mwendesha pikipiki akigombewa kama mpira wa kona na kinamama wenye jazba baada ya kutaka kupita kibabe baada ya wananchi wa Kunduchi mtongani jijini Dar kufunga barabara kulalamikia ajali za kila mara eneo hilo huku hakuna hatua ikichukuliwa.

Kinamama wakimlilia afande shida zao za watu kugongwa
sehemu hiyo kila kukicha kutokana na kutowekewa matuta
watoto wa Kunduchi mtongani wakiangalia wakati matairi yaliyotiwa kiberiti yakiwaka katikati ya barabara kuziba njia ikiwa njia ya kulalamika kwa ajali za mara kwa mara

Wananchi wanaoishi Kunduchi Mtongani jijini Dar, leo walizua kizazaa baada ya kuifunga barabara kuu inayotoka Mbuyuni kuelekea eneo hilo kufuatia gari aina ya Toyota Hiace linalofanya shughuli za daladala kati ya Kunduchi na Mwenge kuwagonga watoto wawili wa familia moja ambapo mmoja inasemekana amefariki dunia.
Vurugu hizo zilisababisha askari wa kutuliza ghasia FFU waliofika eneo la tukio kulazimika kutumia mabomu ya kutoa machozi kuwatawanya wakazi hao waliojawa na jazba, lakini bila mafanikio makubwa. Zogo liliendelea kwa karibu masaa manne kabla ya kutulizwa.

kwa picha na habari zaidi tembela Global Publishers BOFYA HAPA




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 21, 2010

    Haya mambo huwa yanaanza hivi hivi. Inaonyesha ni jinsi gani watu walivyokata tamaa na watawala. No body is listen to them, so they are entitled to protest.

    ReplyDelete
  2. Patrick-MagazetiJuly 22, 2010

    Michuzi,

    Mimi ninaona sasa hii imekuwa kama serikali yetu inatupilia kila tatizo juu ya pesa au fedha. Kutatua ajali barabarani kunahitaji serikali kuu na serikali za mitaa kushirikiana kama hivi:
    1. Wizara ya mambo ya ndani (home affairs) police traffic washughulikie mambo ya sheria za barabarani.
    2. Serikali ni lazima waunde wizara ya usafirishaji na magari, hii wizara hitasimamia utoaji wa leseni na mafunzo ya medereva. Na kuhakikisha madereva wenye leseni wanaelimishwa juu ya usalama wa barabarani kabla ya kupewa leseni.
    3. Mahakama ya Usalama wa magari na Medereva, hii wanashugulikia mashtaka ya madereva. Hii iwe administrative court, juu madereva waalifu.
    4. Majaji wawe wanachaguliwa na wananchi kwa kupigiwa kura kila baada ya miaka 3 au miaka 4.
    5.Serikali kuu lazima wabadili sheria za usalama wa barabarani kwa sababu wizara ya mambo ya ndani pekee imepangia mambo mengi sana.
    3.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 22, 2010

    SOLUTION; JK, huu ni wakati wa uchaguzi, WEKA FRYOVERS, MATATIZO YA KUGONGWA GONGWA WALALA HOI YATAKWISHA MARA MOJA NA KURA TUTAKUPIGIA. We know there will be no more fryovers after election is over.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 22, 2010

    wewe mdau wa Thu Jul 22, 03:28:00 AM fryover ndio nini? na unataka kukaanga nini hasa? kama hujui kiingilishi kwani ni lazima useme?

    ReplyDelete
  5. Mdau, BloomsburyJuly 22, 2010

    Safi sana. Nafurahi kuona waTanzania wakiweka upole usiokuwa na maana pembeni.

    Watanzania sasa wanaamka, wameanza kidogo kidogo sasa itasambaa nchi nzima watu hawataki mchezo na haki zao.

    Kuhusu swala la 'fryover' kwa kweli wewe mdau wa 8.00 am, Would you like to be 'fried over' like an egg? Labda siku moja waTanzania watafunga barabara/andamana kudai watu waandike kwa ufanisi :)

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 22, 2010

    I think that guy/girl aliyeandika "FRYOVER" he was just trying to be funny yet this here is a serious issue...it's time we Tanzanians start talking sense, flipping words and giving funny advises should be now end because this is where most of us are mislead, we do entertain so much of "bullbleep"...as they say, talk is cheap!

    mdau,
    Ashkmatit

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 22, 2010

    SWALI:hivi kuweka matuta barabarani ni sheria au by-laws gani katika Tanzania na imendikwa kwa utekelezaji kwa barabara zipi hasa na aina ya matuta je?

    binafsi siijui wala siielewi

    nijibiwe hili wadau!!

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 22, 2010

    "FRYOVERS"... Huyu kweli ameamua. Au labda ni wale wanaotumia L kwenye R. Maybe he/she wanted to say "FLYOVERS"...kwa kuwa wananchi wamezungumzia magari yanayokimbia sana...this could be the closest word to his own. Peace and Love my TZ people!

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 22, 2010

    mdau 11:16:00 AM

    barabaea za matuta "BUMPING ROADS" au "NO DRIVING ZONE" zipo sehemu nyingi hata katika nchi zilizoendelea,barabara hizi ni muhimu saana katika maeneo ya ukaribu wa shule za watoto au sehemu zenye msongamano wa watu wengi kama masoko au maduka mengi,nafikiri tatizo letu hapo kunduchi mtongani litamalizika kama kutakuwepo na matuta "BUMPING WITH LOW SPEED 15 KM PER HOUR" Tanzania hilo halitokuwa tatizo kubwa la kupoteza maisha ya binadamu tuna mafundi wakitaalamu.

    Mickey Jones
    mdau wa Denmark

    ReplyDelete
  10. Nimefurahi sana kuona hao akina mama wamechukua hatua hiyo! Wamechoka, na sisi tumechoka kwa ujumla. Wanajua kuwa hakuna hatua ambayo ingechukuliwa hadi mtoto wa mkubwa agongwe au mkubwa apate ajali hapo! Waweke matuta ili kulinda maisha ya watu wote!

    AKINA MAMA JUU, JUU, JUU ZAIDI!!!!

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 22, 2010

    Asante kaka Michuzi, tuhesabu siku tuone hayo matuta yatawekwa lini? Naomba utupe feed back.Wanohusika na hizo barabara wapo kwenye mitandao wanasoma wanasubiri msaada utoke nje.Ndiyo waweke matuta.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...