MAREHEMU PRIMTIVA PANKRASI

Aliyekuwa mwandishi wa habari wa gazeti la Mtanzania, Primtiva Pankrasi, amefariki dunia jana mchana katika hospitali ya Lugalo ya Jijini Dar es Salaam, wakati alipofika hospitalini hapo kwa ajili ya matibabu ya kawaida ‘Check up’.

Imeelezwa kuwa Primtiva kabla ya kufikwa na mauti alipatwa na presha ya ghafla na kupoteza uhai wakati madaktari wakihangaika kunusuru maisha yake.

BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA JINA LA BWANA LIHIMIDIWE AMINA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 25 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 27, 2010

    RIP Primtiva; pia nafikiri hiyo pressure ya ghafla itakuwa imetokana na results za matibabu ya kawaida "check up", inabidi mtu aandaliwe kukubali hali mpya ya afya yake kwa ushuri nasaha.

    Mimi binafsi yaliwahi nikuta ila kwa kuwa nilipewa darasa kabla ya check up, tulipoenda na wife akiwa mjamzito na scanning ikaonesha dogo hakui yani something is wrong; hivyo tukatakiwa kufanya kipimo cha "Amnioscentesis" kuanga DNA za dogo ila kuna risk ya 5% abortion. Wife alikuwa analia maana toka tufunge ndoa ilikuwa ni seven years na hiyo ndiyo mimba ya kwanza. Ikabidi nikubali wakafanya na mwisho wakasema placenta haisupply chakula cha kutosha while DNA ikiwa Okay. Option ingine ikawa ni kumtoa dogo ili alishwe nje hapo ndiyo kabisa pressure ikazidi ila kwa ushauri nasaha wakatuhakikishia kuwa dogo atakuwa tu na kutuonesha picha za watoto wengine waliofanyiwa hiyo kitu. Nikapata nguvu na wife nae pressure ikashuka.
    Thanks God leo hii dogo anakimbia kabisa. Nilichokiona hapo ni maandalizi ya kumpatia mgonjwa hali yake halisi ya kiafya kwa kumpa matumaini.

    RIP Primtiva!

    ReplyDelete
  2. What? Yaani regular medical examination inasababisha kifo?Rest in Peace.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 27, 2010

    Poleni wafiwa.

    Hivi, kwa nini unaitwa waandishi wa habari 'wapiganaji'?

    Ni nini kilichokuchochea kuteua jina hilo bwana Michuzi?

    ReplyDelete
  4. David VillaJuly 27, 2010

    Mbigiri una hoja hata mimi sipati picha.R.I.P Prim

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 27, 2010

    roho ya marehemu ipumzishwe kwa amani. amina.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 27, 2010

    Mimi nina wasiwasi na huyo mchungiaji wa kwanza hajui kitu anachokiongea,hiyo ni fani ya watu, wewe ongea tu kawaida na sio too technical kama sio field yako tutakuelewa kuliko kuchanganya mambo, "DNA ikiwa Okay"..!! What does this mean..???!!, what is okay with DNA.??.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 27, 2010

    Anon wa Tue Jul 27, 07:22:00 PM

    Tatizo lako ni kuwa unataka kujifunzia kwenye blog badala ya darasani.

    Nafikiri wewe utakuwa ni MA au huenda hujui ninaongelea nini. Profesionally I am not a Medical Doctor but I have good view of human body from Classes up to form six and private readings.

    Kwa mtu makini angeleewa nilichoongelea hapa si kitu ambacho kinaweza fanyika bongo bali ni nchi za wenzetu (developed countries).

    Wenzetu kabla ya kukufanyia chochote wanakupa darasa la kinadharia na practical juu ya nini kitafanyika katika procudure na matokeo yake yakiwa positive(success) au negative(failure)

    Sidhani hata kama uliisha iona au sikia test inayoitwa "Amnioscentesis - It uses injection through stomach (tummy)aided with a powerful scan to monitor a baby so as to avoid hitting with a needle and suck amniotic fluid for testing - there is 5% chance for miscarriage". lengo la kufanya hii test lilikuwa ni kuondoa possibility ya chromosomal abnormalities before reaching a conclusion for slow baby growth being caused by poor food supply.

