USHAURI WA BURE KWA MSTAHIKI
MEYA WA JIJI LA DAR ES SALAAM

Mstahiki meya wa jiji la Dar es salaam,
Mimi ni mpitaji wa mara kwa mara katika jiji la Dar es Salaam, lakini pia nimepita majiji mengine makubwa kuliko Dar es Salaam. Ninachokiona ni kwamba tofauti na majiji mengine ambako foleni za magari husababishwa na matukio maalumu mfano ajali, marekebisho au kuharibika kwa miundombinu, au vurugu fulani za raia, Dare es Salaam foleni ni mchezo wa kila siku, ambapo unafuu wake unapatikana kwa nadra siku za mapumziko.

Mstahiki meya, taarifa za hivi karibuni kuwa foleni hizo zimefikia hatua ya kuathiri mpaka afya ya wakaazi wa jiji lako! Zimenishitua sana na kunituma kufikiri endapo kweli Dar es Salaam imekuwa kubwa na kulemewa na magari hadi dawa ya kutatua tatizo hili iwe ni mpaka kusubiri ujenzi wa "flyovers" wakati watu wakiendelea kuathirika kiafya na kiuchumi.

Mstahiki meya, nimejaribu kufanya utafiti kidogo na kugundua kuwa tatizo la foleni ni kuwa na taa nyingi za barabarani, hasa sehemu ambazo barabara nne zinakutana. Ni wazi kuwa tatizo hili huwa kubwa nyakati za asubuhi wakati watu wakielekea mjini na jioni wakati watu wakirudi makwao. Asubuhi, siyo kwamba gari zinakuwa zimefurika mjini, bali zingine zinapaki, nyingine zinarudi zilikotoka na zingine ziko katika mizunguko ya kawaida hapo mjini kati na ambazo si nyingi, na jioni siyo kuwa gari zinakuwa zimejaa huko ziendako, mfano ukishatoka Ubungo juu tu kule mbele ni kweupee au ukishatoka Tazara, ukielekea Airport na Ukonga kule mbele tena kunakuwa kweupee wakati wa jioni. Hii yote inasababishwa na kasi ndogo ya uendaji wa magari inayoisababishwa na kuwepo kwa mataa.

Hivyo dawa rahisi, haraka na gharama ndogo ni kuweka mizunguko "roundabouts" katika makutano makubwa yote ya barabara nne, mfano Ubungo, Mwenge, Tazara, na Magomeni na kwingineko kwenye wingi mkubwa wa magari. Mfumo huu utasababisha kasi ya uendaji wa magari kujirekebisha yenyewe, tofauti na mataa amabayo hayasomi wingi wa magari na kurekebisha jinsi ya kuruhusu magari au trafiki mara nyingine msaada wao haujawa mkubwa sana.

Mstahiki meya, naamini ukilifanya hili kabla ya uchaguzi wa mwaka huu, itakuwa moja ya pointi kubwa ya kukufanya urudi tena kwa kishindi katika nafasi yako.

Wakatabahu,
Edwin, S. M.,
Tanzania.
Phone: +255 25 2820002

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 25 mpaka sasa

  1. Wazo zuri lakini nauliza kuna madereva wenye nidhamu na kuheshimu sheria za barabara mfano give way. Hapa Sweden ukiwa ndani ya mzunguko unahaki ya kumalizia round yako na hakuna gari inaweza kukukatiza ndiyo maana hakuna msongamano kabisa iwe Mji mkubwa au mdogo kila dereva anajua cha kufanya siyo ubabe wala ujuaji.
    Kuuliza si ujinga

    ReplyDelete
  2. Mimi naungana na Edwin mia kwa mia, mimi nimeona hapa saudi au middle east yote, ni kwamba every intersection yeyote ina Traffic lights, tena ziko digital traffic yupo kama ushaidi wa kuwepo kazini,na kukiwa magari mengi basi Traffic Officer anaongeza dakika kwenye hizo lights,ni kweli Mwenge pana iitajika Taa za kuongoza magari, Science sehemu nyingi tu, ili kupunguza msongamano, tunaomba hili suala mlifanyie kazi kama mdau alivyosema, kaka michuzi nita kutumia moja wapo wa taa hizo, ila naomba uiweke hapo ili wahusika wa weze kuona.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 14, 2010

    Swali la kizushi: Kwanini idadi ya magari katika barabara za Dar es Salaam huongezeka maradufu mwisho wa mwezi? Madari huwa ni mengi sana na foleni huongezeka kuanzia tarehe 25 hadi tarehe 5 mpaka 10 ya mwezi unaofuata. Naomba wadau wachangie mada hii.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 14, 2010

    Wewe watu wanakimbia round abouts wee unataka tena zirudishwe. Round about kukiwa na magari mengi ni hasara tupu kwa vile kila mtu atajichomeka.

