JK AMEREJEA JUKWAANI MUDA HUU NA TAYARI ANAENDELEA NA HOTUBA YAKE, AKIUAMBIA UMATI KWAMBA 'JAMANI NIMEFUNGULIA' AKIMAANISHA KWAMBA ANA UCHOVU AMBAO BILA SHAKA UMESABABISHWA NA SWAUMU. KAMPENI NDIO ZIMEFUNGULIWA RASMI NA KESHO ANATARAJIWA KUWA MWANZA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. kaka inakuwaje kwa Rais wetu mpendwa chaguo la mungu kudondoka mara kwa mara? Japo husemwa kuwa historia haijirudi lakini tena? Jangwani tena na Mwanza Je?

    ReplyDelete
  2. SIO SWAUM NI KWAMBA KATAMBIKIA KWA WANYONGE WAZEEE WAMLINGOTINI OYEEEEEEEEEE MWANANENU HUYUUUU

    ReplyDelete
  3. Mdau wa Sat August 21 04:37:00, nyie ndio wale hata ukipata mafua unaenda kutazama bao aliyekuroga nani. Wakati unaelekeza kidole kimoja kwa mwenzio vitatu vinakuelekea wewe mwenyewe! Acha shirki!

    ReplyDelete
  4. Lakini kama afya yako ina tatizo kwa nn asiache kufunga! Huyo Mungu c anajua kama ni mgonjwa! Au ahutubie amekaa kwe kiti bac kitaeleweka! Mdau ulieuliza mwz itakuaje USHINDWE!

    ReplyDelete
  5. Natoa pole kwa Mheshimiwa Rais wetu Mpendwa Jakaya Kikwete.

    Hata hapa Marekani mbona wanaSiasa wanaanguka kila mara. Ratiba zao ngumu, na wakati mwingine wanaenda kwenye mikutano hata wakiwa wagonjwa. Wanajikaza kweli. Tusisahau hata kama mtu ni Rais bado ni binadamu.

    ReplyDelete
  6. Mungu akupe afya njema Mh Rais tunakuombea kwa Mungu Daima hiyo ni katika mitihani midogo tu Mungu yupo pamoja nawe endelea na Kampeni na ushindi ni wako tu.

    ReplyDelete
  7. maskini Jk pole sana!

    mariam

    ReplyDelete
  8. Kwanza kabisa JK pole na hali hiyo na tunakuombea Mungu akupe afya nzuri na uendelee na kampeni yako.
    Kwa wadau, sijui issue ni nini hapa. Mara watu wanareta hadithi za Marekanai mara za Slaa, mara ooh.
    Ukweli ni kwamba mhe JK ana matatizo ya afya kama bindamu wengine. Lakini si mara ya kwanza kuanguka tena hapo Jangwani Kwa sababu ya kawaida yetu watu wa CCM tunapenda rangi nyeusi kuiita nyekundu, na nyekundu, nyeusi. Tumezoea. Kwa utamaduni wetu huo kila Mh anapoanguka tunasema ni uchovu. Sasa ndio tu kampeni imeanza ni uchovu wa nini. swaumu mbona siku ndio ilikuwa imeingia kati. Mh ni mgonjwa na kama tungekuwa tunapenda kukirui ukweli angkuwa ameshauriwa mapema tokea hata mwaka jana akachukua likizo ya afya hata ya miezi sita na kutafuta tiba katika nchi zilizoendelea katika utalaam wa tiba , kv Marekani anakotembelea sana au hata China. Mh Mkapa alichukua likizo wakati akiwa madarakani na akatibu ugonjwa uliokuwa ukimsumbua. Tukiendelea na ung'ang'anizi wa kutaka kuita rangi nyeupe nyekundu, tutakuja kujuta. Na hatupendi majuto ambayo yanaweza kuzuilika. Ninapendekeza, kama atapata tena urais, basi achukue likizo ya afya kwa miezi sita ya kwanza. mkabidhi Bilali sijui Balali madarka.
    Ankal, sijachafua hali ya hewa usinitupe kapuni kama ambavyo umekuwa ukifanya katika maoni yangu ninayokutumia.

    ReplyDelete
  9. Msanii tu huyo, hana lolote.

