MABADILIKO YA UKUMBI NA TAREHE
KUTOKANA NA SABABU NJE YA UWEZO WETU TUMERUDISHA NYUMA SIKU MOJA YAANI ALHAMISI BADALA YA IJUMAA AMBAYO NI SIKUKUU MUHIMU HAPA FINLAND (MID-SUMMER-JUHANNUS) KUTAKUWA NA SHIDA YA USAFIRI. PIA KUTOKANA NA KUPOKEA EMAILS NYINGI ZA WASHIRIKI KAMATI YA MAANDALIZI IMECHUKUA UKUMBI MKUBWA NA WA KISASA PALE PALE KATIKATI YA JIJI LA HELSINKI-RAVINTOLA KAISANIEMI (THE HOME OF AFRICAN NIGHT) KAISANIEMENTIE 6.
TAREHE: ALHAMISI 24.6.2010
MUDA: 18.00pm -23.30pm
BAADA YA MKUTANO: KUTAKUWA NA BURUDANI YA NYIMBO ZA KINYUMBANI TU NA DJ. ALTUNEZ.
KWA WALE WANAOJISIKIA KUJA KUFAHAMIANA NA WATANZANIA WENZAO, TUTAKUWA NA MAZUNGUMZO YA PAMOJA NA BAR KUWA WAZI KWAAJILI YA VINYWAJI BAADA YA MKUTANO 21:00.
NB: WANAWAKAMATI WANAFANYA MAWASILIANO NA BALOZI WETU WA SWEDEN AU MWAKILISHI WAKE ILI AWEZE KUWA MGENI RASMI KWAAJILI YA UFUNGUZI.
KUTOKANA NA SABABU NJE YA UWEZO WETU TUMERUDISHA NYUMA SIKU MOJA YAANI ALHAMISI BADALA YA IJUMAA AMBAYO NI SIKUKUU MUHIMU HAPA FINLAND (MID-SUMMER-JUHANNUS) KUTAKUWA NA SHIDA YA USAFIRI. PIA KUTOKANA NA KUPOKEA EMAILS NYINGI ZA WASHIRIKI KAMATI YA MAANDALIZI IMECHUKUA UKUMBI MKUBWA NA WA KISASA PALE PALE KATIKATI YA JIJI LA HELSINKI-RAVINTOLA KAISANIEMI (THE HOME OF AFRICAN NIGHT) KAISANIEMENTIE 6.
TAREHE: ALHAMISI 24.6.2010
MUDA: 18.00pm -23.30pm
BAADA YA MKUTANO: KUTAKUWA NA BURUDANI YA NYIMBO ZA KINYUMBANI TU NA DJ. ALTUNEZ.
KWA WALE WANAOJISIKIA KUJA KUFAHAMIANA NA WATANZANIA WENZAO, TUTAKUWA NA MAZUNGUMZO YA PAMOJA NA BAR KUWA WAZI KWAAJILI YA VINYWAJI BAADA YA MKUTANO 21:00.
NB: WANAWAKAMATI WANAFANYA MAWASILIANO NA BALOZI WETU WA SWEDEN AU MWAKILISHI WAKE ILI AWEZE KUWA MGENI RASMI KWAAJILI YA UFUNGUZI.
Ndugu zangu naona ufagio umewachosha kabisa,rudini nyumbani.home sweet home.karibuni sana
ReplyDeletehongereni wadau mimi lazima nitie timu ndani ya nyumba. Nakuja kwenye mkutano halafu nataka kujikumbusha muziki wa nyumbani
ReplyDeletemdau OULU
Naona life Helsinki limekuwa gumu, lakini maisha kokote...lakini ukumbi kuuhamishia ravintola ni kuibiana tu...
ReplyDeleteNawashukuru wadau wenzangu kwa kuonyesha nia na maendeleo ya nyumbani. Kurudi nyumbani ni lazima na mchango wetu hata wa mawazo utachangia mabadiliko kwa njia moja ama nyingine.
ReplyDeleteMdau tampere
Mbona hamtumbii kuwa mmepigwa marufuku kutumia ukumbi wa chuo kwa shughuri za siasa?
