Mshindi wa kura za maoni kugombea ubunge jimbo la Bumbuli, January Makamba akimpongeza Mh. Henry Shekifu kwa ushindi katika jimbo la Lushoto
wana Bumbuli wakimpongeza January kwenye hafla hiyo Mama January akiselebebuka kwa furaha kwa ushindi wa mwanae
wanaBumbuli wakisherehekea ushindi wa January

IFUATAYO NI HOTUBA YA JANUARY MAKAMBA BAADA YA KUTANGAZWA KWA MATOKEO YA KURA ZA MAONI YA UBUNGE JIMBO LA BUMBULI KWA TIKETI YA CCM ILIYOTOLEWA KATIKA UKUMBI WA OFISI YA CCM WILAYA YA LUSHOTO, JUMATATU TAREHE 2 AGOSTI, 2010 .
(Imeandikwa baada ya kuzungumzwa).
CCM Oyee!
(Oyeee!)
CCM Oyee!
(Oyeee!)
Bumbuli mpoo?
(Tupoo!)
Nashukuru sana.
Sasa, nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa rehema zake. Tupo tumefika hapa leo tulipo kwasababu ameamua iwe hivyo. Ametujalia uhai, uzima na afya kati yetu. Kwahiyo ni muhimu kumshukuru.

Pili, napenda kuwashukuru wazazi wangu kwa malezi mazuri, kwa mchango wao mkubwa kwenye maisha yangu mpaka nimefikia hapa nilipofikia leo. Pia familia yangu – mke wangu na wanangu wawili – bahati mbaya hawapo [hapa] – wamesafiri. Lakini nawashukuru kwa kunitunza, kwa kukubali kukabiliana na hizi presha za siasa, na kuniunga mkono na kuwa na mimi wakati wote. Kwa hotuba yote

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. Asiyekuwepo? ..?

    ReplyDelete
  2. Huyu ana tofauti gani na Yusuf yule msoma mashairi kwenye makwaa ya kisiasa?

    Hakuna jipya hapo

    ReplyDelete
  3. I can read bla bla, eti hotuba

    ReplyDelete
  4. Ndio tayari mbunge au bado hadi october..niwekeni sawa maana sijaelewa mwenzenu.

    ReplyDelete
  5. Mtajibebaa! tutaona hiyo serikali yenu mtakayounda na mtu mmoja tu bila ya wabungee! Haloo haloo alowatwisha atawatua octoba! tumeamua kuwawekea wagombea ubunge vijana wenye ari zaidi, nguvu zaidi na kasi zaidi.

    Karibuni uwanjani na magwanda yenu ya mgambo wa city!!

    CCM oyeee!

    ReplyDelete
  6. Wengine mie nikiwa mmojawapo sipendi watoto wa vigogo pekee wawe wanagombania uongozi, lakini jamani, viongozi wetu hasa wale waliotupatia uhuru mie sioni sababu waendelee kuwepo, mambo yamebadilika mno, hawako karibu yetu na fikra zao ni bado za kizamani, zile za kusema walalahoi sio lazima wapatiwe maji, umeme, elimu na huduma muhimu za jamii.
    Wa kina January tuko nao karibu, tunakunywa wote na ni vijana.
    Kama walalahoi wenzangu wanataka uongozi au jamaa zao, nao wagombee, washindane na kina January, au sio?
    Hongera dogo, ebu tukuone uongozi wako.

    ReplyDelete
  7. Michuzi endelea hivyo hivyo kubania comments zetu, kichwa kama nazi mbovu.

    ReplyDelete
  8. Upuuzi mtupu

    ReplyDelete
  9. Mgosi Januari nakupongeza sana. Ila nakuusia pia usije ukasahau nyumbani kisa umeshakuwa Mbunge. Nionavyo very possible kunasababu kubwa unaweza ukawa the next waziri mdogo...talk of Bendera, Aisha Kigoda na Mwantumu Mahiza kuanguka. Mawaziri watarajiwa kutoka mkoani Tanga ni wewe na Kaka yangu Salehe Pamba.
    Usisahau nyumbani wazee hawa wanavyonekana wamekukubali mno...ambuu uzaiva mghoshi. sijui kama hata hii lugha unaikumbuka. Maana ni unyamwezini na Daisaama du.

    ReplyDelete
  10. He is abusing 40 million Tanzanian people

    Usiige kaka ...njoo na clear methodology of your own

    I pit something is wrong upstairs for this person

    ReplyDelete
  11. MICHUZI LABDA SIO RIZKI WEWE..KWANINI UNABANIA COMMENTS ZETU SASA????

    NA HII BANIA BASI UTAONA.

    ReplyDelete
  12. maanons Wed Aug 04, 10:16:00 AM na Wed Aug 04, 10:55:00 PM...polepole jamani michu ndo alivo,ukigusa ukweli hasa kwa jamaa zake poleni

    ila tunasubiri matokeo ya utendaji wake hawa watoto wa wakubwa kama alibebwa au ana nia hasa ya kukomboa wanainchi...
    pilau hizi??!!

    ReplyDelete
  13. kijana umeoa???

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...