Angalizo: Soma ukiwa kwenye Foleni ndefu ya Magari,
na shiriki kwenye utatuzi wa tatizo hili.
Hoja ya Msongamano Mkubwa wa Magari(Traffic Jam)
jijini Dar-es-salaam
jijini Dar-es-salaam
Naomba nianze kwa kuipongeza Serikali ya awamu wa nne kwa mazuri mengi ambayo Watanzania wanaendelea kuyashuhudia chini ya uongozi wa mpendwa wetu Rais Jakaya Mrisho Kikwete. Sitaweza kuyaainisha Mazuri mengi ambayo watanzania tumeshuhudia kama hatua thabiti zilizochukuliwa na uongozi wake katika kukuza uchumi wa nchi. Waswahili wanasema mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni. Chama chetu pamoja na changamoto nyingi walizokumbana nazo lazima tukipongeze kwa mafanikio ya utekelezaji wa ilani ya 2005 - .
Naomba niendelee kwa kuanza mchango wangu katika mada hii kwa kuwa na mashaka na uamuzi wa Serikali ya awamu ya nne ambayo inamaliza mda wake na kuomba ridhaa ya watanzania kwa kipindi kingine cha miaka mitano kutoa tamko kwa kupitia mgombea pekee wa chama cha Mapinduzi kwamba Serikali itaanza mwaka kesho kujenga barabara za juu ( Fly Over Roads) Kama suluhisho la msongamano mkubwa wa Magari katika Jiji letu mahiri la Dar. Fly Over si sahihi kwa uchumi wa Watanzania walio wengi.
Labda tujiulize maswali ya Msingi. Dolla moja kwa sasa inabadilishwa kwa Shiling ya Tanzania 1,400, hii ni dhahiri kwamba katika ulimwengu wa nchi zilizoendelea Tanzania tuko nyuma, wenzetu wa Kenya ( dola moja hubadilishwa kwa Ksh 80), wenzetu wa South Africa ( Dola 1 hubadilishwa kwa rand 10) Wenzetu wa Ethiopia ( Dola moja kwa 12) na Wenzetu wa Burundi waliokuwa kwenye vita nzito ya kikabila miaka kumi na tano iliyopita ( Dolla 1 kwa sh 450). Sasa labda tujifunze kwa wenzetu hawa je wanazo barabara ngapi zinazopita juu? Ili na sisi tuige mifano yao.
Nimeanza kutoa takwimu hizi ili ziweze kutupa picha ya ni kwa namna gani uchumi wetu bado ni mdogo lakini tunafikiria kufanya mambo ambayo sio kipaombele kwa wananchi walio wengi, Nadhani tatizo ni kwamba, badala ya kuangalia nini tatizo la wingi wa msongamano wa magari Dar, Tunakimbilia kujenga barabara za juu. Labda tunaweza kuipongeza serikali ya awamu ya nne kwa kuhakikisha barabara zote za Mikoa ya Tanzania zina barabara zenye kiwango cha lami na zinapitika kwa kipindi chote cha mwaka. Hii ni Hatua kubwa sana kwa maendeleo ya nchi yetu lakini ladba ni changamoto ya kwanza kwa serikali kwamba badala ya kufikiria kuweka Fly Over roads Dar-es-salaam basi ihakikishe sehemu nyingine za Wilaya, Kata na Vijiji vinafikika.
Nimeanza kutoa takwimu hizi ili ziweze kutupa picha ya ni kwa namna gani uchumi wetu bado ni mdogo lakini tunafikiria kufanya mambo ambayo sio kipaombele kwa wananchi walio wengi, Nadhani tatizo ni kwamba, badala ya kuangalia nini tatizo la wingi wa msongamano wa magari Dar, Tunakimbilia kujenga barabara za juu. Labda tunaweza kuipongeza serikali ya awamu ya nne kwa kuhakikisha barabara zote za Mikoa ya Tanzania zina barabara zenye kiwango cha lami na zinapitika kwa kipindi chote cha mwaka. Hii ni Hatua kubwa sana kwa maendeleo ya nchi yetu lakini ladba ni changamoto ya kwanza kwa serikali kwamba badala ya kufikiria kuweka Fly Over roads Dar-es-salaam basi ihakikishe sehemu nyingine za Wilaya, Kata na Vijiji vinafikika.
