Ajali hii ya kutisha ilivyotokea jana majira ya saa 6 wilayani Kahama kwa kuhusisha basi la Super Najimunisa lililokuwa linatoka Bukoba kwenda jijini Dar Es Salaam na kugongana uso kwa uso lori aina ya fuso. Ajali hiyo ilisababisha vifo vya watu 17 pale pale na wengine kibao kujeruhiwa



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 31, 2010

    Jamani kwa kweli ni ajli mbaya sana, madereva kila siku wanasababishia uhai wa watu ambao hawana atia, Mungu tusaidie tuepushe na ajali.
    Poleni ndugu na jamaa walioondokewa na wapendwa wao, na wale mejuruhi tunawaombea wapone haraka.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 31, 2010

    Mungu tusaidie

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 31, 2010

    Inasikitisha sana.
    Ni nani mwenye makosa? mi nadhani umefika wakati, kama ajali ikitokea kwenye hivi vyombo vya public transport na ikigundulika dereva wake ndio mwenye makosa, inatakiwa hilo basi lifutiwe leseni ya kuendesha biashara ya usafiri.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 31, 2010

    Hii sio ajali.. hii ni MAKSUDI.

    ReplyDelete
  5. ajali ajali mpaka lini?

    Mbaya zaidi asilimia kubwa za ajali ....ni zile ajali ambazo zingeweza kuhepukika...


    Poleni ndugu jamaa,marafiki mliondokewa na wapendwa wenu.

    Mwenyezi Mungu awapumzishe kwa amani marehemu wote.Amina

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 31, 2010

    Endapo Tanzania tungekuwa na uchunguzi madhubuti wa ajali na adhabu kali kwa wote waliohusika, sidhani kama hili wimbi la ajali linalomaliza maisha ya watu lingeendelea kuwa kubwa kiasi hiki

    ReplyDelete
  7. Nukuu "Uko wapi ubindamu wako, iko wapi hadhi yako na utu wako wewe ambaye umeumbwa kwa heshima na hadhi kuliko wanyama wote na mimea, mbona unajigeuza kuwa vile ambavyo Muumba wako hakutaka uwe?

    Amka kutoka usingizini, jitambue ili ujikomboe wewe ni wa thamani kubwa, usijdharirishe kwa tamaa za kijinga, kura yako ndiyo utu wako, ilinde na uitumie vyema haki yako hiyo na utaheshimiwa duniani na mbinguni" Mwisho wa kunukuu.

    Ndio vinaendana, tatizo la ajali ni mfumo uliopo. Tunahitaji mabadiliko makubwa, tena makubwa sana kuikomboa nchi yetu. Ajali zote za barabarani zinaepukika. Tena tusiziite ajali, bali tuite migongano ya magari

    Mungu ibariki Tanzania.

    ReplyDelete
  8. Kila siku ajali? Sheria na adhabu kali ndio dawa.

    ReplyDelete
  9. Ture! Tukibadilisha hawa viongozi na ajali zitaisha. Hizo zote zinaepukika lakini viongozi wamefunga macho na sheria hazifuatwi na wenye magari hawatozwi fain yeyote magari yaoa yakiwa na violation yeyote...

    Kumbuka kura yako ndio itakayokuokoa

    ReplyDelete
  10. Ukiona tatizo limekuwa sugu hasa nchini TZ, ujue KIGOGO YUKO NYUMA YAKE. Madereva hawawezi kusikia cha sheria za barabara wala nini kwa sabb hivi vyombo vya usafiri vicnmilikuwa na wakubwa. Akikamatwa mkosaji, simu inapigwa, utasiki " mmuachie mara moja"

    Tatizo la uvunjaji wa sheria si barabarani tu hata ktk taasisi nyingine. Shida inatokana na waajiriwa kuwa na uhusiano wa karibu na waajiri. Kitu ambacho hakiwezi kuepukika.

    Shida nyingine ni kwamba, madereva wa malori ni kama sheria haiwagusi. Wao huendesha wanavyotaka. Utakuta ajali nyingi za barabara chanzo huwa ni malori.

    Ukichunguza wengi hawana leseni, wavuta bangi, vijana wadogo sana n.k.

    Barabara hazina mlinzi, matrafic njaa kali, hivyo waTZ kuteketea ni lazima.... KILIMO KWANZA, sijui atalima nani?

    ReplyDelete
  11. madereva wa malori ni wehu!!msiseme kabisa na wako free hawaguswi na traffic

    eeh Mungu watie nguvu wafiwa na waponye majeruhi

    ReplyDelete
  12. Hizi ajali mara zote zinasababishwa na madereva wazembe wasiokuwa na utu wala kujali chochote dhidi ya maisha ya watu! Vile vile police wa usalama wa barabarani nao huchangia kwa njia moja ama nyingine kwani wengi wa madereva hao hufahamiana kwani hupita njia hizo kila mara na wao huamua kunyamaza kwa kupokea rushwa. Sasa cha msingi ni hivi sisi kama watu na abiria kwenye mabasi hayo tunapoona ya kuwa dereva hajali na mwendo wake siyo mzuri ni moja kwa moja abiria kuamua kumsimamisha na kama kama kuna kituo karibu ni kum report au kupiga simu police waje kumkamata kama siyo kuadhibiwa na abiria. Inauma sana wa ndugu! Poleni sana familia za waliofiwa na tunamuomba Mwenyezi Mungu awarehemu marehemu wote katika hiyo ajali. Amin!

    ReplyDelete
  13. Hivi ndugu zangu watanzania tutaendelee kufa kwa ajali za kipumbavu mpaka lini, wakati hii serikali haifanyi chochote kuzuia hivi vifo. Utawala dhaifu, tunahitaji uongozi wa sawa sawa. Mungu awapokea marehemu hawa. Amina.

    ReplyDelete
  14. TATIZO HAYA MAGARI NI YA VIONGOZI AMBAO UKIYAKAMATA INAKUWA SHIDA TENA, SERIKALI INANUKA RUSHWA, JESHI LA POLISI HALIWEZI KAZI KABISA KABISA KWA KWELI NASEMA ULE UKWELI WANGU KAMA MTU ATAKATAA SHAURI YAKE.
    KWAKO KAMANDA WA KIKOSI CHA USALAMA BARABARANI UNATAKIWA WEWE NA KIKOSI CHAKO MBINAFSISHWE KWA KUWA UWEZO WENU WA KUFANYA KAZI UMEFIKA MWISHO, HAKUNA KITU ZAIDI YA KUSHINDANA KUTAFUTA PESA ZA RUSHWA KATIKA MAGARI YAENDAYO MIKOANI, LAKINI USALAMA KWA WATUMIAO HIVYO VYOMBO HAMNA HABARI NAO. MKUU HUNA JINSI ULITOA AHADI KIBAO KUMBE HUNA LOLOTE

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...