    Jamaa huku wanampima mtoto tumboni kuanzia uzito, urefu, ukubwa wa kichwa, urefu wa miguu na mikono, internal organs zote unaziona, na mitikasi yake yote ya kupiga misele unaiona. Siyo hivyo vimashine vyenu vya scan hapo bongo vinavyowadanganya wagonjwa kila siku kwa matokeo ya kuhisia.

    Niliposema DNA ipo Okay ni very simple(No abnormalities), test hii huwa ni ya kuangalia abnormalities za chromosomes ili ku-predict kama mtoto aliyetumboni ana chromosomes impairment which can lead into abnormal growth au hata down syndrome "mtindio wa ubongo" (which caused by a child/person having three copies of chromosome 21 instead of two copies. Trisomy 21 causes about 95% of the causes of down syndrome.

    Sasa kwa nini nilitaja DNA sikuongelea chromosomes ni kwamba there is relationship between the two; read below:

    "Genes are relatively small sections of DNA which encode (provide a template for) proteins.

    Chromosomes are molecules that consist of a very long strand of DNA coiled many times, and a few proteins called histones which hold the whole structure together.

    To put things very simply, chromosomes are made up of genes and genes are made of DNA."

    Tatizo lako wewe umeweka mawazo yako kwenye kutambua parenthood tu tunapoongelea DNA you are wrong.

    I hate to lecture you at this post a passed away person but, I hope next time you will behave and give condolence insteady of criticizing some personal stories even if you are a "specialized MD who is working by trial and error"

    Lets pray and wishing Prim a pieceful perpetual resting.

    R.I.P Prim

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 27, 2010

    Masikini mtoto mzuri na hana artificial make ups.
    What a waste!
    RIP beutiful girl, sikukufahamu lakini just from your pose you are so natural.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 27, 2010

    RIP it is sad to loose a person in that way...

    Hata mimi nakubaliana na mtoa maoni ya kwanza. Inatakiwa kuwapa psychologist kazi hata huko hospital...Mtu aende just for a check up halafu unapoteza maisha yako huko huko? Si watu wataogopa kwenda for check up tena? Hivi ni vitu ambavyo vingezuilika kama kungekua na professional people wanaoandaa watu kupokea matokeo ya check up yako.

    Poleni wafiwa..

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 28, 2010

    Aya sasa nafikiri somo kalipata kidogo japokuwa lilikuwa la bure, tatizo lenu mnapenda kuchangia msiyoyajua mkaona wote akili sawa, umeingilia ya watu na wewe tupe yako ya kijiwen sasa

    ReplyDelete
  11. Duh! Yaani unaenda kwenye check-up halafu unakufa! Yaani hospitalini hakuweza kupata First Aid? Kwa kweli ni habari ya kusikitisha. Ndo ameenda kupumzika.

    Rest in Peace Primtiva.

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 28, 2010

    Anon wa Tue Jul 27, 07:22:00 PM
    Mwanzo nilidhani una akili, nikaamua kusoma maelezo yako marefu. Ila ulipoandika ".....Siyo hivyo vimashine vyenu vya scan hapo bongo vinavyowadanganya wagonjwa kila siku kwa matokeo ya kuhisia....". Vimashine vya akina nani? Yaani wewe kwenda ulaya, hivi vimashine havikuhusu, na sisi tunaonuka vumbi huku ndio vyetu. Hi inawezekana wote tuje huko? Wengi wetu hata hizo hati za kusafiria hatuna. Na hata Visa wangegawa bure, nauli hatuna. Sasa ninyi kuwa huko, sio busara kututukana huku na hizi njaa zetu. Hivi mumeshakuwa wazungu tayari? Pregnant pig!

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 28, 2010

    Jamani, watu wana'mambo! RIP dada yetu, i think nilimfahamu huyu dada maskini, kama sikosei ndio mwenyewe ambaye nilisoma nae uandishi wa habari TSJ pale Ilala, (zamani TIMES).. Roho yake ilazwe mahali pema peponi, AMINA...

