Huu ni msikiti mpya ulio Mbezi Beach jijini Dar ambao ujenzi wake ndio umeanza. Shekhe wa msikiti huu wa kwanza eneo hilo amesema katika hutba yake ya Ijumaa kwamba michango ya hali na mali inaombwa ili kukamilisha nyumba hii ya ibada. Maelezo ya namna ya kuchangia yatafuata. Kwa walio Dar wanakaribishwa kupeleka michango yao hapo msikitini katika barabara mpya ya Kawe chini, si mbali sana na eneo la kulenga shabaha la JWTZ



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Mbezi beach kuna matajiri kibao na ni waislamu hivyo sina shaka michango itapatikana ya kutosha sanaaaa na msikiti huu utakuwa state of art. ShefJo, dar

    ReplyDelete
  2. a/alaikum warahmatullah mtume wetu muhammad (s.a.w)anasema ukijenga nyumba ya allah hapa duniani basi allah atakujengea yako tena ya kudumu huko akhera.

    ReplyDelete
  3. kwanini msikiti ujengwe karibu na eneo la kulenga shabaha la JWTZ? hivi hakutakuwa na usumbufu wakati wa swala?

    ReplyDelete
  4. Sheikh Mohammd SultanAugust 15, 2010

    Assallam Allaikhum kutoa ni moyo hao Matajiri MOLA amewapa UTAJIRI kwa mitihani kwa hiyo mwisho wa kutoa utaona watakachotoa wanajilimbikizia watadhani watazikwa nayo.ushari uongozi wa MSIKITI wafungue acount Bank ili tulio UGHAIBUNI tuweze kuchangia kwani huu ni wakati mzuri wa kufanya biashara na MUWEZA ASIYEWEZWA M'MUNGU.

    ReplyDelete
  5. mimi napafahamu hapa mahali ni barabarani karibu na daraja la kwa apson. kiwanja hicho ni cha mtu binafsi ambaye amekigawa nusu anaishi na musu unajengwa msikiti. hivi jiji hawajatenga maeneo maalum ya ujenzi wa nyumba za ibada mbezi beach maana sehemu hiyo ni ndogo na kwa vyovyote hapawezekani kujengwa a state of the art msikiti maana ni padogo mno. wapate kiwanja kikubwa ili ujenwe msikiti mkubwa na mzuri kama yalivyo makanisa.

    ReplyDelete
  6. Ukitaka kusali, hata ndani ya disco unaweza, acha hizo risasi.
    Mwingine nae asema padogo. Jamani acheni MUYUMBA YA MWENYEEZI MUNGU ijengwe!

    ReplyDelete
  7. Nilikuwa sijui kama Michuzi kumbe unabana baadhi za hoja hutoi. Poa Ankal

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 28, 2012

    Inasemekana hichi kiwanja ambacho waislam wa sehemu hii wanategemea kujenga
    msikiti kimeshatiwa kwenye orodha
    ya kufutiwa hati baada ya fitna za
    'watu' kupelekwa wizara ya ardhi.
    bwana Michuzi pse fuatilia msiba huu.

    anonymous

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...