HOJA BINAFSI KUHUSU MALALAMIKO YA KAMPENI ZA UCHAGUZI KWA GLOBU YA JAMII KUA GLOBU YA JAMII INAPENDELEA ZAIDI CHAMA TAWALA. JE NI KWELI?

NANI KASEMA ANKALI ANAFAGILIA ZA CHAMA CHA MAPINDUZI TUU ?NA NANI KASEMA ANKALI KANUNULIWA NA CHAMA HICHO?SASA MBONA ANATURUSHIA NA VYAMA VINGINE?

JAMANI TUSIMLAUMU SANA ANKALI MIMI KAMA MDAU MKUBWA SANA WA BLOG NIMESIKITISHWA SANA NA KAULI ZA WATU KUSEMA ANKALI HATENDEI HAKI VYAMA VINGINE SI KWELI NI KWAMBA HAO WENGINE HAWATUMI HABARI ZAO SASA ANKALI AOTEEE JAMANIIIII TUJIREKEBISHE MIMI NALETA HOJA APA KWENU........

MAANA INAKERA WEWE ANGALIA FACEBOOK NA MITANDAO MINGINE ATA APO KIJIWENI KWAKO MNASHADADIA TUU ANKALI KUA ANAPENDELEA CHAMA CHA MAPINDUZI. TUFIKE MAHALI TUBADILIKE WATANZANIA. NAOMBA KUTOA HOJA

MIMI MDAU WA GLOBU YA JAMII.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 56 mpaka sasa

  1. Ni kweli bwana Michuzi anapendelea CCM na hapendi kurusha habari ambazo zipo kinyume na chama hiko. Nakumbuka binafsi nimeshawahi kumtumia comment kwamba hata credibility yake kama mwandishi wa habari imepungua na kuna idadi kubwa ya watu hawatembelei tena hii blog. Huu ni ukweli na uache ulimbukeni. Kama na hii utabania pia basi ni kwa faida yako mwenyewe.

    ReplyDelete
  2. We upende usipende, Ankal KADA la CCM na yuko bias.
    Tunampenda kwa ripoti zake lakini basi ajirekebishe asioneshe wazi namna hiyo

    Msemakweli

    ReplyDelete
  3. Ni kweli coverage ya uchaguzi inaonyesha picha zaidi za CCM kuliko upinzani. wewe fanya hesabu, kwa kila picha kumi zenye mgombea wa CCM , moja tu ndio ya upinzani.
    Sidhani kama ni kwa makusudi-kumbuka kuwa Michuzi anasafiri na Rais/mgombea wa CCM. Jitahidi bwana michuzi najua huna nia mbaya, lakini blog yako imekuwa muhimu sana watu wanaona kama ni RTD ya aina yake.

    ReplyDelete
  4. Huna haja ya kujitetea sana hata ningekuwa ni mimi ningeheshimu yule anayenisbabishia kula hapahitaji taaluma ya juu katika hili ila sema kwa sababu blog hii ni mali yake na si ya umma inabidi tuwe wapole tu kwanza tuche kwanza uchaguzi ukiisha mambo yatakuwa mswano kama zamani

    ReplyDelete
  5. Kwani uongo bwana ni nani asiyejua kwamba uncle anafagilia CCM tu akijitahidi CCM(B)CUF but anaalegde na CHADEMA

    ReplyDelete
  6. tatizo chadema wanataka kila kitu wao tu,si waende jamii forum mtandao wa wendawazimu,wameshaona kule ni watu 6 tu wanaangalia mtandao wao,ndo kinawauma wanataka na michuzi awaweke huku,mwaka huu ndo mwishowenu,hakuna jimbo mtaliona,karatu imerudi ccm,mohi mjini ccm wamevunja makundi,kwa hiyo ndesamburo asahau kupata kura.hai kwa mbowe wanachama wa chadema wanazidi miminika ccm,tarime imekuwa ngome ya cuf,na kigoma kaskazini cuf wamepata nguvu zaidi.sasa ndugu zetu subirini viti maalum tu ambavyo mtavipata kwa asilimia 5 ya dr slaa.kikwete 77percent,lipumba 11percent.chadema 5 percent,nccr mageuzi 3percent.tlp 2,

