Ni takribani wiki mbili sasa nchi imekosa bidhaa hii adimu wakati tayari Watanzania wengi hususani waishio jijini Dar es Salaam wamevutika kuitumia.
Mwezi ulopita upatikanaji ulikuwa shida vilevile. Katika risala za bajeti zilizopita, si tu kwamba serikali iliahidi kuhamasisha matumizi na upatikanaji wa gesi aina ya Liquidified Petrolium Gas (LPG) na vilevile kuondoa/kupunguza kodi.
Tunakiri matumizi yake yamepunguza kiwango cha mkaa na uharibifu wa misitu. Sasa imekuwa kinyume na kusababisha kero/adha kubwa nchini. Gesi haipatikani na wauzaji wamepandisha bei kiholela kwa ile inayopatikana kwa uchache. Naona tumerudi enzi za awamu ya kwanza watu walipokuwa wakirusha bei ya sukari na petrol. Tembelea maduka ya gesi utaona hayana kitu na wasambazaji wachache wamejifanya miungu watu, wateja wanaunga foleni.

Cha kushangaza hakuna taarifa yoyote (pubic information) inayotolewa na kampuni pekee husika ya Oryx wala wizara husika au EWURA. Nchi za ulaya waziri angejiuzulu. Hao wasambazaji wamekuwa na uchoyo na njaa ya pesa kwani wanaiuza wenyewe rejareja badala ya kuwapatia small dealers. Orys Co LTd imepandisha bei toka Sh 34,000 hadi Sh 35,000 lakini mitaani sasa hivi inarushwa/paa sh. 48,000. Tuseme tatizo kubwa ni ukiritimba au monopoly of the LPG business??

Kubwa zaidi ni ukiritimba wa uingizaji gesi kwani ni kampuni moja tu ya Oryx inayoagiza. Wizara ya Nishati na.. mko wapi???. Absolutely there is no control or regulation of gas in Tanzania. Tume ya ushindani wa biashara mko wapi??
Hili linaweza tu kutokea nchini mwangu Tanzania tuu.
Mdau UmemeJua

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 16, 2010

    Mamlaka ya Nishati EWURA, Bodi ya Magari yendayo Kasi,Tume ya Ushindani,Mamlaka ya chakula na Madawa na wengineo.......wote wamefungua vijiwe/ofisi kuonyesha MBWEMBWE za kuvaa suti.....hovyooooo kabisa!!!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 16, 2010

    wiki iliyopita nilizunguka karibu mji mzima kwa siku 2 mfululizo, kutokea bunju, kawe, morroco, migomigo, namanga shopping, ... nikaja kuambulia kinondoni karibu na makaburini kwa 52,000/- mtungi niliokuwa nanunua kwa 35,000/-!!

    Nchi hii ni kama "tako" kila mwenye "kiboko" uchapa hapo tu!

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 16, 2010

    Huyo waziri wa ulaya angejiuzulu kwa lipi? mimi sijaelewa hapo anahusika vipi, angefanya lipi na kujiuzulu kwake kungesaidia vipi. Labda dawa ni kwenda kuishi hukohuko Ulaya!

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 16, 2010

    Itasababisha watu watake kurudi kutumia nishayti ya kuni ambayo tunajitahidi kuipunguza ili kulinda mazingira katika misitu na kupunguza uchafuzi wa hali ya hewa kwa njia ya moshi. Serikali inapaswa bidhaa zingine isimamie kwa vile zina athari katia sekta zingine. Wahusika (EWURA) wanapaswa kulichukulia hatua swala hili

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 16, 2010

    HII NCHI NINAAMINI INAVIONGOZI WASOMI,LAKINI USHENZI ULIOKO HAPA TANZANIA M/MUNGU NDO ANAYETUSAIDIA TU, AT LEAST WAMEKWENDA SHULE LAKINI NAONA ELIMU YAO HAIWASAIDII KABISAAA.. KAMA WIZARA HUSIKA INAKAA NIMYA BILA KUHOJI HII MAMBO INAKUWAJE, WAMEHUBIRI TUSIKATE MITI TUTUNZE MAZINGIRA WAKAINTRODUCE NA KUSISITIZA MATUMIZI YA GESI WATU WAMEANZA KUITIKIA WITO LAKINI ANGALIA MATOKEO YAKE BEI ZINAKUWA JUU KUPITA KIASI, UOZO MTUPU..

    ELIMU WALIYONAYO HAIWASAIDII BASI WAWE WANACOPY NA KUPASTE TU WACHUKUE RESEARCH WALIZOFANYA NCHI ZILIZOENDELEA WABADILI TITLE YA PROJECT MAISHA YASONGE KWANI TANZANIA TUNA NINI KIPYA ZAIDI YA UPUUZI WA WANASIASA? YES! NASEMA TUCOPY NA KUPASTE KWA SABABU SISI NI NCHI INAYOENDELEA BASI TUCHUKUE YALE YALIYOKO KWENYE NCHI ZILIZOENDELEA TUSONGE MBELE KIDOGO..

    MFANO MDOGO KWA WALE WENZANGU MNAOSAFIRI KWA KUTUMIA NJIA YA NAMANGA TO NAIROBI ANGALIA KIWANGO CHA BARABARA YA LAMI YA TANZANIA NA INAYOANZIA KENYA HATA KWA MTU ASIYEJUA KUTOFAUTISHA VITU KWA UMAKINI ATASHTUKA TU TANZANIA NJAA ZITATUMALIZA....

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 17, 2010

    Bei zinapanda kwani wauzaji wanatumia magari yao kufuata gas baada ya wasambazaji kusitisha huduma hiyo. Wanakazania kuwahi kusomba gesi depot ya Oryx ili kuongeza mauzo yao ya rejareja. Mtu huyohuyo anakuwa Wholesaler na hapohapo ni retailer.Ni kama "A tiger watching the chicken house" umeona wapi hili??. Ndo Tanzania yetu.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 17, 2010

    Hatutafika! tusubiri hotuba ya bajeti ya Waziri wa Nishati tuone atasema nini kuhusu nishati mbadala. Hao big shorts wa Oryx wanakula sahani moja na wasambazaji. nani hajui kuwa wamepewa hisa kubwa. Iweje Oryx wateue wasambazaji kiduchu DSM, Rushwa/Ufisadi chafu. EWURA ndo hawana meno kabisaaa.aaa h.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...