujue ukubwa wa Tanzazo unaendana na bei . Sasa nyi mkikurupuka tu na kukosoa tutafika kweli kama kilakitu ni kuandika tu bila kufanya uchunguzi?
ReplyDeletenajua kuna watu wasiojua hayo nao watakusupport lakini common lets be serious na kujaribu kufanya research before hatujaandika tu.
Kama ni hela nyingi na unaona uchungu nayo pole Lakini comment yako hiyo ya juu haina merit yeyote
Hans bwana utanifanya nianze kushusha shule yangu ya Marketing bure bure. TFF wameuza advertising space kwa ito kila kampuni ilikuwa na uwezo wa kutangaza kama ingekuwa tayari kulipia hio gharama. Pia bei za matagazo zinategemeana sana na sehemu tangazo lako lilipo. Kwa mfano tangazo kwenye ukurasa wa mbele wa gazeti ni bei ghali kuliko ukurasa wa kati kati. Kaka ni vitu vidogo tu avihitaji msuli sana kuvielewa ila naona we mtu wa msuli kiana
ReplyDeleteWatanzania acheni kulalamika kihivyo!!!Eleweni hata Zimbabwe matangazo hayo hayo ya kiBrazil ndio yaliyowekwa uwanjani na sababu kubwa ni kwamba wale ni wadhamini wakuu wa Timu ya Taifa ya Brazil hivyo katika mkataba wa kucheza na hizi nchi zetu moja ya sharti ni kwamba yawekwe uwanjani yale matangazo sabau mechi itarushwa dunia nzima...TFF waliweka matangazo ya makampuni ya kitanzania kwa nyuma kwa sababu tu nao ni wadhamini wa Taifa stars na sio kwamba eti walilipia siku ile., hivyo basi ichukuliwe tu kwamba ni kama Hidden cost out of total real cost ya kuileta Brazil.. mnachotakiwa watanzania ni kujadili kunyimwa walala hoi ambao ndio wapenzi wa soka nafasi ya kuona mechi ya kihistoria kwa kuwekewa viingilio vikubwa tukiconsider Zimbabwe aliweka viingilio vidogo ili wananchi wao waburudike ..je Tanzania wananchi hawajaliwi na viongozi?????
ReplyDeleteKAMAU UMERUDI TENA NA MATUSI KAMA KAWA?
ReplyDeleteBwanae, masuala ya mikataba sisi hatuwezi. Kwanza wavivu wa kusoma hiyo mikataba. tunachoangalia ni je kuna nafasi ya mtia mkataba kupata ulaji kidogo, halafu tunakurupuka kutia sahihi.
ReplyDeleteJamani, tumeshuhudia juzi juzi tu, mswada wa matumizi ya fedha ya uchaguzi ilitiwa sahihi kuwa sheria na hatimaye kurudishwa tena bungeni kujadiliwa baada ya wachache wenye moyo wa kusoma kuusoma na kugundua mapungufu. Sasa tusilaumu kwa hili, mbona ni homa yetu ya kawaida!! Unashangaa kuiona meli bandarini wakati ndiko maeneo yake??
Haya yalikuwa mambo ya kushinikizwa ili yafanyike wakubwa wajiridhishe, yamefanyika, mnagomba nini? Bwana akisema mtumwa atabisha????? Amkeni bwana, msizungukezunguke huku mkijua? Real Madrid hiyo. Yaani mnatuzuga hivi!!
