Msanii wa kizazi kipya Joseph Mbilinyi maarufu kama 2Proud a.k.a Mr II a.k.a Sugu akipokea fomu za kugombea ubunge katika ofisi za Chama cha CHADEMAjijini Dar leo tayari tayari kwa safari ya kwenda jimboni Mbeya
Sugu akisaini fomu zake
Sugu akiwa na washkaji baada ya kukabidhiwa bendera ya CHADEMA
Sugu na washkaji wakikupa alama ya ushindi ya CHADEMA
Sugu akipata maudhui ya kichama kabla ya kuanza safari ya Mbeya





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 29 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 01, 2010

    VERY PROUD. VIJANA TUJITOKEZENI JAMANI. WAKATI NDIO HUU.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 01, 2010

    mtoa form kavaa kofia ya ccm,kazi kweli kweli

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 01, 2010

    we nenda kapoteze hizo hela zako ulipiga box,maana kushinda hushindi,bali ni kupoteza pesa.unadhani watanzania ni wajinga kiasi hicho.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 01, 2010

    safi sanaaa sugu,huo ndio upiganaji halisi na kuonesha huna njaaa.wenye njaa wanajiunga ccm kwenda kujinufaisha binafsi.


    michuzi utajijua ukibania comment yangu kwani kusoma wewe ukweli ni bora zaidi kwani ujumbe umefika hao unao wabania ujumbe wanajua haya yote.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 01, 2010

    mi nataka kujua elimu yake huyu jamaa na kwanini kaenda ichi chama???????

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 01, 2010

    Sugu kafanya leo nijiunge na CHADEMA online nawasihi vijana wenzangu to go for a CHANGE,keep it real brother am down with you.G M.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 01, 2010

    Kujiungana chama moja kwa moja na kuomba ubunge. hizi ni njaa au?

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 01, 2010

    Naomba mnipatie background yake
    (education, politics etc. Then nitajua kama nimpe shavu or not

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 02, 2010

    Kwanini wasanii wanakimbilia Chadema?

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 02, 2010

    Baada ya wimbo wake wa Antivirus, naona hana sifa(hafai) kugombea ubunge maana mbunge anafaa awe kioo cha jamii na sio kutukana na kukashifu watu.
    Nadhani kwa watu waliosikiliza wimbo wa Antivirus wa sugu wanafahamu.

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 02, 2010

    Mi naona huyu jamaa na hasira zake dhidi ya Ruge ndizo zilizokurupusha na kumtuma kwenda kugombea ubunge. Acha kulalamika unaonewa saa zote wakati kesi na facts hunazo, halafu unafanya uhasama binafsi kama sababu ya kutaka kuwatumia wananchi wa Mbeya Mjini kama mbunge wao. They deserve better.

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 02, 2010

    jamani mi nadhani hivi karibuni bunge litakuwa ni la wanamziki manake kila kukicha mwanamziki huyu anagombea hiki jamani ndo sababu tanzania haitokaa iendelee.yani mi mnaniuzi aah!

    ReplyDelete
  13. NITAMPA KURA YANGU, ANAFAA KUWA KIONGOZI! GO ON BRO!

    ReplyDelete
  14. AnonymousJuly 02, 2010

    Mimi ningekuwa Sugu ningeanzisha NGO badala ya kwenda kutafuta ubunge. Kwanza hutashinda. Pili baada ya hapo soko lako la kimuziki litakuwa kwishney. Tatu utakuwa umefulia. CCM ni chama cha damu cha Watanzania. Laana watakayokupa Watanzania ni damu ya Kristo tu ndiyo itakuponya.

    ReplyDelete
  15. AnonymousJuly 02, 2010

    kuna mtu hapo kauliza kwann sugu anagombea kupitia chadema...sababu ni kuwa CCM hua hatusimamishi wagomgea ambao hawana uzoefu na chama au uongozi. Ndio maana hao wanaoutafuta uongozi kwa lazima hua wanaanzia vyama pinzani. Maoni yangu kwa sugu ni kutafuta njia nyingine ya kutafuta pesa na sio siasa.......CCM Oyeee

    ReplyDelete
  16. AnonymousJuly 02, 2010

    nyie watu acheni unafiki !! kwanza wengi wenu amjasomea leadership .kuwa leader so lazima uwe na elumu kubwa au uwe msomi!! kwanza kwani wabunge wamekwenda shule ? kuna wabunge bungeni kazi yao kulala tu !! mimi hata chizi akijaribu kuwa mbunge sioni tatizo kwani walio kuwepo akuna wanachofanya zaidi ya kujirundijia marupurupu na mishaara wakati wana nchi walio wachangua wana ganga njaa !! so mpeni mshikaji mkono anao deserve si kumponda kiivyo!!

