Home
Unlabelled
MDAU WA UK ATEMBEA KILOMITA 108 KUSAIDIA SHULE TANZANIA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Tuambieni wamechangia kiasi gani?Msanjila tunajua wewe ni mwandishi wa habari mbona unatoa habari isiyokamilika?
ReplyDeleteguyz i mailed this site savetheserengeti.org to michuzi, to get broader views and comments or actions. but for his political views, (tied with ccm) he didn't want to post it
ReplyDeleteMaofisa wa Ubalozi nchi gani? Tanzania ina ubaalozi nchi kibao, sasa tutajuwa ni ipi mojawapo?
ReplyDeleteMzungu Atembea Kilomita 108 Kusaidia Shule Tanzania
ReplyDeleteRaia wa Uingereza Bw. Jeremy Silverstone na mkewe Gina wikiendi iliyopita wamefanya matembezi ya hiyari ya umbali wa Kilometa 108 kuchangisha fedha kwa ajili ya kusaidia Shule ya Msingi ya Mawanda nchini Tanzania.
Matembezi hayo yaliyoanzia mji wa Silverstone, Northamptonshire siku ya Ijumaa (9 Julai 2010) hapa nchini Uingereza na kumalizikia ofisi za Ubalozi wa Tanzania, London Jumapili (11 Julai 2010) jioni yalipokelewa na baadhi ya maafisa wa Ubalozi, wakiongozwa na Mkuu wa Utawala na Fedha (HOC), Bibi Caroline K. Chipeta na mwakilishi wa Jumuiya wa Watanzania hapa Uingereza, Bw. Goodluck Mboya.
Bw. Silverstone na mkewe Gina wameazimia kutembelea Tanzania mwezi Septemba na kufanya ukarabati wa angalau madarasa matatu, kuchimba na kujenga vyoo 14 na jiko katika Shule hiyo iliyoko Wilayani Rombo, Mkoa wa Kilimanjaro.
Mara tu baada ya kuwasili Ubalozini, muingereza huyo akiandama na baadhi ya ndugu wachache wa familiya yake walikaribishwa kwa vinywaji baridi na vitafunio vya kitanzania. Aidha HOC alitoa salamu fupi za shukrani kwa niaba ya Kaimu Balozi, Bw. Chabaka Kilumanga.
Katika salamu hizo HOC alisema kwamba wafanyakazi wa Ubalozi wamehamasishwa sana na hatua ya Bw. Silverstone na mkewe kujitolea kutafuta fedha kusaidia watoto wa kitanzania, kabla hata ya kuwahi kufika nchini humo. Hii itakuwa ni safari ya kwanza kabisa kwa Bw. Silverstone kufika Tanzania.
Akimkabidhi mchango wa maafisa wa Ubalozi kwa matembezi hayo, HOC alisema kwamba hii itakuwa ni changamoto kwetu sote kuwa wabunifu kutafuta fedha ili kusaidia mahitaji mbalimbali nyumbani kwetu.
Kwa mujibu wa Bw. Silverstone, Shule ya Msingi ya Mawanda ina jumla ya wanafunzi 232, wakiwemo chekechea 25. Ukosefu wa vyoo na vyumba bora vya madarasa shuleni hapo vimedaiwa kutishia afya za watoto hao na pia kuzorotesha uwezo wao kimasomo.
HABARI NDIYO HIYO
WEWE AMOS PUNGUZA KULA MABAGA NA KUKU WA HAPA LONDON
ReplyDeleteWe Anonymous 11.52 wamtakia nini mtoto wa watu Amos kumsakama hivyo wewe inakuuma nini?
ReplyDelete