
Tanzania Association taifa ambayo inasimamia swala hili ikisaidiwa na ubalozi, imeyatambua maeneo matatu ambayo Dr Kamara atayatembelea na tarehe na muda kama ifuatavyo:

Inategemewa kwamba wanajumuiya waishio Luton, Oxford, Milton Keynes, Slough, Bristol, Birmingham, Coventry, Northampton na maeneo mengine ya karibu watahudhuria kongamano la London au Reading.
Vile vile inategemewa kwamba wanajumuiya waishio Leicester, Leeds, Liverpool na maeneo mengine ya kaskazini mwa UK watahudhuria kongamano la Manchester.
Hata hivyo, hakuna kinachomzuia mwananchi kuhudhuria kongamano lolote kati ya hayo hapo juu iwapo tu atatimiza sharti moja kama ilivyoorodheshwa hapo chini.
Angalizo: Ili kuhakikisha kwamba wananchi wengi wanapata nafasi ya kuhudhuria na kushiriki kikamilifu katika hali ya usalama na isiyo na usumbufu, wananchi wanatakiwa kujiandikisha katika mkoa ambapo kongamano wanalotegemea kuhudhuria litafanyika.
Kwa mkoa wa London:
Ukumbi:- TANZANIA HIGH COMMISSION
3 STRATFORD PLACE W1C 1AS
LONDON.
Kwa maelezo zaidi tafadhali tumia:
Email: communications.talondon@gmail.com
Simu: 07960811614
Blog: www.tanzaniaassociationlondon.blogspot.com
Kwa wakazi wa Manchester
Ukumbi:- INTERNATIONAL SOCIETY
OXFORD ROAD
M13 9PG
Karibu na Natwest Bank – University of Manchester
Kwa maelezo zaidi piga: 07739155289 – Joyce.
Kwa wakazi wa Reading:
Ukumbi ni:- NOVOTEL HOTEL
25B FRIAR STREET
READING
RG1 1DP
Kwa maelezo zaidi kwa wanajumuiya wa Reading tafadhali tumia:
Email: tzra2009@gmail.com
Simu: +447865673756.
Blog: www.tanzaniaassociation-reading.blogspot.com
Kabla ya kuanza kwa mkutano na Mh waziri, wakina Mama wa Reading watakutana na kiongozi wa kinamama wa taifa ambaye ni Makamu wa Mwenyekiti Taifa. Bi Nsemwa. Ambao utakuwa katika ukumbi huo kuanzia saa saba mchana mpaka saa nane. (1pm – 2pm). Wakina Mama wote mnakaribishwa kwenye kikao hicho kitakacho kuwa kikijadili maswala ya maendeleo ya jamii kina mama na watoto. Kwa maelezo zaidi wasiliana na Bi Wendy Namba 07897277303.
Kwa maelezo zaidi kuhusiana na ziara hii tafadhali wasiliana na TA taifa hapa: watanzaniauk@hotmail.co.uk
07846783365 or 07536497772
KWA NIABA YA UBALOZI NA TA WOTE MNAKARIBISHWA
By Director of Communication - TA National
WellDone! Kazi Nzuri . TA sasa mnaonekana mnajitahidi kufanya mambo yanayoeleweka.
ReplyDelete