Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM,Dk. Mohamed Gharib Bilal akimnadi mgombea Ubunge wa Jimbo la Mtwara Vijijini, Hawa Ghasia wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika Kijiji cha Ntiniko Wilaya ya Mtwara Vijijini Mkoa wa Mtwara.
Mgombea Mwenza Dk. Mohamed Gharib Bilal akipita katikati ya chipukizi baada ya kupokelewa katika mpaka wa Wilaya ya Mtwara Mjini na Tandahimba Mkoa wa Mtwara wakati akiwa kwenye ziara yake ya mikutano ya kampeni leo mchana.
Mgombea Mwenza wa nafasi ya urais, Dk. Mohamed Gharib Bilal akizungumza na Wananchi wa Kijiji cha Nanguruwe Wilaya ya Mtwara Vijijini baada ya kusimama eneo hilo wakati akielekea Kijiji cha Ntiniko katika mkutano wa kunadi Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) leo.
Wananchi wa Kijiji cha Nahyanga Wilaya ya Tandahimba Mkoa wa Mtwara, wakimsikiliza Mgombea mwenza Dk. Mohamed Gharib Bilal wakati wa mkutano wa kampeni.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Nafikiri mimi kweli uvumilivu unanishinda michuzi inawezekana vipi ukafanya kampeni kwenye blog yako three quarter ya habari za uchaguzi zinahusu CCM kivipi najua ni walewale lakini sifikiri maadili ya uandishi wa habari inarusu hivo bwana umepata heshima nyingi sana kwa kupitia blog hii lakini kama unafikiri it just came like that we endelea tu...........kifupi UMENIBOA SANA MZEE TANZANIA WE NEED CHANGE BIG TYM TUNAMATATIZO KIBAO INFLATION YA HATARI MALIASILI ZINAUZWA KWA BEI YAKUTUPWA WE KWASAABU UMELELEWA KWENYE CHAMA BASI YOU WANT TO BRAINWASH PEOPLE THAT CCM IS DOING GOOD.......COME ON YOU CAN DO BETTER THAN THAT BANA PLEAAAAASEEEE!!!

    ReplyDelete
  2. Babu miaka imeenda lakini CCM ushindi lazima. CCM OYEE!!!

    ReplyDelete
  3. michuzi..mbona humu habari za ccm zimejaa sana?! hii blog ni ya ccm???!!! naona hata team ya libeneke linaongozana na jk..y not chadema or othr parties???!!!!!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  4. JAMANI EEH NYIE WANACHAMA WA KULALAMA MNATUBIA SASA, HII NI BLOGU YA MTU BINAFSI SIO MALI YA SERIKALI WALA CHOMBO CHA UMMA. MWENYEWE ANAWEKA VITU ATAKAVYO NA BADO ANAWAWEKEA MAKAMPENI YENU LAKINI KILA SIKU MKO MICHUZI UNATUBANIA UNATUBANIA, ANAWABANIA NINI? AU NAYE KAWA FUNDI CHEREHANI MAANA HUYO NDIO ANABANA NGUO ZIKIPWAYA.

    MBONA GAZETI LENU HALIANDIKI HABARI ZA MIKUTANO YA WAGOMBEA WENGINE, NA WATU WANANUNUA KWA PESA ZAO? MBONA KUNA BLOGU ZISITAJI MAJINA HAWATOI MIKUTANO YA CCM? KUDADADEEK KAMA NIWATIE BAKORA KIDOGO!

    ReplyDelete
  5. Michuzi BIg UP...Usisikilize hizo kelele za wasio na akili timamu. Nani amewaambia hawa watu kuwa hii blog ni ya Serikali au Chama fulani, hii ni kazi yako na unaamua kuandika au kuweka picha ya chama unachokitaka wewe na sio wao. Wapinzani badala ya kutangaza sera zao wao wanalalamika tu , kila kitu wanaona wanaonewa....Upinzani kazi jamani ohoo. Kila mtu ana haki ya kuanzisha blog yake na kufanya anachotaka. Hapo roho zinawauma kuona rangi ya kijani na njano. Na bado mwaka huu mtaziona rangi zote kwa mchanganyiko...Kuntuuuuuuu CCM Oyeeeeeeeeee

    ReplyDelete
  6. Kaka Michuzi,
    Tuwekee na picha za uzinduzi wa kampeni ya CHADEMA

    ReplyDelete
  7. kaka michuzi tupostie na picha za uzinduzi wa kampeni za CHADEMA

    ReplyDelete
  8. we ndugu uliyetoa maoni hapo juu naona uwezo wako wa kufikili ni mdogo, hii blog ni ya mtu binafsi kwa ajili ya watu wote na itikadi tofauti, sasa inakuwa inaboa kuona mwandishi anayeheshimika akiegemea upande mmoja tu, ni vyema akawa anaandika habari kwa usawa au ndio wale wakina "KIKWETE PRESS" kaka michuzi tunaiheshimu kazi yako ila kuwa fair kwa vyama vyote au unataka ubunge wa kuteuliwa na rahisi?? UNABOAAAAAAAAAAAAAAA

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...