    ReplyDelete
  7. serikali ya mseto,rais JK,waziri mkuu lipumba,waziri wa madini zito kabwe,waziri wa sheria mgombea urais wa nccr,mkuu wa mkoa mrema,na balozi wa tz vatican padri wilbroad slaa

    ReplyDelete
  8. Acha upimbi wewe kifupi liko wazi kwamba misupu anapewa mlungula na na chama twawala, kwani yupo kabisa kwenye msafara, kama hapendelei mbona timu yake haipo na CUF AU CHADEMA. Najua misupu unaweza usiirushe hii lakini ndio hivyo na mtoa mada ujumbe nadhani umefika

    ReplyDelete
  9. Ndugu yangu umejuaje kama vyama vingine havitumi habari zao. Yeye ankal ndio alitakiwa kusema kwamba hatumiwi habari na vyama vingine, lakini inashangaza wewe ndio unongea hivyo. Taratibu ndugu yangu, tunajua unakipenda chama lakini isifikie hatua hiyo...........

    ReplyDelete
  10. Hii sio hoja ya msingi! Mheshimiwa naomba uiondoe hoja yako. Kwa maelezo yako inaashiria kuwa unataka kumchanganya Ankal kama walivyojichanganya TBC kwenye kuonesha Uzinduzi wa kampaini za CHADEMA. Sasa nakuomba usimuweke Ankal kwenye mazingira yale. Unatakiwa ubadirike watanzania wameshadirika isipokuwa wewe tu. Hoja kama hizi huwa tunaita ni za kichochezi. Nimemaliza!

    ReplyDelete
  11. NI KWELI KABISA WALA HAIHITAJI HATA DARASA MOJA KUJUA ANKAL KANUNULIWA. PICHA ZA KARAGWE ZINAFIKA KWA HARAKA KULIKO PICHA ZA JANGWANI WAPI NA WAPI? BINAFSI NILIKUWA NAKUAMINIA SANA LAKINI SASA NAKUONA KAMA MSALITI TUU. UJUE NAFSI ZA WATANZANIA ZITAKULILIA SIKU YA MWISHO. YAANI UNAUZA UZALENDO WAKO KWA AJILI YA HUTO TUSHILINGI TWA WIZI TENA ALIYEIBIWA NI HUYO HUYO MTZ? KWELI MICHUZI??? HATA USIPOWEKA KOMENTI HII NAJUA UJUMBE WANGU UMEFIKA.

    ReplyDelete
  12. Mtoa hoja ya haja kuna kitu muhimu ambacho unatakiwa kuzingatia.
    1. hii ni blog binafsi inaandika kile mwenye nayo anataka kitoke, na inaendeshwa anavyotaka yeye, hakuna wa kumpangia.
    2. Ankal 1995 alikuwa kwenye timu ya kampeini ya uchaguzi ya Ben Mkapa akiwa na jukumu maalum la kuongozana na Mwl. JK Nyerere, mwaka huu yupo kwenye timu ya kampeini ya JK (CCM) sasa yuko na timu ya Kikwete, nauli malazi na maroroso mengineyo CCM wanagharamia alafu awe busy muda wa kampeini wa CCM anaandika habari za Vyama vingine sidhani kama ungekuwa wewe mgombea wa CCM ungafurahi?
    3.Demand and supply ndio hutawala soko huria, hizi ni za kupita tu, siku CCM watakapokuwa wapinzani upepo utabadirika,
    4. Hatuna sababu ya kulia na kumlazimisha mtu kujiunga kwenye timu yetu, upepo hubadirika ipo siku atakuja mwenyewe kama alivyoenda Liverpool mwenyewe.

    ReplyDelete
  13. Mbona ankali Mishuzi kaanza kuweka habari za vyama vingine juzijuzi tu wakati kampeni zimeanza siku nyingi? Tena kaanza kuziweka habari za vyama vingine baada ya watu kumwuliza why anaweka za SiSiEmu tu? Acha mikwara aloo.

    ReplyDelete
  14. Umewasilisha kweli, ankal amekutuma?

    La Msingi ni kujua kuwa Uchaguzi ukiisha maisha yanaendelea kama kawaida na kama akiwaudhi wadau blog yake itapungua umaarufu na wasomaji watapungua hivyo wadhamini watajitoa kumsponsor.

