Home
Unlabelled
mambo ya GADO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Respect Gado kwa kuchora hii cartoon inayojieleza kwa kila kitu kuhusu mashindano ya kombe la dunia yaliosha SA. Respect vile vile kwa kuwa na broad mind ambayo ni adimu hapa kwetu TZ.
ReplyDeleteWa Brazil walivyoletwa mie nilikuwa mmojawapo wa wale tuliopiga kelele bila kusikika, hela imepotea, wajanja wakina mwakalebela siajabu wanazitumia baadhi ya hizo kugombea ubunge!
Wa TZ tuli host ule mkutano mkubwa wa uchumi, barabara zikafungwa, miti (ambayo imeshakauka) ikapandwa, wajanja wakala hela zao, natumaini wametumia kujenga mahekalu tayari, na kuongeza uchungu kwetu walalahoi, JK na waandaji wakadondosha bonge la party la kijisifia na kupongezana kwa kuzitafuna vizuri hela za mlalahoi!
Kamai huwa anakuja na malalamiko yake kuhusu tunavyopenda sherehe, iwe harusi, graduation, communion, confirmation, baptism, yaani kisingizio cha aina yoyote, ili watu wanywe, wale na waserebuke!
Ndio maisha yetu waafrika.
SA kombe la dunia limeisha, lilivyokua linaendelea, walalahoi, hasa wamachinga wa kule SA, walikatwa katu katu kuuza bidhaa za aina yoyote, ndani, na nje ya uwanja, hata mijini, polisi walikuwa wanapiga mkwara si mchezo.
Sasa wageni wameondoka, uzuri infrastricture zilizowekwa, kama treni, barabara, umeme, mijengo n.k. labda wananchi watafaidika nazo, kama msauzi mmoja alivyodai, this was a very expensive party, almost 30 bilion rands imemwagika chini, ila matatizo ya walalhoi yako bado pale pale, waandaji hawakufikiria kuwa labda katika hizo hela nyumba kama za NHC hapa kwetu zingeweza kuwasaidia wananchi kule, labda maswala ya maji na umeme tena sio mabli kutoka kwenye hivyo viwanja yangesaidia.
Ila wajanja kama mnavyoona katuni isemavyo, wameondoka na ma rands na dollars kibao!
Walalahoi wa SA wanabakia wakishangaa, hawajui cha kufanya, wajinga ndio waliwawo. FIFA wamefanya kila liwezalo mzee Mandela aje kwenye ufunguzi na ufungaji wa mashindano, yote kama kuhalalisha biashara yao walioifanya hapo SA! Ingekua wamefanya nilioyasema hapo juu kama kuleta maji, umeme, kazi za muda mrefu na nyumba, basi hata mie ninge wa salute FIFA!
Ila wamewafanyia wa SA kile wajerumani, waaarabu, wafaransa, wareno na waingereza walichotufanyia wakati wa ukoloni.
Wame tu rape tena, na tena maliasili zetu, na sie tutabaki tukisifia bila kuangalia kwa makini walichotufanyia!
Wajinga kweli ndio waliwao!
asante sana kwa hii cartoon. waiio faidika kwenye hii world cup ni makampuni makubwa, wafanya biashara wakubwa na fifa. game imeisha wameondoka na mifuko yao imejaa pesa lakini watu wa kawaida nchini humo wamebaki maskini kama siku zote.
ReplyDeleteTrue dat.It's nothing but business.Hahahahahahaha
ReplyDeleteWaswahili bwana kweli hawajui watendalo! yaani makelele yoote kuwa Africa inanyimwa kombe la dunia.... sijui nini... leo mnalalamika kuwa hawakufaidika? Sasa hizo barabara na improved public transport pamoja na huduma nyinginezo zilizowekwa nani atafaidi kama sio wao Africa ya Kusini?
ReplyDeleteAcheni kulalama tu bila sababu au mlifikiri kombe la dunia halina gharama?
Basi siku nyingine msiombe tena ingawa mnafikiria kuomba Olimpiki.
Mnakera sana...