Wote mliomponda Hans ndio mambumbumbu na ndio mliokuwa mnadesa,ukweli hata kama TFF wamelipwa na hayo makampuni mnapaswa kujiuliza hivi kulikuwa na umuhimu wa Tanzania kuwanyonya watanzania kwa kuwatoza kiingilio kikubwa? pili Tanzania imenufaika na nini, kama ni kisoka tusidanganyane wale wachezaji watanzania most of them wana miaka inayofika jioni kwa football hawana future ya kusema watatupeleka popote from here, pili kama ni utalii mnatakiwa no way hakuna mtu anayekuja kutalii Tz kwa kuona Tz inacheza na Brazil kiwango kibovu cha sdoka kisichovutia hata mawakala wa wachezaji, Wenzenu kenya leo wana wachezaji Italy France wanacheza League kubwa kama chmps league eg Maliga na Oliech, nyinyi mnajipa moyo eti wamekenda Denmark,Norway, Sweeden, Canada, tukubaliane tu hapa ni kwamba sasa watanzania mnapaswa kuamka ili kieleweke hapa watu wamekula pes, hizo Ticket zilizonunuliwa za laki 2, mbona watu hawakujaa, pale pa mia hasa ndio kabisaa patupu, msijifanye mwajua shule mabo mwingine hata mjinga anaelewa namaana hata kipofu anaweza kujeng a taswira ya asilolijua, kwa taarifa yako tu ni kwamba Brazil wamekwenda Zimbabwe Serikali ya Zim imetoa asilimia 33% ya total cost, wakati the rest imelipwa na Net One kampuni ya simu, Zimplant kampuni ya madini na CBZ benki ya biashara ya Zimbabwe hakuna jasho la maskini hapo the gate collections was them income of the ZIFA, the total cost to invite the team was us$ 1.3Milion about Tshs 1.8 Billion sisi huku tunaambiwa 6 Billions tumeibiwa na hawa jamaa mi nashangaa serikali Corrupt hata TFF corrupt, The whole deal of bringing Kaka with his mates is surrounded with rushwa hivi lini watanzaniania tutaaamka, Nakuunga mkono Hans achana na vinuka mkojo wanaokupinga. Nimeamini ni kweli wasomi wa bongo wamenunuliwa na wanasiasa. Ikumbukwe Zimbabwe sio tu wanawavutia wawekezaji na watalii wanajitangaza kuonyesha nchini kwao kuko shwari.
ReplyDeleteMzalendo Halisi
Hans maswali yako ya msingi yanatakiwa kujibiwa. Hakika una hoja ya msingi hususani juu ya matangazo ya kibiashara uwanjani.
ReplyDeleteLakini hatuwezi kuvumilia yeyote anayetaka kutusahihisha (awe MTz au wa kuja) kwa kututukama.
Kamau hakutumia lugha inayokubalika wewe unatumia lugha inayokubalika kama ninavyotumia lugha inayokubalika sasa.
kuna watu nadhani akili zao si timamu ama zina walakini..mdau ametanguliza kusema ni swali anaomba ufafanuzi..vipi muanze kumshambulia?
ReplyDeleteMdau Hans kwa nini usiende kugombania ubunge wewe ni msomi na msemaji mzuri ambaye vilevile umepata wafuasi wengi. wenye kutaka kujua ukweli. nakushauri elimu uliyokuwa nayo unaweza kuwanufaisha walala hoi wengi.
ReplyDeleteMimi ni tz, nakupa big up ankal kamau, ukweli sikuzote lazima unauma, nawewe umetupaka ukweli jamani watanzania wenzangu nusu tumrarue ankala kamau - haya - mechi imepigwa yaliyo onwa na ankal ndo yametokea - semeni tena wabongo tumelala na tutazidi kulala tu.
ReplyDeleteWadau kuna kitu kimoja wengi naona mmeshindwa kukielewa, Timu ya Taifa ya Brazil imeingia mkataba na television GLOBO yani TV GLOBO kuwa popote Brazil itakapocheza yenyewe pekee ndio mhuhusika wa kurusha live mechi zake na ndo maana na kama mnavyojua TBC ilikuwainaonyesha ile mechi sasa jiulize kama DSTV moja ya channel zake ni TBC kwanini waliitoa TBC kabla ya matangazo kurushwa?Jibu ni kwamba DSTV walikuwa hawana haki ya kurusha matangazo yale, kwa watu wenye cable watakuelezea vizuri kwani wengi wao GLOBO tv waliipata, swala la matangazo nikwamba mengi kama sio yote ni yakibrazil kwasababu yalikuwa yanatangazwa na GLOBO TV na sio TBC. Natumaini hapo japo kidogo kimeeleweka, MDAU BIG, MKUU WA KATUMBA
ReplyDeleteSasa wadau wa uchumi mtaendelea kudai eti sababu mchezo umeonyeshwa nje basi ndo maana matangazo yetu hayakuwepo, au makampuni na mashirika yetu hayana michuzi, ila tukumbuke TFF imewalipa CBF mamilioni ya dola, sasa kwanini?
