HAKI YA KUPIGA KURA, HAKI YA URAIA WA NCHI MBILI KWA WATANZANIA WAISHIO UGHAIBUNI: Ni stahili au siyo?
Kuna makundi makuu ya aina tatu ya watanzania waishio ughaibuni kwa sababu mbali mbali. Kundi la kwanza linaundwa na wanafunzi waliochaguliwa kujiendeleza kimasomo nje ya nchi, katika fani mbali mbali za kitaaluma kama vile Udaktari, uhandisi, elimu, uchumi, afya n.k. Aidha kwa kupitia udhamini wa serikali, udhamini toka nchi au vyuo husika, udhamini toka kwa mashirika na hata udhamini toka kwa watu binafsi na familia.
Katika kundi hili la kwanza, wapo wale ambao masharti yao ya udhamini yanawalazimu kurejea nyumbani baada ya kuhitimu mafunzo yao. Mbali na hawa kuna wale ambao hawabanwi na masharti yeyote ya kurudi nyumbani wamalizapo masomo yao. Baadhi yao hubakia ughaibuni katika kile ambacho tunaweza kukiita utafutaji wa malisho bora, kwa lugha ya kiingereza greener pastures.
Miongoni mwa wale wasiobanwa na sheria ya kurejea nyumbani baada ya kuhitimu masomo, wapo waliofanikiwa kupata hati ya kudumu ya kuishi ughaibuni au ukipenda permanent stay kwa kimombo, hawa wanayo hiari ya kubadili au kutobadili uraia kwani wanaweza kuishi muda wowote kwa kadiri wapendavyo katika nchi husika ya ughaibuni. Vilevile, wamo wale ambao wameamua kubadili kabisa urai kwa hiari yao lakini pengine kwasababu tu ya harakati zao za kuwinda haya malisho ya kijani.
Kundi la pili linawahusu waajiriwa katika taasisi mbalimbali zilizopo nje ya nchi, kwa kimombo expatriates, mfano, wahadhiri katika vyuo vikuu, madaktari n.k. Kama ilivyo kwa kundi la kwanza, hapa kuna waliobadili uraia na wasiobadili uraia pia .
Kundi la mwisho ni la watanzania wanaoishi nje ya nchi aidha kwa kuoa au kuolewa na raia wa nchi za kigeni. Kama ilivyo kwa makundi mengine ya awali hapa pia kuna waliobadili uraia na wasiobadili uraia.
Kabla sijaendelea na mada hii, ningependa kila mmoja wetu atafakari kwa kujiuliza swali hili, Je watanzania waishio ughaibuni wanao mchango au faida yeyote kwa taifa? Hapa nitategemea majibu mbali mbali, pengine ya ndiyo au hapana, lakini napenda nijipendelea mwenyewe kwa kuanza kutoa majibu ya ndiyo kabla ya wachangiaji wa makala hii.
Japo mimi siyo mchumi, lakini kwa mtizamo wangu, watanzania waishio nje ya nchi wanachangia kwa namna moja au nyingine katika katika kuleta maendeleo kwa njia mbali mbali. Kwa uzoefu wangu wa kuishi nje ya nchi, nimejifunza kitu hiki, ukienda western union money transfer, hapo utakuta foleni kubwa ya watu toka bara la Afrika wakimo watanzania, wakihangakia kutuma pesa kwa njia hii aidha kwa familia zao kama vile wazazi, wake, waume, kaka, dada, mjomba, shangazi, binamu, wakwe au pengine marafiki kwa sababu mbalimbali zikiwemo za kusomesha, matibabu, ujenzi, biashara n.k
Kijamii, kwa kupitia vyombo mbali mbali vya habari mtandaoni kama vile magazeti ya mtandaoni na mablogu, watanzania waishio nje ya nchi kwa kushirikiana wenzao wa nyumbani wameonesha ushirikiano na mshikamano wa hali ya juu kwa kutoa michango yao kimawazo na kifikra kupitia vyombo hivi vya mtandaoni. Siyo, hayo tu bali pia ushiriki wao kuitangaza nchi yetu nje ya mipaka yake na kudumisha utamaduni wetu. Kama ninadanganya kwa hili basi utembelee pale kwenye blogu ya MUHIDIN ISSA MICHUZI, ukipenda, ANKAL/ MZEE WA LIBENEKE.