Mzozaji
tatizo la nyie washwahili ni wanafiki ndomana sikuzote hamuendelei. sio kila kitu mna lia lia tu!! kwanza badala ya kuwa concert about other country yakwenu yanawashinda !! tatizo lenu mnajifanya mnajua sana wakati hamjuhi chochote wa janja wanakaaga kimiya sikuzote uku wana achia vitendo vifanye kazi!! kila kitu mnalia lia lia tu!! je kabla ya world cup malalamiko yenu walikuwa wapi ? During the world cup mlikuwa wapi? NYIE NDO WALE MMANAO ALIKWA KWENYE ARUSI THEN MKISHA SHIBA NDO MNALALAMIKA OH BIBI ARUSI AKUPENDEZA OOOH CHAKULA KILIKUWA KIBAYA !! CULTURE YA WATANZANIA NI WANAFIKI NDOMANA KATU HAMTA ENDELEA!! CHECK HATA KWENYE MAMBO YA POLITICS MARA MNAPONDA CCM WAKATI HUO HUO MNAWAPIGIA KURA OH OH MAFISADI f##%%$$ THAT !! NJAA NDO HINA WASUBUA!!
ReplyDeleteHuu ulikuwa wakati wa Afrika kuonyesha sura nyingine kwa watu wa nje jamani! Umasikini wetu na matatizo yetu si ya kuisha kesho wala hivi karibuni. Tuachane na ujinga wa kulalamikia kila kitu na kudai tunaibiwa hata pasipo. Sasa msanii na walalamikaji hapa mnatakaje? FIFA isifaidike na gemu zima? Waache pesa zote .ZA? Au nchi gani isiyo na umaskini kwenye bara letu ilistahili kuhost? Furahini South Africa imefanya kazi nzuri kutuwakilisha kama Waafrika kwa sasa, puliza vuvu kwenye gemu zetu za mchangani kuanzia sasa, afu nyamaza!!
ReplyDeletekatoon hiyo imeelezea sio tu SA hapa kwetu bongo km alivyosema mdau mmoja hapo juu. wabrazil walikuja zimeteketea bil 3 wananchi vijijin wanataabika!!!hv sisi waafrika hasa wabongo lini tutaachana na huyu uzezeta!!!!
ReplyDeleteCongratulations to South Africa for hosting a very succesful World Cup.
ReplyDeleteSasa tuwageukie nyinyi wachangiaji watatu wa mwanzo: (1) 2.8 BILLION US DOLLARS ZIMEINGIA KATIKA UCHUMI WA SOUTH AFRIKA IN FOREX. Idadi hii itaongezeka wakati update itakapotolewa na Beki kuu ya SA. (2)Kumekuwa na wafanyabiashara wadogo accredited (rasmi) zaidi ya laki nane 800,000+. (3) Madereva taxi na wafanyabiashara wadogo wamepata biashara kuliko wakati wowote ule katika historia ya SA kutokana na kuwahudumia kibiashara wageni 720,000 waliokuwa SA kwa mwezi mmoja huo wa WC. (4) Makadirio ya awali ya Wizara ya uchumi inaonyesha kuwa GDP ya SA itaongezeka kwa zaidi ya 2% kwa ajili ya huo mwezi mmoja tu wa WC. (5) miundombinu iliyoboreshwa (hususan barabara na umeme) vitaendelea kuwepo kwa manufaa ya nchi (6) Zaidi ya USD milioni 50 FIFA itakayoipa SAFA zitatumika chini ya mpango wa "legacy programme" zitatumika katika elimu na kukuza michezo katika maeneo yaliyoachwa nyuma. (7) Vyombo vya habari vya mabeberu (BBC, CNN, SKYNEWS) vilifanya kampeni kubwa ya kuonyesha kuwa eti SA haitakuwa tayari on time, uhalifu utakuwa mkubwa, viwanja vitakuwa vitupu, bla bla bla...lakini kila kitu kimekwenda vizuri sana!!!!!mpaka mabeberu yenyewe yamekiri kuwa WC hii ilikuwa 'special' (8) WC hii imeiuza SA kitalii vizuri sana . Mimi nilikuwa huko kwa wiki mbili na nusu (just come back). Wageni wote niliyeongea nao walisema watarudi tena SA kwa sababu (a) SA is a beautiful