Labda unaweza usielewe ninamaanisha nini ! Tuanze na mkoa wa Dar-es-salaam ambao ndio mkoa mama katika nchi yetu, je Wilaya zote, Kata zote na Mitaa yote ina barabara zinazopitika. Swala la Ujenzi holela nadhani ndio chanzo kikuu cha tatizo hili hapa Dar-es-salaam, Hili linasikitisha sana kwani vibali vya ujenzi hutolewa na Manispaa husika ili hali wakijua maeneo yanayojengwa hayaruhusiwi. Ni budi tumpongeze Mh. Mkuu wa mkoa wa Dar, Bw Lukuvi kwa jitihada alizozionyesha hivi karibuni za kuwashughulikia wafanyakazi wa Manispaa waliohusika kwenye uuzaji wa maeneo ya wazi kinyemela.
Lakini badala ya kuendelea kuilaumu Serikali labda sasa ni muda muafaka kuishauri Serikali ni hatua zipi za haraka zinaweza kuchukuliwa, hata kama tutakuwa tunasubiria fly over ambazo kwa ushauri wangu zingetakiwa kuja kwenye miaka ya 2050 kama kasi ya uchumi wetu itaendelea hivi hivi.
ICT Ambassador De Africa,
Sesil C. Latemba
+255 713 335480
.....itaendelea kesho
umeogea ukweli tunahitaji vitu vidogo sana kupunguza traffic jam tanzania hamna magari mengi kiasi hicho cha kuhitaji fly over tanzania hatuna road signs, hamna road displine..... simple yellow box (keep clear) zinatosha hazitumii gharama it is just is simple logic. fly over tuwaaachie wenzetu because they need them tanzania hatuitaji not even in the 100 years. tuige mambo yenye msingi na yenye manufaa.
ReplyDeletesioni kwanini kesho uendelee kama una mawazo finyu namna hii. Je unajua ni kiasi gani mkoa wa DSM unachangia katika pato la taifa ( kwa njia ya kodi)? fanya tathmini ya kutosha ili ujue madhara ya msongamano wa magari kwenye utendaji wa kazi na kwa wawekezaji. Suluhisho la kitu hii ni muhimu si kwa wakazi wa dar tu bali kwa taifa zima. kuwa macho!
ReplyDeleteUlichoandika ni upuuzi.Kwa hiyo tatizo la msongamano wa DSM ni ujenzi holela? Pumba tupu.
ReplyDeleteNDUGU lATEMBA NAKUPA HONGERA KWA UCHAMBUZI WAKO WA KINA KIFUPI!! NAPENDA UFAHAMU KUWA NI KWELI KUNA MATATIZO MENGI SANA NA MPK SASA KIPATO NI TOFAUTI KUBWA SANA KATI YA ALIE JUU NA ALIE CHINI HALI NI DUNI SANA LAKINI KUHUSU DAR,KAMA ULIVYOSEMA HAPA NI MAMA WA MIKOA YOTE MAMBO HAPA YAKIENDA SAWA NA HUKO YATAKUWA MAZURI SERIKALI YETU ILIANZA MUDA MWINGI KUTAFUTA SULUHISHO LA TATIZO LA FOLENI,IKATOA IKAKARIBISHA MAWAZO NA ILIUNDWA KAMATI MAALUMU KWA HILO NA NI JUZI TU WAMEKABIDHI SERIKALINI, NA HILI NI MOJA YA HAYO MAAMUZI, HAYAWEZI KUKAMILIKA UTAKAVYO WEWE.HAYA NI MAENDELEO HAPA DAR NDIO KIONGOZI WA NCHI NZIMA NA SPIDI IKIWEPO HAPA NDIO SPIDI YA WILAYANI NA VIJIJINI, HUWEZI KUWAZUIA WATU WASIENDE AGHAKHAN AU HINDUMANDAL ETI KUNA WATU BADO WANALALA CHINI KULE AMANA!! KAZA BUTI NA HUO MFUMUKO WA BEI USIKUTISHE UTASHUKA KIASI,
ReplyDeleteTUKUBALI MATOKEO KUKIWA NA KIZURI TUKIPOKEE NA KIBAYA TUKIKARIPIE TUHOJI MABAYA,MAZURI TUSIFIE KULIKONI?