    SAMCHOM InTheMixx

    ReplyDelete
  14. Sitisho UKJuly 28, 2010

    Jamani kuchangia mawazo siyo vibaya kwani kuna kuelimishana. Lakini cha kwanza kabisa ni kuomba huyo mwenzetu aliyetutoka alazwe mahali pema. Na pia pole kwa wafiwa!

    Kwa kifupi napenda kuongelea vitu viwili:
    1. ni kwamba haieleweki kama huyo mama alipata mshutuko wa moyo baada ya kupata matokeo ya check up!
    2. Kukusoana ni kwaida. Nafikiri kuwa nje ya nchi haina maana yoyote hasa ukiunganisha na uhai wa binadamu. Hapa ninaona huyo jamaa aliyesema hivyo vimashine vya trial and errors ametumia lugha ambayo kwa watu wengi hawatailewa. Inawezekana kuna watu ambao wana chezea maisha ya watu hasa wanapotumia mashine amabazo haziwezi kutowa majibu ya uhakika ingawa wenyewe wanajua kuwa ni hivyo.

    Kwa maana hiyo ningeomba huyo jamaa anayejua mashin zenye uhakika atwambie zinapatikana ktk hospital gani au kwa clinics zipi.

    ReplyDelete
  15. AnonymousJuly 28, 2010

    wrong arena lakini hoja ya kwanza imenigusa sana. vimashine ni vimashine kweli. na lazima tuviongelee tukitaka kwenda mbele. mie historia yangu ya vimashine hii hapa: nilienda pima dogo kabla hajafanyiwa normol procedure ya kumngoa jino la nyongeza. wakatumia sindano ya ganzi lakini kwa vile dogo wazazi tunatokea bongo ikabidi apimwe kama ana circle cell ambayo ni common kwa bongo. result zikaja positive ila hajahathirika ni mbebaji tu carrier inamaana mimi au mamake mmja wetu ni mbebaji pia. kupima nikakuta negative. kwa maana hiyo basi mama mtoto lazima angekuwa positive. nikatuma vipaundi bongo ili tuwe na uhakika. kwanza doctor akamuliza wee mtu mzima unapima ili iweje? akatoa damu mjibu kesho yake negative!!!!mimi majibu nilisubiria wiki mbili bongo siku mbili na pesa dr akachikichia.
    watu watauliza kipimo cha kujua una trait kinasaidia nini? jibu huyu dogo akija akaoana na mmatumbi mwenzake ambaye na yeye ni mbebaji watoto wao ndo hivo tena full blown circle cell anemia hivo siku dogo akiniletea boyfriend au mchumba kama mungu akijaalia ntampa darasa kwamba lazima wakapime. japokuwa wabebaji hawajahadhirika lakini wana abdomality za red blood cells hivo wakati wa ganzi wanahitaji extra oxygen. nachangia. nilikuwa simjui huyu mpiganaji lakini najua she will be turning in her grave akiona hii changamoto ya maoni . rest in piisi. amen

    ReplyDelete
  16. AnonymousJuly 28, 2010

    annon July 28,08:41 am

    yani nimevunjika mbavu uwiiii

    ila umenena sawa kabisa,maana kama nje watu wanaishi na wameishi saana tu ila mtu mwenye utu huwezi TUKANA wabongo na maisha yetu,kisa umeweza pata vijisenti na familia yako ukenda hospitali za wazungu basi unaona wengine wote mafala.sijui uyo jamaa wa ughaibuni hakuzaliwa na mwafrika/m-Tz???

    me kutukana kiongozi mzembe tuliyempa dhamana apo kweli ingawa nayo haisaidii adi tutapotumia kura zetu vizuri
    ...i've no idea kwanini atusi hali ya watu hivi...

    ReplyDelete
  17. AnonymousJuly 28, 2010

    anony Tue Jul 27, 02:38:00 PM na ambaye umejibu tena kama anony Tue Jul 27, 10:59:00 PM ebu tema mate chini. jiulize pamoja na kuwa second class hapo ulipo, imekuwaje ukapata mtoto mwenye matatizo? kwani mwenzetu husomi au kusikia habari za makosa ya kiutabibu kwenye dunia ya kwanza au ni tanzania tu? na hapo unapanga foleni 'mwananyamala' ya ulaya je ingekuwa unaenda 'agakhan'?

