Waziri Mkuu Mstaafu Dk. Salim Ahmed Salim
akitembelea viwanja vya maonesho ya sabasaba leo
Dk Salim Ahmed Salim akipatiwa maelezo katika banda
la Jeshi la Wananchi alipolitembelea leo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 06, 2010

    Kwa viongozi wachache ambao mwalimu alipenda waliongoze taifa letu ni pamoja na huyu jamaa,uongozi alianza zamani tofauti na hawa yebo yebo wetu wa sasa ambao nafikiri rais wa awamu ya pili ndio aliwabeba na kuwaonyesha jua la madaraka na sasa roho zinawatoka.Kampeni za 2005 maneno mengi yalisemwa eti kamuua karume sasa iweje kama aliua awe free watanzania tutabakia kudanganyika tu.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 06, 2010

    Uhalifu, mauaji nje nje!


    Eneo la Mbezi wilayani Kinondoni hivi sasa ndilo linaloongoza kwa matukio ya uhalifu katika Jiji la Dar es Salaam.

    Kuna mlolongo wa matukio ya ujambazi katika maeneo ya Mbezi ambapo watu kadhaa wameuawa miezi ya karibuni kwa kupigwa risasi kwa kuvamiwa nyumbani na wengine kuvamiwa wakiwa kwenye magari yao wakati wakijiandaa kuingia nyumbani na kupigwa risasi.

    Miongoni mwa matukio yaliyotokea Mbezi ni la takribani wiki moja iliyopita na kulihusisha kundi la watu saba waliokuwa na silaha za moto ambao walivamia kwenye nyumba inayomilikwa na mfanyakazi wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Elinawinga Massawe mkazi wa Mbezi Msakuzi, Makondeko kata ya Kibamba, na kumuua kinyama kwa kumpiga risasi ya kichwa Nkingwa Mboja (25), mfanyakazi wa kiume wa nyumba hiyo.

    Aidha, katika tukio hilo watu wawili walijeruhiwa ambao ni mwalimu wa Shule ya Chekechea iliyopo eneo hilo, aliyetambuliwa kwa jina moja la Ndimpo ambaye alipigwa risasi kifuani wakati mama wa baba wa nyumba hiyo, Mamboloo Massawe (85) alijeruhiwa na kitu chenye ncha kali kwenye mkono wake wa kushoto.

    Jeshi la polisi lilifanikiwa kuwatia mbaroni watuhumiwa wanne.

    Juni 13, mwaka huu, Padri wa Kanisa Katoliki Parokia ya Mavurunza, Athanas Zengo, akitoa mahubiri ya Jumapili, alilaani matukio ya ujambazi pamoja na mauaji ya raia wasio na hatia katika maeneo ya Kimara na Mbezi na kuwatupia lawama viongozi wa serikali wenye dhamana ya usalama wa raia kutokuwajibika.

    Alisema kila baada ya siku chache anashiriki kuwazika raia wasio na hatia wanaouawa na majambazi.

    Padri huyo alisema viongozi hao walioshindwa kutimiza wajibu wao ni afadhali wakajiuzulu na wasipofanya hivyo, wananchi wasiwachague katika uchaguzi mkuu ujao.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...