country na (b) standard za hoteli na value for money ni za kuvutia mno. Wakati bodi ya Utalii ya SA ilikuwa inafikiri mwaka huu SA ingelipata watalii milioni nane "tu" sasa wengi katika sekta hiyo wanajizatiti kupokea jumla ya watalii milioni 10 over 2010 kuishia 31/12/2010 (9) Formula one wametangaza azma yao kuiongeza SA katika circuits zao (a first for Africa) in the next three years. (10) Wa-South Afrika wameona jinsi wakiungana wanaweza kufanya lolote (yes we can) na wamepata "the feel-good factor" ya kujiamini as a nation. 11) Dunia imethibitishiwa kuwa Afrika pia inaweza kutayarisha event kubwa kama hii. (12 )Ninachoweza kusema ni kuwa ukweli ni kuwa, ijapokuwa mimi ni Mtanzania, katika safari zangu in four continents, sijawahi kuona watu wenye wivu, gere na chuki dhidi ya mafanikio kama Watanzania. Hii ni nchi inayoongoza kwa PHDs (pull him down syndrome), na yote hii inatokana na uvivu na/au ulevi na kukaa na kutaka tufanyiwe kila kitu. (13) laiti ingelikuwa ni nchi ya ulaya imefanikiwa hivyo kama SA, tusingeliona matapishi hayo ya wivu na chuki ambayo tunaiona katika katuni hiyo na hizo comments tatu za mwanzo. (14) Nawashauri mpate kwanza data hizo katika tovuti za uchumi na blogs za WC kabla hamjabwata hovyo simply because an African country has succesfully delivered a "once in a lifetime WC". AMANDLA. God bless Tanzania, God bless South Africa, God bless Afica!!!!Amen. Mdau wa uchumi, (ex-lecturer in SA).
Wacheni wivu nyinyi bongo losers! manufaa ya kiuchumi ya World Cup hii kwa MSanzi (Afrika Kusini) yatakuwa makubawa sana na ya kudumu. Hapa siopo mahali pa nyinyi kuexhibit ujinga wenu. Abigail.
ReplyDeleteWatanzania bwana....wivu utatumaliza...badala ya kusherehekea mafanikio ya kombe la dunia barani afrika ibilisi wa wivu ameibua kichwa chake kibaya...he he he...MadibaFanZone.
ReplyDeleteHii ndio maana umasikini hauishi Bongo.Kila kitu kulalamika tu kiwe kizuri au kibaya.Nyie wakosoaji mlidhani WC ingeondoa umasikini waote SA? Kila kitu kupiga domo tu na vikatuni kibaooo lakini mwisho wa siku hiyo mijamaa yote inayolalamika itapiga kura kuchagua viongozi mafisadi..Umasikini hauwezi kufutika SA eti kwa ku-host World Cup thats lame way of thinking.Kila mwananchi amekuwa politician maneno mingiii no action.Tufanye kazi,tujenge viwanda, tuchague viongozi waadilifu,Tusomeshe watoto sio kuvizia event flani ndio itutoe kwenye umasikini...
ReplyDeleteNyie mnaolalamika kama SA isingepata nafasi ya ku-host World cup si ajabu mngelalamika pia kama kawaida yenu.Hiyo yote sababu ya akili tegemezi kila kitu kwenu ni deal tu instead of working hard you are just waiting for FIFA to change your life, aint that crazy?
Inategemea maendeleo yanamsaidia nani. Kama ni watu wachache hayana maana. Majumba makubwa maeneo ya mijini Tanzania hayamsaidii chochote mtu wa kijijini (ambako ndio kuna watu wengi).Takwimu na maendeleo yasiyo ya moja kwa moja kwa wengi (indirect) havisaidii. Hoja ya kuinua maisha ya wengi majority) ni ngumu. Ndio maana nam - miss baba wa taifa, Nyerere...