ReplyDeleteHapa TFF walichemka, walitakiwa wawe wagumu na makini, kwamba kama wanawalipa CBF basi matangazo yote pale uwanjani, urushaji wa TV, promotion, endorsements na marketing zote zilitakiwa ziwe mikononi mwa TFF. Kilichotokea ni wabrazil wamewazidi kete TFF, wakaweka vipengele vyao, TFF wakakubali kila kitu mezani na kuwa short sighted kwamba watatengeneza pesa kupitia viingilio, angalia sasa ilivyokula kwao, MIKATABA WAZEE, TUISOME MIKATABA KABLA YA KUSAINI CHOCHOTE, na kila kipengele utakachotunga hakikisha kinakufaidisha wewe, kwa kweli huu ni mfano na elimu nzuri kwetu wabongo.
Je kama viingilio vingekua labda alf 50, 30 na 10. Matangazo yote pale yangewahusisha AZAM, TBL, TCC, TOC, watu wengine wa vinywaji, bidhaa na upukupuku si ingekua pesa io.
Je kama TFF wangetengeneza vi t-shirts na vi scarves vya Tanzania na Brazil? Au Je kama TFF wangewalipisha mashirika ya kutangaza io soka, wale wa America, Europe, Asia, Arab countries and Africa ingekuaje.
Hili pambano lilitakiwa kurudisha na kutengeneza nyomi kinoma. TFF hawakujiandaa, labda shule na mbinu hawana na ndo maan hili pambano limeleta hasara tu.
Tujiulize, hivi kweli tunaweza hata kuandaa African Cup of Nations kwa muundo huu tutaweza??
Tujijibu wenyewe
Ama kweli tanzania itaendelea kuwa maskini kama ninyi mnaosema mmesoma uchumi ndo hao mnaomtukana hans. Point ya Hans iko very clear.
ReplyDeleteKama TFF waliweka matangazo ya Brazil ili kufidia gharama za kuwaleta then hakukuwa na haja ya kuwaleta hapa Tanzania maana hizo 3billions ni nyingi sana kwa nchi maskini kama ya kwetu.
Fine , tumecheza na Brazil na wameondoka, tumetangaza nini? Kwanini hakukuwa na matangazo ya TTB hata kama serikali ingelipa kwa ajili yake? Lengo lilikuwa ni kuitangaza nchi nje na si tu kupata hela za muda mfupi. Kuna mdau kasema yalikuwa ni matangazo ya sponsor wa Brazil national team; unafikiri kwanini wanatangaza? Tulipaswa kuhakikisha tunatumia hata hela za ziada ili kuweka matangazo ya ndani ili kuitangaza nchi yetu.
Hata ile TV ya ndani sikuona tangazo hata moja zaidi ya kilimo kwanza.
Hivi unasoma uchumi then unaponda kutoweka matangazo ya ndani, hiyo elimu ya uchumi inakusaidia nini katika kuendeleza nchi?
Tukubali TFF wamefanya kosa kubwa sana kushindwa kuweka matangazo hasa ya bidhaa ambazo tunaweza kuziuza nje ya nchi maana hakuna lolote linalohusu Tanzania lilionekana nje ya nchi. Mbaya zaidi hata TBC walirusha mpira kwa local chanel na si kwenye satelite chanel; tunaelekea wapi watanzania?
Serengeti mbona mnapoteza hela zenu bure kama style yenyewe ndo hii.
lazima tuamke tuwe na focus fo the future.
Mara ngapi TTB wanaenda kufanya promotion nje ya nchi kwa millions of money, walishindwa nini kuweka matangazo uwanjani siku ile. Hivi mwisho nani ana ushahidi kuwa Brazil hawajaletwa na pesa ya walipa kodi? Zile 7Billions hamjui kama ziliwekwa kwenye bajeti ya nchi? Tunahitaji maelezo ya TFF na serikali.