    ReplyDelete
  18. AnonymousJuly 28, 2010

    RIP Dada yangu.nakumbuka nimekufundisha tuition pale kilombero day, Ifakara.

    ReplyDelete
  19. AnonymousJuly 28, 2010

    Mungu aiweke mahali pema roho ya ndugu yetu, rafiki yetu Primtiva. Ni jambo la kumuomba Mungu kwa sababu dunia ya tatu, ujauzito ni ugonjwa tofauti na wenzetu wa dunia ya kwanza. Mchangiaji wa kwanza ana hoja ukiacha hayo mengine kwamba ameponda vimashine. Hoja yake ni kwamba hata madaktari wetu wengi hawana muda wa kukaa na mgonjwa kwa zaidi ya dakika 10 kutokana na foleni inayokuwa ikimsubiri. Hata hizi hospitali za Aga Khan, unashangaa kuona unalipa fedha kibao lakini bado unapanga foleni tangu asubuhi hadi jioni kwa ajili ya kumuona Daktari bingwa wawanawake.
    Nina mfano halisi, kwa mfano Dk Shafik wa Aga Khan ni kimbilio la wanawake wengi, lakini unaweza ukakuta siku ya kliniki, ana kazi ya kuwaona wanawake wengine wasio wajawazito wenye matatizo, bado wakati mnasubiri kwenye foleni au ukiwa ndani ya chumba, unaweza kustukia anapigiwa simu akiambiwa kuna emergency ya upasuaji. Unadhani kwa mtindo huo, hata kama una matatizo yanayokusibu, utapata muda wa kuzungumza naye akupe ushauri nasaha?
    Kwa kweli tuzidi kumuomba mungu hali ni mbaya siyo tu kwenye hospitali za KAYUMBA bali hata hizi tunazodhani ni za VIBOSILE tatizo la upungufu wa madaktari ni kubwa.

    ReplyDelete
  20. Naomba kuchangia mada ukweli unauma. Bongo hamna hospital full stop. Ndo maana watu wanapelekwa India na South. Ndugu yangu kidogo afariki dunia kupima tu kisukari ilikuwa inawatoa kamasi. Big hospitals and so many times and they could not diagnosis diabetes.
    Jinsi miaka inavyokwenda huduma za hospital zimefifia labda pia kwa kukosa vifaa. Labda kuna hospital chache kama Muhimbili na KCMC ambazo bado zinajitahidi. Lakini pia umuone huyo daktari iko kazi. Kwahiyo alivyosema “hivyo vimashine vyenu” yuko sawa kabisa, labda kwa upole alitakiwa kusema hivyo vimashine vyetu.
    Pia alichosema kwa kifupi kinaitwa Counseling especially majibu yanapokuwa sio mazuri. Inatakiwa kuwepo na utaratibu mzuri wa kukupa majibu yako kwa magonjwa makubwa kama Cancer, AIDS na mengineyo. Ingekuwa huku lawyer tayari ameshapata kazi halafu familia ina SUE!

    RIP Primtiva na pole kwa wafiwa

    ReplyDelete
  21. AnonymousJuly 28, 2010

    Kwanza dada Primativa, Mungu aiweke roho yako sehemu nzuri. Poleni waliofiwa.

    Pili, nindependa tu kusema kuwa hospitali za "mwananyamaya" za ulaya au Marekani ni bora kuliko Muhumbili yetu. Nasema hivyo kwa kuwa ulaya daktari akifanya kosa kazini na kuua mtu, anapokonywa leseni ya kuwa daktari. Je, umeshasikia hata siku moja daktari Bongo kapokonywa leseni au tuseme hawaui wagonjwa au kufanya makosa kazini na kuua?