ReplyDeleteWakubwa,wadau na Watanzania wote kwa ujumla muishio nchini Finland, tunawashukuru sana kwa maoni yenu.
ReplyDeleteKama hiki kipeperushi kinavyojieleza, karibuni mje kuhakikisha,kuhakiki na kutukeleza haki zenu za kuwachagua wakilishi wenu watakoa kwa njia moja au nyingine wawakilisheni nyinyi ndani ya Chama Cha Mapinduzi.
Zoezi hili ambalo ni haki ndani ya Katiba ya Chama cha Mapinduzi ni muhimu na hiari kwa kila Mwananchi, kama "Motto" wetu sisi Wabeba Maboksi mamtoni unavyosema
"Blame time is over Get involved and help make the Changes".
( "Mavuvuzela ,kilele, za uoshaji vinywa na uanoymous contribution za wachache wasio penda maendeleo yetu na Taifa kiujumla hautusaidi lolote).
Karibuni sana.
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI 2010 Na Zaidi.
Wenu Mratibu wa muda
Aliko Mwakanjuki.
hongera sanaaaaaaaaaaaa, wadauziiiiiii sasa wale waosha vinywa kazi kwenu,
ReplyDeleteCCM oyeeeeeeeeeeeee
Kikwete safiiiiiiiiiiii
Vijana Finland je???????
Safiiiiiiiiiiiiii
Mdau Kada wa CCM London
INGAWA SIJUI KIMOMBO VIZURI KAMA KAMAU; LET ME TRY TO CONGRADULATE YOU GUYS; THANK YOU FOR THIS JOB; I KNOW HATERS; CYNICS;HYPOCRITES AND ENEMIES MUST BE ANGRY; THE VENUE IS THE BEST OPTION
ReplyDeleteKEEP IT UP GUYS;
MDAUZ: BINTI KAMAU
SASA HAPO WANAKAMATI NAWAPONGEZA UKUMBI SAFI SANAAAAAAAA; HAPO MMEPATIA KABISAAAAAAAA; MAANA KILA MTU ATAFIKA BILA SHIDA,
ReplyDeleteWATANZANI HATA WALE WASIO WADAUZ WA CCM KARIBUNI KUANZIA SAA TATU USIKU NJOO TUFAHAMIANE ACHENI MAJUNGU
MDAU OULU
hongera sana mratibu wa muda kwa kazi nzuri,
ReplyDeletemimi nakuja na vijana kibao kutoka Tampere, nawapongeza ukumbi safi sana.
mdau-Tampere
wewe annoy 08:13 pm wa tano kutoka juu, wewe ni hater, mtu mwenye fitina, chuki, roho mbaya na mzushi sana. Kwanza hakuna mtu yeyote aliyekuwa ameomba ukumbi chuo kikuu, tulikuwa tumeomba eneo linaitwa Snellimaninkatu 10 kwenye public pub, rejea tangazo la wali. Sasa kwanini wewe unapoteza muda kuzusha uongo ili upate faida gani???? kweli mswahili ni mswahili tu hata kama akae ulaya miaka kibao lakini bado atabaki ni mswahili tu.
ReplyDeleteCCM OYEEEEEEEE
TAWI LA CCM HELSINKI OYEEEEEEEE
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI
MWANAKAMATI
Ha!Ha!Ha! Kaaazi kweli kweli. CCM imeona nyumbani kwa moto sasa inahamisha matawi ughaibuni. Poleni sana. Safisheni uozo ndani kabla hamja-export nchi zingine. Tunatia aibu watanzania. Kisheria it is not acceptable kuweka political party nchi ya watu. Mlisikia lini kuna branches za Republicans (USA), Democrats (USA), Labour ya UK, Tories, Liberal Democrats n.k ndani ya Tanzania? Iweje leo kwenye nchi za watu muanze kupiga kampeni? Uchaguzi unawaelekea vibaya? Kumbukeni there was once the great Roman Empire, ikaanguka kutokana na matatizo ya ndani. Ukiona hivi jua siku za CCM zinayoyoma. Mfa maji haishi kutapatapa.