Awali ya yote, napenda kuipongeza serikali kwa kukubali kuwepo kwa uraia wa nchi mbili kwa watanzania waishio ughaibuni. Sasa basi tukija kwa upande mwingine wa shilingi, sote twaelewa fika kuwa haki ya kupiga kura na kupigiwa kura kwa mujibu wa katiba ya jamhuri ya muungano wa tanzania ni haki ya msingi ya kila raia ili mradi tu awe na sifa ya kufanya hivyo.
Kitendo cha serikali kukubali na kuridhia suala la uraia wa nchi mbili kwa watu wake waishio ughaibuni, inaashiria picha kamili kuwa serikali inatambua umuhimu na mchango wa watu wake waishio nje ya nchi. Kama hivyo ndivyo basi, je serikali itachukua hatua zipi za haraka ili kuwapa fursa watanzania waishio nje ya nchi kushiriki katika upigaji wa kura kwa njia ya mtandao? Kwa minajili ya kuwapa raia wake haki yao ya msingi na kikatiba kuwachagua viongozi wanaowapenda .
Kuna nchi kadhaa katika bara la Afrika ambazo zimekwisha ruhusu ushiriki wa raia wao waishio ughaibuni katika uchaguzi kwa kupiga kura kupitia tovuti za uchaguzi kwa njia ya mtandao. Nchi hizi ni kama vile, Afrika ya kusini, Burkina Faso, Mali, Rwanda, Ghana na Kenya. Nchi zingine ambazo zipo mbioni kufanikisha mchakato wa upigaji kura kwa njia ya mtandao kwa raia wake waishio nje ya nchi ni kama vile, Uganda, Nigeria, Liberia, n.k.
Mwisho, kama utaratibu huu wa uraia wa nchi mbili na haki ya kupiga kura kupitia tovuti za uchaguzi za mtandaoni umefanikiwa kwa baadhi ya nchi za Afrika, hii ikiwa ni pamoja na jirani zetu Kenya na Rwanda, hivyo basi nimatumaini yangu kuwa serikali itasikia na kuzingatia kilio cha watanzania wenye mapenzi mema na nchi yao.
--
Malkiory William Matiya,
Bachelor of Education with honours ( UDSM) & M.Sc in Public Health ( University of Tampere, Finland)
Address: Yrttikatu 1 B 16, Tampere 33710, Finland.
Mobile: +358505261479
Emails: malkiory@gmail.com or malkiory.matiya@ymail.com

KABLA YA MAONI YA URAIA WA NCHI MBILI MICHUZI LETA AFISA WA UHAMIAJI ATOE UFAFANUZI KUHUSU NANI NI RAIA WA TANZANIA MAANA SWALA LA HUSSEIN BASHE LIMETUACHA GIZANI KUJUA YEYE SI RAIA SABABU YA WAZAZI WAKE WOTE WAWILI KUWA WASOMALI? AU KWA SABABU YA BABA YAKE KUWA MSOMALI.
ReplyDeleteMFANO BABA YAKE BASHE ANGEKUWA MASOMALI NA MAMA YAKE MNYIRAMBA WA TANZANIA JE HUSSEIN BASHE ANGEKUWA RAIA WA TANZANIA BILA KUKANA URAIA WA BABA YAKE KWA SABABU MAMA YAKE NI MTANZANIA? JE HAPO VIPI TUNAOMBA UFAFANUZI.
Wenzio weshakata tiketi za ndege kurudi kupiga kura hiyo octoba wewe wangoja nini? Au ndiye wale wakimbizi wa Somalia na Burundi? Nyie si ndio wale kila siku mnasema Bongo hamrudi kunanuka, kuna vumbi leo mnataka kupiga kura?
ReplyDeleteHalafu hujatueleza wewe ni wa kundi lipi na mchango wako ni upi kwa taifa hili.
Mwisho umeona nyomi la Jangwani, na la Mwanza? Hata wote mlioko ughaibuni mkimpigia kura mgombea wenu bado hamfiki popote. Weraa weraaa kipenga kishalia hicho kuwa muwazi baba ulikuwa ukilalamika Michuzi hatoi post zako unazomuandikia hizo nini? Leo hajawa sekuriti gadi?