    ReplyDelete
  17. AnonymousJuly 02, 2010

    nyie anon wa 11;08 pm na 11;56 pm mbona mnaboa...kwani elimu ndio kigezo cha viongozi bora...mbona kuna maprofesa kibao na ma dr kwenye bunge letu na ni wapuuzi na wanalala tu bungeni bila hata kutatua matatizo ya wananchi....

    hebu acheni mawazo mgandoo!!!

    ReplyDelete
  18. AnonymousJuly 02, 2010

    kwani tz hawaangalii kama una criminal record?? si ndio juzi tu jamaa alitiwa ndani huyu? halafu ndio atuwakilishe sie watu wa mbeya mmmh ajikomboe kwanza yeye mwenyewe na watu aliokuwa nao wote ni wachovu haswa. wawaachie wanaojua kazi hizi kama mohammed dewji

    ReplyDelete
  19. AnonymousJuly 02, 2010

    Mheshimiwa Sugu swali lanyongeza.... Hamna noma kichaa wangu spika, unajua hivi vituo vya redio vya kizushi sio kabisa wanawabania sana wasanii wakongwe, sasa wewe waziri unaonaje mimi ndio niwe msajiri wa hivi vituo kudadeki watanikoma. na wewe spika hebu fanya mambo tuwe tunaingia n viwalo vyetu majinsi tusichomekee mashati. au vipi nipeni majibu basi. guys does it sound good????????????? mhhhhhhh sijui

    ReplyDelete
  20. AnonymousJuly 02, 2010

    Sugu ni bora kuliko asilimia 80 ya wabunge walioko bungeni sasa! Katika uelewa, uchapakazi na utetezi wa wanyonge. Na mnaoulizia elimu nyie ndo hamjui msemalo,wale wafuata upepo anaosema Kikwete..elimu sio madarasa uliyosoma, ni kile unachofahamu!! Uelewa wa Sugu ni mkubwa kuliko wabunge wengi wenye Masters au Degrees zao pale Bungeni!! SUGU,pamoja sana!

    ReplyDelete
  21. Habari wachangiaji.Mimi nina mpongeza Mr II kwa kujitokeza kugombea Ubunge anafaa.Kuna watu wachache wanamazo fivyu wajue ya kuwa hakuna chuo cha kufundishwa ubunge hata Uraisi na usifikiria viongozi wote hapa duniani wana PHD.uongozi ni wite na pia katiba yetu inasema kiongozi aweze kusoma na kuandika nafiki wengi wanajua kusoma ni kiingereza hayo mawazo fivyu kama umepata bahati kuona nchi za wenzetu wengine viongozi hawajui kiingereza na wanaongoza. kuna mmoja wetu hapo juu amesema kuwa jama amevaa kofia ya ccm ile ni rangi tu kwanini asiseme ni kofia ya yanga.Tuna viongozi wamesoma lakini hawajaleta maendeleo yeyote na ufisadi wanaufanya.Mpeni nafasi awe mbunge uenda akasaidia

    ReplyDelete
  22. AnonymousJuly 02, 2010

    sifa ya mbune ajue kusoma na kuandika,elimu kitu gani? wenye PhD ndo wanaotusainia mikataba mibovu,ufisadi na takataka zinggine, SUGU NENDA KAPAMBANE.

    ReplyDelete
  23. AnonymousJuly 02, 2010

    It is so sad kuona watu atleast naamini kwamba you have been exposed ndo mnakuwa wa kwanza kumponda Mr 2 sa je watanzania wakawaida ambao wanakaa huko vijijini na ambao hawajasoma.the brother is just showing us that its time for change i think wasaniii wameona kwamba when they go to opposition parties it has an impact kwa watu kuliko mtu mwingine yoyote wa kawaida.Maximum respect nawafeel ile kinoma thats how all the tanzanians should be

    ReplyDelete
  24. AnonymousJuly 02, 2010

    kwakweli uongozi sio kusoma na Phd,,lakini kuelimika ni vizuri atukatai, hawa waliosoma mbona ndio hao hao wanaenda kusaini mikataba mahotelini? kusoma kwao kunawasaidia wao kujua njia nyingi tu za kutuibia kwaiyo afadhali tu kijana mwenye uchungu na nchi agombee ameishi nje ya inchi uyo angalau anaelewa dunia inavoenda kuliko wakina flani wa darasa la saba na ni wabunge wa kudozi tu bungeni...