    Tutumie research wanazofanya wenzetu. Kuna research imetoka hivi juzi juzi ya jiji sijui lipi hapa USA lakini kilichonivutia ni haoa wasomi waliovumbua kuwa tatizo la trafic sio trafic lights ni muda wa ile taa unavyosimama. Wamesema kama waweza kuongeza muda wa taa ya green light kwa wakati magari huwa mengi wa asubuhi na jioni japo kwa dsekunde 30 tu inasaidia kupunguza kwa msafiri kukaa kwenye barabara kwa saa moja. Au wenye uwezo kuweka control sensors za magari. Taa iwe inajigeuza kutokana na magari yalivyo mengi green light inakaa upande huo wenye magari muda mrefu. Na kukiwa hakuna magari basi inajijeuza haraka haraka na kurudi kwenye ule upande wenye magari mengi...This makes sense to me..Utakuta kuna wakati unasubiri upande mwingine hauna gari lakini you have to wait.

    Lakini kurudi kwa round abouts ni kwenye miji yenye magari machache. Magari mengi wewe utalala hapo njiani na ukikuta madereva wenye kiburi wasiojali wengine watajichomeka tu na waoga watabaki kusimama hapo hapo na kuongeza traffic zaidi.

    ReplyDelete
  5. Solution nyingine ambayo huwa inatumika miji ya wenzetu (mfano London) ni kutumia "smart traffic lights"

    Inakuwa hivi metal detectors zinawekwa barabarani ili kupima urefu wa foleni.

    Kwa kuwa kila gari lina metal, ni rahisi kudetect gari la mwisho kabisa toka kwenye intersection liko umbali gani.

    Kisha taarifa hii inaingizwa kwenye computer inayocontrol traffic lights, na hivyo kurekebisha muda wa taa ya kijani kuwaka automatically kutegemea na upande upi una foleni kubwa.

    Ni kama kuwa na traffic police kwenye junction, lakini hii ni ya uhakika maana iko computerized.

    Na ili kuhakikisha matatizo ya TANESCO kukata umeme hayaathiri traffic lights, traffic lights zote zifungiwe umeme wa solar.

    Fanyia kazi suala hili Meya. Wakazi wa Dar tuna imani linawezekana kabisa.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 14, 2010

    wewe hapo umeongea point ya maana sana,ya kwamba watafutwe wataalamu wa kubuni utundu zaidi,swali ni kwamba jamani mstahiki wetu wa jiji hana nafasi mda umeisha tumbo joto sasa labda miujiza itendeke arudi kipindi kingine,jiji chafu mitaro ya maji taka kila sehemu hilo limeshindikana ,litawezekana kupunza foleni?

    ReplyDelete
  7. MIMI SIUNGANI NAWE KUPUNGUZA TRAFIC LIGHT SIO SOLUTION KWANI AJALI ZITAONGEZEKA NA FOLENI ITAONGEZEKA!!CHA MSINGI SERIKALI IJENGE BARABARA ZA NDANI!!TATIZO TZ MTU ANAYETOKA BAGAMOYO KUJA POSTA,AMA KARIAKOO NA YULE ANAYETOKA TEGETA,MBEZI, MWENGE, MAKUMBUSHO,VICTORIA WOTE TUNATUMIA BARABARA MOJA TU!!SASA HILI NI TATIZO BARABARA ZENYEWE NI NYEMBAMBA!!ZINGEJENGWA BARABARA ZA NDANI YA MITAA!!MFANO KUTOKA MWENGE UNAPITA NDANINDANI UNATOKEA MAKUMBUSHO,MWANANYAMALA, KINONDONI, UKIJAKUIBUKA UPO FAYA AU UPANGA HII ITAPUNGUZA SANA FOLENI!!MIJI MIKUBWA YOTE BARABARA ZA MITAANI ZIMEBORESHWA NA DIYO MAANA HAKUNA FOLENI KWANI SIO WATU WOTE WANATUMIA HIGHWAY HIVYO FOLENI HUPUNGUA.
    PIA KTK MAKUTANO YA BARABARA ZIJENGWE FLY OVER AMA UNDERGROUND ROAD. TANZANIA KUNA MAGARI MACHACHE SANA ILA MIUNDOMBINU MIBOVU.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 14, 2010

