Afisa Elimu Mkuu Idara ya Uratibu wa Elimu ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI akimweleza ,Naibu waziri wa TAMISEMI Mhe. Aggrey Mwanri namna ya usimamizi na uendeshaji wa Elimu wakati wa sherehe zakutimiza mwaka mmoja tangu KILIMO KWANZA kuanzishwa wakati wa maonyesho ya nanenane mjini Dodoma. Waziri wa Nchi ,ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI) Mhe. Celina Kom bani (kushoto)na wa pili kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Bahi ndugu Betty Mkwasa wakimsikiliza Ofisa mwandamizi wa Karadha ya Fedha ,Benki ya Rasilimali Tanzania ni ndugu Betty Massanja kwenye Maonyesho ya Nanenane Mkoani Dodoma.Mwenyekiti wa kikundi cha Tupendane kilichoko katika kijiji cha Nala Wilayani Dodoma Bwana Peter Lenjole akimpa maelezo jinsi wanavyolimia Trekta ndogo za kulimia (Power Tiller) Waziri wa nchi ,Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI)Mhe.Celina Kombani (wan ne kushoto) kwenye Maonyesho ya Nanenane Mkoani Dodoma.
Waziri Mkuu (TAMISEMI) Mhe. Celina Kombani wa pili kulia akimsikiliza kwa makini Ofisa wa Kilimo (Kilimo na Lishe) bi. Stella Kimambo jinsi mashine iliyopo mbele yao ijulikanayo kama (Cassava Grater)inayosaga Mhogo mbichi na kupata machicha ambayo unaanika nakusaga tayari kwa unga au unaukamua tayari kuwa wanga na ukautmia kama dawa ,na ukatumika kwa kutengenezea chapatti ,kwenye maonyesho ya nanenane Mkoani Dodoma.
Nyumba za bei nafuu na za kisasa zilizojengwa na Kampuni ya Space Creation zilizoko kwenye maonyesho ya Nanenane Dodoma.
Alfred Katata (wa kwanza kushoto ) wa Kibaha Education Centre akimwelezea Naibu Waziri wa (TAMISEMI)namna ya Uzalishaji wa kuku kwa ajili ya kupiga vita Umasikini wakati wa Maonyesho ya nanenane mjini Dodoma.
wanafunzi wa St. Home Primary School wakifurahia Magazeti ya Nchi yetu yanayotengenezwa na Idara ya Habari Maelezo na magazeti ya Utamaduni wetu yanayotengenezwa na Wizara ya Habari,Utamaduni na Michezo wakati wa Maonyesho ya Nanenane Mkoani Dodoma walipotembelea banda hilo.

(Picha zote na Anna Itenda wa Globu ya Jamii - Dodoma)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Jamani hizo nyumba za bei nafuu zina madirisha! au macho yangu. Nyumba gani hizo. Hizi nyumba si kama zile za mabati zilizo kwenye vituo kadhaa vya polisi au kandokando ya njia ya reli ya kati.

    Bila shaka zinawasubili walimu.

    Mi naona zijengwe mikoa ya baridi tu, other wise bila madirisha si nyumba hizo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...