    Tatu, hospitali za Tanzania hazina dawa au vifaa vya kileo kutokana na umasikini. Ni makosa tunaposema kuwa hospitali yetu ya Agha Khan ni sawa sawa na za "mwananyamara" za ulaya wakati mdau hajui tofauti ya nchi tajiri na masikini. Sisi ndio kwanza tumeanza kutiba magonjwa ya moyo, wenzetu wanatabu sasa bila ya upasuaji mkubwa na kutumia robot na camera ndogo mwilini.

    Nne, Mzazi alipopata heart attack. hamna mtu muhimbili aliweza kumsaidia na kumwacha katika benchi mpaka daktari wa kichina alimpitia macho tu na kujua moja kwa moja kuwa mzazi amepata heart attack baada ya kuongea naye dakika mbili. Bila yeye, mzazi angekufa pale pale katika benchi. Na bila ya fedha binafsi, asingeishi miaka mingine 20 kwa kuwa alihijaji matibabu ambayo hamna Bongo. Angekuwa mlala hoi basi angekufa nyumbani kwake mwaka ule ule.

    Madaktari Bongo ni tabu kuwapata hasa ukiumwa mwisho wa wiki. Kama mgonjwa kapata mshuto wa moyo ama anahitaji huduma ya dharura, inakuwa vigumu kutibiwa katika miji mikubwa kama Dar, vijijini ni moja kwa moja maburini.

    ReplyDelete
  22. AnonymousJuly 28, 2010

    Nimesoma story, still DNA okay, does not make sense, the thing does fit in kwenye story unless definition ya DNA inayotumika siyo tunayoijua.

    Poleni wafiwa.

    ReplyDelete
  23. AnonymousJuly 29, 2010

    Angalia logic behind story ya DNA anchosema mchangiaji hapo "inabidi mtu aandaliwe kukubali hali mpya ya afya yake kwa ushuri nasaha".
    Halafu akatoa mfano wake ambapo mtoto alikuwa hadevelop tumboni ikabidi watoe DNA sample ili waweze jua kama mtoto anaweza kuwa na any risks of genetic issues such as sicke cell anemia. Na during hii process after seven yrs of marriage mkewe akaanza kulia sana na kulikuwa na uwezekano wa abortion kama hali ingekuwa mbaya. Chukulia huu ni mfano wa jinsi walivyoweza shauriwa kwani labda wife wake na kilio angeweza naye pata heart attack!

    ReplyDelete
  24. AnonymousJuly 29, 2010

    jamani haya matatizo ya uzazi yataisha lini ? hasa hizi pressure za ujauzito nakubaliana na mchangiaji namba moj a, kweli hapa kwetu madaktari wachuka vitu easy easy sana , wanaopona ni wale ambao hawana complication kwenye ujauzito . hizi kesi ni nyingi kama mnakumbuka Jan mwaka huu tulimpoteza Habiba Kawawa kwa tatizo kama hili . Mimi mwanyewe ni victim Nimepoteza watoto wawili karibu kujifungua kwa tatizo hili la presssure disorder during pegnancy . na case zote niliatend clinic kwa madaktari bingwa wa akina mama. Jamani tukubali tu huduma za afya huku kwetu , zinategemea kudra za mwenyezi Mungu .serekali yenyewe imekaa kimya hili tatizo linapata asilimia tano ya wanawake wajawazito , . nainasababisha vifo vya wanawake wengi sana na watoto kufia tumboni kabla ya kujifungua .
    sijui tutafanye wenye tatizo hili kwa sababu hujijui Kama una shida .we unajiona poa ndo maana dada yangu kaenda clinic kwa check up kumbe mambo yamshakuwa mabaya . serekali inatakiwa kutao campgn ya awareness kuhusu hili tatizo , na madaktari wawe wawazi kumuelezea mgonjwa anapokuwa mjamzito presssuer ikipanda kuna madhara gani , na nini kifanyike a. na dalili ziwe wazi maana hakuna maumivu yoyote mjamzito anayoyahisi . jamani elimu sio darasani tu au hata kusubiri daktari . google kwenye net kujua hili tatizo kiundani . utajua how risk it is !!!1 RIP prim

    ReplyDelete
  25. AnonymousJuly 29, 2010

    Rest in peace.Amen.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...