MABADILIKO YA UKUMBI NA TAREHE

KUTOKANA NA SABABU NJE YA UWEZO WETU TUMERUDISHA NYUMA SIKU MOJA YAANI ALHAMISI BADALA YA IJUMAA AMBAYO NI SIKUKUU MUHIMU HAPA FINLAND (MID-SUMMER-JUHANNUS) KUTAKUWA NA SHIDA YA USAFIRI. PIA KUTOKANA NA KUPOKEA EMAILS NYINGI ZA WASHIRIKI KAMATI YA MAANDALIZI IMECHUKUA UKUMBI MKUBWA NA WA KISASA PALE PALE KATIKATI YA JIJI LA HELSINKI-RAVINTOLA KAISANIEMI (THE HOME OF AFRICAN NIGHT) KAISANIEMENTIE 6.

TAREHE: ALHAMISI 24.6.2010
MUDA: 18.00pm -23.30pm
BAADA YA MKUTANO: KUTAKUWA NA BURUDANI YA NYIMBO ZA KINYUMBANI TU NA DJ. ALTUNEZ.
KWA WALE WANAOJISIKIA KUJA KUFAHAMIANA NA WATANZANIA WENZAO, TUTAKUWA NA MAZUNGUMZO YA PAMOJA NA BAR KUWA WAZI KWAAJILI YA VINYWAJI BAADA YA MKUTANO 21:00.

NB: WANAWAKAMATI WANAFANYA MAWASILIANO NA BALOZI WETU WA SWEDEN AU MWAKILISHI WAKE ILI AWEZE KUWA MGENI RASMI KWAAJILI YA UFUNGUZI.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 23 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 21, 2010

    Ndugu zangu naona ufagio umewachosha kabisa,rudini nyumbani.home sweet home.karibuni sana

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 21, 2010

    hongereni wadau mimi lazima nitie timu ndani ya nyumba. Nakuja kwenye mkutano halafu nataka kujikumbusha muziki wa nyumbani

    mdau OULU

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 21, 2010

    Naona life Helsinki limekuwa gumu, lakini maisha kokote...lakini ukumbi kuuhamishia ravintola ni kuibiana tu...

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 21, 2010

    Nawashukuru wadau wenzangu kwa kuonyesha nia na maendeleo ya nyumbani. Kurudi nyumbani ni lazima na mchango wetu hata wa mawazo utachangia mabadiliko kwa njia moja ama nyingine.

    Mdau tampere

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 21, 2010

    Mbona hamtumbii kuwa mmepigwa marufuku kutumia ukumbi wa chuo kwa shughuri za siasa?

    ReplyDelete
  6. Wakubwa,wadau na Watanzania wote kwa ujumla muishio nchini Finland, tunawashukuru sana kwa maoni yenu.
    Kama hiki kipeperushi kinavyojieleza, karibuni mje kuhakikisha,kuhakiki na kutukeleza haki zenu za kuwachagua wakilishi wenu watakoa kwa njia moja au nyingine wawakilisheni nyinyi ndani ya Chama Cha Mapinduzi.
    Zoezi hili ambalo ni haki ndani ya Katiba ya Chama cha Mapinduzi ni muhimu na hiari kwa kila Mwananchi, kama "Motto" wetu sisi Wabeba Maboksi mamtoni unavyosema

    "Blame time is over Get involved and help make the Changes".

    ( "Mavuvuzela ,kilele, za uoshaji vinywa na uanoymous contribution za wachache wasio penda maendeleo yetu na Taifa kiujumla hautusaidi lolote).

    Karibuni sana.

    KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI 2010 Na Zaidi.


    Wenu Mratibu wa muda

    Aliko Mwakanjuki.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 21, 2010

    hongera sanaaaaaaaaaaaa, wadauziiiiiii sasa wale waosha vinywa kazi kwenu,

    CCM oyeeeeeeeeeeeee
    Kikwete safiiiiiiiiiiii

    Vijana Finland je???????
    Safiiiiiiiiiiiiii

    Mdau Kada wa CCM London

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 21, 2010

    INGAWA SIJUI KIMOMBO VIZURI KAMA KAMAU; LET ME TRY TO CONGRADULATE YOU GUYS; THANK YOU FOR THIS JOB; I KNOW HATERS; CYNICS;HYPOCRITES AND ENEMIES MUST BE ANGRY; THE VENUE IS THE BEST OPTION

    KEEP IT UP GUYS;

    MDAUZ: BINTI KAMAU

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 21, 2010

    SASA HAPO WANAKAMATI NAWAPONGEZA UKUMBI SAFI SANAAAAAAAA; HAPO MMEPATIA KABISAAAAAAAA; MAANA KILA MTU ATAFIKA BILA SHIDA,

    WATANZANI HATA WALE WASIO WADAUZ WA CCM KARIBUNI KUANZIA SAA TATU USIKU NJOO TUFAHAMIANE ACHENI MAJUNGU

    MDAU OULU

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 21, 2010

    hongera sana mratibu wa muda kwa kazi nzuri,

    mimi nakuja na vijana kibao kutoka Tampere, nawapongeza ukumbi safi sana.



    mdau-Tampere

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 21, 2010

    wewe annoy 08:13 pm wa tano kutoka juu, wewe ni hater, mtu mwenye fitina, chuki, roho mbaya na mzushi sana. Kwanza hakuna mtu yeyote aliyekuwa ameomba ukumbi chuo kikuu, tulikuwa tumeomba eneo linaitwa Snellimaninkatu 10 kwenye public pub, rejea tangazo la wali. Sasa kwanini wewe unapoteza muda kuzusha uongo ili upate faida gani???? kweli mswahili ni mswahili tu hata kama akae ulaya miaka kibao lakini bado atabaki ni mswahili tu.

