Yusuf Manji na Francis Kifukwe


Siku mbili baada ya kuteuliwa kuwa mwenyekiti wa Yanga Lloyd Nchunga amemteuwa Francis Kifukwe kuingia kwenye baraza la wadhamini la klabu hiyo.

Uteuzi huo umekuja kufuatia agizo la mdhamini wao Yusuf Manji alilotoa siku ya Jumapili wakati wa uchaguzi mkuu wa klabu hiyo ya kutaka mwenyekiti yoyote atakayechaguliwa lazima amteuwe Kifukwe kuwa mjumbe wa baraza la wadhamini, na iwapo itakiukwa yupo tayari kubwaga manyanga ndani ya klabu hiyo na pia iwapo rais huyo wa zamani wa Yanga atateuliwa hana budi kukubali.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jana, Nchunga ambaye kwa taaluma ni mwanasheria alisema iwapo Kifukwe atakubali uteuzi huo atakuwa miongoni mwa wadhamini na kufanya idadi hiyo kuwa watatu, wengine ni Yusuf Manji na Fatma Karume.

Alisema kuwa uongozi wake unataka Yanga iwe moja na shirikishi na tayari imemtumia Kifukwe waraka wa kumteua.

"Kwa kutambua mchango wa Kifukwe na ufadhili wake wa muda mrefu, busara na mchango wake katika kuleta muafaka ndani ya klabu yetu, kwa niaba ya kamati ya utendaji tumekuteua kuwa mjumbe wa bodi ya wadhamini."alisema Nchunga.

Alisema uteuzi huo umekuja kwa mujibu wa sheria za wadhamini sura ya 318 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.

"Kwa maana hiyo atashirikiana na Yusuf Manji na Fatma Karume ili kuleta maendeleo ndani ya klabu hiyo."alisema Nchunga na kopi ya taarifa yake kuituma pia kwa Yusuf Manji na Fatma Karume.

Naye mdhamini mkuu wa klabu hiyo amemsihi Kifukwe kukubali ombi hilo la kuwa miongoni mwa wadhamini ili kuileta Yanga mafanikio makubwa.

"Kwa miaka mitano iliyopita uliniomba mimi kukubali kuwa mfadhili wa Yanga na nashukuru kwa kunipa nafasi hiyo kwa mapenzi makubwa, pia chini ya uongozi wako tulifanya kazi pamoja ya kutatua matatizo makubwa yaliyokuwepo ya muda mrefu na kuondoa mpasuko ndani ya Yanga na kurejesha umoja.

"Kwa mujibu wa barua ya mwenyekiti mpya Lloyd Nchunga aliyotuma kwangu Julai 20 ambayo amekuteua kuwa mjumbe wa bodi ya wadhamini ni nafasi kubwa kwako, Yanga si tu klabu kubwa bali ni taasisi muhimu yenye historia ya pekee."ilisema sehemu ya taarifa ya Manji ambayo anamsisitiza Kifukwe kukubali ombi hilo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 22, 2010

    NAONA WANA KANDAMBILI WOTE KIMYAAAAAAAAAAAAA, HAWANA CHA KUSEMA.
    INGEKUWA SISI LUNYASI TUMETOKEZEWA NA HAYA MNGEANZA KUOSHA VINYWA!
    MI NASHINDWA KUSHANGAA DEMOKRASIA YENU WANA KANDAMBILI IMEKAAJE, MAANA SIJAPATA KUONA VIROJA KAMA HIVI!
    IWEJE MTU MMOJA TU KWA SABABU YA VIPESA VYAKE AKAWA NA MADARAKA YA KUAMUA NANI ATEULIWE KUONGOZA?
    KISHA YANGA NZIMA, MMEKAA HAPO, WENGINE ETI WASOMI, MNAAMUA KUMKUBALIA?
    TENA ANASEMA BILA AIBU WALA SONI, ETI KAMA KIONGOZI AMTAKAE YEYE HAKUPEWA CHEO YEYE ANAACHIA NGAZI!
    MBONA NYIE YANGA MNAKUBALI UNYONGE KIASI HIKI?
    NI MASIKITIKO NA SIMANZI KUONA KILABU KIKUBWA KAMA CHENU MNANYANYASWA NA WENYE PESA.
    I WAPI BASI THAMANI YA TIMU YENU?
    DEMOKRASI INA NAFASI GANI KWA WANA YANGA?
    KWA MAANA HIYO, HATA HAWA VIONGOZI YAWEZEKANA SANA WATAONGOZA KWA FIMBO YA MANJI!!
    BORA BASI MBADILISHE JINA, MJIITE DAR ES SAALA MANJI AFRICANS SPORTS CLUB!
    MMELIABIBISHA SOKA NA DEMOKRASI YA TANZANIA!
    Mndengereko, Ukerewe

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 22, 2010

    Aliye tajiri nji hii ni mtu mmoja tu, US Blogger wa Oxford, wengine ni wazushi.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 22, 2010

    njaa mbaya jamani

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 22, 2010

    Ukweli ni kwamba hatujamsikiliza Manji ila tumewasikiliza maelfu ya wafuasi wa Kifukwe. Yanga timu kubwa, baba lenu ndo maana hii migogoro midogo midogo hatuwezi kuiruhusu. Kwa kubalance hivyo, tayari tuko level!! Yanga ni moja, fleva kibao....Yanga Asili, Yanga Kampuni, Yanga Bomba, Yanga Technic (New generation) lakini kuna 'One Yanga Policy'. Yanga Afrika...Daima Mbele, Nyuma Mwiko!!

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 22, 2010

    Wana Yanga, hivi mmiliki wa Yanga ni nani??? Ni ninyi wanachama au Manji??? Kwanini mnakubali kudhalilishwa kiasi hicho???? Yaani klabu yenye maelfu ya wanachama inaburuzwa na mtu mmoja????

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 22, 2010

    Mbona nchi inaburuzwa na mtu mmmoja na chama kimoja na watoto wa wenye chama kimoja we usemi unaona ya Yanga tu. Tumia akili, busara na fikra kabla ya kuandika. Alafu ukigundua chukua amka shtuka chukua ataua si unafamilia wewe?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...