According to Speech ya rais ya kuahirisha Bunge last week.Foleni Dar ni Dalili za Maisha bora kwa kila Mtanzania.......Jamani kweli tukubaliane naye? Sidhani kwani jibu ni miundo mbinu mibovu....Je kukithiri kwa majambazi Dar ni dalili za maisha bora kwa kila Mtanzania?
ReplyDeleteMheshimiwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete ameshatamka bayana kuwa msongamano wa magari ni ishara ya maisha bora kwa kila Mtanzania.Tuuondoe ili tuonekane masikini?
ReplyDeleteHalafu unapozungumzia uchumi wetu mdogo mbona unapuuza ukweli kuwa tunamudu kuwalipa wabunge wetu mamilioni ya shilingi,sambamba na utitiri wa magari ya thamani kwa matumizi ya viongozi wetu na matumizi mengine chungu mbovu ya anasa?
Na alokwambia Roma ilijengwa kwa siku moja ni nani?Na unadhani reli ya kati au tazara zilijengwa kwa mwezi mmoja?Tuanze lini miradi kama hiyo ya flyover kama si sasa?
Naomba nikushukuru ndugu Sesil C. Latemba kwa mchango wako , ningependa tu na mimi kuchangia hoja juu ya mada hii. Kwanza nchi ulizozitaja ingawa zina exchange rate yake against dollar inaonekana ina nguvu haimanishi kuwa the economy is better off, kwa mfano Ethiopia na Burundi ambazo ulisema exchange rate ya currencies zake against dollar ni 12 Birr na 450 BIF (Burundian Franc
ReplyDelete) respecitvely,ukicheki kwenye 2009 UNDP report on Development, both HDI ranking zao ni below tanzania, at 171 na 174 place respectively,ni muhimu kuelewa kwamba kuwa na strong currency against the dollar doesnt mean kuwa the counry is more developed, at todays exchange rate u will see kuwa 1.00 USD= 86.9948 JPY (Japanese Yen) whereas 1.00 USD = 3.21500 MYR (Malaysian Ringgit) (source: http://www.xe.com/), does that mean kuwa Malaysia is more developed than Japan just because their currency is stronger ? if so then why would Malaysia be listed in the high development category same as Brazil and Turkey whereas Japan is listed in the Very High Human development category same as and The United Kingdom, The United states and other such developed nations? Ningependa kukumbusha Life expectancy, Education levels na Per Capita GDP are some of the determining factors za Development rather than our percerption kuwa exchange rate is the only determining factor, because you will realise that Oman has an exchange rate 1.00 OMR = 20.1849 HKD (HONG KONG DOLLAR), but they r still in the high human development category whereas the Hong Kong (SAR) which has a weaker exchange rate compare to the Rial is in the Very High Human Development category, Ni muhimu kukumbuka kuwa Tanzania tuna Life Expectancy level ya juu zaidi (at 55yrs)as compared to ya burundi na ethiopia at(50.1 and 54.7) respectively, education index ya 0.673 as compared to 0.403 na 0.559 ya Ethiopia na Burundi respectively, na GDP ya 0.416 as compared to (0.343 na 0.205) ya Ethiopia na Burundi respectively. Hizo ni some of the criteria to determine development, lakini pia naomba nikumbushe kuwa infrastructure development is very important in order to stimulate economic growth, the amount of money wasted on fuel that in turn goes 2 waste waiting around in traffic jams could be put to better use if Fly-Overs were constructed, i therefore agree with our Prezzo. :-) Mh. Jakaya M Kikwete on that, as long as other important sectors of our country arent neglected in the process such as healthcare and education development should also be given equal priority.(source : http://hdr.undp.org/en/media/HDR_2009_EN_Complete.pdf)
Naona kuna mchanganyiko wa mada hapa,kuna suala la fly over na mambo ya currency evaluation.Uhusiano wa hivi vitu viwili upo mbali kidogo kwa maoni yangu mimi.Nadhani muandishi kawa na jazba ,lakini ujumbe umefika.
