Katibu mkuu wa CCM Yusuf Makamba akimkaribisha Mwenyekiti wa CCM Taifa,Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika ukumbi wa White House tayari kuongoza kikao cha kamati Kuu ya CCM mjini Dodoma leo asubuhi.
Mwenyekiti wa CCM Taifa ,Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongoza kikao cha Kamati kuu ya CCM mjini Dodoma leo asubuhi.Wengine waliokaa meza kuu kutoka kushoto ni Rais Mstaafu awamu ya Tatu Benjamin Mkapa, Rais Mstaafu awamu ya Pili ali Hassan Mwinyi, Rais wa Zanzibar Amani Abeid Karume,Katibu Mkuu wa CCM Yusuf Makamba, makamau mwenyekiti wa CCM Bara Pius Msekwa na Rais Mstaafu wa Zanzibar Salmin Amour.
Wagombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM Makamu wa Rais Dr.Ali Mohamed Shein na Waziri kiongozi wa SMZ Shamsi Vuai Nahodha wakisalimiana katika viwanja vya makao Makuu ya CCM mjini Dodoma leo asubuhi.
Mgombea Urais wa Zanzibar ambaye pia ni Waziri kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Shamsi Vuai Nahodha akisalimia baadhi ya wanachama wa CCM mjini Dodoma muda mfupi kabla ya kuanza kikao cha Kamati kuu ya CCM.
Mgombea urais wa Zanzibar Balozi Ali Karume akisalimia baadhi ya wanachama wa CCM mjini Dodoma leo asubuhi.(picha na Freddy Maro)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 09, 2010

    Ankal hivi hao ni wagombea urais wa Zanzibar au ni watu waliomba kuteuliwa na CCM ili wagombee urais wa Zanzibar???

    Hapo unanichanganya kuwaita ni wagombea uraisi

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 09, 2010

    Sijuwi nimlaumu Freddy Maro au nani manake wote walioomba kugombea urais wa Zanzibar wanatambulishwa kama wagombea. Au mchakato umeshapita na sasa CCM itasimamisha wagombea watatu kwa mkupuo Zanzibar?

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 09, 2010

    ZANZIBAR INAWAGOMBEA WANGAPI WA CCM WA URAIS! HII NI MPYA! CUF WATASHINDA KWELI HAPO KAMA WAGOMBEA KIBAO WA CCM NA MMOJA WA CUF SI WATAAMBULIYA PATUPU HAPO!!!

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 09, 2010

    VP atasaidia anaonekana si mtu anayehimiza kujitenga kama huyu jamaa wa sasa

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 10, 2010

    http://issamichuzi.blogspot.com/2009/11/nolndozzzz-saut-leo.html

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...