ReplyDeleteBy the way, huu uchaguzi kufanyikia ravintola usiku wa African Night ni coincidence au ilikuwa imepangwa? duh!! JK anakataa siasa na biashara naona wadau wake huku wanamuangusha kwa kuitumia CCM kuvutia biashara ya muziki.
ReplyDeleteTatizo wanakamati wote hawana ajira, halafu ni vyatungi kwa kwenda mbele...
ReplyDeleteWanakamati,
ReplyDeleteTatizo mlilokosea ni kuweka hiyo list ya majina yenu hadharani, kwa kifupi hakuna mtu mwenye akili timamu anayeweza kuja. Wadau walishaanza kupiga makelele ya kuwa hili ni dili la wajanja walioshindwa maisha, nilijua mngetumia ujanja wa kutupiga changa la macho angalau kwa hatua hizi za mwanzo, lakini kitendo chenu cha kuhamishia mkutano kwenye ukumbi ambao kuna disco la AN ni usanii tuliokwishautabiri.
Mwenye CV za wanakamati wa muda naomba aniwekee hapa, pamoja na address zao.
ReplyDeleteONYO: kwa wale wote ambao makaratasi yao hayajakaa sawa, wasithubutu kuja au kuhudhuria kwenye huu mkutano, kwani nimepata taarifa kuwa haters walishawajulisha WAZEE na WAZEE wamepata taarifa na bila shaka watakuja kuhakikisha kuwa wote wanaohudhuria makaratasi yao yako kamili.
ReplyDeleteDaah kweli CHAMA KIMESHIKA HATAMU hadi huku Helsinki! mhh halafu wadau hawa hawa waliokuwa wanaona CCM haifai leo hii ndio wako mbele kufungua branch.jamani jamani njaa mbaya. anyway all the best kama kweli mnadhani mtaweza kuleta mabadiliko kwa CCM na kwa Tanzania ingawa kama wahenga walivyosema Fimbo ya mbali haiui nyoka.
ReplyDeletewee mpuuzi hapo anoy 11:21 juu fuatilia Maswala kabla ya kurusha pumba zako tulikua na Democrats hadi Daresalaam,Arusha nk wakimpigia Obama kampeni achana huko London Paris, indonesia, Kenya etc vipi wewe??
ReplyDeleteKidumu chama cha mapinduzi
Mdau-Tampere.
ReplyDeleteWeka vizuri bandiko lako, ili kuweza kuwapata vijana wengi wa Tampere, tafadhali
Mkutano mpaka saa sita usiku??? Pumba 2pu.
ReplyDeleteHao watu wa Ubalozi kutoka Stockholm wahakikishe wanatumia pesa za CCM na wala sio za serikali, au sivyo zitawatokea puani. Usalama wa Taifa (kivuli) unaangalia!!
ReplyDeleteBlame time is over? Is our suffering over? Tunyamaze wananchi wa Tanzania wakati tunaona nchi inadidimia? Acha mzaha bwana na maisha ya watu. Mnaleta usultani na umwinyi Tanzania bila aibu na sisi tunyamaze? Kha! Siku yenu inakuja, mtaficha nyuso zenu kwa haya ambayo kwa sasa hamuijui maana yake. Wanaotoa maoni yao dhidi ya CCM ya ufisadi mnawaita haters na wajinga. Hiyo ni dalili ya kushindwa kwa kutukana pale ambapo usemi unatamkwa. Makaburu enzi za apartheid waliwa-demonize ANC na wapigania uhuru wa Afrika ya Kusini na kuwaita terrorists. Lakini leo wale wale terroists wamekuwa sio tena kwa vile baada ya muda ukweli hujitenga na uongo. Mnajua wazi ndani ya mioyo yenu kuwa CCM sio chama cha kuleta mapinduzi katika maisha ya Watanzania, ila ni chama cha kudumisha ufisadi na kuwakamua Watanzania. Na ninyi mnataka kuendeleza hayo makamuzi. Kuna wakati Mwalimu Nyerere (Mungu amuweke mahali pema, alisema,: 'There is a limit to milking a cow.' Kuna limit ya kuwakamua Watanzania.
ReplyDelete