ReplyDeleteSuluhu ya makutano ya juu (Flyover) ni uamuzi wa kisiasa. Watu wengi wa pande zote za mirengo waliisha kataa hii suluhu. Kwa kuwa watanzania ni wabishi na wasiotaka kufikiria mbali bado wanafikiri makutano ya juu yatajengwa Dar Es Salaam.
ReplyDeleteJiji la Dar halikupangiliwa vizuri toka enzi za mkoloni ukilinganisha na Kampala au Nairobi. Nyingi ya barabara zake ni finyu ingali magorofa marefu yanaendelea kujengwa katikati ya jiji.
Marehemu Nyerere aliliona hilo miaka ya 70 akaamua kuepusha msongamano kwa kuhamishia makao makuu ya nchi Dodoma. CDA ikaanzishwa. Mpaka sasa ni Bunge tu na labda mikutano mikuu ya CCM ndio imehamia Dodoma. Bahati mbaya hata yeye mwenyewe (Nyerere) alishindwa kuhamishia Ikulu Dodoma kwasababu alipenda upepo mwanana wa magogoni ihali akamsukumia Waziri Mkuu aende Dodoma, ambaye bado anaofisi Dar. Sasa shughuli zote za kiserikali zimerundikana katikati ya mji na kila mtu anataka kwenda pale kwani ataweza ku-faulisha kitu na kujipatia vijisenti kwa riziki ya siku.
Kuna jamaa mmoja alishauri ofisi zote zilizo katikati ya Jiji zisambazwe pembezoni mwa mji. Mfano ondoa TRA na ipeleke Gongo la mboto, nyingine peleka Boko, Kimara,kibaha, n.k. Bila kusahau Ikulu ihamie Dodoma, kwani pesa kibao zimeisha tumika kustawisha makao makuu. Halafu anagalia kama kutakuwa na foleni Dar.
Suluhu ya makutano ya juu (Flyover) ni uamuzi wa kisiasa. Watu wengi wa pande zote za mirengo waliisha kataa hii suluhu. Kwa kuwa watanzania ni wabishi na wasiotaka kufikiria mbali bado wanafikiri makutano ya juu yatajengwa Dar Es Salaam.
ReplyDeleteJiji la Dar halikupangiliwa vizuri toka enzi za mkoloni ukilinganisha na Kampala au Nairobi. Nyingi ya barabara zake ni finyu ingali magorofa marefu yanaendelea kujengwa katikati ya jiji.
Marehemu Nyerere aliliona hilo miaka ya 70 akaamua kuepusha msongamano kwa kuhamishia makao makuu ya nchi Dodoma. CDA ikaanzishwa. Mpaka sasa ni Bunge tu na labda mikutano mikuu ya CCM ndio imehamia Dodoma. Bahati mbaya hata yeye mwenyewe (Nyerere) alishindwa kuhamishia Ikulu Dodoma kwasababu alipenda upepo mwanana wa magogoni ihali akamsukumia Waziri Mkuu aende Dodoma, ambaye bado anaofisi Dar. Sasa shughuli zote za kiserikali zimerundikana katikati ya mji na kila mtu anataka kwenda pale kwani ataweza ku-faulisha kitu na kujipatia vijisenti kwa riziki ya siku.
Kuna jamaa mmoja alishauri ofisi zote zilizo katikati ya Jiji zisambazwe pembezoni mwa mji. Mfano ondoa TRA na ipeleke Gongo la mboto, nyingine peleka Boko, Kimara,kibaha, n.k. Bila kusahau Ikulu ihamie Dodoma, kwani pesa kibao zimeisha tumika kustawisha makao makuu. Halafu anagalia kama kutakuwa na foleni Dar.
tatizo la msongamano linaweza kupungua kwa kuacha kujenga kati ya jiji majigorofa kila kukicha wanabomoa gorofa tatu wanajenga ishirini that means idadi ya watu inazidi kuongezeka mjini hapa viongozi cjui wanafikiri nn kuendelea kuruhusu haya magorofa katikati ya jj badala ya kutoka nje ya mji na wizara zimesongamana mjini kwa nn zisihame jamani au kwa kuwa wao hawakai kwenye foleni
ReplyDeleteKama ni kuongea mambo mazuri tu basi anony wa Wed Jul 21, 02:40:00 PM,ameongea vitu vya maana sana ameongea point na kuzitetea kwa kutoa reference.