ReplyDeletemaulidi isiyokuhusu watandikia jamvi,wasouth wamefaidika sana acha umbea chora katuni za kikwete na maisha bora yenu kwa kila mtanzania,world cup imecreate jobs nyingi kuna reli ya kwenda kasi ,mahoteli ya kitalii ambayo ni makali,maivesta kibao wanataka kuja south kuivesti ninyi mmepata uhuru tangu miaka ya sitini hamna hata barabara kareli ka kati tu kukaendesha hamuwezi,shirika la ndege limekufa mpaka waje wazungu,nimesoma south vyuo vyake ni one of the best in the world ni watu wachapa kazi wana uchu na maendeleo,na sio wambea,kila kitu wanafanya wenyewe,huwezi amini viwanja vyote wamejenga maarchitecturer wa kisouth no mzungu from ulaya au america,they deserve sifa,swali je ninyi bongo mejitangaza vp kipindi cha world cup,au mtaishia kwenda kuzamia south tu.big up to peter kamau
ReplyDeleteNtajaribu kumjibu mdau hapo juu, point kwa point
ReplyDelete(1) 2.8 BILLION US DOLLARS ZIMEINGIA KATIKA UCHUMI WA SOUTH AFRIKA IN FOREX. Idadi hii itaongezeka wakati update itakapotolewa na Beki kuu ya SA.
Ukisema 2.8 b zimeingia kwenye uchumi , ndo unamaanisha SA ime spend hiyo hela kwa ajili ya ujenzi na matayarisho au? Sababu according ESPN, (http://reason.com/blog/2010/07/12/south-africas-world-cup-hangover), (naomba utizame na hiyo video ya kuonyesha slums na matatizo waliobaki nao walalahoi wa huko). SA wametumia 6 bilion dollars, Je wamevuna kiasi gani? Maana nijuavyo, ni makampuni makubwa ya vinywaji, nguo, TV na mawasiliano yaliovuna mahela hapo. 6 bilion dollars is a lot of money to spend just for the fond memories!
Na tukumbuke hizi hela nyingi zimetumika kwenye viwanja, mahoteli, usafiri na ulinzi. Mie nauliza wale wananchi ambao wanaishi karibu na viwanja, umeona nyumba zao? Hawana maji! Hawana umeme! Sasa hela zote hizo zinafaida gani kwao?
(2)Kumekuwa na wafanyabiashara wadogo accredited (rasmi) zaidi ya laki nane 800,000+.
Hebu fuatilia vizuri, hao wajasiriamala watafanya biashara gani kwa sasa kwenye hivi viwanja vitupu? Biashara ya mwezi mmoja tu inaweza kweli kutatulia matatizo yako ya siku 365?
(3) Madereva taxi na wafanyabiashara wadogo wamepata biashara kuliko wakati wowote ule katika historia ya SA kutokana na kuwahudumia kibiashara wageni 720,000 waliokuwa SA kwa mwezi mmoja huo wa WC.
Sawa tena hiyo kwa mwezi tu, baada ya hapo kuna nini? Walete Olympics?
(4) Makadirio ya awali ya Wizara ya uchumi inaonyesha kuwa GDP ya SA itaongezeka kwa zaidi ya 2% kwa ajili ya huo mwezi mmoja tu wa WC.
Si kweli maana wenyewe wanavyodai, katika vitu muhimu kuliko vyote vilivyofanyika ni ufunguzi wa treni na bus routes! Tunarudi pale pale kuhusu matatizo ya walalahoi!
(5) miundombinu iliyoboreshwa (hususan barabara na umeme) vitaendelea kuwepo kwa manufaa ya nchi
Ni kweli, treni na bus routes, ila kwa hela za viwanja, kama wangejenga nyumba kama za NHC, wakawapa umeme na maji, afya na elimu, hapo tungesema, haya mashindano yameacha bonge la legacy!
(6) Zaidi ya USD milioni 50 FIFA itakayoipa SAFA zitatumika chini ya mpango wa "legacy programme" zitatumika katika elimu na kukuza michezo katika maeneo yaliyoachwa nyuma.