    Mdau wa juu uliyehigh light your text umetoa pointi niliyotaka kutoa,kwamba round abouts ni nzuri lakini sio safe kwenye intersection za magari mengi.Watu wengi hawana ustaarabu wa kumuheshimu mtu mwenye haki.Nilikuwa Tanzania december last year,nikawa naongea na rafiki yangu kwamba,ktk barabara ya Ally Hassan mwinyi,pale Sayansi,panatakiwa traffic lights kwani watu hawana nidhamu barabarani,in less than a week jamaa wakaweka traffic lights,nilifurahi sana.Tatizo kubwa ni kwamba,muda wa taa kuwa kijani ulikuwa ni sawa kwa magari yanayoelekea Rose garden-kijitonyama na kwa yale mwenge-posta,sasa hili ni jambo la ajabu sana kwa sababu barabara ya mwenge-posta,ina magari mengi zaidi ya barabara ya kuelekea rose garder/msasani na kuelekea kijitonyama.Kwa hiyo cha muhimu ni kuwa na traffic lights ambazo zitaadjust according to the traffic of the cars.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 14, 2010

    Hapa tujadili kujifurahisha wenyewe maana mstahiki meya hali sio shwari kwa sasa Oktoba inakaribia, kurudisha round about ni hatari sana. Mfano ni pale makutano ya Uhuru na Msimbazi. Pale mara nyingi mchana trafiki lazima akae vinginevyo hali huwa mbaya sana. Sheria ya aliye kulia mpishe apite kwanza haizingatiwi sana kwenye mizunguko,bali aliyespidi hupishwa ili kuepusha ajali.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 15, 2010

    Wakuu smart traffic lights zipo hata South Africa. Ukienda western cape hadi vimiji vidogo zipo. A good thing ni kwamba ile ni teknolojia ya hapo hapo SA. hIVYO BASI inaweza kuwa ni rahisi kidogo as compared to hizo teknolojia za overseas!

    ReplyDelete
  11. Nina waunga mkono wadau walio toa hoja ya kuwa kuwepo sensor kwaajili ya kuwezesha Traffic light micro controller kuelewa muda gani itoe sehemu kuna magari mengi na ambako hakuna magari mengi, pili kuangalia muda wa jioni na asubuhi kupewa muda mrefu kwa upande wenye magari mengi. Mimi nilifanya project moja ya traffic light system (nili design traffic light and car sensor Micro controller) for my University ambayo nili design traffic light micro controller ilikuwa na uwezo wa kupata information from car sensor micro controller and emergence car micro controller(Ambulance and misafara kama ya raisi kwa ajili ya kuingiza information kwenye traffic light micro controller ili itoe green kwenye line ya emergence car ilipo). Mimi nitampa offer ya hii technology huyu Meya free of charge ili apunguze hili tatizo kama akitaka ila yeye tu anunue vifaa nitakavyo hitaji na sio ghali vifaa vyenyewe kwani mimi ilinigharimu kama laki moja na nusu kutengeneza na inaweza kuwa chini ya hapo. mdau viwanjani

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 15, 2010

    Mimi naishi Finland, na ni muda mrefu sasa kiasi cha kuona mabadiliko. Wenzetu wanaondoa traffic lights na kuweka roundabouts ili kupunguza matatizo ya msongamano. Traffic lights zinaleta shida sana hasa pale panapokuwa hakuna umeme, kitu ambacho Dar ni kitu cha kawaida

    ReplyDelete
  13. Wadau mmetoa mawazo mazuri sana.

    Kwa sasa nipo Stockholm,Sweden Kikazi.Nimeangalia wenzetu wanafanyaje kuondoka na tatizo la foleni na nimegundua kwa mtindo ambayo mnashauri foleni Dar,Arusha na Mwanza ninapoishi zitakuwa maradufu miaka ijayo.

    Suluhisho:
    Hapa Stockholm kuna aina 2 za usafiri wa umma.Mabasi makubwa(Ikarusi) na treni(Metro).Treni hizi sehemu nyingi zinapita underground kwa asiye wahi kuziona kama mimi kusema ukweli nimestaajabu.Mwenyeji ameniambia wamejenga hizi tunnels miaka ya 50.

    Makutano ya barabara ni chache sana walichofanya ni kutumia round about lakini hizi ndugu zangu si kama zile za msimbazi na uhuru nooo.Hizi ni fly overs.So gari inakuwa kwenye mzunguko muda mwingi.Trafiki light zipo lakini chache sana.