    Ushauri wa BURE mimi si shadadii chama chochote ila ni vema akaweka matukio ya vyama vyote ili ajiongezee umaarufu na Blog yake.

    Otherwise ankal atapoteza umaarufu muda si mrefu na blog yake.

    Ukweli ni kwamba, Blog siku hizi ni biashara, ndo maana ametanguliza matangazo ya voda hapo juu na mengine.

    ReplyDelete
  15. Tatizo la number TEN bei yenu ikoo juu sana wakati mna wadhamini kibao. Acheni hizo fanyeni hata book 2, ili lisomwe na watu wengi.

    Mtavuna tu hata mkishusha bei, mbona voda wameshusha hadi vocha za shilling miatatu ili kukamua hadi mwananchi wa mwenye kipato cha chini, nyie mnasubili nini?

    ReplyDelete
  16. Mimi natofautiana na wewe. Hoja ni vyama vya siasa ila pia hata kwa mambo mengine huwa haweki hewani. Labda angetupa vigezo vyake anavyotumia ili watu tuwe tunamletea habari kwa kufuata hivyo vigezo. Ni kweli blog ni yake lakini kwa kuwa ni inahusu mambo ya jamii na habari za hapa na pale, ni vizuri basi akawa "fair" pande zote na kwa kila kitu. Nasema hivi kwa kuwa mie nimemtumia habari tofauti tatu ambazo ni za kusaidia wananchi wenzangu lakini mara zote hajaweka hata moja. Isitoshe kuna watu kama wawili tena ambao nao walimtumia habari kadhaa lakini hajawahi kupost hata moja yapo. Ni vyema tukajua vigezo; kama ni vya picha au vya uandishi wa habari za magazetini au mtandaoni. Maana kwa uelewa wangu ni kuwa habari za issamichuzi zote ni za kutumiwa na si ya yeye mwenyewe kuziandika. Kibaya zaidi kuna tofauti kati ya uandishi habari na upiga picha.

    ReplyDelete
  17. kwa upande wangu naona kweli kanunuliwa na CCM , anawapendelea sana tena sana , mimi ni mwana ccm ila nimeliona hilo , sasa akitaka akikubali ukweli ndio huo , DEAL WITH IT , mwenyewe anajitetea kwa kusema upatikanaji wa habari wa ccm ni rahisi kuliko vyama vingine , wakati si kweli , ccm wamewanunua , habari anazotoa ni za KICCCM KICCM tuuu , mara kikwete yuko kule mara huku mara salma kikwete yuko kule mara yuko huku , cuf na chadema mara moooja mooja ndo anatoa , mtashangaa mimi ni CCM lakini nasema hivi ni kwamba ukweli nasema siangalii chama , ankal kama muandishi asifanye hivo atakuwa anakosea , ajirekebishe...ni hayo tu

    mdau
    morogoro

    ReplyDelete
  18. HUYU MTOA HOJA NI ANKAL MWENYEWE , ASITUZUGE , UNAPENDELEA CCM HUO NDO UKWELI

    ReplyDelete
  19. katika baru zoooote michuzi kaamua kiuchaisha hii inayomfagilia..ukweli ni kwamba hii ni blog ya ccm kundi lake la libeneke niaongozana na j.k mbona hawaongozani na vyama vingine?! michuzi ur the legend but ur starting 2b boriiiiiiiiiiiiiiiiing..!jst b fair 2every chama!

    ReplyDelete
  20. Issa Michuzi unapendelea CCM hii sio siri mbona hauko kwenye Misafara ya vyama vingine??wewe ni mfayakazi wa serikali na ni mnazi wa CCM,Mbona polisi,wanajeshi,na askari magereza mnawapiga mkwara wasiegemee chama chochote?Hata Michuzi usiwe na upendeleo.Ukitaka bana wasiione kwani tumekuzoea,ujumbe umefika.Ni sisi walipa kodi ndio tunawalipa mishahara sio CCM.

    ReplyDelete
  21. Next time tumia small caps. Itasaidia sana watu kuelewa message yako na sio ku shout.

    ReplyDelete
  22. ACHA KUPIMA STATUS!! UMEJISHTUKIA MWENYEWE.NI WEWE MWENYEWE NDIO UMEEANDIKA HII ARTICLE.
    JARIBU KUBALANCE HABARI LASIVYO FUNERAL YA HII GLOB NI BAADA YA UCHAGUZI.hata usipost.message SENT.
    status: SUCCESSFULLY DELIVERED!!