Rahisi kusema zitatumika, ila tujieulize kama FIFA wataacha 50m USD, je FIFA wametengeneza USD ngapi? Around 3.2 bilion USD!
(7) Vyombo vya habari vya mabeberu (BBC, CNN, SKYNEWS) vilifanya kampeni kubwa ya kuonyesha kuwa eti SA haitakuwa tayari on time, uhalifu utakuwa mkubwa, viwanja vitakuwa vitupu, bla bla bla...lakini kila kitu kimekwenda vizuri sana!!!!!mpaka mabeberu yenyewe yamekiri kuwa WC hii ilikuwa 'special'
ReplyDeleteHuo ndio uhuru wa demekrosia, inabidi uwe tayari kukoselewa na kukosoa!
(8) WC hii imeiuza SA kitalii vizuri sana . Mimi nilikuwa huko kwa wiki mbili na nusu (just come back). Wageni wote niliyeongea nao walisema watarudi tena SA kwa sababu
Bila WC bado watalii wataendelea kwenda, isiwe sababu ya kutokufanya mambo ya maana kwa kusingizia WC ilifanyika sababu ya watalii tu, maji, umeme, afya, makazi na elimu ndio muhimu kwa wananchi.
(11) Dunia imethibitishiwa kuwa Afrika pia inaweza kutayarisha event kubwa kama hii.
Sio Africa, sema SA, maana hakuna nchi nyingine yoyote inaweza kufanya na kutayarisha haya mashindano!
(12 )Ninachoweza kusema ni kuwa ukweli ni kuwa, ijapokuwa mimi ni Mtanzania, katika safari zangu in four continents, sijawahi kuona watu wenye wivu, gere na chuki dhidi ya mafanikio kama Watanzania. Hii ni nchi inayoongoza kwa PHDs (pull him down syndrome), na yote hii inatokana na uvivu na/au ulevi na kukaa na kutaka tufanyiwe kila kitu.
Now you are being naive, hakuna swala la wivu wala gere kwa SA, kama kuna makosa yanaonekana, tena kwa walalahoi walio wengi, lazima sie tuseme ukweli!
(13) laiti ingelikuwa ni nchi ya ulaya imefanikiwa hivyo kama SA, tusingeliona matapishi hayo ya wivu na chuki ambayo tunaiona katika katuni hiyo na hizo comments tatu za mwanzo.
Ofcourse tungesema kama matatizo yangetokea, usijifanye uko very patriotic na matumizi mabaya ya hela za wananchi wa SA kwa kuwanufaisha wachache na muliti-national companies! Wewe umesoma, deep down unajua nani hasa kafaidika na hii WC!
(14) Nawashauri mpate kwanza data hizo katika tovuti za uchumi na blogs za WC kabla hamjabwata hovyo simply because an African country has succesfully delivered a "once in a lifetime WC". AMANDLA. God bless Tanzania, God bless South Africa, God bless Afica!!!!Amen. Mdau wa uchumi, (ex-lecturer in SA).
Well, sie sio lazima twende shule tufungue macho tuone yalio tendeka na yanayotendeka, sa ingine shule inakufanya usiwe broad minded na kukufanya ujione wewe uko sawa kila wakati, please open your eyes to the reality!
Well said Mtzwadar we think SA will send some free money to each mlalahoi? dreaming of freerides and always jealous. JE TUTAFIKA???????????
ReplyDeleteHuyo Mtzwadar ana very negative mindset. Simlaumu , kuna watu wameumbwa hivyo. Kwa maana yake ni kuwa World cup ikifanyika Ujerumani basi watu wa chini ndio wanafaidi au?
ReplyDeleteAlikuwa wapi kusema hivyo kabla ya Worldcup?