    Pia hawa jamaa wametengeneza njia ya watumia baiskeli na waenda kwa miguu kwa kila njia inakopita gari.

    Madereva hapa wana nidhamu ya hali ya juu.Kwenye pundamilia wakiwepo watu lazima gari isimame.

    Nimeona kitu kingine kuwa wanawajali vipofu kwenye Zebra.Kipofu huku anaweza kukatiza barabara bila ya msaada wa mtu.Ni rahisi kwenye taa za kuongozea magari kuna kifungo ambacho akibonyeza kitamjulisha kwa kupiga kengele pale taa ya kijani itakapowaka!!!!!!!!!!

    Hitimisho:
    Viongozi tulionao kwa sasa wana mtizamo mfupi.Ingawa wengi wamefika huku Ulaya nashindwa kuelewa kwa nini hawataki kutuongoza kuelekea mafanikio.Vijana wenzangu tubadilike na tuchague watu watakaotuletea mabadiliko bila kujali watokako.!!!!!

    Salam toka Slussen,Stockhom

    Sangawe

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 15, 2010

    all those ideas are bugger this is a solution, ban daladala or put congestion charges to enter city centre

    ReplyDelete
  15. AnonymousJune 15, 2010

    Hizo sensors tayari zipo, hakuna cha kuvumbua ni ku-implement tuu technologia ambayo ipo. Technologia hii inatumika nchi nzima ya marekani katika miji mikubwa na midogo. The controller reads the sensors through loop, and decides which one to start, at the end of the cicle(3min max), it starts all over again which route to turn green.
    You will have the box with your micro-controller at the light poll.

    ReplyDelete
  16. AnonymousJune 15, 2010

    Hii rearch ya Edwin mimi naona ni fake sana. Yaani hata bila kufanya rearch ni wazi kuwa round abouts zinaoongeza tatizo mara dufu. Solution ni kuwa na trafic lights za kisasa. Mfano hapo USA trafic lights za hapa zinaongozwa na computers,ziko computerised. Kama upande fulani hakuna gari,hakuna taa ya kijani kuwaka,inawaka nyekundu tu..!Badala yake taa ya green itawaka kwenye upande wenye magari ili kuepeuka kupoteza muda kwenye upande amabao either una magari kidogo sana au hauna magari kabisaa..!!.Na ndiyo maana wakati mwingine ukikaa vibaya kwenye barabara,junction trafic light haita-sense kama hupo, matokeo yake utaganda hapo kutwa.Hii ndiyo best solution for now.

    ReplyDelete
  17. AnonymousJune 15, 2010

    TATIZO NI TRAFFIC LIGHTS KURUHUSU MAGARI KWA MUDA MFUPI WAKATI WA ASBH NA JIONI, NA WALA SI KUWE NA ROUND ABOUTS. WAZI-PROGRAM TU ZIFANYE HIVYO NDO DAWA YAKE, MBONA NCHI NYINGINE WANAWEZA?

    ReplyDelete
  18. AnonymousJune 15, 2010

    Wadau wote nyie mmechemsha big time!
    Subirini nitakuja na plan kamili na nini chakufanya! Maoni naomba yaishie hapa kwani hakuna hata mmoja aliye na wazo la kitaalamu all ideas based on assumptions hakuna aliyefanya research ya uhakika.
    I will be back with you guys with the proper solution.
    Thanks

    ReplyDelete
  19. AnonymousJune 15, 2010

    Wizara wa Miundo Mbinu may be at fault here. I work for a company in Dar that wanted to do a comprehensive study on traffic congestion and how to solve it in Dar and we had a proven solution tested and in use around the world - we got shot down, eti "...kuna kampuni kama 9 hivi zimekuja na similar proposition..." Really?

    Kuna mtu hapo juu ametoa wazo ambalo nakubaliana nalo. Mpango ufanywe barabara zote ndogo ndogo zitengenezwe vizuri kuondoa magari kuelekea barabara kuu. Mfano, kama mtu anakwenda Sinza akitokea mjini, ile barabara ya Home Boys (Hombu) pale Biafra ikiboreshwa ipanuliwe na barabara zote zinazopita Kijitonyama (zile zenye majina ya nchi mbalimbali ambazo zinarun parallel to one another)ziboreshwe manake zote zile zinakuja tokea Shekilango. Hizi barabara yataka moyo kupita kwa hiyo mtu anakaa Mabatini kwa mfano na anatoka mjini basi anaamua kuenda na Ali Hassan mwinyi mpaka Sayansi wakati angeweza kupita kwa urahisi zaidi Kijitonyama ndani ndani. Huko AHM anashare na mtu anaeyekaa Mikocheni Garden Road mpaka kwa Mwalimu Old Bagamoyo road. Old Bagamoyo road watu wote wa Kikocheni, Kawe, Mbezi Beach, Mbezi, Kunduchi, Tegeta, Msasani etc wanatumia hiyo hiyo wakati kutoka kutoka kwa Mwalimu kuna njia ambazo zikiboreshwa zitapunguza trafiki na kudistribute magari yapite Masaki. Mfano barabara ile ipitayo TANESCO (Chama) kwenda Msasani village na kutokea Kimweri etc.