ReplyDeleteMtoa mada hajatoa sababu za maana za msongamano wa magari(foleni) DSM.Huna reference na kuhusu kutumia exchange rate kama kigezo cha uchumi imara sio kweli nafikiri anony wa Wed Jul 21, 02:40:00 PM ameelezea kila kitu.
Wazo la mchangiaji mmoja kuwa na ofisi pembezoni mwa mji ni zuri.
Ni vizuri mtoa mada akajipanga vizuri akapangilia point zake akielezea background of the problem(baada ya kufanya utafiti),the current situation na nini kifanyike(solution) kwa mtazamo wake yeye ili wachangiaji waendelee kujadili Nini kifanyike.Sasa unapotoa takwimu au data ambazo hazina kichwa wala miguu unatushangaza.
Mkumbuke humu kunatembelewa na watu mbali mbali wakiwemo wachumi,wataalamu wa mipango miji na wataalamu wa miundo mbinu.
Dada mtoa habari yenye kina kifupi kama wanavyosema wachangiaji. Asante sana kwa kuonyesha uwezo wako mdogo unapoishia. Juu ya mambo ya pesa umeula wa chuya kwani Japan wanatakiwa kuwa masikini zaidi ya hao akina SA, Ethiopia na labda kuwa sawa na Kenya.
ReplyDeleteInapokuja kwenye mambo ya Fly-Over, nakushauri wewe na Vihiyo wenzio kuwa TRAFFIC ENGINEER ni somo unalotakuwa kusoma, kuwa na kipaji na uzoefu. Siyo kila Mhandisi anaweza kuwa Traffic Eng. Kwa sababu hiyo, kama hata UJENZI hukusoma, wee chemsha tu maharage, ule na Ulale Salama. Acha Wanaume/Wanawake wenye uwezo wa hayo mambo wafanye kazi zao. ukipata muda basi pitia Jamiiforums kuna mijadala mingi ilifanywa juu ya hili tatizo na solution zake. Kumbuka Dar ni kubwa sasa, haiwezi kuendelea kuvaa NEPI. Inataka Kaptura/suruali.
Nadhani Elimu pungufu ni hatari kuzidi kutokuwa na elimu! Ila kwa kuwa umetoa wazo lako basi tunategemea utakuwa na subira kusikiliza mawazo ya wengine. Katika exchange rate zako umeisahau JAPAN NA CHINA. Ambao exchange rate zao kwa Dola Kenya, Botswana na South Africa ziko mbali mno. Nnachosema ni kwamba usitishwe na exchange rate. Ethiopia inawezakana kuwa ndio yenye Shirika la ndege Bora barani Afrika lakini pia wao ndio yawezekana ni masikini kuliko wote Afrika(I stand to be corrected)!!!
ReplyDeleteKenya Airways yaweza kuwa ya pili barani Afrika, ila nahisi ndege zote ni za KLM. The point is vitu vinavyopelekea hizo better exchange rate havihusiani na wananchi wa hizo nchi kuwa na uwezo wa kumiliki magari ama ongezeko la watu kwenye hizo nchi.
Ukiondoa mabasi madogo madogo, daladala, na kuleta mabasi makubwa yenye kuchukua abiria 300 kwa wakati mmoja, halafu mabasi yawe na muda wa kuingia na kutoka kituoni, baraba za mitaa zi jengwe, trafic light ziwekwe sehemu zinazo takiwa, madereva pamoja na raiya wa elimishwe sheria za barabara, I don't think we will need fly over roads. At least , not know.
ReplyDeleteMTOA MADA UKO SAHIHI.
ReplyDeleteWANAOJENGA FLYOVERS HAWANA NJIA NYINGINE ZA KUONGEZA KWANI BARABARA ZIMEPENYA KILA KONA MITAA YOTE.
BONGO MWATAKA KUJENGER FLYOVERS WAKATI BARABARA ZINAZOUNGANISHA VIUNGA VYA WILAYA NA VITONGOJI HAVIJAJENGWA HAPO NI KUCHEZA KAMARI YA KISIASA.