    Ugonjwa! Kwani kuumwa kaanza yeye? Mtu ni head of State na ana all the necessaries halafu anajiangusha-angusha! Je wale wagonjwa na wasio na hizo necessaries ndio wasemaje?

    Akajiunge zake Kaole huko!

    Na bado!

    ReplyDelete
  10. Michuzi, Kikwete hakusema, "JAMANI NIMEFUNGULIA."

    Alisema, "NIMEFUNGULIA JAMANI."

    ReplyDelete
  11. Chemi habari!
    Unaposema hata hapa marekani wanasiasa wanadondoka tupe mfano ni nani? Najua kulikuwa senetar Bird na Tedy ambao walikuwa na long time condition (saratani) ndio walianguka katika mkutano. JK anacondition gani? Kuhusu ramadhani sikubali kabisa maana hajaanza leo kufunga a kama mgonjwa anayoruhusa kuacha. Ukisikiliza hiyo hutuba utaona kuna kama his speech was slur for a minutes before he went down.They need to check on him. Lakini unajua wanasiasa ni wajanja mno. Nadhani JK alijifanya kuanguka ili watu wampe sympathy baada ya mapungufu yaliyotokea dodoma kupitisha wagombea wenye kashfa.

    ReplyDelete
  12. mzee kama vipi njoo ufungie ramadhani uk huku kibaridi cha maana sio utahutubia kwa TELECONFRENCE TU-FANYA KAMA VILE RAISI WA SOMALIA SERIKALI NZIMA INAKAA KENYA NCHI IPO SOMALIA

    ReplyDelete
  13. Mdau hapo juu umesema kweli wanahitaji afanyiwe uchunguzi wa afya yake na kupumzika pia. Jamani duniani humu muungu kaumba maradhi mengi, mimi nilikuwa mara kwa mara napata kizungu zungu na kuishiwa pumvi na kuishiwa nguvu hasa penye mikusanyiko ya watu, hewa nilikuwa naiona haitoshi. I can imagine how our president was feeling. Lakini tatizo halikuonekana kwenye hospitali za nyumbani kabisa. Mpaka siku moja nilipotaka kuanguka dukani uzunguni kwenye seli yaani duka lilifurika watu, kidogo niitiwe ambulance, nikaitwa mtu wa first aid, nikawekwa mahali kwenye upepo, na kupewa maji ya kunywa ya baridi, nikarudi mzima!

    Kupimwa hospitali kumbe mimi cells zangu ni sickle, yaani siugui sickle cell bali nina cells ambazo nyingine ni sickle wenyewe wanaita AS, ukiwa sickler ndio wanaita SS. Nimesema haya ili watu wajue kuwa unaweza kutembea ukijiona mzima kumbe una tatizo, fikiria miaka karibu 50 ndio tatizo linaonekana. Kwa hiyo kuanguka kwa mheshimiwa jukwaani si kitu cha ajabu, hasa kwenye umati na msongamano wa watu kama waliokuwepo hapo Jangwani.

    ReplyDelete
  14. Tufanyeje ili kuthibiti kwamba sisi tunachukia na kupambana na rushwa.Tuna kazi kubwa mbele yetu lakini inatuagiza mapambano hayo bila kuchoka. Tuna waahidi watanzania wakitupa ridhaa yao tutafanya zaidi. Tumetekeleza mengi na tutafanya zaidi. Aisee tupeni ridhaa yenu tutafanya zaidi, tutafanya zaidi,tutafanya mambo,mambo..MKUU NAONA HAPA NAFSI TU ILIMSHINDA MUHESHIMIWA. HAPA LOWASA NDIO KAMUANGUSHA JK. LOWASA ASIKAE KARIBU NA JK. TENA AMA ATAKUA ANA ANGUKA KILA SIKU.

    ReplyDelete
  15. kufunga + uchovu lazima mtu utaanguka. jamani kufanya kampeni sio jambo dogo ni kazi nzito sana. ndio maana unakutwa wagombea huwa wanakunywa maji mdogo mdogo sasa sembuse JK aliekuwa amefunga.

    ReplyDelete
  16. HEHEHEHEHEHEHEHEHE Sijaharibu hali ya hewa wadau maana msije kunirarua kwa mijineno MIE NAPITA TU MHHHHHHHHHHHHHH

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...