Yaani anashindwa kuona kuwa kuondoa umasikini ni mchakato wa muda mrefu na sio kitu cha mwezi mmoja? Hawa ndio watu wanaoshindwa hata kusherehekea kuzaliwa kwao eti kwa sababu kesho anaweza akafiwa.. Anashindwa kuona kuwa kuna faida pia watu wa chini wamepata ila hataki kuangalia hilo. Anashindwa kuona kuwa sasa kuna miundo mbinu ya uhakika, kupungua foleni(lilikuwa tatizo south), treni za kasi zipo, wageni walilala hoteli zao wakalipa, nyumba zao walipangisha wakalipa, chakula chao walinunua, walitembela mbuga zao wakalipa,vuvuzela walinunua, watu walipata ajira ya muda(World cup ni mwezi mmoja tu, usitegemee maajabu ya milele) k. Kwenye nchi kama South africa sekta nyingi ni rasmi. kwa hiyo cha maana hapo ni watu kupata ajira, kutangaza nchi kiutalii nk sio wamachinga kuuza DVD feki zaidi.
Mzozaji
Acheni kulalamika, nyinyi mnachoweza kufanya ni ku-host warsha za kiutapeli, mpate posho. Wakati Tanzania hapo mnashindwa hata kuweka maji na umeme lakini mnajuaa kuwaambia SA namna ya ku-run uchumi wao. Sasa mnataka FIFA watoke mikono mitupu. FIFA siyo responsibility yao kujenga mashule, barabara, nk; ndio maana nchi huwa zinagombania ku-host WC. Shida ya Tanzania ni kupenda miteremko, halafu kila mtu anajua siasa, uchumi lakini hamna common sense. Ndiyo legacy ya ujamaa. Mnashindwa mambo madogo madogo lakini mnajua South Africa uchumi wao waundeleze vipi, au Marekani wafanye nini, lakini Bongo vigogo wameshikilia.
ReplyDeleteNashangaa kwa nini Tanzania imekuwa ni katika nchi maskini duniani, wakati economic geniuses wako katika kila kijiwe!
acheni upuuzi wenu na kujifanya nyie ndo mnajua uchumi saaana wakti huku kwenu ni ziiii, mbona kila mtu africa alifurahi kusikia kwa mara ya kwanza world cup itachezwa africa? baada ya wc kwisha ndo mnaanza kuchonga wakati mandela alipendekeza sa i host wc watu waliipuka kwa nderemo, ni nyinyi wabongo tuu mnaokufa na umaskini ndo wa kwanza kulalalmika, na africa isingepewa nafasi humu ndani kusingetosha, manake ungeimbwa wimbo wa ubaguzi weeee, leo wameleta world cup midomo juu kama kong'ota ovyo kabisa, na hizo nchi zooote ambazo zimewahi kuhost world cup mbona ziko poa tuu, msilinganishe uchumi wenu wa kifisadi na wasouth mkomee, hayawahusu yenu yamewashinda mnaanza kwa jirani anko kamau akiwachamba mnakuja juu, na wasouth wakianza na siye itakuwaje? kama ni maendeleo nafikiri tanzania ingeweza kuwa kwenye top 3 ya utajir africa lakini viongozi wetu ni full mafisadi umimi tuu ndo uko kwenye oblangata zao hawajali wengine ni kukomba tuu wala hawafikiriii maendeleo hivyo hasira zenu za mkizi msiwaambukize wengine , walaumuni hao mnaowaita viongozi shupavu!
ReplyDeletemichuzi unamatatizo gani mbona kila nikituma comment unanibania? afu hii utaitoa wakati haina point wakati zile zenye point huziweki..hii kweli blog ya jamii..
ReplyDeletekijijini,sentro yuropu
Mkianza kulalamikia kombe la Dunia kuja SA. Mtalalamika hata mkiletewa paradiso hapa duniani.
ReplyDeleteTuache mtazamo ulio - pinda.
Kwani Gado siku hizi umekuwa mkomunisti?
Sio kosa lake ni tatizo la kuwa narrow minded..What you don't know you don't know...
ReplyDeleteUmasikini wetu hauwezi kuondolewa kwa game ya mwezi mmoja lakini walichokifanya SA ni kitu ambacho kimeipatia sifa sana Africa...Nyie msio jua kitu kaeni kimya. Pumbafu
Na nilifurahi sana pale SA walipotia mkataba na waandishi wa habari hamna kupeleka picha za kudhalilisha Africa....
Sasa hivi kila ninayefanya naye kazi anaplan vacation SA mwakani...