MKAZI WA MBAGALA HANA NJIA NYINGINE YA KUFIKA AIRPORT, YOMBO, SEGEREA AU PUGU MPAKA APITIE KILWA ROAD MTONI KWA AZIZI HUO NI MFANO TU. SASA UTAJENGA FLYOVERS MBAGALA KUPUNGUZA HUO MSONGAMANO?
HIVI WAHUSIKA HAWAJIULIZI MAGARI YANAYOSONGAMANA MJINI YOTE YANASHUGHULI NJINI AU YANALAZIMIKA KUPITIA KATIKATI YA JIJI KWA VILE HAKUNA NJIA NYINGINE ZA KUFIKIA WANAKOKWENDA?
WENGI WENYE UZOEFU WA KUONA WALIOENDELEA WALIVYOFIKIA WALIPO WAMETOA MAPENDEKEZO MENGI MAZURI NA WENGI WANASHAURI UJENJE WA BARABARA NYINGI JIJINI ILI KUPUNGUZA USUMBUFU WA KUPITIA JIJINI LAKINI NAONA WAHUSIKA HAWATILII MAANANI.
TUNAO WASOMI WENGI NA HUTEMBELEA NCHI NYINGINE WANACHOONA NI FLYOVER TU BILA KUONA JINSI KILA MTAA ULIVYOSHEHENI BARABARA ZA UHAKIKA. ILA FLYOVERS TU?
YANGU MACHO NA MASIKIO JENGENI FLYOVERS HAMTAPATA SULUHISHO NA KISHA MTARUDIA KUJENGA BARABARA TUNAZOWASHAURINI WAKATI MMESHAZIKA MAPESA AMBAYO YANGEONGEZA BARABARA NYINGI BADALA YA FLYOVER MOJA.
Tanzania is not ready with for the flyover road, not high ways. People are so ignorant, i would almost call the roads the killing fields. The buses are driven with very young people whom have no value of human life. Stop the corruption, get good leadership and then move another step. Build better roads, train your traffic officers.......education!
ReplyDeletenjia rahisi ya kupunguza foleni dar ni kupeleka ofisi za serikali nje ya jiji badala ya zote kuzirundika hapo.
ReplyDeleteserikali ikipeleka ofisi zake nje ya jiji misongamano ya foleni itapungua badala kupoteza hela kujenga fly overs kwenye nchi ambayo inaongoza kwa miundo mbinu mibovu.
na jinsi watu wanavyo penda kula hela tusije kujengewa fly over za kichina tukaja kuua watu.barabra za kawaida tu hazipitiki mtu unawaza fly overs.siwezi kumlaumu JK kusema kwamba foleni za sasa hivi zinatoakana na maisha bora kwa mtanzania kwani speech zake nyingi zinakuwa na maneno ya utani utani tu sio kwamba yuko serious.mara nyingi huwa anatania manake kama huwa hatanii maneno yake basi itatufanya tujiulize kiwango cha elimu yake.
Uliyezungumzia kuhusu leadership nakupa five! Unaanza na good leadership. Good leader anafanya research, anakua na priorities then plan alafu uwe na watu mahiri(mawaziri, wakuu wa wilaya, mikoa etc) waku-implement.Ukiwa na wachapa kazi watakupa takwimu sahihi ya matatizo makubwa huko mikoani/wilayani, mapendekezo etc na wewe unakaaa na cabinet yako ya watu mahiri mna-brain storm kuangalia facts na suggestions nyingine kabla ya kwenda kutembelea hizo sehemu.Bila hivyo tutaishia kuropoka tu. Sasa kweli maendeleo ya mtanzania yanapimwa na magari ya Dar. Kwanza asilimia ngapi ya watanzania wanaishi Dar? Na kwanini watu wanahamia Dar? Ukiweza kujibu hayo yote na mengine mbona utakua na solution ya hiyo chaos hapo Dar. Kweli mnataka kusema barabara ni nzuri za kwenda huko Bukoba, Mara, Mtwara, etc mpaka tuanze na kujenga barabara za juu kwa juu? Kwanini Watanzania huwa hatutafuti long time solution tunaharibu kila wakati. Nini kimetupata tunakua hivi? Samahani kwakuchanganya lugha.