    CCM OYEEEEEEEE
    TAWI LA CCM HELSINKI OYEEEEEEEE
    KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI
    MWANAKAMATI

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 21, 2010

    Ha!Ha!Ha! Kaaazi kweli kweli. CCM imeona nyumbani kwa moto sasa inahamisha matawi ughaibuni. Poleni sana. Safisheni uozo ndani kabla hamja-export nchi zingine. Tunatia aibu watanzania. Kisheria it is not acceptable kuweka political party nchi ya watu. Mlisikia lini kuna branches za Republicans (USA), Democrats (USA), Labour ya UK, Tories, Liberal Democrats n.k ndani ya Tanzania? Iweje leo kwenye nchi za watu muanze kupiga kampeni? Uchaguzi unawaelekea vibaya? Kumbukeni there was once the great Roman Empire, ikaanguka kutokana na matatizo ya ndani. Ukiona hivi jua siku za CCM zinayoyoma. Mfa maji haishi kutapatapa.

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 22, 2010

    By the way, huu uchaguzi kufanyikia ravintola usiku wa African Night ni coincidence au ilikuwa imepangwa? duh!! JK anakataa siasa na biashara naona wadau wake huku wanamuangusha kwa kuitumia CCM kuvutia biashara ya muziki.

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 22, 2010

    Tatizo wanakamati wote hawana ajira, halafu ni vyatungi kwa kwenda mbele...

    ReplyDelete
  15. AnonymousJune 22, 2010

    Wanakamati,
    Tatizo mlilokosea ni kuweka hiyo list ya majina yenu hadharani, kwa kifupi hakuna mtu mwenye akili timamu anayeweza kuja. Wadau walishaanza kupiga makelele ya kuwa hili ni dili la wajanja walioshindwa maisha, nilijua mngetumia ujanja wa kutupiga changa la macho angalau kwa hatua hizi za mwanzo, lakini kitendo chenu cha kuhamishia mkutano kwenye ukumbi ambao kuna disco la AN ni usanii tuliokwishautabiri.

    ReplyDelete
  16. AnonymousJune 22, 2010

    Mwenye CV za wanakamati wa muda naomba aniwekee hapa, pamoja na address zao.

    ReplyDelete
  17. ONYO: kwa wale wote ambao makaratasi yao hayajakaa sawa, wasithubutu kuja au kuhudhuria kwenye huu mkutano, kwani nimepata taarifa kuwa haters walishawajulisha WAZEE na WAZEE wamepata taarifa na bila shaka watakuja kuhakikisha kuwa wote wanaohudhuria makaratasi yao yako kamili.

    ReplyDelete
  18. AnonymousJune 22, 2010

    Daah kweli CHAMA KIMESHIKA HATAMU hadi huku Helsinki! mhh halafu wadau hawa hawa waliokuwa wanaona CCM haifai leo hii ndio wako mbele kufungua branch.jamani jamani njaa mbaya. anyway all the best kama kweli mnadhani mtaweza kuleta mabadiliko kwa CCM na kwa Tanzania ingawa kama wahenga walivyosema Fimbo ya mbali haiui nyoka.

    ReplyDelete
  19. AnonymousJune 22, 2010

    wee mpuuzi hapo anoy 11:21 juu fuatilia Maswala kabla ya kurusha pumba zako tulikua na Democrats hadi Daresalaam,Arusha nk wakimpigia Obama kampeni achana huko London Paris, indonesia, Kenya etc vipi wewe??
    Kidumu chama cha mapinduzi

    ReplyDelete
  20. AnonymousJune 22, 2010

    Mdau-Tampere.
    Weka vizuri bandiko lako, ili kuweza kuwapata vijana wengi wa Tampere, tafadhali

    ReplyDelete
  21. AnonymousJune 22, 2010

    Mkutano mpaka saa sita usiku??? Pumba 2pu.

    ReplyDelete
  22. AnonymousJune 22, 2010

    Hao watu wa Ubalozi kutoka Stockholm wahakikishe wanatumia pesa za CCM na wala sio za serikali, au sivyo zitawatokea puani. Usalama wa Taifa (kivuli) unaangalia!!

    ReplyDelete
  23. AnonymousJune 22, 2010

    Blame time is over? Is our suffering over? Tunyamaze wananchi wa Tanzania wakati tunaona nchi inadidimia? Acha mzaha bwana na maisha ya watu. Mnaleta usultani na umwinyi Tanzania bila aibu na sisi tunyamaze? Kha! Siku yenu inakuja, mtaficha nyuso zenu kwa haya ambayo kwa sasa hamuijui maana yake. Wanaotoa maoni yao dhidi ya CCM ya ufisadi mnawaita haters na wajinga. Hiyo ni dalili ya kushindwa kwa kutukana pale ambapo usemi unatamkwa. Makaburu enzi za apartheid waliwa-demonize ANC na wapigania uhuru wa Afrika ya Kusini na kuwaita terrorists. Lakini leo wale wale terroists wamekuwa sio tena kwa vile baada ya muda ukweli hujitenga na uongo. Mnajua wazi ndani ya mioyo yenu kuwa CCM sio chama cha kuleta mapinduzi katika maisha ya Watanzania, ila ni chama cha kudumisha ufisadi na kuwakamua Watanzania. Na ninyi mnataka kuendeleza hayo makamuzi. Kuna wakati Mwalimu Nyerere (Mungu amuweke mahali pema, alisema,: 'There is a limit to milking a cow.' Kuna limit ya kuwakamua Watanzania.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...