Kikosi kizima cha FFU wa Ngoma Africa Band kinatarajiwa kutua kwa nguvu zote katika maonyesho ya Afrika & karibik yatakayofanyika jumamosi 7-08-2010 katika viwanja vya Robestock Park,mjini Frankfurt,Ujerumani. Maelfu ya washabiki wa mziki wanaisubiri kwa hamu bendi hiyo maarufu barani ulaya kwa kuwapandisha mzuka! washabiki na mdundo wao maarufu kama "Bongo Dansi". Baada ya onyesho hilo ! Kamanda wa kikosi hiko Ras Makunja ataliongoza karandinga la FFU.
Katika onyesho lingine kubwa la wazi Music Festival,litakalo fanyika mjini Kaiserlautern, Ujerumani siku ya Jumapili 8-08-2010 ambako washabiki washajiweka tayari tayari kwa kwenda mchaka mchaka na mdundo wa Ngoma Africa band. FFU wa "Ngoma Africa Band" sasa wanatamba na singo CD mpya "Jakaya Kikwete 2010" CD ambayo inasemekana imeshaweka wingu nchini Tanzania na wakati wowote inaweza kutingisha anga za mziki za Afrika mashariki na popote pale !
CD ambayo ukisikiliza utapata vitu vyote kuanzia mziki mkubwa,ujumbe ambao utakupa majibu ya maswali mengi unayojiuliza moyoni mwako!
Jipe Raha at www.myspace.com/thengomaafrica
Jipe Raha at www.myspace.com/thengomaafrica
Ndio Kaka yangu nakuona
ReplyDeletemkuu kamanda naona virungu vinanukia huko frankfurt,najua hapalaliki....unaponiacha hoi unapomaliza kazi lazima utokee mlango wa nyuma sijui kwa nini?
ReplyDeletevichaa kazi yenu inakubalika kimataifa kazeni buti
ReplyDelete