ReplyDeletethe main problem with CCM govt is that they dont think on their feet all they care is that they get to do things so as to get 10% but not to do things that will make them proud.Just see what Mkapa did in his home region to where people were eaten by crocodiles now they pass through a bridge..... to where pple were taking six days to reach dar by bus now takes 2days....these are the realy solutions to real problems...
ReplyDeleteKikwete is from pwani region but even thinking of creating a road that will join bagamoyo and kibaha or taking thorough to airport is unthinkable to him that would have reduced the congestion in morogoro road....
ABOVE ALL NO COUNTRY HAS EVER BUILT A FLYING OVER BEFORE EXHAUSTING ALL LAND THAT HAS BEEN PLANNED FOR ROADS.....
sIDHANI KMA FLYOVERS NI SULUHUSHO MIMI NAONA KUNA MAKAMPUNI BINAFSI MENGI MFANO MABANK TUCHUKULIE STANBIC BANK WANA STAFF 300 PALE MAKAO MAKUU WOTE HAO WANA KUJA NA MAGARI MADOGO WAKATI WANAWEZA KUNUNUA STAFF BUS 3 KUCHUKUA STAFF WAO JAM HAPO ITAPUNGUA ,KUNA BOT,VODACOM,NMB,CRDB,TIGO ETC PIA WAANGALIE MAKAZI BORA SIO WANAJENGA KUUZIANA WAO KUKIWA NA MAKAZI BORA NIRAHIS HIZO STAFF BUS KWENDA KUPICK STAFF WAO KWENYE HIZO ESTATE JAMNI ZITAKUJA FLY OVER'S TATIZO LITAKUWA PALEPALE PARKING ZITAKUWA TABU
ReplyDeleteMada kama hizi ndio Mzee wa blog nio zinatakiwa kuletwa humu watu tujadili na kutoa solution za maswala yanayogusa uchumi na wananchi kwa jumla, sio mnatuletea mamabo ya Big brother or Miss kinondoni which are not helping to Tanzanian citizen. Sasa basi nachukua nafasi hii kuchangia swala hili pi, in reality ukifuatilia kwa karibu HAPO DAR FOLENI YA MAGARI UTAGUNDUA KUWA INASABABISHWA NA GOV YENYEWE KUKOSA KUINVEST IN TECHNOLOGY YA KISASA KATIKA UENDAJI WAKE WA KISASA. MFANO WIZARA ZOTE ZIKO DOWN-TOWN INGAWA KUNA BAADHI ZINA BRANCH OUT OF DOWN-TOWN MFANO TRA MY POINT HERE IS MTU AKITAKA KUFUNGUA BIASHARA, KULIPA KODI,AU BILLS, SHOPPING VITU VYOTE HIVYO VIMEELEKWEZWA DOWN-TOWN KWAHIYO UTAKUTA ASUBUHI KILA MTU ANAENDA DOWN-TOWN SII UNAONA LAZIMA KUWE NA FOLENI!!!! SOLUTION INGEKUWA VIZURI KWA WIZARA ZA SELIKARI KWENDANA NA TECHNOLOGIA KAMA WENZETU HAPA ULAYA, FUNGUA BRANCHES ACCROSS THE CITY ZIPE DECENTRALIZED RESPONSIBILTY SIO MTU KULIPA KODI AU BILL LAZIMA AJE DOWNTOWN, PIA FUNGUENI WEBBSITE MTU ANA UWEZO WA KUINGIA HAPO ANALIPA BILLS ZAKE , ANAPATA INFORMATION ANAZOTAKA DON'T NEED TO GO DOWN-TOWN UNLESS U HAVE TO. ALTHOUGH WATANZANIA WENGI HAWANA MTANDAO BASI TUMIENI BRANCHES KURAHISISHA TRANSACTION SIO MPAKA MTU AJE DOWN-TOWN!!!! SWALA LAKUJENGA BARABARA ZA JUU NI MUHIMU SANA KWENYE CONJUCTION MFANO PALE FIRE NA BAADHI ZA CONJUCTION LAKINI LA MUHIMU KAMA NILISTATE HAPO JUU GOV NEED TO USE SIMPLE SOLUTION TO REDUCE TRAFFIC JAM BY EXPANDING BRANCHES OUT OF DOWN-TOWN AND GIVE THOSE BRANCHES POWER TO ACCOMPLISH TRANSACTION.