    ReplyDelete
  23. Anzisheni blog zenu muandike mnavyopenda. Michuzi anafanya anachoweza.
    Wabongo midomo sana. Utadhani ni ajira yake kuwapa habari mnazotaka.
    Give him a break dudes!

    ReplyDelete
  24. Wabongo mabingwa wa kuchonga. Ni mazoea. Wanatafuta nani wa kumpotezea stress.

    Michuzi is doing wat he is doing. Salimi wengine watengeneze blog yenye kuandika mnayotaka

    ReplyDelete
  25. Ni kweli Ankal anapendelea chama tawala,na kuviminya vya upinzani akijitetea kuwa hawatumi habari zao...
    Hizo unazoziona ameziweka baada ya malalamiko ya wadau wengi humu ndani na nje ya blog hii...

    Hata hivyo siyo mbaya sana ana lea mkate wake usije ingia mchanga....

    Ankal najua kama kawaida yako utaiminya hii comment yangu. ila Ukweli ndio huo teh teh teh chonde chonde usinipeleke mahakamani Ankal!

    ReplyDelete
  26. Wabongo mabingwa wa kuchonga. Ni mazoea. Wanatafuta nani wa kumpotezea stress.

    Michuzi is doing wat he is doing. Salimi wengine watengeneze blog yenye kuandika mnayotaka.

    Yuko kazini na anaweka anachotaka kuweka na anachoweza kuweka

    ReplyDelete
  27. Waambieni watu wenu wamtumie picha na habari za vyama vingine.

    He cant do everything

    ReplyDelete
  28. acha longo longo wewe na ankal wote mmekunywa maji ya bendera ya ccm-mdau toronto

    ReplyDelete
  29. Ankal post unachotaka kwa wakati unaotaka. Hii sio blog ya serikali, hivyo mwenye blog ana haki zake, maslahi yake na utashi wake. Sisi wadau tunaridhika vilivyo na juhudi zako za kutuhabarisha. Kulalamika ni desturi yetu, hivyo piga kazi Ankal, usikatishwe tamaa!

    ReplyDelete
  30. wewe unayesema tubadilike ndo uliye nunuliwa,ukweli utabaki palepale kuwa michuzi kanunuliwa na CCM!

    ReplyDelete
  31. Acha unafiki ww uliepost hii ishu.Hakuna haja ya kumtetea Michuzi,jamaa ni kada wa CCM waziwazi.Kuna siku hapa alipost tangazo la cassete za nyimbo za Kikwete na akatangaza kwamba zinapatikana kwa mawakala wa CCM na hata kwake yy binafsi Michuzi,ilikua night wadau tukarespond na kumwambia kwamba anakiuka maadili ya uandishi wa habari akazitoa usiku ule ule.So howcomes Michuzi awe supplier wa cassette za Kikwete yy akiwa km mawanahabari.Acheni unafiki huwezi kulificha jua lisionekane wakati wa mchana,swala la Michuzi kuwa mpiga debe wamafisadi lipo wazi km jua la saa saba mchana.Anaweka habari1 ya chama cha upinzani na 11 za CCM.Alafu nyie mnaosema hii ni blog ya mtu binafsi anauhuru wakufanya anachotaka,sawa hatukatai lkn asidanganye awe wazi kwamba yy anapigia debe CCM then aone km watu tutalaumu.Tunachofanya ni kupinga unafiki.Alafu huwezi kusema eti km vp tufungue blog zetu nyie mnaosema hivyo inaonekana jinsi upeo wenu wakutafakari ulivyo mdogo,huwezi kuwaambia wadau maneno km hayo ilhali unadai hii ni blog ya Jamii au nini maana ya kitu kuwa cha jamii?Tutaendelea kumueleza ukweli Michuzi mapaka aache unafiki na awe mtu huru co kuuza utu wake kwa thamani ndogo.Hatumchukii Michuzi bali tunampenda ndio maana tunamrekebisha asiuze utu wake kwa faida ndogo na ya muda mfupi,mtu kuwa mnafiki ni kupoteza uhuru wako na kuwa mtumwa wa kifikra kwa kuinyima akili yako uhuru.