    ReplyDelete
  25. AnonymousJuly 02, 2010

    hivi watanzania kwanini mnashindwa kutumia za mbayuwayu plus za kwenu,nawasihi acheni itikadi za vyama na chagueni watu wanaofaa,ni vizuri kuwaunga mkono wagombea vijana kama hawa ambao ni wachache hujitokeza,hivi nyinyi wana ccn,hamtumii hizi barabara mbovu?wake zenu hawatoi rushwa wanapojifungua?watanzania sio wajinga kiivyo,wana tambua rasilimali walizonazo na vipi zinavyo wanufaisha wachache,ungeni mkono vyama vyenye kutetea maslah ya umma,na nyie mnao jifanya wenye chama angalieni sana siku ambayo nanyi mtaachia madaraka haya mambo yanayofanyika sasa yatawauma kuliko.nchi ni dhamana ya wananchi na kila dhuluma mbele ya haki mtailipa,maisha ya dunia ni ya kupita tu

    ReplyDelete
  26. AnonymousJuly 02, 2010

    huyo aliyevaa kofia ya ccm anaitangaza ccm au?

    tupo pamoja sugu.

    ReplyDelete
  27. mpenda mabadilikoJuly 02, 2010

    KUNA MDAU MMOJA KAZUNGUMZIA ETI UZOEFU,NAMUULIZA HIVI,ZITTO KABWE WAKATI ANAGOMBEA UBUNGE MIAKA MINNE ILIYOPITA ALIKUA NA UZOEFU GANI?NA JE YEYE ZITTI NA HAO WAZOEFU NANI AMEKUA NA MCHANGO MKUBWA BUNGENI?MDAU ACHA SIASA ZA MAJI TAKA...HUU NI WAKATI WA VIJANA TENA WA VYAMA VYOTE KUCHUKUA NAFASI,NASHANGAA KINA RIDHIWANI ETI WANAKUBALI KUZUNGUKA KUTAFUTA WADHAMINI WAKATI HUU NI WAKATI WAO,WALITAKIWA WAWE MAJIMBONI KUJIPIGIA KAMPENI ZA KUUKWAA UBUNGE ILI WAINGIE MJENGONI DODOMA WAKAPAMBANE NA VIJANA WENZAO KINA ZITTO,MNYIKA,HALIMA MDEE,NAKAAYA SUMARI,MR TWO N.K.LA SIVYO WATASHUHUDIA UPINZANI UKING'AA MJENGONI KUPITIA KWA VIJANA WAO KAMA TULIVYOSHUHUDIA ZITTO KABWE AKIFANYA HIVYO FOR ALMOST ALL 5 YEARS JAPO ANNE KILANGO ALIJARIBU KUPAMBANA NAE LAKINI UMRI UKAMBEBA ZITTO NA WENZAKE KINA HALIMA MDEE NA LUCY OWENYA

    ReplyDelete
  28. AnonymousJuly 02, 2010

    mr thugu, taratibu mudhee, hayo unayoingia maji marefu baba.
    Dar mpaka Mbeya mbali sana magurudumu huchomoka na kupata pancha, angalia sana.

    ReplyDelete
  29. AnonymousJuly 03, 2010

    Manaouliza elimu yake wote nyie CCM kawanza naona kuna mtu anarudia comments mara nne huchoki...Elimu ya hao wabunge unaijua wewe? Kuna mmbunge yupo hapo nilizoma naye na anasema ana master uwiiii nenda bunge site yao uone...uwiiii kadanganya sasa elimu ni ipi ya kudanganya au ya kuona maisha...Huyu ana exposure kubwa sana kuliko mtu aliyemaliza mkimani na kukariri vitabu.

    TEMBEA UONE....ukirudi home unaona zaidi ya watu ambao hawajatoka hapo.

    Hat ahuku tuliko wazungu wenye upeo wa mawazo ni wale waliotoka nje ya nchi ambao hawajatoka ni kama mavuvuzela tu yanazubiri kupulizwa tu..

    GO SUGU GO SUGU

    Vijana ndio wakati huu wa kuwabadilisha hao watu akili zao na kuwaonyesha how the real business is done

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...