ReplyDeleteMDAU.usa
BARABARA ZA JUU SI SULUHISHO,UNATAKA KUNIAMBIA HIZO BARABARA ZA JUU ZITAJENGWA DAR NZIMA, KWANI KUNA FOLENI HATA TEGETA SO HATA TEGETA, MBAGALA KUTAKUWA NA BARABARA ZA JUU, HATA HUKO KWA WENZETU HIZO BARABARA ZA JUU ZIPO KWENYE MAKUTANO SANA KULIKO SEHEMU ZINGENE, SASA UNATAKA KUNIAMBIA FOLENI ZIKO KWENYE MAKUTANO TU;
ReplyDeleteCHA MSINGI NI KUPANUAWA BARABARA ZETU IKIWEZEKANA ZIWE NA LANE TATU EACH WAY, OFISI NYINGI ZIHAMIASHIWE NJE YA MJI NA IKIWEZEKANA ZINGINE ZIHAMISHIWE MIKOA MINGINE, NA PIA KUWE NA BARABARA NYINGI NDANI YA DAR ZENYE KIWANGO CHA LAMI ZA MKATO KWA FANO MTU WA TEGETA ANATAKA KWENDA AIRPORT AWE NA BARABARA NJE KWA NJE ITAKAYOMFIKISHA AIRPORT YA BILA KUJA MWENGE,PIA KUWE NA ALAMA NA TAA ZA BARABARANI KWA WINGI, NA MABASI YAWE MAKUBWA NA SI DALA DALA.
Hili tatizo la Msongamano wa Magari linaweza kutatuliwa kwa njia nyingi mojawapo kama jiji limeamua kuzipa wilaya za Dar hadhi ya Manispaa kwanza zinatakiwa zijitegemee kwa kila kitu siyo unataka hati ya kiwanja Mbagala unatakiwa uende ofisi za Ardhi kati ya mji huo ni mfano mmoja kitu kingine hao wajenzi wa maghorofa kule mjini wanatakiwa wawe na parking spaces kwa ajili ya wateja wao hivyo serikali kabla ya kutoa kibali cha kujenga wanatakiwa wakague mchoro kwasababu foleni ya mjini inaletwa na kutokuwa na parking mjini na kila mtu anatakiwa kwenda mjini kwa shughuli za kila siku.Wadau wengi wametoa mawazo tofauti na yenye msingi kinachotakiwa hapa ni kujaribu kukusanya hayo mazuri na kuyaweka pamoja....1.Ofisi za Serikali ziwafuate wananchi walipo.
ReplyDelete2.Parking za kutosha kwa ajili ya watu wanaokwenda huko mjini ili barabara ziwe nyeupe na siyo kupaki barabarani.
3.Punguza msongamano husio na lazima kwa kuweka Toll but at same time serikali inabidi watekeleze ule mradi wa mabasi yaendayo kasi.
Hayo ni baadhi ya vitu ambavyo serikali inaweza kufanya kupunguza foleni Mjini.
Mdau
USA, UK, Japan, S.Africa, India karibu nchi zote ziloendelea na zinazoendelea pamoja na mafy-over yao bado nao wana traffic jams, magari mengi ni ishara ya kukua kiuchumi, kadiri uchumi unavyokua na uwezo wa wananchi kununua magari unaongezeka na sio rahisi kuondoa hilo tatizo ila tujitahidi kuziboresha miundombinu ya nchi na hili la fly-over sio baya kwa darisalama.
ReplyDeleteTatizo la trafic tanzania ni kutokana na makazi, financial institutes and businesses kua located sehemu moja the government needs to think about this cause thats the only way to solve the congestion problem.
ReplyDeleteConsultants have started to design fly-overs for Dar es Salaam, which experts described as a permanent solution to the chronic problem of traffic congestion in the country’s busiest urban centre.
ReplyDelete“Contractors are currently drawing up the designs of the fly-overs,” James Nyabakari who is Tanzania National Road Agency (TANROAD) Dar es Salaam regional manager, told The Guardian in an exclusive interview yesterday.
Aisee get ur facts ryt South africa Dollar moja ni rands 7.22
ReplyDelete