    ReplyDelete
  32. mnalalamika nini kama hakuna matukio mbalimbali ingieni kwenye jiachie blog mtapata kila kitu mimi ndio naingia siku hizi achagui chama

    ReplyDelete
  33. Ankal anatafuta ukuu wa mkoa, hivyo msishangae kukipendelea chama tawala.... Watu kama hawa uwa wanapata wakati mgumu sana pale wananchi watakapo fanya mahamuzi ambayo hawaku ya tegemea na mwisho wao uwa mbaya sana...

    Waswahili ni wanafki sana na ni waoga, ukiwaambia ukweli wanakuchukia na kukufanya adui wao.
    Ankal badilika usiwe mtuwa wa kundi la watu kwenye kazi zako binafsi.

    ReplyDelete
  34. aise mkiachiwa nchi nyinyi mtapiga marufuku mpaka hata facebook, nimewashtukia.

    ReplyDelete
  35. SAFI SANA UJUMBE UMEFIKA MPAKA UMEJITUNGIA MWENYEWE UNAJIFANYA MDAU KAANDIKA EITHER WAY KWANI HUKO CCM HUWA WANAMTUMIA AU ANAJIPELEKA MWENYEWE TUJUE MAANA YA CHOMBO CHA HABARI HAIMAANISHI MMILIKI ANAFANYA APENDAVYO KUNA MIPAKA NA KANUNI ALAAAAAA KUNYWA TU MAJI YA BENDERA NA USIPOANGALIA TUPA KULEEEEEEEEEE BLOGU YA JAMII IKIITWA NA TUONA UJAMII ETI OH FUJO HATURIPOTI UNAONA YA CHADEMA TU HAO WANAOKUPA VIJIPESA VYA KUNUNUA VIJIFULANA NEW YORK HUONI ENHEEEE HATUTONYAMAZA MPAKA KIELEWEKEEEEEEEEE poooooooooooooW

    ReplyDelete
  36. Kawaida wakati wa kampeni utaona haya. Blog hii ni sawa na wanavyofanya HABARI LEO, DAILY NEWS, na TBC. Huwezi amini hapa UK kwa mfano-wengi mnajua-haya yasingetokea. Ulimwengu wa sasa ni kutafuta maendeleo kwa kuleta ushindani kiasi kwamba anayeshinda anaongoza nchi.Haya yataitafuna nchi huko tuendako maana idadi ya wanao chukia UTAWALA na wapambe wao na vyombo vyao inaongezeka kila siku. Tuweni makini.

    ReplyDelete
  37. tuache lawama za kijinga sisi wabongo,kwanza tunatakiwa kua na uelewa wa tunavyovichangia sio uchangie kila kitu...mnaosema michuzi kanunuliwa na CCM kwani mwanzo alikua chma gani?michuzi ni CCM na anafanya kazi kwenye gazeeti la serikali sasa mlitaka atoe habari za kuwaminya wanampa tonge?akifukuzwa kazi au kuchukiwa na wakubwa nyie mnaochonga chonga hapa mtamuajiri?...na kosa lake nini kupendelea habari za CCM wakati kuna blog kibao zinaandika habari za wapinzani tuu?,TUKUMBUKE KUA HII BLOG PAMOJA NA KUTUPA HABARI PIA NI MALI YAKE BINAFSI NA BILA KUJISHAU HAPA KILA BINADAMU ANACHUNGA MASLAHI YAKE KWANZA NA HATA NYIE MNAONGEA HAPA SI MNATAKA MASLAHI YA VYAMA VYENU....ALIEKUFA KWA AJILI YA WENGINE NI YESU PEKEAKE,MSITAKE KUMSULUBU MICHUZI KWA FAIDA ZENU AU MNAVYOPENDELEA NYIE

    ReplyDelete
  38. NA MIMI NGOJA NISHINDILIE HAPA HAPA TENA KWA HERUFI KUBWA TU.

    MICHUZI ALIVYOANZISHA HII BLOGU AKAPAYUKA WADAU HII BLOGU YENU MIMI NIPO HAPA KU-PUBLISH TU NYIE NDIO MTAKUWA MNASEMA NINI MNATAKA KAFUNGUA KINYWA WEEEEH WOTE MAROGEKA NA UCHAWI WAKE WA AKILI.