Mdau Faustin wa DSM.
"...you need to be tough to be Kenyan leader..."
ReplyDeleteCheck: You need to get rid of tougher guys like Ouko and the like and have some muscles like Kenya first lady!
"...Don`t continue to be Dummies as you are, learn from Kenya be like Kenyans"
Check: Tunanunua mapanga Kamau, almost ready, we gonna start crazy throat slashing"
"...Tanazians are changing corrupt leaders one from the other..."
Check: Statistics shows Kenya is corruption free country, ranks second to none
"...Kenyans don't need statistics when building an argument"
Check: Tanzanians will copy that...bla! bla! A-Z
and lastly we gonna start our Mungiki as you've requested!
Nyinyi acheni kumweka kiti moto Hans. Hayo matangazo TFF haijaambulia kitu. Brazilians katika mkataba wamekuja na matangazo yao na rights za kuair the game ni zao. Hapo TFF haijaambulia kitu ndio maana kina NMB wamewekwa nyuma.
ReplyDeleteSwali KUBWA la kujiuliza, Waziri Mkuchika alisema fedha ya kuwaleta Brazil TFF wamekopa NMB, sasa jiulizeni zile $6m Mh. Kawambwa alisema wametenga kwa ajili ya kuleta timu zinazoelekea Afrika Kusini zimekwenda wapi?? Hapo ndipo mlipopigwa changa la macho na nyinyi mko bizee mnamdiskasi Kamau!!!!
Jamani huyo jamaa ndio TZ ONE? Hatuna kipa
ReplyDeleteWengi tunafikiri tunajua uchumi lakini kumbe ni kwamba tunasimulia hekaya za abunuwas.
ReplyDeleteGharama za michezo kiasi kikubwa hulipwa na matangazo ya biashara na kiasi kidogo kinachobaki ni viingilio vya milangoni.
Mfano gharama za magazeti pesa unayotumia kununua nakala ya gazeti inachangia kidogo sana, ila matangazo ndo yanayoechangia kiasi kikubwa.
Ieleweke kuileta timu ya brazil bongo si pesa ya tanzania tu ila kuna makampuni yaliyodhamini kwa matangazo yao.
Ikumbukwe kwamba mechi ile imeonyeshwa kwenye mataifa 160, mataifa yaliyoona mechi hiyo ni kwa hisani ya makampuni yaliyodhamini mechi hiyo ili kutangaza bidhaa zao.
Bidhaa za bongo haziwezi kushinda dau la soko la makampuni makubwa yaliyodhamini mamilioni ya pesa ndo maana mabango yao wenyeji yakawekwa nyumba ili kumpisha tembo apite. Kiwango cha makampuni yetu mengi ni kutangaza mechi za ligi ya yanga, simba, azam, majimaji nk.
Hapa ieleweke kwamba marejesho ya gharama za kuileta brazil si malipo ya viingilio milangoni tu, ila matangazo ya biashara. Ila tu chama cha mpira safari nyingine kisifikirie kupata pesa za viingilio ndo suluhisho kwani kuingiza mashabiki zaidi ndo kuingiza pesa zaidi kuliko kupandisha viingilio na hatima kuonekana ni game la wenye nacho tu.
kamau tupe baba tupe...tupende tusipende kamau ameongea jambo la mbolea... tanzanians we are so scared. kwani? jamani we need to wake up! hatuna cha amani wala imani ni njaaa tu. we lack so much information na wala hatujisumbui kuzitafuta...jamani sikuhizi kuna goolge you can easly get anything.... ndugu zangu tuamke. hans thank you for noticing lakini nanyie msimshambuli mwenzenu atleast ameaona mnatakiwa kucorrect tu kiaina. kama field yake ni ya uchumi basi is not the same as that of marketing. kwa hiyo wewe mwenye marketing you need kuelimisha na hapo tutafika. moja jumlisha moja ni tatu au sio.