WEWE WILLIAM MATTIYA NI MBUMBUMBU KWELI KWELI SASA HAPA MBONA NI MAPUMBA UNATUELEZA TAYARI KWANZA YOU HAS STAY IN EUROPE FOR QUIET SOMETIMES ALTHOUGH YOU HAS SAID THAT ABOUT VOTE OF TWO COUNTRY I CANT DENIE YOUR POINT IS NOSENSE BECAUSE OF THAT YOU CAN NOT BE OF CITIZEN OF TWO COUNTRY AND VOTE FOR TWO COUNTRY? EVEN IF BIBLE SAYS YOU CAN NOT HAVE TO BE WITH TWO HUSBAND MEANING THAT HUWEZI KUTUMIKIA MABWANA WAWILI. THEREFORE WHAT IS YOUR POINTS WILLIAM. YOU HAS LET ME DOWN YOU NEEDED MORE EDUCATIONS AND RESEACH TO PREACH US TO UNDERSTANDS YOUR LOWEST POINT. ON SHORT NO VOTES FOR PEOPLE OF TWO CITIZENS. AND IF YOU THINK TO SEND 2 HUNDRED DOLLARS IN WESTERN UNION IS A BIG DEAL WE DONT WANTS THAT MONEY AND GO BUY BURGER, TANZANIA DEPENDANTS ON ITS CITIZEN NOT ABROAD MY COMRADE YOU NEED TO WAKE UP, CIAO PEACE IN HEAVEN!
ReplyDeleteUraia wa nchi mbili ni vizuri ikaletwa kura ya maoni maana ni suala zito sana.
ReplyDeleteChe
Nashauri tafuta Tanzanian Citizenship Act No.6 of October 1995 ujisommee kabla hujasema mengi.
ReplyDeleteAngalia pia http://www.unhcr.org/refworld/type,LEGISLATION,,TZA,3ae6b5734,0.html.
Mtandao una kila kitu.
Ahsante
Mdau
ningependa kuwafahamisha hao wazalendo wawili hapo juu,hivi ni kwanini tunachukiana sisi watanzania na kuwapa nafasi wageni?mko hapo kutia maneno machafu mara tu anapo ongea mzalendo wa ughaibuni kama vile sio mwenzenu?acheni wivu usiokuwa na maendeleo na ushukuru mungu kuwa ni raia wa tanzania!!!mimi niko kwenye kundi la tatu au la nane siju but inabidi tupendane jamani cos wenzetu wanalindana but sisi twauzana si maajabu hayo??namuunga mkono mzalendo alie toa hili hoja kwani linanihusu hata mimi mtu wa rangi mbili nimezali bongo nimesoma bongo na niko ughaibuni cos mzee wangu mzungu!!but niulize kwenu wapi ni bongo!!!haya huku ugaibuni wajua mimi ni raia wao lakini bado watanitenga na kusema mimi mbongo ingawa nondo haionyeshi hivyo,nikija bongo naambiwa ndio nyinyi manao ukana uraia wenu!!!but sija chagua nizaliwe wapi au na nani ni kazi ya mola,tuelimike ndugu zangu na tusichukiane,na pia nakubaliana mzalendo hapo juu kuh..huyo msomali mimi nafikiri mtanzania wa kweli na mwenye haki yake ni rai wa bongo sio ule wa kununua kwa vijisenti cos wenzetu hawafanyi hivyo na ndio maana wanamaendeleo,tusuze uraia wetu kwa vijisenti anaestahili apewe na ningeomba serikali iwape raia wake nafasi ya kuwa raia wa nchi mbili kwa sababu nyingi tu muhimu awe na haki zote za kuwa raia na sio wa kununua.asanteni wazalendo na naomba tupendane na tuwe na wivu wa maendeleo. from Italy mc pales Mlalahoi
ReplyDeleteWewe huna dili kabisaaa naona umelewa mabox tena una bahati ungekuwa karibu yangu ningekupa ngumi za pua shuwani wewe, hiyo bachelor na adress vya nini?? watu wana PHD na kazi bomba wametulia wewe unajishaau nini? akili zako hazina akili
ReplyDeleteMatiya,
ReplyDeleteShukrani kwa uchambuzi na uwasilishaji wako wa hoja hii.
Sahihisho kidogo.
1. kuna kundi la nne la watz waliojilipua (si wanafunzi wala si expatriates wala walio na ndoa na wasio watz)
2. Makundi hayo si lazima kuwa ni exclusive to each other yaani mtu anaweza kuwa yuko shule na pia ameolea nje au ameoa nje na pia ni expatriate n.k
Wazo langu ni kuwa Uraia wa nchi mbili ni sawa lakini kwangu naona si lazima mana unaweza toa tu mchango hata kama huna uraia wa nchi za nje.