    BLOGU IKAWA MAARUFU, WATU WAKAANZA KUNUNUA NAFASI ZA MATANGAZO, UMAARUFU UKAONGEZEKA MARADUFU.ANKAL AKAANZA KUPATA VISAFARI VYA HAPA NA PALE. SASA HAPA TEMBO NDIPO LILIPOANZA TIWA MAJI.

    ANKAL AKAJISAHAU KUWA HII NI GLOBU YA JAMII, AU ALISHASAHAU KUWA WANAJAMII WAMECHANGIA KWA KIASI KIKUBWA KUFIKA HAPA ILIPOFIKA LEO. KIKUBWA ALICHOSAHAU JAMII HII SI YA CHAMA KIMOJA NI YA VYAMA VINGI.

    CHAMA KIMOJA KATI VYAMA VYA WANAJAMII VIKAMNUNUA WAKATANGAZA DONGE NONO KAMA SIJAKOSEA, GLOBU IKAANZA KUTOWATENDEA HAKI WALE WANAJAMII WASIO WANACHAMA WA KILE CHENYE DONGE NONO.
    SASA MASWALI YANAKUJA HII SI GLOBU YA JAMII? ANKAL NI NINI UMERUDISHA KWA JAMII ULIWAHI KUTUMIA VILE VIJISENTI VYA MATANGAZO HATA KUWANUNULIA WALE WATOTO YATIMA JUICE ZILE ZA YEBOYEBO AU KUWANUNULIA FUTARI YA MIHOGO KWENYE KIPINDI CHA MFUNGO RAMADHANI. AU UMESAHAU ULIPOTISHA BAKULI TUKAKUCHANGIA FEDHA YA KUNUNULIA KAMERA. NA T-SHIRT JE?

    LABDA SIJUI MDAU AMESEMA VYAMA VINGINE HAVIKULETEI HABARI LAKINI HIKI KIMOJA UNAKIFATA MPAKA KULE KUSIKOFIKA MOTOKAA ILI MRADI UTULETEE HABARI WAMEFANYA NINI NA WAMEKUTANA NA NANI, TENA BILA AIBU KATI YA KAMERA UNAYOTUMIA NI ILE ULIYOPITISHA BAKURI NA WANAJAMII WA BLOGU HII WAKAKUCHANGIA AMBAYO NI JAMII YA VYAMA VINGI. JE SISI WANAJAMII TUSIO KWENYE CHAMA CHOCHOTE UNATUNDEA HAKI KWELI?

    HII KWELI NI GLOBU YA JAMII? AU ULIKUWA UNATULISHA CHUMVI TU ILI MRADI UPATE UPENYO NA UKIDHI MATAKWA YAKO? MUOGOPENI MUNGU NDUGU ZANGU KAMA KWELI TUNAABUDU NA KUAMINI MUNGU YUPO.

    MUNGU IBARIKI GLOBU YA JAMII NA WANAJAMII WOTE? MUNGU MBARIKI NA ANKAL NA AJENDA ZAKE ZA SIRI.

    UKIWEKA KWENYE MESSAGE HII SAWA HATA USIPOIWEKA NAJUA IMEKUFIKIA NA MESSAGE DELIVERED.

    MWANAJAMII ASIYE NA CHAMA CHOCHOTE CHA SIASA.

    BUCKINGHAMSHIRE, UKEREWE.

    ReplyDelete
  39. nilituma message mbona hukuweka?? nafikiri iligonga point....
    mlalahoi

    ReplyDelete
  40. Nani hajui kama issa ni mwajiriwa wa serikari ya chama tawala? nani mbumbumbu hajui sasa? hivyo sioni ajabu kuandika habari za ccm tu.michuzi rais kadondoka jangwani kaandika nini kuhusu kudondoka kwa raisi? haikuwa habari ya hata watanzania waishio nje kujua? aaaaaah uzushi mtupu

    ReplyDelete
  41. Kanunuliwa bwana kama hamtaki mbona kuna msg kibao za ukweli katumiwa na kaziminya michuzi yuko kwenye msafara wa kikwete tena ndioo moja kati ya wadau muhimu kwenye swala la habari kwenye kampeni za ccm tuone kama hiyo hela walioo kupa itakumalizia matatizo yako yote ya miaka mitano ijayo kwa kuwa ndioo kawaida ya wabongo kipesa kidogo tuu wanasahau kila kitu we need fair game kama hauwezi basi achana na taalluma ya habari nenda kwenye siasa...ccm kitu gani bwana yote yana mwisho...