ReplyDeleteLILOPO NA KUBWA NI KWAMBA JIRANI YAKO AU WEWE MWENYEWE UKIPATA NAFASI BASI USIANGALIE NYUMA HATA TUKIANGALIA SERA ZA NCHI ZINASEMA MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA TUOMBA KUONGEZEWA MSHAHARA TU WA KIWANGO KIDOGO TUNANYIMWA NA KUTUKANWA NA KUONEKANA KUWA HATA KURA ZETU HAZIMSAIDII MTU JE KUONGEZA MAJIMBO NA KUONGEZA MSHAHARA KWA HAO WABUNGE WA MAJIMBO MAPYA HAWAONI KUWA WANAZIDI KUMKANDAMIZA WA CHINI? KIUKWELI HAKUNA CHA KUSEMA KUNA UONGOZI WA NCHI WA MPIRA KWA KUWA HATA SASA HIVI UKIWAENDEA TFF UKIWAULIZA NI KIASI GANI KIMEPATIKANA NA MATUMIZI UTASABISHA KULOGWA NA HATA USHINDWE KUFIKA NYUMBANI
ReplyDeleteWatanzania acheni ubishi wa kijinga,matangazo yanawekwa kulingana na pesa uliyolipa we unaetaka kutangaza,sasa kama makampuni ya tz hayakutoa pesa ya maana kwa nini yawekwe mbele?mlishazoea bure tu.
ReplyDeleteHUYU KAMAU ATATUPELEKA PABAYA JAMANI, HIVI MUMEMUONA ALIVYOCHANGIA HAPO JUU, YAANI NI MATUSI YANGUONI KWA UTAMADUNI WA KI-AFRICA. NA ANASEMA HUWEZI KUWA KIONGOZI WA KENYA KAMA SI NGANGARI, NA VIONGOZI WETU NI WABABAISHAJI NA WALARUSHWA. HIVI KWELI WAKENYA WANALIWA NA HAWANA UELEWA WA KUTOSHA. HIVI WANAJUWA KIONNGOZI WAO MKUU MMOJA ANA NYUMBA ZA KUPANGISHAZAIDI YA 1000 KENYA YOTE NA ANA KAMPUNI YA SIRI INAYOSHUGHULIKIA HIZO NYUMBA, HIVI KIONGOZI WA UMMA MTENDA HAKI ANAWEZA KUWA NA MAJUMBA 1000 NA MENGI NI YA GOROFA ZAIDI YA MBILI! HIVI ANAJUWA KIONGOZI WAO MKUU MMOJA ANA ACCOUNT NJE YENYE PESA YA KUTISHA, HUO NI UNGANGARI? WAKENYA WAMELALA. NA UNASEMA SISI TUNAIOGOPA SERIKALI YETU NA CCM YAKE NDO MAANA ATAUFANYI KITU CHOCHOTE HATUFURUKUTI. JAMANI EBU CHAMBUENI MCHANGO WAKE HAPO JUU JAMANI, HUYU NI HATARI SANA.
ReplyDeleteKAMAU NI MJINGA NA WALA SIDHANI KASOMA, KENYA UKISIKIA KASOMA ETI KUMALIZA FORM 4 NA KUJUWA KUONGEA ENGLISH BASI NDO KASOMA, HADI LEO HII UKISIKIA KENYA MTU ANASEMA JAMAA KASOMA BASI ETI KUMALIZA FORM 4, NDO MAANA HAPO TRUTH KAANADIKA TRUETH, HATA SISI WA-TANZANIA MNAOSEMA ATUJASOMA HATUWEZI KUANDIKA TRUETH BADALA YA TRUTH. HUYU JAMAA NI MJINGA TU NA MCHONGANISHI NA ANA WIVU NA TANZANIA
ReplyDeleteMimi sitaki kuingilia Mpira ila Ninaomba Mungu akupe uzima, Ankal KAMAU, nakuahidi ndani ya miaka tisa njoo tanzania halafu ulinganishe na Kenya japo ungelijua jinsi sasa watu tuna mpango wa kubadili Tanzania bila vita na chama kitaendela ni hichohicho cha CCM kwa kupiga kazi, plan iliyo pangwa kufatwa na kumwomba Mungu. Maneno yako sio mazuri sijayapenda kabisa Ankal KAMAU
ReplyDelete