Nashauri kuwa endapo itakubaliwa kuwa mtu anaweza kuwa na uraia wa nchi mbili au zaidi basi aruhusiwe tu kupiga kura lakini asiruhusiwe kuomba nafasi ya uongozi wa nchi kwa ngazi yeyote vinginevyo akitaka aukane uraia wa nchi nyingine na akae kama miaka mitano hivi ndipo aombe kuchaguliwa.
wewe mtoa mada umekuja lini ulaya?inaelekea hujui kinachoendelea unaongea ongea tu. Kundi la kwanzani sisi wanariadha aka wakimbizi, sisi ndio tupo majority. makundi yote yanasemwa tu lakini wote ni wanariadha either wanafunzi, madactari n.k. Ilaijulikane wanariadha walifanya hilo kwa sababu za kiuchumi na ndio tunaosaidia nchi yetu kuliko wanaoishi bila papers. wanariadha hatulipi council tax, nyumba, wala maji na tunapata dole. sisi ndio tuna servings kubwa na ndio tunaotuma mishiko huko bongo. Mimi najivunia kuwamwanariadha sababu naamini wazungu walikuja bongo kama wamisionari baadae wakaiba dhahabu na kurudi kwao. sisi tumekuja kama wanafunzi, madaktari, manesi, wanascouts, vikosi vya kwaya na kadhalika tukaamua kujipeana ili tuendelee kuwepo na kusaidia jamii yetu huko Africa. kwa hivyo sijutii nilichofanya na nataka serikali itambuemchango wetu, at the endof the day najua nimezaliwa Mheza.
ReplyDeleteSenk you
Mwanariadha mkongwe- Milton keynes
Kura zikipigwa kupitia tovuti haitawezekana KUCHAKACHUA
ReplyDeleteNalitolelaaaaaaa Peter wa Canada Ex Muzumbe Murogoro and Ex St. Antony Mbagala ninakubali wewe ni mtu wa Kimbombo na Msomi wa New Generation Big Ups Peter Nalitolela we need your braves Sir!
ReplyDeleteEwe Peter Nalitolela nakushukuru sana, your entry is most fascinating, not in content...hasha laa...but in your use of the foreign language. English is really foreign to you, you could be arrested kwa kubomoa lugha ya wenzio mtindo huo. All the same thanks and cheers.
ReplyDeleteWewe PETER NALITOLELA haujiami umepitwa na wakati bado una mawazo ya enzi za TANU na TAA.
ReplyDeleteWatu wanao pinga urai wa nchi mbili ni sawa na wale waliokuwa wakipinga mfomo wa vyama vingi ,Walifunga mabakuli yao pale Manaume wa shoka Mwalimu J.K Nyerere alipo simama na kuunga mkono mfumo wa vyama vingi.Jamaa wa nje wanachofanya ni kuingiza $$$ ndani ya nchi wabaya ni hawa akina PETER wakisha pata madaraka waendekeza UFISADI na kutafuna pesa za umma.Kuwapa urai wa nchi mbili tutawasafishia njia, ya kuwekeza with more confidence here in TZ.SWALA LA KUSEMA URAI WA NCHI MBILI UTAHATARISHA USALAMA WA TAIFA NI UNAFKI MTUPU.
PETER NALITOLELA KWELI KAJITOLEAS KUTUVUNJA MBAVU!!!!! MBAVU ZANGU JAMANI!!! MWE!! HICHO KIDHUNGU MIMI KIMENIACHA HOI KWAKWELI. KEEP IT UP NALITOLELA
ReplyDeleteEEH nawe mwekezaji feki kinakushinda nini kuwekeza sasa? Unafikiri unaweza kuwekeza kwa dola 200 au 2000, mawee! HUWAONI wawekezaji wa ukweli wanavyowekeza na HAWANA hatas uraia wa BONGO.
ReplyDeletehebu wekezeni kama wazungu tuwaone, kununua nyumba tu na viwanja mnapiga kelele humu mnalialia bei kubwa bei kubwa. nikikwambia nikopeshe dola 10,000 hapo niende China huna, afadhali HATA KINAMAMA WAFANYABIASHARA WA KARIAKOO WANA PESA ZA KUWEKEZA! lakini sio nyie.
nyie subirini mhurumiwe mpewe tu lakini hakuna la maana mtakalofanya wala kuwekeza