    ReplyDelete
  42. Mimi naungana na wote wenyekusema kuwa michuzi anapendelea CCM, ukifuatilia kwa makini utaona amekua kwenye msafara wa Kikwete na hata kizibao chao amepiga picha nacho bila kificho. Kwa wenye kumtetea tunajua hii ni blog yake na anaweza kuweka anachokitaka; kama hivyo ndivyo anavyofikiria basi ni vizuri kwa wakati huu aondoe title ya "BLOG YA JAMII" kwa sababu jamii sio CCM tu jamii ni watanzania wote bila kujali imani za kidini au kisiasa. Kwanini vyama vingine vimtumie picha za matukio wakati za Kikwete anazifuata jikoni!!!!!!??????????

    ReplyDelete
  43. Ukweli ni kwamba Michuzi kama wa;ivyo waandishi wengine wa habari Tanzania wanapewa cho chote au kutishiwa na CCM ili waandike habari za upendeleo. Kwa mtindo huu, hii si Blog ya Jamii tena bali ni Blog ya CCM na ni wakati muafaka kuiweka pembeni kwa maslahi ya taifa letu.
    Mdau-Japan

    ReplyDelete
  44. Mimi nakupongeza ankal kwa kuliazisha libeneke ambalo sisi wengine tunaiga mfano wako.

    ReplyDelete
  45. Hivi wewe Justin na wasio waelewa wenzako. Jiulize hiyo message ambayo umeandika humu kuna mtu aliituma kwa niaba yako? Si wewe mwenyewe ndiyo umepost? Sasa kwa nini hivyo vyama vingine visifanye kama wewe ulivyofanya. Yaani watume. Come on men Ankal habari za CCM zinatumwa na CCM kwani hu hamsomi majina ya mdau kama Freddy Maro na wengineo? Acheni hizo bwana!!!

    ReplyDelete
  46. Mtoa hoja ananitia mashaka juu ya elimu yake na uelewa wake; Anayeweza kujua upendeleo unaolalamikiwa, ni michuzi na watoa maoni ambao wameshiriki mara nyingi kutoa maoni ya upande mwingine ambayo hayaandikwi. Huu si ustaarabu wa haki ya kupeana habari kwani mtoa maoni huingia gharama akitegemea maoni yake yatasikilizwa. Hivyo basi wale waliowahi kutoa maoni na kisha kutoyaona kwenye blog wanayo haki ya kulalamika, wana CCM mnakuwa kama wajukuu wanaolelewa na bibi hampendi kusemwa mnapokosea! Huu si uungwana.

    ReplyDelete
  47. Ankal na mafisadi wa CCM dugu moja babake! Lakini ndo naye anapokula! Huoni kajenga nyumba yake kule njia ya kwenda bagamoyo sijui kunaitaje vile!!! alafu alipiga picha na Mjengwa akatuonyesha lile fridge lake la china lakini liko bomba anatesa kwa bongo. Mwisho nasema tena, Ankal na CCM/JK dugu moja. Unabisha? toa hii na uone washkaji watakavyounga mkono hii hoja lakini najua kama kawaida ya makada utaifukia. Fisadi weeee!!

    ReplyDelete
  48. naamini atajirekebisha sasa,ila nao vyama vingine vyote basi watume picha na matukio yao ktk blog hii au sie wadau kama tuna matukio ya vyama vingine basi tutume ankal aweke humu mf chama cha TEA,TLP,SAUT nk nk

    ila kukwepa ccm ni ngumu sana kwa mstakhabari wa uhai wako bongo!!lol
    na hasa ukiwa unalipiwa kila kitu almost...