    ReplyDelete
  20. AnonymousJune 15, 2010

    Ankal, tuma wazo na maoni yote haya kwa Meya. sio mijadala inawekwa huku na walengwa haiwafikii itakua haina maana, mana najua hawaingii kwenye hii blog hawa.

    ReplyDelete
  21. AnonymousJune 15, 2010

    ROUND ABOUT ZIMESHINDIKANA NAIROBI, NILIKUWEPO HUKO LAST WEEK WANALALAMIKA WANATAKA KUONDOA ROUND ABOUT NAIROBI. ZIPO NYINGI SANA. KWA HIYO USHAURI WAKO SIO SAHIHI

    ReplyDelete
  22. AnonymousJune 15, 2010

    MAJADILIANO YOTE NI MAZURI SANA LAKINI HILI LA KUBORESHA BARABARA ZA MITAANI LINAPATA KURA NYINGI ZA NDIYO LIKIFUATIWA NA WAZO LA KUWA TAA ZENYE UWEZO WA KUTAMBUA WINGI WA MAGARI KATIKA BARABARA HUSIKA.

    ReplyDelete
  23. AnonymousJune 15, 2010

    dar si mahali pa kuishi sasa!!
    ovyooooo,watu wanaambiwa hamieni dodoma hawataki!!

    mihotel viwanda viwanja nk vimelundikwa dar unategemea nini!!

    ReplyDelete
  24. AnonymousJune 15, 2010

    its a good discussion for the development of our LOVED POOR COUNTRY. Like every one explain according to what he/she experience. The neext question is ask ur self according to the city plann untill this time did we have inaf places and resources to implement those all idea.
    Kwa sababu in kariakoo u can say foleni inasababishwa na Upakiji wa magari barabari so then thy narrow up njia ya kupita magari. NO PARKING mtu anajenga gorofa nane anategemea parking ya njiani...

    Sensor traffic light, nazani kwa mstahiki meyor computer iko kwa secretary tuu, no offense trust me, thats is a new technology.

    WHAT I THINK....
    Weka Toll tu, kwenye any intrance ya kuingia town, ukija mjini na gari u have to pay charges then ,THEN
    Establish public transport..

    KAMA HIYO NGUMU

    Fufua reli ya ubungo, mabibo, ile pale inayopita chini kamata, inaoza nazani, inafika mpaka karume, iungne na ile inayoingia bandarini kwenye mafuta, along that side, inakuwa ishafika posta..

    WAKAWE NA KUNDUCHI
    Speed boat, kama ilivyo kigamboni Ferry, inakuwa fery mpaka kawe, wemgine unwashusha mbezi beach.

    WAMBEZI SHAMBA:
    Wanawekewa reli inayopita segerea kinyerezi wanatokea ukonga, wanakutana na reli ya uko, inawaunganisha na wengine town..

    existing miundo mbinu can be used, bila kuleta effect kubwa kwa jamii..

    NINI TATIZO..
    Mji ni mdogo, barabara bado za mwalimu, magari kila yanaongezeka

    NB:
    GARI BINAFSI KUINGIZA MJINI 5000 KWA SIKU..

    ReplyDelete
  25. AnonymousJune 15, 2010

    You are very right mdau uliye suggest kuwepo kwa roundabout ili kupunguza foleni. mfano mzuri ni ile roundabout ya kuingia Mlimani City ukitokea mwenge au ubungo, inasaidia sana na watu wanakuwa wastaarabu wapende wasipende. Pia mdau aliyesema kutengenezwa njia za ndani (mitaani) zinasaidia sana, japo kwa kiasi fulani kwa sababu ukitoka njia hizo inabidi uungane na mainroad ambayo ni moja tu kuelekelea mjini. Yote hayo yanawezekana kama watendaji watafanyakazi zao badala ya kukaa maofisini na makotikoti yao badala ya kwenda kwenye field.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...