askari wa usalama barabatani akiandika maelezo ya ajali iliyotokea hivi punde maeneo ya Oysterbay.
gari zilizopata ajali zikiwa bado zipo eneo la tukio huku zingine zikipita kwa shida kutokana na ajali hiyo.
sehemu ya vibao vinavyolalamikiwa kuwa ndivyo vinavyosababisha ajali kutokana na kuwekwa bila mpangilio.

Uncle Michuzi,

Hebu naomba uturushie hii kwa wadau wanaohusika hasa hasa watu manispaa hapa junction ya karibu na Oysterbay Primary school , hivi vibao vilivyowekwa hapa bila utaratibu mzuri vimekuwa kero kubwa kwa watumiaji wa barabara kwa kusababisha ajali mara kwa mara karibu kila wiki tunashuhudia ajali.

Hivi ninavyoandika hii email ni punde ajali imetokea kama inavyoonekana kwenye hizo picha hapo.

Mfano hiki kibao cha vodacom uwekaji wake si mbaya sana kwa kuwa kipo juu lakini hivi vingine huwezi kuona gari linalokuja mpaka uingie kidogo barabarani kitu ambacho ni hatari. Tunaomba mamlaka husika ishughulikie uwekaji wa hivi vibao au kuweka taa au matuta pande zote nne za barabara kuwezesha kupunguza ajali za mara kwa mara kama walivyofanya junction ya migombani karibu na nyumbani kwa mheshimiwa.

Tunaomba Uncle utusaidie kuturushia hii kwa wadau husika.

Angalia hivyo vibao vilivyojaa bila mpangilio

Ndimi mdau Oysterbay

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. Hii ajali unayozungumzia haina uhusiano wowote na hivi vibao. Hii rav 4 imetokea masaki kwenda st peters na huyu jamaa wa nissan anatokea msasani kuingia barabara kubwa alitakiwa asimame wa rav 4 anayetoka kushoto barabara kubwa apite. vibao vipo upande wa kulia ukitoka msasani. ni kweli vibao vingi barabara za dar es salaam vinazuia kuona barabara kwenye makutano ila kwa hii ajali kuna uzembe au tatizo lingine kwa dereva wa nissan.

    ReplyDelete
  2. mizinga juction hiyo ya barabara ya Haile Sellasie na Karume eneo la O'bay primary school halijaanza leo, maana tangu mie nasoma hapo O'bay primary ktk miaka ya 1970s na 1980s, ingawa kulikuwa hakuna vibao vya matangazo kabisa, ajali zilikuwa nyingi tu.

    Hii inaonyesha kuwa suala kuu hapa ni uzembe wa madereva kutofuata sheria na hili la vibao ni kisingizio tu.

    Sheria za barabarani zifuatwe na wote yaani madereva na pia halmashauri ya jiji kuhusu wapi panafaa kuweka mabango.

    Pia Chuo Kikuu cha University of Dar-es-Salaam wafanye research kwa nini ajali hutokea eneo hilo hata wakati wa miaka ambayo mabango hayakuwepo na kutoa ripoti kwa kamanda wa polisi trafiki na umma kwa ujumla.
    Mdau1

    ReplyDelete
  3. Vibao vya matangazo vinaweza kua pia ni sababu, lakini sababu ya msingi hapo ni mwenye gari aina ya Rav 4 ya blue. Huyu alipashwa kumwachia huyo mwenye pikup apite kwanza kwani ndiye aliye kulia kwake na sheria inasema hivyo sehemu yenye makutano isiyo na taa, basi sheria ya ile ile ya eneo la mzunguko "round about aka keep left" ndio inayopewa kipaumbele. Pole kwa mwenye Rav 4 maana hapo imekula kwake

    ReplyDelete
  4. ni hapohapo mzee vijisenti alipokula mzinga uliompeleka mahakamani mpaka usawa huu...

    ReplyDelete
  5. hivi kesi ya zombe iliishia wapi?

    ReplyDelete
  6. Ndugu yangu uliaandika maoni yako 11:59:00 kama ungesoma maoni ya 11:32:00 ungekuwa umepata elimu nzuri ya usalama barabarani, mahali barabara zinapokutana sheria ya keep left haitumiki, inatumika tu mahali palipo na mzunguko, ila kwa udereva wa kujihami inashauriwa kuchukua tahadhari kila wakti unapoondesha chombo cha moto barabarani. Aliyekuwa barabara ya Haile Selassie analindwa na sheria ya kuwa barabara kuu ukilinganisha na hiyo nyingine ya kuelekea kushoto au kulia kwake. Yeye ndiye aliyeingiliwa katika eneo la njia yake kwa wakati huo. Lakini sitashangaa iwapo anaweza kunyimwa haki hiyo kwani wapindishaji wa mambo wana nguvu.

    ReplyDelete
  7. hiyo ajali mimi niliishuhudia ni kwamba huyo mwenye nissan aliingia bila kuangalia magari yanayokuja kwenye main road (au aliangalia lakini hakuona) hiyo Rav4 ilikuwa inatokea masaki kuelekea saint peter ilijaribu kukwepa hiyo nissan lakini ikashindikana na kugongana papohapo hiyo nissan ilikuwa ikiendeshwa na m-mama wa makamo. cha msingi hapa kama mdau alivyoshauri yawekwe matuta pande zote kutoka masaki, kutoka saint peter na kutoka kwa makam wa rais na upande wa pili ili kupunguza mwendo wa magari yanayopita kwenye junction hiyo.lakini pia vibao hivyo vinachangia kutopata clear vision hasa ukiwa na gari ndogo (ya chini)

    ReplyDelete
  8. he! we! zombe alishaachiwa siku nyingi...alishinda ile kesi..we uko nchi gani vile?maana swali lako duh!

    ReplyDelete
  9. ... Pia na zile kelele za New Maisha Club zifuatiliwe.... Yule mama mpenda pesa ajifunze kuwa klubu imezungukwa na makazi ya watu yaani binadamu.... Kinamshinda nini kuweka sound proof???????? Michuzi safari hii usiibanie!

    ReplyDelete
  10. kwenye juction zote zina hitajika matuta, speed zipunguwe.na unga mkono Ndimi mdau O BAY.

    kAMA HATUNA TRAFFIC LIGHTS AT LEAST KOKOTO NA LAMI TUNAWEZA KUIAGIZA china KWA AJILI YA MATUTA.lakini traffic watakula wapi jamani?

    ReplyDelete
  11. Hivo vibao bomu, pia vinaweza kusababisha ajali, sie tunafanya mambo kienyeji tu bila kujali usalama wetu hata siku moja.
    Pia magari yetu, tumeamriwa kujaza stika za nenda kwa usalama, insurance n.k.n.k. mpaka dereva hujui kama kioo cha mbele ni cha ma traffic au cha gari!
    Sie wabongo na usalama wetu na kama mbwa na paka kabisa!
    Bure kabisa!

    ReplyDelete
  12. Hapa 'matrafiki' wa nje ya uwanja tutakuwa wengi, mimi naona kama barabara ya kutoka masaki kuelekea saint Peters ndio main road, kwa hiyo yoyote atokaye pembeni kuingia barabara hii lazima awe makini zaidi. Na kwa hapo naona rav 4 ilibidi isubiriwe ipite kwanza.

    Mara nyingi uzembe wa madereva ndio husababisha asilimia kubwa ya ajali za barabarani, kila mtu ana haraka, sasa haraka nyingine mwisho wake ndio huu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...