    ReplyDelete
  49. nyie mavii tuu,kwani JAMII FORUM SI BLOG YA JAMII?na mbona hamlalamiki inapoandika habri za kuiponda CCM tuu nawala hawaaandiki za kuisifu?na mbona wao wanapigia kampeni CHADEMA na wala hamuongei?hii ipo dunia nzima nyie mliokua nje ya TANZANIA acheni viherehere makjiona ndio mnajua kila kitu duniani,nyie vipi...mbona vyombo vya habari vikubwa tuu vinakua upnde flani kwenye kampeni?nani hakuona bbc walivyokua wanampigia debe brown?na sky news james cameroun?mbona hamkosema kitu?vyombo vyote vya habari vinafanyia kazi maslahi yao bana hata wao wanatizama upande ambao ukishinda chombo chao kitafanya kazi vizuri.gazeti la MWANA HALISI kwa mfano ni la upinzani mbona hamuongei kua kazi yake ni kuiponda CCm tuu.
    MICHUZI kua katika kampen ya CCM nini kosa lake si wamemlipa?hao chadema na vyama vingine je wamempa fungu akakataa?mbona hamuongei kua kwenye blog kuna matangazo ya VODA tuu n TIGO hamna?au PRECISION AIR na hamna COASTAL AIR?hii ni biashara bana nyie mnaongea mnamchangia gharama za uendeshaji hii blog?,ccm wamelipa na hao watu wenu watoe mkwanja hamna cha bure hapa nanai awafanyie kampeni bure?wamlipe ankal waone akatae

    ReplyDelete
  50. Ankal Michuzi, Ninakuunga mkono 100%!!! CCM ndicho chama pekee kinachowaunganisha Watanzania wooote wa makabila, dini na rangi tofauti. Mbona Chadema, TLP, NCCR na CUF wana magazeti ambayo yanawapendelea na hamna mtu kalalamika???? Mimi niko hapa Arusha ambako sasa hivi Chadema kimekuwa ni CHAMA CHA KABILA MOJA TU, kwa hivyo hapa Arusha uchaguzi utakuwa ni kati ya watu wote (CCM) versus kabila la Mr M...... Kwa hivyo Ankal uzi ni huo huo, usitetereke msimamo ni ule ule wa Baba ya Taifa. Wacha walalamike, wewe DO THE RIGHT THING. M. R. Mollel. Daraja 2 Arusha.

    ReplyDelete
  51. Haya tutatuma habari za vyama vingine. Ngoja tusubiri tuone kama ankali ataziweka.

    ReplyDelete
  52. ......Sasa Ankal balance ! tuma vijana wako wawili timu ya Caf, wawili Chadema, na mmoja mmoja kwa wengine. vinginevyo kuwa muungwana waambie wadau CCM wamekushikisha kitu kidogo.....tutakuelewa tu we wetu bwana! Mbona chenge na lowasa tumewaelewa kwamba wao hawahusiki na tunawarudisha tena Bungeni.
    GONGEO.

    ReplyDelete
  53. Aisee Ankal kuna sms inazunguka inamsaga Marando kweli kweli. Unataka kuniambia hujatumiwa? Ebu itume humu ili watu wajionee na wamfahamu uchafu wa Marando. ...babake. Anajifanya mtakatifu kuliko pope. Mamae...

    ReplyDelete
  54. Mdau wa 6:36, Nakumbuka 1995, NCCR ilikuwa ina nguvu zaidi ya chadema ya sasa. Hiyo sms sikuiona lakini wakati huo wana-nccr mageuzi walidai kuwa marando alikidhoofisha chama hicho na baadaye kupewa ubunge wa EAC kwa tiketi ya CCM. Hata hivyo mdau naomba tusitumie matusi ya nguoni kuwatukana watu. Huo si uungwana wa Ki-TZ. Matusi inamdhalilisha anayetukanwa na kumdhalilisha ZAIDI mtukanaji.

    ReplyDelete
  55. Kada wa CCM na ni mwajiriwa wa Habari leo,daily news, wote wanaipigia debe CCM nukta.

    ReplyDelete
  56. Hebu achen zenu hizi nyie mijitu ya ughaibuni .. mnajifanya wajuaji sana kama .mnauwezo si mrudi nyumbani ..mkagombee nafasi KWENYE HIVYO VYAMA ...Michuzi anatoa anachopenda ,msimpangie sheria..wala hamjamuajiri nyie..michuzi ni best wa JK hata kabla hajawa Rais Hebu ingia kwenye Search engine ya google image tafuta picha ya Michuzi na JK wakiwa Chalinze wakivuka mto ..

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...