JK na Dk Ghalib Bilali wakiwa wameshikana mkono baada ya kurejesha fomu za kuwania kugombea urais kwenye uchaguzi mkuu ujao katika Tume ya Uchaguzi jijini Dar leo. CCM ndio ilikuwa ya kwanza kurejesha fomu hizo. Kwa leo vyama vinavyorejesha fomu ni kama ratiba inavyoonesha hapo chini. Picha na Francis Dande wa Globu ya Jamii



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. ccm masaa mawili, wengine wanafanya kubanana kwenye saa moja. tutafika tu.

    ReplyDelete
  2. Marangu OneAugust 19, 2010

    Anony wa Kwanza, ni kwamba JK bado ni Rais. Kuna masuala ya usalama lazima yafuatwe. Inabidi advance party ipate fursa ya kuhakiki eneo kwa muda wa kutosha kabla ya kuwasili kwa POURT.

    ReplyDelete
  3. Sasa ni saa tisa, mbona hakuna picha ya Slaa akirudisha fomu au bado hajarudisha nini? au michuzi wewe ni CCM? acha hizo michuzi....weka picha ya wagombea wa vyama vingine cCM tumewachoka.

    ReplyDelete
  4. Eeeh mdau wa kwanza kumbe umeona kama mimi. Extra one hour kwa ajili ya kampeni.

    Tutafika.

    ReplyDelete
  5. kikwete tumbo hilo fanya mazoezi usiwe kama mkapa mdowea ftari.

    ReplyDelete
  6. Mtoa mada hapo juu kweli ameichunguza ratiba kikamilifu. Je tume ya uchaguzi mnaanza upendeleo asubuhi na mapema kabla hata mbio za kampeni hazijaanza? Mbona CC mmmm, wamepewa jedwali lenye masaa mawili? Na Chama ka Chadema wakapewa jedwali ndogo? Tutafika tuu, hakuna matata. Kenya hawakujua watakuwa hapa, Marekani hawakujua kama kutakuwa na mabadiliko, CHANGES..Zimbabwe pia, na sasa mwenzio akinyolewa, na wewe jiandae......Change is coming to tanzania...change is inevitable...now!!!

    ReplyDelete
  7. Ankal acha ubaguzi wa wazi kabisa.
    Inakuwaje uweke picha za ccm tu wanaorudisha fomu wakati kuna vyama vingine pia vimerudisha fomu leo tena ni DSM. Iweje picha ya Mbeya iwekwe kwanza? Acha hizo bwana,lakini nililitegemea hilo kwa kuwa wewe na ccm ni damu.
    Tunawasuburi kwenye masanduku Oktoba.

    Upinzani Oyee, Dr.Mabunduki Oyeeeee!

    ReplyDelete
  8. hii chama mpya iliyokuwa CCJ baadae ikaama kuwa CCK mbona siioni kwenye list

    ReplyDelete
  9. Wabongo kwa kulalamika bila kufanya uchinguzi hamjambo. Yani kitu kidogo hata hamfahamu kitu lakini mnaanza ooh mbona masaa mengi, mara ooh tumbo...inahusu nini. Inaonekana nyie hata maisha yenu hayako sawa..au mna matatizo kichwani. Kabla hujalalamika fanya uchunguzi kwanza ndio uanze malalamiko. Sasa na bado mwaka huu ushindi wa kishindo kupita historia inavyojionyesha. Manependa kubwatuka tu halafu hata vitambulisho vya kupiga kura hamna....chenji kabicha

    ReplyDelete
  10. Mtoa mada wa pili acha kutuzingua kwa kisngizio cha Urais na Usalama..huu ni uonevu wa wazi wazi tena mapemaaa!!

    Ingekuwa ni chama kingine kimefanyiwa hivyo ungemuona Makamba u Msekwa anaanza ktuishia na barua za malalamiko kwenye vyombo vya habari-Mwaka huu "Mtu mzima Hatishiwi Nyau".

    ReplyDelete
  11. Kagame wakati wa kampeni aliacha kila kitu cha Ikulu na kutimia vyake binafisi, mpaka gari hakutumia la selikari alitumia lake binafsi.

    Sasa subiria uone kampeni za CCM,kudadadadadekiiiiiiiiii.....!!!! mpaka kijiko cha ikulu kitumika.

    ReplyDelete
  12. Hicho ndicho chama tawala bwana.Ingia barabarani mpige picha na siyo kunungunika.Angalia msije kukosa hata hiyo nafasi ya 3 kwani janja yenu ya helkopta CCM wameijua na wanazo.Mgonjwa wa watu angeachwa akahangaika kurudi bungeni sasa mtakosa mwana na maji ya moto.Mnadhani siasa ni madhabahu au ukumbi wa bunge.Kama ni kujenga hoja mbona mpambanaji Tundu Lisu yupo?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...